Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Jasusi Sehemu Ya Tano (05)
    Hadithi

    Jasusi Sehemu Ya Tano (05)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaDecember 2, 2024Updated:December 3, 20249 Comments8 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishiaย  “Fuata maelekezo yangu, kuwa makini hao Watu wana akili yaย  ziada sana wakati mwingine Watu hawaamini kama Huyo Mzungu niย  Binadamu, wana akili iliyozidi…unaweza kuwa umetegwa, kablaย  ya kutoka Msibani hakuna ishara tata?” Alimpa wakati waย  kufikria, Zola akasemaย 

    “Nilikuwa makini kuliko kawaida, hakuna aliyeniona ila wakatiย  natoka…” Ukimya ukatawala, Mzee Dawson akamuuliza Zolaย 

    “Enhee ilikuwaje?” Zola akafikiria alipokuwa akitoka paleย  aliparamiana na Mwanamke mmoja mzuri sana, hakutaka kulisemaย  hilo akiamini sio ishara ya kumueleza Mzee Dawsonย 

    “Sio ishara!”ย  Endeleaย ย 

    “Sawa endelea kuwa makini na gari hilo” Gari hiyo ndogoย  nyeusi iligota katika moja ya hoteli maarufu sana Mjini hapoย  iliyoitwa Sarafina Hotel, Muda huu jamaa mwenye upara alikuwaย  akishuka bila kuonesha wasiwasi wowote huku Zola akiwaย  anatafuta sehemu rahisi ya kupaki Gari yake, Jamaa wa uparaย  akaingia kwenye lifti wakati Zola akiwa amejibanza mahaliย  anamchungulia, haraka akapandisha ngazi kuelekea juu kwaย  spidi ambayo kila mmoja alishangaa kwa Mzee kama Zolaย  kupandisha zile ngazi kwa spidi kubwa kama umeme, Naamย  ilikuwa ni kawaida kwake kutokana na mafunzo aliyoyapataย  zamani nchini Mexico na Cuba.ย 

    Alipofika Floo ya pili alipokelewa na ukimya, akili yakeย  ikamwambia kuwa Jamaa wa upara atakuwa Floo ya juu yake yaaniย  ya tatu, basi Zola kwa spidi ile ile alizidi kupandisha ngaziย  na kuendelea kustaajabisha Watu aliopishana nao, mwisho waย  Floo ya pili alimuona jamaa wa Upara akikata kona upande waย  kushoto, Zola hakutaka kupoteza muda alizidi kumfuatilia iliย  ajuwe Jamaa yule alikuwa akienda wapi, huku akili yakeย  ikimwambia kuwa ni miongoni mwa wale waliousuka ule mpango waย  vifo vya Robert na Bosco na hatimae kumtumia Anastanzia kamaย  mchezo wa kuigiza ili kuficha jambo ambalo kwa asilimia kubwaย  lilifanikiwa. Alipokata kushoto alianza kuhisi hali yaย  tofauti, achilia mbali ukimya bali kulikuwa na milango miwiliย  ambayo ilikuwa wazi tena ikiwa inacheza kuashilia kuwaย  ilikuwa imeguswa sekunde chache zilizopita.ย 

    Zola akakunja mkono wake wa kushoto ambao alipendelea kuuitaย  Mkono Wa Mungu, kisha akachomoka na Bastola yake yenyeย  kiwambo maalum cha kuzuia mlio wa risasi kutoka, tayariย  alikuwa na hisia kuwa alikuwa ameingizwa mtegoni, akachomoaย  Ear phone masikioni baada ya kuhisi mawasiliano kati yake naย  Mzee Dawson yalikuwa yanasuasua na hakutaka kuzungumza kwaย  sauti kubwa, Kitendo cha Zola kuchomoa zile Ear Phoneย  masikioni kilimpa ishara Mzee Dawson, akahisi pengine Zolaย  yupo kwenye mtego wa kifo, haraka akachukua gari kuitafutaย  Sarafina Hoteli ilipo, Naam! Zola alikuwa akinyata kama pakaย  aliyekuwa akimvizia panya ili aweze kumla, alipiganisha akiliย  yake huku macho akiwa anayaelekeza kwenye ile milango miwiliย  iliyo waziย 

