Mvua kubwa ilikua ikinyesha, baridi Kali lilikua limekivamia Kijiji Cha Nzena. Giza nalo tayari lilikua limeshatua, palikua Kimya. Pazia la chumbani kwa Zahoro lilifunuliwa, Mzee Miroshi alikua amesimama akimtazama Zahoro aliyekua Usingizini.
Mwanga hafifu wa kibatari ulikua ukiendelea kukifanya chumba Kiwe na Nuru kidogo, Mzee Miroshi aliingia chumbani Kisha aliketi juu ya kitandan Cha Kamba alicholala Mwanaye
Aliutazama uso wa mwanawe kwa muda mrefu, kana kwamba alikuwa akijifunza kitu kutoka katika kila mstari wa uso wake. Pumzi yake ilikuwa nzito, macho yake yakionesha huzuni iliyojificha kwa miaka mingi.
“Zahoro…” aliita kwa sauti ya chini sana, karibu kama mnong’ono, lakini kijana huyo hakuamka. Mvua iliendelea kupiga dari ya nyasi kwa nguvu, kila tone likiambatana na sauti kama ya dondosha ya mshituko.
Mzee Miroshi alinyosha mkono wake polepole, akaushika mkono wa Zahoro. Mikono ya kijana huyo ilikuwa baridi—baridi isiyo ya kawaida, kana kwamba mwili wake haukuwa na uhai.
“Samahani, mwanangu,” alizungumza tena kwa sauti ya chini, “lakini kuna jambo lazima lifanyike kabla ya alfajiri.”
Ghafla, nje ya chumba, paka mweusi alilia kwa sauti ya kutisha. Mbwa wa jirani wakaanza kubweka kwa hofu. Ndani ya chumba, mwanga wa kibatari ulianza
kuyumba-yumba, kana kwamba ulikuwa ukipigana na upepo wenye nguvu isiyo onekana.
Mzee Miroshi alisimama, akafungua mfuko mdogo wa ngozi alioubeba tangu asubuhi. Ndani yake kulikuwa na kitu kilichofunikwa kwa vitambaa vitakatifu vya miaka mingi. Alikitoa kwa hofu na kumtazama mwanawe kwa mara ya mwisho kabla ya kuanza kulia kimya kimya.
Kimya cha kijiji kilikatizwa na mlio wa radi kali—na hapo ndipo kila kitu kilianza kubadilika…
Radi ilipopiga, mwanga wake uliangaza kwa sekunde chache chumba cha Zahoro, na kwa mara ya kwanza, Mzee Miroshi aliona kivuli kikisimama pembeni ya mlango wa chumba hicho. Moyo wake uliruka. Hakuweza kusogea. Kivuli hicho hakikusogea pia, kilionekana tu kama kimya kilicho hai—kikitazama.
Alifumba macho, akavuta pumzi ndefu, kisha akakifunika tena kile kitu alichokitoa kwenye mfuko wake wa ngozi. Alijua hakikuwa wakati wa kukikabidhi bado, japo ndicho kitu pekee kinachoweza kumlinda Zahoro na kuvunja kile alichoamini kuwa ni laana ya Bi. Lugumi.
“Usiingilie muda,” sauti ya kike ilisikika ikinong’ona karibu na sikio lake. Aligeuka kwa haraka, lakini hakuona mtu. Jasho lilianza kumtoka. Alijua alikuwa amechelewa. Alijua macho ya kale yanamtazama, yakihoji, yakimlaumu.
Zahoro alianza kuhema kwa nguvu, uso wake ukionekana kuteseka na ndoto nzito. Alipiga kelele moja, kisha akanyamaza tena ghafla—kimya kama kifo. Mzee Miroshi alinyanyuka haraka na kumtikisa, “Zahoro! Mwanangu, amka! Usimruhusu akuone!”
Lakini Razaro hakuamka. Badala yake, midomo yake ilianza kunong’ona maneno yasiyoeleweka—lugha ya kale, isiyo ya kawaida. Mwanga wa kibatari ukazima ghafla. Giza likatawala.
Ndani ya giza hilo, sauti ya mtoto ikasikika kutoka kona ya chumba. “Mbona mmechelewa tena…?”
Sauti hiyo ilimfanya Mzee Miroshi asimame barabara, uso wake ukiwa mweupe kama karatasi. Alijua sauti hiyo. Ilikuwa ya Masumbuko—mtoto wa kwanza wa kijiji aliyechukuliwa miaka mingi iliyopita, usiku kama huo.
Papo hapo, Zahoro alishtuka kutoka Usingizini na kugundua ilikua ni ndoto mbaya iliyomshtua. Jasho lilikua likimtoka, ndevu nyingi zilikua zimemwota. Umri wake haukua ule wa awali, Miaka Thelathini ilikua imepita tayari
Alikua ndani ya pango, Miaka yote hakufanikiwa kutoka ndani ya Kijiji Cha Nzena, Kijiji kilicholaaniwa. Aliishikilia Sehemu ya kifua ambayo moyo hukaa hapo, alihisi mapigo yasiyo ya kawaida. Aliitazama Kando yake, palikua na Mwanamke aliyelala pamoja na Mtoto wa Miaka mitano.
Taratibu Zahoro alinyanyuka. Alishafikisha Miaka 52, alikua Mwanaume aliyekamilika lakini aliyechoka Maisha ya kutisha. Alisogea taratibu Hadi nje ya Pango, akasimama juu ya Mlima na kulitazama jua likiwa linazama.
