Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 05

    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 04

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 05
    Hadithi

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 05

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaAugust 31, 2025Updated:August 31, 20258 Comments10 Mins Read1K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 04

    “Nina amini, Mji wa Patiosa una majibu ya maswali mengi. Siri nyingi  zitafunguka” alisema akimtazama Anna ambaye alianza kuonesha Mashaka huku  akijiuliza kama Zahoro aliota jambo lingine aliloamua kulifanya Siri. Wakati  wakiwa hapo wanazungumza, Alice alikua amesimama kwa mbali akiwatazama. 

    “Kuna jambo lingine uliliota?” akauliza Anna. Zahoro akamjibu 

    “Hakuna zaidi ya nilicho kusimulia. Lakini Nina uhakika na Mji wa Patiosa,  utaenda kutegua kitendawili” Alisema Zahoro Kisha alimshika mkono Anna  wakashuka taratibu Hadi chini, Zahoro alionekana kua makini sana, aliangaza  huku na kule kabla ya kuanza kutafuta Mtumbwi. 

    SEHEMU YA TANO

    Bahati nzuri walipata Mtumbwi mmoja ukielea, waliingia humo Kisha walianza  safari ya kuelekea Mji wa Patiosa. Walikua kimya kama shimo tupu, akili zao  zilikua zikiwaza safari hiyo na mambo mengi yasiyo na Majibu.

    Anna alikua alijaribu kuisoma akili ya Zahoro lakini aliambulia patupu, Zahoro alionekana kuficha jambo huku akitazama mbele. Taratibu walipiga Kasia za  Kimya kimya wakiliacha eneo waliloishi kwa Miaka Mingi.  

    “Hatimaye tunamwacha Adui Kimya nyuma yetu” alisema Zahoro, maneno yake  yalikua mithiri ya Fumbo la Siri sana ambalo lilimfanya Anna awaze kwa kina  zaidi. Anna aligeuka nyuma, alimwona Alice akiwa amesimama juu ya jiwe  akiwatazama. Alishtuka na kuhisi huwenda Zahoro alianza kuitambua Siri yake na  Adui Kimya aliyeuwa Watu wengi wa Kijiji Cha Nzena. 

    “Una maanisha nini?” aliuliza kwa wasiwasi Anna. Zahoro alishusha pumzi na  kumuuliza Anna  

    “Ni Adui gani aliyetunyima Usingizi kwa Miaka yote kama siyo Kimya?. Basi ni  yeye, tunamwacha, Nina hakika tunaenda kukutana na Adui mwingine” alisema  huku akikata Kasia kwa mikono yake iliyojaa kwa mazoezi. 

    Anna alishusha pumzi Kisha aligeuka tena Nyuma, hakumwona Pacha wake Alice.  Waliondoka pole pole kwa kutumia Mtumbwi kuelekea Patiosa. ** 

    Patiosa, Mji wa Damu. 

    Huu ni Mji wa kale uliopotea kwa Miaka Mingi sana. Ni miongoni mwa Miji  iliyopewa laana na kutoweka kwenye uso wa Dunia. Mji huu ni tofauti na Miji  mingine iliyolaaniwa, Mji wa Patiosa haukukumbwa na vifo, waliishi huko  wakitengwa na Dunia halisi. 

    Waliunda mifumo ya kiutawala, waliishi kwa amani japo walikua Kuzimu.  Walitengeneza jeshi, walijenga Kuta ndefu za kuwakinga na Watu wengine kutoka  kwenye Miji iliyo laaniwa. Baada ya kuangushwa kwa utawala wa Mfalme Munis ambaye ni Baba wa Anna na Alice, Mji huu ulibadilisha taswira yake. 

    Ulitawaliwa kwa kumwaga Damu na Mfalme katili Selasi, aliugeuza Mji wa  Patiosa kua Mji wa Damu. Ni Mji ulioshamili Mauwaji ya kutisha sana. Mji  uligeuza Wakazi kua Watumwa, Mfalme Selasi hakutaka Mtu yeyote mwenye  nguvu aishi kwenye Ufalme wake, aliuwa Watu alioamini wangempindua na  kuchukua madaraka.

    Alilitumia jicho lake kama silaha ya kutisha ya kutawala, tofauti na Mfalme Munis aliyeitumia Pete ya ajabu kutawala.  

    Kila baada ya mwezi mmoja wanatumwa askari wa Mji wa Patiosa kufanya doria  kuuzunguka Mji mzima kwa nje, sauti za farasi zilikua zikisikika. Kisha sauti ya  kupulizwa kwa kitu mfano wa Pembe ya Myama ilisikika. Askari waliotumwa  walikua wakirejea, mara Moja lango lilifunguliwa kisha Askari waliingia ndani ya  Mji wa Patiosa kupitia lango refu sana lenye geti kubwa la Chuma. 

