Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Mbili) KOTI JEUSI – 12
    Hadithi

    KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Mbili) KOTI JEUSI – 12

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 8, 2024Updated:May 8, 202425 Comments7 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Riwaya Ya Koti Jeusi
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Najua kila Mtu atanipa jina analoona linanifaa lakini hakuna kati yenu ambaye angeliweza kustahimili nitakacho waeleza. Atakaye niita Muuwaji ni sawa kwasababu nastahili kuitwa hivyo” Sofia akaanza kumsimulia Mpelelezi Marcus namna alivyogeuka kua Muuwaji. “

    Tuendelee sasa

    Sehemu Ya 12

    Miaka kadhaa iliyopita. Jijini Mwanza.

    Sofia alikua akiishi Jijini Mwanza kwa maelekezo maalum ya Baba yake Bilionea Yusuf, alipewa kazi ya kusimamia kiwanda cha Kusindika Samaki aina ya Sato na kusafirisha kuelekea Nchini Italia. Siku moja Mchana akiwa amechoka aliamua kupitia kwenye Mgahawa mmoja maarufu sana hapo Mwanza.

    Akaagiza ndizi na Samaki wa kuchemshwa, akala kidogo kisha akawaona Watu wawili Mwanamke na mwanaume wakiwa wameingia hapo. Walionekana kua na Maisha ya chini lakini nyuso zao zilijaa upendo uliomiminika hadi kwenye Maungio yao. Walisimama eneo la kuagiza chakula, Sofia alijikuta akipendezwa nao, akaacha hata kula akiwatazama kwa Maana walimvutia mno.

    Hata alisimama huku akitabasamu kisha alitoka na kuelekea nje, akiwa anataka kuingia kwenye gari aliwaona wakitoka hapo wakiwa wameshikana, akajikuta akiwatazama tena. 

    Mwanaume alidondosha pochi akiwa anaiweka kwenye mfuko wa nyuma, Sofia alipojaribu 

    kumshtua waliingia kwenye Bajaji kisha waliondoka hapo, Sofia akaiyokota Pochi hiyo, akaiweka kwenye gari kisha akaondoka hapo, alikua akipendelea kwenda Mgahawani hapo hivyo aliamini atakaporudi pengine atawaona tena na kuwapatia pochi yao.

    Usiku ulipoingia aliona aikague ile pochi pengine angekuta mawasiliano ya Wapenzi wale, ndani ya pochi hiyo alikutana na picha iliyopigwa na kuhifadhiwa humo, picha yenye sura za wapenzi hao. Nyuma ya picha palikua na majina ya wapenzi hao, Mwanaume alitwa Julius na Mwanamke aliitwa Salma.

    Alikuta pesa kidogo na kadi moja ya mawasiliano, kadi hiyo ilikua ya mawasiliano ya yule Mwanaume anayeitwa Julius, akaamua kuipiga namba huyo, kweli iliita na kupokelewa na Mwanaume ambaye baada tu ya kuongea, Sofia alikubali ndani ya moyo wake kuwa alikua na sauti nzuri mno.

    “Samahani wewe ni Julius?” aliuliza Sofia

    “Ndiyo, nazungumza na Nani?”

    “Naitwa Sofia, nimeokota pochi yako mgahawani sijui utaipataje?” Sauti ya Mwanaume Julius 

    ilichangamka baada ya kusikia habari hizo, basi kutokana na umuhimu wa ile pochi akaomba 

    aelekezwe mahali alipo Sofia ili akaichukue Usiku huo huo. 

    Baada ya kuelekezwa alichukua Pikipiki hadi Hotelini, kwanza alipofika hapo ilitosha kumwambia kua aliyeokota pochi si Mtu mwenye shida kabisa, maana ni gharama sana kuishi hapo Hoteli yenye hadhi ya nyota tano.

    Akampigia simu Sofia, muda huo mvua ilikua inaanza kunyesha, Sofia akamwelekeza mahali alipo, Julius alipanda hadi juu na kukutana na Sofia. Kwanza tu alipomwona alijiambia mwenyewe kua alikua ni Msichana mzuri sana na mwenye pesa. 

