Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Jasusi Sehemu Ya Tano (05)
    Hadithi

    Jasusi Sehemu Ya Tano (05)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaDecember 2, 2024Updated:December 3, 20249 Comments8 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    IlipoishiaΒ  “Fuata maelekezo yangu, kuwa makini hao Watu wana akili yaΒ  ziada sana wakati mwingine Watu hawaamini kama Huyo Mzungu niΒ  Binadamu, wana akili iliyozidi…unaweza kuwa umetegwa, kablaΒ  ya kutoka Msibani hakuna ishara tata?” Alimpa wakati waΒ  kufikria, Zola akasemaΒ 

    “Nilikuwa makini kuliko kawaida, hakuna aliyeniona ila wakatiΒ  natoka…” Ukimya ukatawala, Mzee Dawson akamuuliza ZolaΒ 

    “Enhee ilikuwaje?” Zola akafikiria alipokuwa akitoka paleΒ  aliparamiana na Mwanamke mmoja mzuri sana, hakutaka kulisemaΒ  hilo akiamini sio ishara ya kumueleza Mzee DawsonΒ 

    “Sio ishara!”Β  EndeleaΒ Β 

    “Sawa endelea kuwa makini na gari hilo” Gari hiyo ndogoΒ  nyeusi iligota katika moja ya hoteli maarufu sana Mjini hapoΒ  iliyoitwa Sarafina Hotel, Muda huu jamaa mwenye upara alikuwaΒ  akishuka bila kuonesha wasiwasi wowote huku Zola akiwaΒ  anatafuta sehemu rahisi ya kupaki Gari yake, Jamaa wa uparaΒ  akaingia kwenye lifti wakati Zola akiwa amejibanza mahaliΒ  anamchungulia, haraka akapandisha ngazi kuelekea juu kwaΒ  spidi ambayo kila mmoja alishangaa kwa Mzee kama ZolaΒ  kupandisha zile ngazi kwa spidi kubwa kama umeme, NaamΒ  ilikuwa ni kawaida kwake kutokana na mafunzo aliyoyapataΒ  zamani nchini Mexico na Cuba.Β 

    Alipofika Floo ya pili alipokelewa na ukimya, akili yakeΒ  ikamwambia kuwa Jamaa wa upara atakuwa Floo ya juu yake yaaniΒ  ya tatu, basi Zola kwa spidi ile ile alizidi kupandisha ngaziΒ  na kuendelea kustaajabisha Watu aliopishana nao, mwisho waΒ  Floo ya pili alimuona jamaa wa Upara akikata kona upande waΒ  kushoto, Zola hakutaka kupoteza muda alizidi kumfuatilia iliΒ  ajuwe Jamaa yule alikuwa akienda wapi, huku akili yakeΒ  ikimwambia kuwa ni miongoni mwa wale waliousuka ule mpango waΒ  vifo vya Robert na Bosco na hatimae kumtumia Anastanzia kamaΒ  mchezo wa kuigiza ili kuficha jambo ambalo kwa asilimia kubwaΒ  lilifanikiwa. Alipokata kushoto alianza kuhisi hali yaΒ  tofauti, achilia mbali ukimya bali kulikuwa na milango miwiliΒ  ambayo ilikuwa wazi tena ikiwa inacheza kuashilia kuwaΒ  ilikuwa imeguswa sekunde chache zilizopita.Β 

    Zola akakunja mkono wake wa kushoto ambao alipendelea kuuitaΒ  Mkono Wa Mungu, kisha akachomoka na Bastola yake yenyeΒ  kiwambo maalum cha kuzuia mlio wa risasi kutoka, tayariΒ  alikuwa na hisia kuwa alikuwa ameingizwa mtegoni, akachomoaΒ  Ear phone masikioni baada ya kuhisi mawasiliano kati yake naΒ  Mzee Dawson yalikuwa yanasuasua na hakutaka kuzungumza kwaΒ  sauti kubwa, Kitendo cha Zola kuchomoa zile Ear PhoneΒ  masikioni kilimpa ishara Mzee Dawson, akahisi pengine ZolaΒ  yupo kwenye mtego wa kifo, haraka akachukua gari kuitafutaΒ  Sarafina Hoteli ilipo, Naam! Zola alikuwa akinyata kama pakaΒ  aliyekuwa akimvizia panya ili aweze kumla, alipiganisha akiliΒ  yake huku macho akiwa anayaelekeza kwenye ile milango miwiliΒ  iliyo waziΒ 