    Walikua wamekamata Watu watatu katika doria Yao, miongoni mwao walikua  Wanaume wawili na Mtoto mmoja. Taarifa ilipelekwa Ikulu kwa Mfalme Selasi,  akagiza Watu hao wapelekwe Ikulu. 

    Akiwa amesimama juu ya jengo la ghorofa Moja, alikua akitazama chini. Aliona  Watu waliokua wamekamatwa, Walikua ni Wanaume wawili na Mtoto, Wanaume  hao walijitambulisha kua walikua wametokea kwenye Kijiji kiitwacho Nzena,  Naam‼ walikua ni wale waliondoka na Mtoto Moana waliyemfunga kitambaa  usoni  

    Mfalme Selasi alinogewa na Hadithi hiyo, akaamua kushuka Hadi chini. Alivutiwa  zaidi na Mtoto Moana, alichuchumaa Kisha akaondoa kitambaa usoni kwa Moana, akajikuta akitabasamu Kisha akamuuliza Mtoto. 

    “Unaitwa Nani?” Moana alimtazama Mfalme Selasi Kisha akamjibu bila hofu. 

    “Moana, Mtoto wa Zahoro” Basi, Mfalme Selasi akajikuta akicheka kidogo.  Hakujua huyo Zahoro ni Nani na kwanini Mtoto alijiamini sana. 

    Mfalme Selasi, alisimama na kujipangusa mikono yake, alikua na jicho Moja.  Akawageukia Wanaume wale Wawili, sura yake haikuonesha tabasamu kama  alivyofanya kwa Moana, Kisha akawauliza 

    “Kipi kimewaleta hapa?” Wale Wanaume wakatazamana Kisha mmoja akajibu. 

    “Kutafuta mahali salama pa kuishi, Kuna kiumbe kimeuwa Watu wote katika Mji  wetu” Mfalme Selasi akaachia tabasamu Kisha akawaambia walinzi. 

    “Hakikisheni mnawaua na kuwatupa mtoni, Mtoto akiwa miongoni mwao” alisema  akiwa anaondoka eneo Hilo lakini kabla hata hajapandisha ngazi akasikia sauti  ikimwita

    “Mtukufu Mfalme” aliitambua sauti hii, ilitoka kwa mtabiri wa Ufalme wa Patiosa.  Aligeuka akamwona Bibi mmoja  

    “Unasemaje Segebuka?” akamuuliza. 

    “Machoni mwa huyu Mtoto nimeona hatari, Si Mtoto wa kawaida, ametoka  kwenye uzao wenye Kisasi na nguvu kubwa” alisema kwa heshima na adabu Kisha  aligeuka chini. Kidogo sura ya Mfalme Selasi ilibadilika 

    Hakumtazama kwa tabasamu Moana, akamuuliza Mtabiri Segebuka. “Una hakika?” 

    “Hakika Mtukufu, ujio wake hapa Patiosa ni ishara ya mwisho wa enzi zako.  Wazazi wake watakuangusha sababu wako njiani kuja hapa” alisema Mtabiri  Segebuka, alimghadhabisha sana Mfalme Selasi, Kisha Mfalme akaagiza sasa  Moana apelekwe mbele yake ndani ya chumba Cha Siri 

    Wale Wanaume wengine wakaenda kuuawa isipokua Moana pekee ambaye  alihitajika na Mfalme Selasi, Kisha Mtabiri Segebuka akaungana na Mfalme  pamoja na walinzi wa Mfalme Selasi. Tayari ujio wa Moana ulianza kubadilisha  mambo kwenye Mji wa Patiosa. 

    Waliingia ndani kabisa kwenye chumba Cha Siri Cha Mfalme Selasi, akaketi  kwenye kiti chake Kisha akamuuliza Moana. 

    “Umetumwa kuja hapa kwa lengo Fulani si Ndiyo?” Moana alikaa kimya,  Segebuka akaingilia kati na kumwambia Mfalme. 

    “Hakuna alijualo, lakini hii ni ile Damu ya Munis. Naogopa kinachokuja mbele  yetu” Mfalme alisimama kwa mshituko Mkubwa sana.  

    “Unasemaje, Munis?” aliuliza, yeye ndiye aliyerithi kiti Cha Mfalme Munis baada  ya kuuawa na Mwanasayansi Steve Mbasa. Kisha aliwafukuza Watoto wa Mfalme  na jamaa zake wengi aliwauwa kikatili, alimfunga Mama Yao Akina Anna kwenye  Gerezani la Siri kwa Miaka Mingi sana Hadi umauti ulipomfika akiwa gerezani. 