    Akauchagua mlango mmoja akaingia taratibu kisha akafungaย  mlango bila kuruhusu sauti ya kufungwa kwa mlango huoย  kusikika, mbele aliona kuna korido iliyo kimya sana, akawaย  anaifuata. Alikuwa amejikunja kama duma vile huku akijuwaย  kuwa kosa lolote atakalo lifanya linaweza kuondoa uhai wake,ย  akaupita mlango wa kwanza na wa pili, akili ikamwambiaย  aufungue mlango wa tatu, alikuwa ni mwenye hisia kali kamaย  Mbwa wa polisi vile, alihema taratibu sana, alifundishwa kuwaย kuhema kwa nguvu kunaweza kusababisha shabaha kwenda tofautiย  jambo ambalo hakutaka litokee pale, akiwa ameshikilia kitasaย  hicho huku akivuta taratibu Zola alikutana na teke kaliย  lililomnyumbisha na kusababisha bastola yake kuanguka chini,ย  akiwa anataka kuiokota Bastola hiyo ilipigwa teke naย  kuburuzika mita kadhaa, Ndipo Zola akajuwa sasa yupo katikaย  hatari mno, kwa umakini akageuka taratibu kumtazamaย  aliyempiga teke.ย 

    Alikutana na sura ya Malaika, ambaye yeye alimtambua kamaย  Judith tena alikuwa katika sura bandia ambayo Zola alikuwaย  akiijuwa. Mzee Zola akayakumbuka maneno ya polisi aliyempigiaย  simu na kumtaarifu juu ya mauwaji ya polisi katika kituo chaย  polisi, akautumia muda huo kuyatazama maungio ya Msichanaย  huyo mwembamba lakini hatari sana akagundua ana ujuzi mkubwaย  wa kareti.ย 

    Zola hakutaka kupoteza muda wake japo alijuwa Msichana huyoย  ni hatari sana kwake, akakunja mguu na kutupa teke lililofikaย  hadi kwenye mbavu za msichana huyo ambaye aliudaka mguu waย  zola kisha akaukunja na kumsababishia Zola maumivu mkali,ย  akapigwa kwenye ngoko ndipo Zola alipotoa sauti ya maumivu,ย  akauvuta mguu haraka ili usivunjwe, akawa na maswali mengiย  kichwani aliyotaka kumuuliza Msichana huyo lakini aligunduaย  kuwa hana muda wa kupoteza hapo.ย 

    Akaweka mikono yake vizuri ili aweze kutupa shambulio,ย  Malaika akajirusha na kutua kwenye mikono ya Mzee Zola ambayoย  ilikuwa imekazwa, kisha akavingirika na kumpa teke la usoย  Mzee Zola akaangukia pembeni, akamfuata na kuanza kumpigaย  sehemu ya tumbo huku akimwambiaย 

    “Wewe ni mahiri sana kwa upelelezi lakini mwisho wa kuifanyaย  kazi hiyo ni leo, nakuuwa Hapa ili kupeleka ujumbe kwaย  aliyekutuma” Zola alikuwa akigugumia kwa maumivu, harakaย  akauvuta mguu wa Malaika na kumuangusha akapata muda waย  kujipanga upya,,, safari hii Zola hakuwa na bahati kabisa,ย  Malaika aliutumia ujuzi wake wa mapigano na kumpiga kisawaย  sawa Zola hadi akatema Damu, akamuinua na kumkaba shingoniย  huku akiwa amemgandamiza ukutani, Zola akaitumia nguvu chacheย  iliyobakia akampiga teke sehemu nyeti ikawa auheni kwake,ย  Malaika akaanguka chini haraka akajiokota, ni kama vileย  alikuwa amemchokoza basi Zola alikutana na Ngumi za usoย  mfululizo hadi akachanganikiwaย 

    Akajikuta muda mchache ameanguka chini na kushindwa kuinuka,ย  Malaika alipoona Zola hawezi tena kurudisha majibu yaย  mpambano huo uliopigwa kisiri ndani ya Hoteli hiyo, akavuaย  sura ya Bandia ndipo Zola akapata kuiona sura halisi yaย  Mwanamke huyo.