    “Samahani kwa kukusumbua” alisema Sofia, Julius akajichekesha kidogo

    “Hata usjali, ni muhimu nimeipata leo maana kulikua na pesa muhimu sana” Baada ya kupatiwa pochi akataka kuondoka lakini Sofia akamwuliza

    “Utaondokaje na mvua kubwa kiasi hiki?” Mvua ilishakomaa, ilitiririsha maji kwenye vioo vya Hoteli

    “Baki hapa kidogo angalau mvua ipungue” alisema Sofia akamkaribisha ndani ya chumba chake, 

    wakawa wanaongea mambo kadhaa yaliyowajia kwenye fikra zao, mwisho wakajikuta wote 

    wamegongana kwenye Unywaji wa pombe ili kujichangamsha na Baridi. Sofia akaagiza pombe wakawa wanakunywa, tena ni pombe za gharama sana. Walikunywa wakalewa, wakazima hapo chumbani.

    XXX

    Asubuhi mapema, Sofia alikua wa kwanza kudamka, kwanza alisikia harufu ya pombe. Kilichomshtua kando yake alikua amelala Mwanaume, haraka akakumbuka kilichokua kimetokea Usiku, akajikagua na kuona alikua amefanya mapenzi na Mwanaume huyo asiye mfahamu vizuri. Haraka Sofia akakimbilia chooni kujisafisha, akasimama mbele ya kioo akijitafakari

    “Nimefanya nini sasa, nipo katika siku zangu za Hatari” alijisemea, mara moja alimfuata Julius na kumwamsha huku akimfokea na kumtaka aondoke haraka sana, hakumpa nafasi ya kuzungumza kabisa, akamtimua Hotelini kisha akaketi kitandani akilia. Muda huo huo alipigiwa simu na Baba yake, simu iliyomtaka kufunga ripoti zote za Kibiashara na kurudi Dar, tena akiambiwa kuwa ataenda kuwa Msaidizi wa karibu wa Baba yake, angalau simu ya Baba yake ilimrejeshea tabasamu.

    Baada ya siku tano akarejea Dar na kuanza majukumu mapya kama msaidizi wa karibu wa Bilionea Yusuf, wiki mbili mbele alianza kuhisi dalili za Ujauzito, kizunguzungu na kichefuchefu vilimtawala sana.

    Alipoenda Hosptali kupima alikutwa na Ujauzito wa wiki tatu na siku mbili, alichanganikiwa sana Sofia.

    “Katika Maisha yako kamwe usije ukatoa Ujauzito Sofia, utajipa mkosi mkubwa” aliyakumbuka 

    maneno ya Marehemu Mama yake, lakini aliwaza angeweza vipi kuzaa huku Baba wa Mtoto akiwa amepotelea Hewani? 

    Aliomba ruhusa kwa Baba yake na kurudi tena Mwanza huku akiwa na kazi moja ya kumtafuta Julius, alishapoteza namba ya simu ya Julius. Mahali pekee ambapo angeweza kumpata ni pale Mgahawani, akarudi tena Mgahawani na kumwulizia kupitia kwa Mtu wa mapokezi.

    “Oooh! Hajafika hapa wiki moja sasa, si yule Msonjo mwenye pua ndefu?”

    “Eeeh ni yeye”

    “Anaishi Mtaa wa sita kutoka hapa, kuna mahali pana kipoozo cha Umeme, ukiuliza hapo utampata” akasema Mtu wa Mapokezi akionesha kumfahamu vizuri Julius

    Akaelekea alipoelekezwa, hapo akakuta Wamama wawili wakisukana, akawauliza

    “Julius kahama hapa juzi baada tu ya harusi yake” alisema Mmoja aliyekua akimsuka mwenziye, Sofia alishtuka

    “Ameowa?”

    “Ndiyo juzi tu hapa”

    “Anaishi wapi kwa sasa?”

    “Kahamia Nyegezi sijui ni sehemu gani ila anaishi nyegezi kwa sasa” akagongelea Msumari wa moto kwenye moyo wa Sofia, hakuwajibu chochote akarudi zake kwenye gari kisha Hotelini. Tumaini la kumpata Baba wa Mtoto aliye tumboni lilionekana kupotea taratibu.