    Akauchagua mlango mmoja akaingia taratibu kisha akafungaΒ  mlango bila kuruhusu sauti ya kufungwa kwa mlango huoΒ  kusikika, mbele aliona kuna korido iliyo kimya sana, akawaΒ  anaifuata. Alikuwa amejikunja kama duma vile huku akijuwaΒ  kuwa kosa lolote atakalo lifanya linaweza kuondoa uhai wake,Β  akaupita mlango wa kwanza na wa pili, akili ikamwambiaΒ  aufungue mlango wa tatu, alikuwa ni mwenye hisia kali kamaΒ  Mbwa wa polisi vile, alihema taratibu sana, alifundishwa kuwaΒ kuhema kwa nguvu kunaweza kusababisha shabaha kwenda tofautiΒ  jambo ambalo hakutaka litokee pale, akiwa ameshikilia kitasaΒ  hicho huku akivuta taratibu Zola alikutana na teke kaliΒ  lililomnyumbisha na kusababisha bastola yake kuanguka chini,Β  akiwa anataka kuiokota Bastola hiyo ilipigwa teke naΒ  kuburuzika mita kadhaa, Ndipo Zola akajuwa sasa yupo katikaΒ  hatari mno, kwa umakini akageuka taratibu kumtazamaΒ  aliyempiga teke.Β 

    Alikutana na sura ya Malaika, ambaye yeye alimtambua kamaΒ  Judith tena alikuwa katika sura bandia ambayo Zola alikuwaΒ  akiijuwa. Mzee Zola akayakumbuka maneno ya polisi aliyempigiaΒ  simu na kumtaarifu juu ya mauwaji ya polisi katika kituo chaΒ  polisi, akautumia muda huo kuyatazama maungio ya MsichanaΒ  huyo mwembamba lakini hatari sana akagundua ana ujuzi mkubwaΒ  wa kareti.Β 

    Zola hakutaka kupoteza muda wake japo alijuwa Msichana huyoΒ  ni hatari sana kwake, akakunja mguu na kutupa teke lililofikaΒ  hadi kwenye mbavu za msichana huyo ambaye aliudaka mguu waΒ  zola kisha akaukunja na kumsababishia Zola maumivu mkali,Β  akapigwa kwenye ngoko ndipo Zola alipotoa sauti ya maumivu,Β  akauvuta mguu haraka ili usivunjwe, akawa na maswali mengiΒ  kichwani aliyotaka kumuuliza Msichana huyo lakini aligunduaΒ  kuwa hana muda wa kupoteza hapo.Β 

    Akaweka mikono yake vizuri ili aweze kutupa shambulio,Β  Malaika akajirusha na kutua kwenye mikono ya Mzee Zola ambayoΒ  ilikuwa imekazwa, kisha akavingirika na kumpa teke la usoΒ  Mzee Zola akaangukia pembeni, akamfuata na kuanza kumpigaΒ  sehemu ya tumbo huku akimwambiaΒ 

    “Wewe ni mahiri sana kwa upelelezi lakini mwisho wa kuifanyaΒ  kazi hiyo ni leo, nakuuwa Hapa ili kupeleka ujumbe kwaΒ  aliyekutuma” Zola alikuwa akigugumia kwa maumivu, harakaΒ  akauvuta mguu wa Malaika na kumuangusha akapata muda waΒ  kujipanga upya,,, safari hii Zola hakuwa na bahati kabisa,Β  Malaika aliutumia ujuzi wake wa mapigano na kumpiga kisawaΒ  sawa Zola hadi akatema Damu, akamuinua na kumkaba shingoniΒ  huku akiwa amemgandamiza ukutani, Zola akaitumia nguvu chacheΒ  iliyobakia akampiga teke sehemu nyeti ikawa auheni kwake,Β  Malaika akaanguka chini haraka akajiokota, ni kama vileΒ  alikuwa amemchokoza basi Zola alikutana na Ngumi za usoΒ  mfululizo hadi akachanganikiwaΒ 

    Akajikuta muda mchache ameanguka chini na kushindwa kuinuka,Β  Malaika alipoona Zola hawezi tena kurudisha majibu yaΒ  mpambano huo uliopigwa kisiri ndani ya Hoteli hiyo, akavuaΒ  sura ya Bandia ndipo Zola akapata kuiona sura halisi yaΒ  Mwanamke huyo.