    “Naitwa Malaika! Najua huna uwezo wa kufanya chochote hapoย  Zola sababu zimebakia sekunde chache nikupoteze, kamaย  ulifikiria kuwa mtaweza kupambana na Mafia Gang basi huu uweย  ujumbe kwa wajinga wenzako, Mtakufa wote endapo mtaendeleaย  kutufuatilia” Malaika akachomoa kisu chake kutoka katikaย  mfuko wa koti alilovaa, akamsogelea Mzee Zola akamwambiaย 

    “Kwakuwa umefanikiwa kunijuwa basi huna haki ya kuendeleaย  kuishi” Malaika akanyanyua kisu ili amchome Zola sehemu yaย  moyo, Ghafla alisikia mlango ukifunguliwa huku risasiย  zikimiminwa mfululizo, akajirusha na kuanza kukimbia kwaย  kuzikwepa hadi akazama kwenye korido, alikuwa ni Mzee Dawsonย  ndiye aliyemsaidia Zola pale vinginevyo Zola angeuawa pale.ย 

    “Pole Zola” alisema huku akiwa amempa mkono Zola awezeย  kusimama, akamsaidia akasimama kisha Dawson akaiendea Bastolaย  ya Zola ambayo ilikuwa sakafuni akampatiaย 

    “Mshenzi yule alikuwa anaondoa uhai wangu na kama sio weweย  basi mgekuja kuchukua maiti yangu hapa”ย 

    “Bado siamini kama msichana yule amekukalisha chini Zola!”ย 

    “Dawson! Niliposikia hadithi ya yule Msichana ya kuuwa polisiย  zaidi ya 15 katika kituo cha polisi nilifikiria ni utaniย  lakini leo nimeamini kwanini aliwashinda polisi, ana ujuzi waย  Kareti kitu ambacho ni hatari zaidi kwetu”ย 

    “Oooh!! Mungu wangu, hatuna muda wa kupoteza hapa, tuondoke”ย  Alisema Mzee Dawson, mara moja wakashuka hadi chini kilaย  mmoja akaingia kwenye gari yake na kuelekea alipopafahamu.ย 

    Zola alikuwa na hasira sana akiwa ndani ya gari, kupigwa naย  Malaika kulimuumiza sana lakini alifanikiwa kuijua suraย  halisi na jina la huyo Mwanamke ambalo ni Malaika, akili yakeย  ikamtuma aelekee kituo cha polisi, Mkono mmoja ulikuwa naย  maumivu makali sana lakini alijikaza, alichotaka kujuwa niย  mafaili gani yule Malaika aliyaiba ndani ya kituo cha polisi,ย  akaambiwa kuwa mafaili hayo yalikuwa ya kesi mojaย  iliyoshikiliwa na kitengo cha Ikulu.ย 

    Kesi hiyo ilimuhusu jamaa mmoja aliyeitwa Jamaal, ambayeย  alikamatwa siku moja baada ya tukio la kuuawa kwa Makam waย  Rais kutokea, Historia ya jamaa huyo ilimuelezea kuwa ni Mtuย  aliyepitia mafunzo maalum ya kijeshi ya ulengaji wa shabahaย  ya masafa marefu na upiganaji, alikamatwa katika uwanja waย  ndege baada ya msako mkali uliokuwa ukiendelea.