    Akamaliza wiki huko Mwanza akimtafuta Julius kila kona, akatumia pesa kadili alivyotaka kuhakikisha anampata, Bilionea Yusuf kila alivyompigia simu Sofia hakuambulia cha Maana zaidi ya kusubirishwa, 

    Sofia alichanganikiwa sana. Ndipo Mzee Yusuf akamtuma mpelelezi kumpeleleza Sofia huko 

    Mwanza.Wiki moja ilimtosha Mpelelezi wa siri kugundua kilichompeleka Sofia huko, taarifa ya mpelelezi ilimpa hasira sana Bilionea Yusuf, akamtuma Mpelelezi amuuwe Julius kisha amteke Salma kwasababu aliamini mahusiano hayo yangeharibu muelekeo wa Maisha ya Binti yake Sofia.

    Siku tatu mbele, kamanda wa Jeshi la polisi Jiji la Mwanza alithibitisha kifo cha kikatili cha Julius na kutoweka kwa Mke wa Julius aitwaye Salma.Tukio hilo lilimwacha Sofia na maumivu makali sana, aliona Mtoto wake angezaliwa Bila Baba lakini kwa kulipa kisasi cha Baba wa Mtoto wake akaona awekeze nguvu kuhakikisha anamnasa Salma.

    Kwa Mujibu wa jeshi la Polisi alitajwa kuwa mhusika namba moja wa Mauwaji hayo yaliyotokea ndani ya nyumba waliyopanga, mwili wa Julius ulikutwa umechomwa visu zaidi ya vitatu.Sofia alirudi Dar lakini aliajiri Mtu wa kumsaka Salma kila kona ya Tanzania, aliapa atamuuwa endapo atamnasa huku akimpachika kosa la kuhusika na Mauwaji ya Baba wa Mtoto wake.

    Mwezi mmoja ukapita, Salma akiwa amefichwa kwenye Godauni huko Mwanza. Alipatiwa chakula na mahitaji mengine, siku moja Bilionea Yusuf akawasiliana na Muuwaji aliyempa kazi, akahitaji kumwona Salma kwa picha. Muuwaji akampiga picha Salma na kumtumia Bilionea Yusuf, hakika alistaajabu na uzuri wa Salma.

    Akamwagiza Muuwaji awasiliane na polisi kisha Salma akamatwe na kufikishwa Mahakani kisha atamtafutia wakili mzuri wa kumtetea na Mwisho angeonekana si Muuwaji angeachiwa huru, Kisha Bilionea Yusuf angejitokeza na kumwambia Salma kuwa yeye ndiye aliyemsaidia akiamini angeutumia Mwanya huo kumuoa Mwanamke huyo akiamini hafahamiani na Binti yake Sofia, kumbe Sofia alikua akimfahamu kwa sura na aliapa kulipa kisasi.

    Mpango huo ukafanikiwa, Salma akakamatwa na kufikishwa Mahakamani kisha akaachiwa baada ya kushinda kesi, Bilionea Yusuf akajitokeza na kuitumia nafasi hiyo ya Kumsaidia ili amuoe, Salma asingeliweza kuikataa fursa hiyo ya kuolewa na Bilionea Huyo.

    Aliolewa na Bilionea Yusuf, akabadilishiwa Maisha yake na kupewa nafasi ya msaidizi wa karibu wa Bilionea Yusuf, nafasi ambayo Sofia alikua akiitumikia akapewa Mwanamke huyo, kisasi kikawa kizito moyoni kwa Sofia ambaye alichagua kukaa kimya, akaapa kua ziku moja atamuuwa Salma ili kulipa kisasi kwa ajili ya Binti yake huku naye akiamini kua Baba yake alimwoa Salma kimakosa kwani Sofia hakumweleza chochote Baba yake juu ya kumfahamu Salma, kumbe Mzee Yusuf alikua akifahamu kila kitu hadi ujauzito wa Binti yake.

    Akamzaa Adela, akafanya siri kubwa sana mbele ya Baba yake kuhusu Baba wa Mtoto huyo, akamwambia Baba yake kuwa Baba yake Adela yupo nje ya Nchi, uwongo huo haukua na Mashiko kwa Bilionea Yusuf ambaye alikua na siri ya kumwua Baba wa Adela.