    “Naitwa Malaika! Najua huna uwezo wa kufanya chochote hapoΒ  Zola sababu zimebakia sekunde chache nikupoteze, kamaΒ  ulifikiria kuwa mtaweza kupambana na Mafia Gang basi huu uweΒ  ujumbe kwa wajinga wenzako, Mtakufa wote endapo mtaendeleaΒ  kutufuatilia” Malaika akachomoa kisu chake kutoka katikaΒ  mfuko wa koti alilovaa, akamsogelea Mzee Zola akamwambiaΒ 

    “Kwakuwa umefanikiwa kunijuwa basi huna haki ya kuendeleaΒ  kuishi” Malaika akanyanyua kisu ili amchome Zola sehemu yaΒ  moyo, Ghafla alisikia mlango ukifunguliwa huku risasiΒ  zikimiminwa mfululizo, akajirusha na kuanza kukimbia kwaΒ  kuzikwepa hadi akazama kwenye korido, alikuwa ni Mzee DawsonΒ  ndiye aliyemsaidia Zola pale vinginevyo Zola angeuawa pale.Β 

    “Pole Zola” alisema huku akiwa amempa mkono Zola awezeΒ  kusimama, akamsaidia akasimama kisha Dawson akaiendea BastolaΒ  ya Zola ambayo ilikuwa sakafuni akampatiaΒ 

    “Mshenzi yule alikuwa anaondoa uhai wangu na kama sio weweΒ  basi mgekuja kuchukua maiti yangu hapa”Β 

    “Bado siamini kama msichana yule amekukalisha chini Zola!”Β 

    “Dawson! Niliposikia hadithi ya yule Msichana ya kuuwa polisiΒ  zaidi ya 15 katika kituo cha polisi nilifikiria ni utaniΒ  lakini leo nimeamini kwanini aliwashinda polisi, ana ujuzi waΒ  Kareti kitu ambacho ni hatari zaidi kwetu”Β 

    “Oooh!! Mungu wangu, hatuna muda wa kupoteza hapa, tuondoke”Β  Alisema Mzee Dawson, mara moja wakashuka hadi chini kilaΒ  mmoja akaingia kwenye gari yake na kuelekea alipopafahamu.Β 

    Zola alikuwa na hasira sana akiwa ndani ya gari, kupigwa naΒ  Malaika kulimuumiza sana lakini alifanikiwa kuijua suraΒ  halisi na jina la huyo Mwanamke ambalo ni Malaika, akili yakeΒ  ikamtuma aelekee kituo cha polisi, Mkono mmoja ulikuwa naΒ  maumivu makali sana lakini alijikaza, alichotaka kujuwa niΒ  mafaili gani yule Malaika aliyaiba ndani ya kituo cha polisi,Β  akaambiwa kuwa mafaili hayo yalikuwa ya kesi mojaΒ  iliyoshikiliwa na kitengo cha Ikulu.Β 

    Kesi hiyo ilimuhusu jamaa mmoja aliyeitwa Jamaal, ambayeΒ  alikamatwa siku moja baada ya tukio la kuuawa kwa Makam waΒ  Rais kutokea, Historia ya jamaa huyo ilimuelezea kuwa ni MtuΒ  aliyepitia mafunzo maalum ya kijeshi ya ulengaji wa shabahaΒ  ya masafa marefu na upiganaji, alikamatwa katika uwanja waΒ  ndege baada ya msako mkali uliokuwa ukiendelea.