    Haraka Mfalme alimsogelea Segebuka na kumshikaa shingoni Kisha akamwambia 

    “Unakumbuka ulisema kuwatenganisha ilikua ni njia sahihi ya kumaliza Ukoo  wao, ulikua unasema uwongo si Ndiyo?” Kisha alimwacha akiwa anakohoa.

    “Hapana Mtukufu, hatma imebadilika. Sikuoni ukiwa Mfalme wa Patiosa tena, huu  Ndiyo ukweli Mfalme Wangu” alisema Segebuka Kisha alipiga goti, alikua  amemtia hasira sana Mfalme Selasi. Kisha aliagiza askari kuzunguka Kila kona  kutafuta Watu waliosalia hai na kuwaleta kwenye Ufalme. 

    Askari wa kutosha wakasambazwa Kila kona ya Mji ya Patiosa, nje na ndani ya  Mji huo. Eneo lote la mto linaloingia katika Mji wa Patiosa lilizungukwa na askari,  mitumbwi ikasambazwa kuhakikisha hakuna Mtu anayeingia Patiosa. Ulikua ni  Mpango wa Mfalme Selasi kuzui jaribio la mapinduzi ambalo Mtabiri Segebuka  alimweleza Mfalme. 

    ** 

    Jioni iliingia, ikawakuta Anna na Zahoro wakielea taratibu majini, wakielekea  Patiosa—bila kujua kwamba walikuwa wakisubiriwa ili wakamatwe na kuuawa  mbele ya Mfalme Selasi. Palikuwa kimya; hakuna aliyeongea. 

    Hisia zao ndizo zilizokuwa zikizungumza—kila mmoja alijaribu kusoma mawazo  ya mwenzake kwa macho. Midomo yao ilikuwa na mipauko kwa ukimya mrefu,  mikono yao imechoka kwa kupiga kasia. 

    Zahoro alimwangalia Anna, na kila alipomtazama, alihisi kuna jambo alilokuwa  akilificha. 

    “Nafikiria tunaweza kutafuta sehemu ya kupumzika sasa,” alisema kwa sauti ya  upole. Safari ilikuwa ndefu na mikono yao ilihitaji pumziko. Anna alitikisa kichwa  kukubaliana, kisha akajiegemeza kwenye ukingo wa mtumbwi. Macho yao  yakatazama jua likizama taratibu. 

    “Tuna bahati kumpata Moana. Sisi ni wazazi wa kujivunia. Najua ni jasiri, na  naamini hakuna baya lililomkuta,” alisema Anna, akishusha pumzi ndefu.

    “Ndiyo,” alijibu Zahoro, “Mtoto wa simba ni simba pia. Tumelea askari imara.”  Hali ya baridi ilikuwa inaanza kujitanda. 

    Mitumbwi ya askari kutoka Patiosa iliendelea kuzunguka mtoni, wakisaka  manusura. Giza lilianza kuingia polepole hadi anga likawa jeusi. 

    Anna na Zahoro waliamua kutua kando ya mto, mahali penye miti mingi.  Walikumbatiana mithili ya makinda ya ndege wakijilaza ardhini. 

    Wakiwa wamesinzia kwa uchovu, mitumbwi ya askari iliendelea kusogea.  Hatimaye mtumbwi mmoja, ukiwa na askari watano, ulifanikiwa kuona kivuli cha  mtumbwi wa Anna na Razaro ukielea pembezoni mwa ziwa. Moja ya tochi  ilimulika moja kwa moja machoni mwa Anna. 

    Akastuka. Kwa haraka, aliketi kimya na kumtikisa Zahoro. Naye alishtuka na  kuwa shahidi wa kilichoonekana. 

    “Hawa ni watu kutoka mji tunaoelekea?” Zahoro aliuliza kwa sauti ya chini. “Sina hakika. Lakini lazima tujiokoe,” Anna alijibu kwa tahadhari. 

    Akili yake ikaanza kufanya kazi ya haraka—alijua wazi kwamba huo haukuwa  mtumbwi wa kawaida. Ulikuwa ni ujio wa askari waliotumwa kwa amri ya  Mfalme Selasi. 

    Askari hao walivuka kuelekea upande walikokuwa wamejificha. Hatari ilikuwa  hatua chache tu mbele yao… 

    Anna alichuchumaa taratibu, akashika kisu kidogo alichokuwa nacho kiunoni.  Mikono yake haikutetemeka, lakini moyo wake ulikuwa ukipiga haraka kama 

    ngoma ya vita. Alimwangalia Zahoro, wakatizamana kwa muda mfupi kana  kwamba walikuwa wakikubaliana bila maneno. 

    “Tochi yao ikipita tena, tusogee upande wa pili wa mti mkubwa pale,” alisema kwa  sauti ya chini, akionyesha kwa kichwa. 