Macho yake yalikua mazito sana, yalijaa uzito usio wa kawaida. Alijilazimisha kulitazama jua Kisha akauliza
“Kanakwamba unanitazama na huwezi kunisaidia?” jua liliendelea na safari yake kama vile halikusikia swali lililoulizwa, Zahoro alikohoa kidogo kabla ya kuisikia sauti nyuma yake
“Hujachoka?” ilikua ni sauti ya Kike, nyuma yake alisimama Mwanamke aliyemtazama Zahoro kwa jicho kavu. Zahoro alipogeuka akasema
“Anna, aliyechoka ni yule aliyepata. Nafikiria kuhusu Binti yetu Moana, bahati mbaya kwake hajawahi kumwona Binadamu tofauti na Mimi na wewe” alisema kwa huzuni sana Zahoro.
“Mh! Nani angefika Kuzimu Baba Moana, tumesubiria sababu ya kurudi Duniani kwa Miaka yote Hadi tumepata Mtoto huku. Wote wamekufa, ni sisi pekee Ndiyo tunaishi huku” alisema Kisha akamsogelea karibu Zahoro.
“Tuna Kila sababu ya kufanya safari kutoka hapa. Tukatafute Sehemu nyingine ya Kuzimu, pengine Kuna Mji mwingine uliopotea kama Kijiji Cha Nzena” alisema Zahoro.
“Sawa, lakini sasa Adui yetu ni Kimya. Ni ngumu sana kupambana na Adui anayewinda Sauti Zahoro, lakini kuendelea kuishi pangoni hakutasaidia, ni Bora tufanye safari kama ulivyosema”Alisema Anna. Taratibu aliondoka na kurejea pangoni.
Razaro hakuacha kulisindikiza jua likizama mbele ya macho yake, Kisha Nuru ya Giza iliingia, alitembea Kurudi ndani ya Pango.
***
Siku iliyofuata, Zahoro, Mtoto Moana pamoja na Anna. Walikua tayari kwa ajili ya kuondoka ndani ya Pango ili kutafuta Makazi mengine. Ilikua ni huzuni kuondoka ndani ya Pango Hilo salama ambalo waliishi kwa Miaka Thelathini.
“Baba, tunaenda wapi?” aliuliza Moana, alikua amevalia nguo chakavu. Zahoro alichuchumaa na kumwambia Moana kwa sauti ya utaratibu sana.
“Tunaenda kuishi Sehemu nyingine salama zaidi. Usijali” Moana aliachia tabasamu, sura yake ya mviringo na macho ya kudumbukia ndani vilimfanya aonekane ni Mtoto mzuri sana, bila kujalisha wanaishi Maisha gani alikubaliana na Hali halisi licha ya kuisikia TU Hadithi ya Dunia ilivyo.
Walibeba chakula kidogo walichobakiwa nacho, mizizi na baadhi ya mabaki ya nyama. Kisha Zahoro akamfunga kitambaa usoni Moana, halafu wao wakajiweka sawa kwa kulegeza vitambaa kichwani.
Adui Yao Mpya alikua ni KIMYA. Yeye ni Adui waliyemwogopa sana kuliko sauti ya Bibi Lugumi. Waligeuka kulitazama Pango kwa huzuni sana, waliishi hapo kwa usalama kwa Miaka Mingi.
Taratibu Anna alimtazama Zahoro, ulikua ni wakati wao wa kuondoka. Walianza safari taratibu, kwa utulivu wa Hali ya Juu sana. Walishuka kutoka Kilimani Kisha waliupa mgongo.
Taratibu wakaingia Msituni huku lengo lao likiwa ni kuelekea Mtoni, wasafiri kupitia Maji ya Mto huo.
Msitu ulikua kimya na wenye kutisha sana, palikua na kinvuli Kila walipopita kutokana na Kua na miti mingi mikubwa. Majani mengi yaliyooza yalikua aridhini, hapakua na njia rasmi isipokua vichochoro.
Anna alikua amembeba Moana Mgongoni, Zahoro alikua ameshikilia kifurushi Cha chakula. Mioyoni Yao ilizungumza zaidi, huku lugha pekee waliyokua wakiitumia ilikua ni ishara.
Zahoro alikua ndiye kiongozi wa msafara, alihakikisha anafanya awezalo waufikie Upande wa Pili wa Mto. Wakiamini pengine wangeliweza kupata msaada huko, anga lilikua la kahawia, huku jua Kali likiendelea kuwaka.
Hapakua na sauti yoyote iliyosikika, hapakua na Ndege wala wadudu waliopiga kelele. Ghafla Zahoro alisimama, akatoa ishara kwa Anna kusimama pia
Sauti ya ajabu ilianza kusikika kama kuna kitu kikubwa kinakaribia kutokea juu. Zahoro, aliyekuwa ni mtu wa tahadhari, hakutaka kugeuka haraka. Badala yake, alivuta hisia zake kwa umakini zaidi. Taratibu, aligeuka na kutazama juu— palikuwa na nyoka mkubwa mweusi aliyekuwa akishuka kwa taratibu, kwa mtindo wa kuvizia.
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
1 Comment
Somebody essentially lend a hand to make significantly articles Id state That is the very first time I frequented your website page and up to now I surprised with the research you made to make this actual submit amazing Wonderful task