    Baada ya kumnasa walikuta Bunduki na risasi ambayo ilitumikaΒ  kumuuwa makam wa Rais, moja kwa moja alishtakiwa kwa kosaΒ  hilo na kufungwa kwa siri katika gereza moja la siri sana,Β  Jamaal alikutwa na vitambulisho vilivyomuonesha kuwa anaΒ  Uraia wa Nchi nane ikiwemo Marekani na Ukraine jambo ambaloΒ  liliwashangaza sana lakini Jamaal alizungumza lugha nyingiΒ  vizuri sana japo alikuwa na asili ya Somalia. Pia taarifaΒ  ilienda mbali zaidi na kusema kuwa Jamaal alikutwa naΒ  vitambulisho vya kijeshi vilivyoonesha kuwa aliwahiΒ  kulitumikia jeshi la Israel na Palestina ndani ya miakaΒ  miwili,Β 

    Zola alikaa chini na kujishika kichwa chake kisha akaulizaΒ 

    “Kwasasa Jamaal anashikiliwa gereza gani?” Swali hiliΒ  lilimfanya polisi aliyekuwa akimueleza Zola akae kimya kidogoΒ  kisha akasemaΒ 

    “Gereza lipo Ikulu ya Nchi, sisi hatuhusiki tena na kesi hiyoΒ  Zola” Zola akauliza tenaΒ 

    “Kwanini mafaili ya kesi bado yalikuwa hapa?”Β 

    “Kwasababu kesi ilianzia hapa lakini cha kushangaza baada yaΒ  kukamatwa tuliondolewa katika kesi hiyo”Β 

    “Nani alitoa oda ya Nyie kuacha hii kesi na ikaenda sehemuΒ  nyingine wakati nyie ndio mnakazi hiyo?”Β 

    “Aliyetoa oda ni Rais wa Nchi” Zola aliondoka baada ya kupataΒ  majibu yaliyochanganya akili yake kisha akawasiliana na MzeeΒ  Dawson wakapanga kukutana katika makazi ya siri ya Zola,Β  Usiku Dawson alienda kuonana na Zola, kama kawaida yaoΒ  waligida pombe ili maongezi yaanzeΒ 

    “Enhee umegundua nini Zola?” Aliuliza DawsonΒ 

    “Mafaili yaliyobiwa katika kituo cha polisi yalikuwa ya kesiΒ  ya Mtu anayedaiwa kuwa alihusika kumuuwa Makam wa Rais”Β  Alisema ZolaΒ 

    “Unasemaje? Ina maana polisi wanajuwa ni nani alihusika?”Β 

    “Sio polisi pekee hata Mkuu wako wa Nchi ambaye anakupa kaziΒ  ya kulisaka kundi la Mafia Gang anajuwa na kibaya zaidiΒ  ametoa amri ya jeshi la polisi kuiacha kazi hiyo” Mzee DawsonΒ  alionekana kushangaa sanaΒ 

    “Inawezekanaje Zola?”

    “Hiyo ndio hali halisi ndio maana nimekuita hapa iliΒ  tuzungumze, nahisia mbaya juu ya Mkuu wa Nchi lakini sitakiΒ  kujiaminisha chochote”Β 

    “Unataka kusema Mkuu wa Nchi kuna kitu anakificha hapa?” WoteΒ  waliacha kunywa pombe wakazama katika maongezi yaoΒ 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SITAΒ  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ 

    Β  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx

    jasusi riwaya za kijasusi

    9 Comments

    1. Fadhili on December 2, 2024 5:03 pm

      Lit

      Reply
    2. Charz jr😎 on December 2, 2024 5:19 pm

      ✌️✌️

      Reply
      • G shirima on December 2, 2024 8:47 pm

        Naona inaelekea ukingoni

        Reply
      • Gabriel Luis Fabian on December 3, 2024 3:11 pm

        Nimekipenda kitabu hiki,
        Nikama macho yanafumbuka πŸ€”πŸ€”πŸ€”

        Reply
    3. Cathbert on December 2, 2024 5:52 pm

      Iko poa sanaaa

      Reply
    4. Mussa on December 2, 2024 10:53 pm

      Fantastic

      Reply
    5. Gabriel Luis Fabian on December 3, 2024 3:12 pm

      Nimekipenda kitabu hiki,
      Nikama macho yanafumbuka πŸ€”πŸ€”πŸ€”

      Reply
    6. Darius Amdun karyabwezile on December 3, 2024 5:17 pm

      Nimeipenda mno kiongoz ongera na asante ongeza bidii

      Reply
    7. Fawziya Hassan on December 6, 2024 12:09 pm

      MAMBO NI πŸ”₯

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.