    Baada ya kumnasa walikuta Bunduki na risasi ambayo ilitumikaย  kumuuwa makam wa Rais, moja kwa moja alishtakiwa kwa kosaย  hilo na kufungwa kwa siri katika gereza moja la siri sana,ย  Jamaal alikutwa na vitambulisho vilivyomuonesha kuwa anaย  Uraia wa Nchi nane ikiwemo Marekani na Ukraine jambo ambaloย  liliwashangaza sana lakini Jamaal alizungumza lugha nyingiย  vizuri sana japo alikuwa na asili ya Somalia. Pia taarifaย  ilienda mbali zaidi na kusema kuwa Jamaal alikutwa naย  vitambulisho vya kijeshi vilivyoonesha kuwa aliwahiย  kulitumikia jeshi la Israel na Palestina ndani ya miakaย  miwili,ย 

    Zola alikaa chini na kujishika kichwa chake kisha akaulizaย 

    “Kwasasa Jamaal anashikiliwa gereza gani?” Swali hiliย  lilimfanya polisi aliyekuwa akimueleza Zola akae kimya kidogoย  kisha akasemaย 

    “Gereza lipo Ikulu ya Nchi, sisi hatuhusiki tena na kesi hiyoย  Zola” Zola akauliza tenaย 

    “Kwanini mafaili ya kesi bado yalikuwa hapa?”ย 

    “Kwasababu kesi ilianzia hapa lakini cha kushangaza baada yaย  kukamatwa tuliondolewa katika kesi hiyo”ย 

    “Nani alitoa oda ya Nyie kuacha hii kesi na ikaenda sehemuย  nyingine wakati nyie ndio mnakazi hiyo?”ย 

    “Aliyetoa oda ni Rais wa Nchi” Zola aliondoka baada ya kupataย  majibu yaliyochanganya akili yake kisha akawasiliana na Mzeeย  Dawson wakapanga kukutana katika makazi ya siri ya Zola,ย  Usiku Dawson alienda kuonana na Zola, kama kawaida yaoย  waligida pombe ili maongezi yaanzeย 

    “Enhee umegundua nini Zola?” Aliuliza Dawsonย 

    “Mafaili yaliyobiwa katika kituo cha polisi yalikuwa ya kesiย  ya Mtu anayedaiwa kuwa alihusika kumuuwa Makam wa Rais”ย  Alisema Zolaย 

    “Unasemaje? Ina maana polisi wanajuwa ni nani alihusika?”ย 

    “Sio polisi pekee hata Mkuu wako wa Nchi ambaye anakupa kaziย  ya kulisaka kundi la Mafia Gang anajuwa na kibaya zaidiย  ametoa amri ya jeshi la polisi kuiacha kazi hiyo” Mzee Dawsonย  alionekana kushangaa sanaย 

    “Inawezekanaje Zola?”

    “Hiyo ndio hali halisi ndio maana nimekuita hapa iliย  tuzungumze, nahisia mbaya juu ya Mkuu wa Nchi lakini sitakiย  kujiaminisha chochote”ย 

    “Unataka kusema Mkuu wa Nchi kuna kitu anakificha hapa?” Woteย  waliacha kunywa pombe wakazama katika maongezi yaoย 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SITAย  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย 

    ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx

    jasusi riwaya za kijasusi

    9 Comments

    1. Fadhili on December 2, 2024 5:03 pm

      Lit

      Reply
    2. Charz jr๐Ÿ˜Ž on December 2, 2024 5:19 pm

      โœŒ๏ธโœŒ๏ธ

      Reply
      • G shirima on December 2, 2024 8:47 pm

        Naona inaelekea ukingoni

        Reply
      • Gabriel Luis Fabian on December 3, 2024 3:11 pm

        Nimekipenda kitabu hiki,
        Nikama macho yanafumbuka ๐Ÿค”๐Ÿค”๐Ÿค”

        Reply
    3. Cathbert on December 2, 2024 5:52 pm

      Iko poa sanaaa

      Reply
    4. Mussa on December 2, 2024 10:53 pm

      Fantastic

      Reply
    5. Gabriel Luis Fabian on December 3, 2024 3:12 pm

      Nimekipenda kitabu hiki,
      Nikama macho yanafumbuka ๐Ÿค”๐Ÿค”๐Ÿค”

      Reply
    6. Darius Amdun karyabwezile on December 3, 2024 5:17 pm

      Nimeipenda mno kiongoz ongera na asante ongeza bidii

      Reply
    7. Fawziya Hassan on December 6, 2024 12:09 pm

      MAMBO NI ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 15, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya tatu Mke alipoisoma ile karatasi aligeuza macho kumtazama Mume…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.