    Mzee Yusufu akamtendea mazuri Salma huku akiwa na siri ya kumuulia Mume wake, akamtendea mazuri zaidi Adela kwa kumpa Utajiri mwingi kisiri kama fidia ya kumfanya awe Yatima. Je, Nini kitaendelea?

     

    Jiunge WhatsApp Channel Ya KIJIWENI Ili Kuwa Wa Kwanza Kupata Updates Za RIWAYA Hii Kwa Kubonyeza Hapa 

    SOMA Uchambuzi Na Makala Mbalimbali Kwa Kubonyeza Hapa

     

     

     

    KOTI JEUSI Koti Jeusi Kijiweni riwaya ya koti jeusi

    25 Comments

    1. Pretty naah on May 8, 2024 3:07 pm

      admin unastahili maua yakoh😏

      Reply
      • Mhariri on May 8, 2024 3:39 pm

        Pamoja Sana Familia

        Reply
      • DEOGRATIUS MLANGWA on May 8, 2024 3:53 pm

        Duuuuh aisee story nzr sana,yan uwezikuchoka kuisoma

        Reply
      • Zacharia on May 8, 2024 5:12 pm

        Love story

        Reply
        • Bintii kimmy on May 9, 2024 12:31 pm

          🔥🔥huna baya Tajiri

          Reply
      • King on May 9, 2024 1:41 am

        Mtumie hata ya soda sasa

        Reply
    2. Rumbyambya Jr on May 8, 2024 3:15 pm

      Hii Imeenda what a story all styles included including Flashbacks
      Good work Admin

      Reply
      • Mhariri on May 8, 2024 3:39 pm

        Shukran Sana

        Reply
      • Becka on May 8, 2024 3:53 pm

        Puliza sana admn
        Tuone Panapo vuja

        Reply
    3. Imma MK on May 8, 2024 3:18 pm

      Nani anapingana na huu unyama 🙌🙌

      Reply
    4. Novath sombe on May 8, 2024 3:19 pm

      Mtunzii nichek 0768016908
      Nina zawadi yako

      Reply
    5. Imma MK on May 8, 2024 3:19 pm

      Nani anapingana na huu unyama 🙌🥶

      Reply
    6. OMARY on May 8, 2024 3:29 pm

      Dah admin nakuomba sana nicheki 0626 152 175 ni kuhimu ndugu nicheck

      Reply
      • Mhariri on May 8, 2024 3:40 pm

        Poapoa

        Reply
    7. Lus twaxie on May 8, 2024 3:31 pm

      Sikuizi kama stories inaishia mapema sana jmn admin …. Yahn unasoma kidogo tuu imeisha

      Reply
      • Mhariri on May 8, 2024 3:40 pm

        Mkuu unataka nimalize stori mapema? ahahah

        Reply
    8. Ediger on May 8, 2024 3:46 pm

      Asante sana kiongozi sema tuweke mzigo wa kutosha boss

      Reply
    9. Massay on May 8, 2024 4:00 pm

      Patamu hapo

      Reply
    10. Sadick on May 8, 2024 4:33 pm

      Onhooo burudan 2 hongera admin

      Reply
    11. Obado steven on May 8, 2024 5:07 pm

      Simulizi nzuri sanaa hii simulizi ilivyotokaga tu nilisomaga sehem ya 1 tyu nikaipotezea kumbe ni bonge moja la simulizi leo ndo nimeisoma kuanzia 2-12 aisee bongee moja la simulizi admin unaitaji maua yako tuma basi ata no yako tukulushie hela ya sodaa😂😂😂

      Reply
    12. Enock S on May 8, 2024 5:10 pm

      👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿

      Reply
    13. Zeyy Tabasamu✨🥰 on May 8, 2024 5:44 pm

      Alooooo Admin una kiti chako peponi🙌

      Reply
    14. Julius on May 9, 2024 8:39 am

      Ungetupa na love story

      Reply
    15. Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tatu) KOTI JEUSI – 13 - Kijiweni

    16. Mackson on June 12, 2024 11:52 pm

      Aiseee😥😥 hii story nimeipenda imegusa hisia za ndani like movie hivi harafu mm nipo ndani ya movie please writer of this story continue 🙏

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.