    Zahoro alikubali kwa kutikisa kichwa tu. Waliuvuta mtumbwi wao kidogo nyuma  ya mawe yaliyokuwa karibu na miombo. Miti mirefu iliwasaidia kujificha vizuri  zaidi. 

    Sauti ya maji ikichapwa kwa kasia za askari ilizidi kusikika karibu. Mmoja wao  aliinua tochi juu na kusema kwa sauti ya amri: 

    “Panuka upande huu!” 

    Walikuwa karibu sana. Hatua chache tu. 

    Anna alimpapasa Zahoro begani na kumwambia, “Kama wakitukaribia zaidi,  tupige mbizi upande wa kulia. Kuna kivuli cha majani, tutajificha huko.” 

    Zahoro akakubali tena kwa kichwa. 

    Ghafla, mmoja wa askari alisimama juu ya mtumbwi wao, akamulika upande wa  Anna na kusema kwa ukali: 

    “Naona kivuli!” 

    Anna na Zahoro hawakusubiri tena. Kwa haraka, walijirusha majini na kupiga  mbizi kwa kasi upande wa kulia kama walivyopanga. Maji yalikuwa baridi, lakini  wakayavumilia.

    Askari walipofika mahali walipokuwa wamejificha, hawakuwakuta. Moja ya tochi  ikamulika juu ya maji, lakini ilionyesha tu mawimbi madogo yaliyosababishwa na  mbizi yao. 

    “Walikuwa hapa! Haraka! Piga taa upande wa kulia!” 

    Anna na Razaro walikuwa tayari wamezamia chini ya kichaka kimoja kilichozama  majini, wakivuta pumzi kwa taabu huku wakificha miili yao na vichwa vyao ndani  ya majani makavu yaliyokuwa yakielea juu ya maji. 

    Mioyo yao ilipiga kwa nguvu, lakini hawakutikisa hata jani moja. Walijua— wakigundulika hapa, kifo kilikuwa hakiepukiki. 

    Upande mwingine wa mto, mbali kidogo, mlio wa miale ya moto ukapita hewani.  Ilikuwa ni alama ya ishara—mmoja wa askari alikuwa ametuma ujumbe kwa njia  ya moto—kuashiria kwamba wamepata alama za watu. 

    Anna na zahoro walitazamana tena. Macho yao yaliungana kwa matumaini moja  tu—kupona. 

    Lakini walijua wazi… safari ya kuelekea Patiosa haikuwa tena ya kutafuta msaada.  Ilikuwa safari ya maisha au kifo. Kutupwa kwa miale ya moto ni ishara ya Ujio wa  askari zaidi eneo Hilo, palikua Giza huku taa kadhaa zilizobebwa na askari  zikijitahidi kupambana na Hali hiyo ya Giza  

    Anna akamwambia Zahoro.

    “Hatuwezi kufia hapa Zahoro, Moana anatusubiria. Hatma ya Maisha yetu Ipo  hapa sasa hivi, ikiwa tutashindwa kujinasua hapa tutakua tumepoteza Kila kitu”  alisema Anna huku akitetemeka kwa baridi. 

    Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya sita

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx 

    riwaya riwaya mpya riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni

    8 Comments

    1. Cooper3391 on August 31, 2025 3:13 pm

      https://shorturl.fm/O0YOW

      Reply
    2. Ryder Larson on August 31, 2025 4:05 pm

      Your ability to distill complex concepts into digestible nuggets of wisdom is truly remarkable. I always come away from your blog feeling enlightened and inspired. Keep up the phenomenal work!

      Reply
    3. Marilie Kohler on August 31, 2025 10:31 pm

      I have been browsing online more than three hours today yet I never found any interesting article like yours It is pretty worth enough for me In my view if all website owners and bloggers made good content as you did the internet will be a lot more useful than ever before

      Reply
    4. J on August 31, 2025 11:24 pm

      Hadith ni nzur kinoma sema mnachelewa kutoa mwendelezi had mnatutoa kwenye leli dah…!

      Reply
    5. Ryan1052 on September 1, 2025 12:11 am

      https://shorturl.fm/4w0sW

      Reply
    6. Everett3925 on September 1, 2025 1:43 am

      https://shorturl.fm/ZILzg

      Reply
    7. Hosea Johnston on September 1, 2025 2:27 am

      Your blog is a treasure trove of valuable insights and thought-provoking commentary. Your dedication to your craft is evident in every word you write. Keep up the fantastic work!

      Reply
    8. Ruthe Davis on September 1, 2025 3:47 am

      Hi Neat post There is a problem along with your website in internet explorer would test this IE still is the market chief and a good section of other folks will pass over your magnificent writing due to this problem

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi August 31, 2025

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 05

    Ilipoishia Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 04 “Nina amini, Mji wa Patiosa una majibu ya maswali…

    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 04

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 03

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.