Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Jasusi Sehemu Ya Sita (06)
    Hadithi

    Jasusi Sehemu Ya Sita (06)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaDecember 3, 2024Updated:December 4, 202443 Comments10 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Inawezekanaje Zola?”

    “Hiyo ndio hali halisi ndio maana nimekuita hapa iliย  tuzungumze, nahisia mbaya juu ya Mkuu wa Nchi lakini sitakiย  kujiaminisha chochote”ย 

    “Unataka kusema Mkuu wa Nchi kuna kitu anakificha hapa?” Woteย  waliacha kunywa pombe wakazama katika maongezi yaoย  Endeleaย 

    SEHEMU YA SITA

    “Kama hausiki kwanini atoe amri kwa jeshi la polisi? Kwaniniย  Mtuhumiwa afungwe katika Gereza lililopo Ikulu?” Alihoji Zolaย  huku Dawson akionesha kuanza kuvuta picha ya maelezo ya Zola.ย 

    “Mimi nafikiria kwasasa tujikite zaidi na upelelezi kuhusuย  Mafia Gang, hili jambo tuliweke kiporo Zola” Alisema Mzeeย  Dawson, ni wazi kilichomfanya akae kimya kwa muda mrefuย  kilikuwa ni hicho.ย 

    “Wewe ni mwalimu mzuri sana Dawson, kuliacha hili jambo niย  sawa na kumega Mkate alafu ukajiaminisha kuwa hakunaย  kilichotoka, umefundisha vijana wengi masuala ya upelelezi naย  Ujasusi, sidhani hata hicho unachokizungumza kinatoka katikaย  akili yako, sitaki kuamini pia kuwa pombe imekuingia kiasiย  hicho. Ili tuukate huu mti ni lazima tukubali kung’oa miziziย  ya Mti wenyewe ili usichipue tena”ย 

    “Zola tunaanzia wapi kumpeleleza Mkuu wa Nchi ambaye ndiyeย  ametupa kazi hii, kama hili kundi lina maslahi kwake kwaniniย  ameagiza tulifyeke? Nachelea kusema anaweza kuwa hausikiย  hapa” Alisema Dawson huku macho yake madogo kama ya pakaย  yaking’aza huku na kule, pombe ilikuwa ikishuka kwenye kooย  lake lenye koromeo kubwa, kisha alibakuaย 

    “Ni bora kuachana na kazi hii Dawson kuliko kuruhusu dosaliย  kwenye upelelezi huu, nimeweka Maisha yangu rehani, mwenyeweย  umeona nilitaka kuuawa kama sio wewe kuwahi kuniokoa,ย  tukubaliane hapa kuwa Rais apelelezwe kuhusu Mfungwaย  aliyefungwa magereza ya Ikulu” Ulikuwa ndio msimamo wa Zola,ย  Dawson alimuamini sana Zola akamwambiaย 

    “Kama ni hivyo basi uwanja ni wako Zola, siku ukithibitishaย  kuwa Rais anahusika na Mauwaji haya utanijulisha,” Ilikuwaย  ndio kauli ya mwisho ya Dawson, umri wake ulionesha ni jinsiย  gani alikuwa akipambana na akili za uzee alizonazo licha yaย  kuwa ni Mtu aliyeaminiwa sana na Idara ya Usalama wa Taifa,ย  akamuaga Zola huku akimuachia ujumbe kuwaย 

    “Wakati unawatafuta wao wapo macho wanakutafuta” Alisemaย  kisha alijizoa na kuondoka pale kwa kutumia gari yake yaย  kifahari, licha ya uzee lakini alimudu kuliendesha mwenyewe.ย  Muda huo mvua ilikuwa ikinyesha, Zola akawa anamtazama Dawsonย kupitia dirisha la kioo, Mzee Dawson alikuwa fundi waย  kuendesha gari jambo lililomchekesha Zola akajikuta akisemaย 

    “Ng’ombe huyu amegoma kuzee Maini yake” Akarudi kuketi hukuย  akizidi kutafakari, akamkubuka rafiki yake Mmoja aliyeitwaย  Sande Olise aliyekuwa uhamishoni Nchini Botswana,ย  alipomkumbuka alijikuta akitabasamu kisha akaenda ukutaniย  ambapo kulikuwa na picha waliyopiga pamoja.ย 

    Sande Olise alikuwa ni miongoni mwa Wanafunzi waliopelekwaย  Nchini Mexico kujifunza masuala ya upelelezi, Sandeย  alipishana umri wa miaka saba na Zola, tabia zao za kupendaย  wanawake ndizo zilizowafanya wakafahamiana, akakumbuka Jinsiย  walivyopigana vita vya kukiokoa kisiwa kimoja kilichopo Njeย  kidogo ya Mji Mkuu, kisiwa hicho kilivamiwa na Waasi kutokaย  Nchi jirani na kukiweka chini ya Ulinzi kwa zaidi ya sikuย  saba.ย 

    Zola alikaa chini akafikiria kumpigia simu Sande Olise,ย  alipekuwa baadhi ya nyaraka fulani akakuta namba ya Sandeย  kisha akampigia huku akitabasamu. Simu ilipokelewa huku sautiย  nzito ilisikika upande wa piliย 

    “P045 Olise! Kuna mpango maalum?” Alichofanya Zola alipigaย  simu ya Sande kwa kutumia namba maalum za siri, Wapeleleziย  wote walikuwa na simu za siri hivyo Sande alipoona simu hiyoย  alijuwa kulikuwa na shida mahali, japo sauti yake ilioneshaย  kuwa alikuwa ameamshwa na simu ya Zola lakini alikaza sautiย  yakeย 

    “P102 Zola! Over..” Alisema Zolaย 

    “Over!! Zola, za miaka mingi rafiki yangu” Alisema Sandeย  Olise huku ile sauti ya ukakamavu ikiwa imetoweka baada yaย  kugundua aliyekuwa akimpigia alikuwa ni rafiki yake kipenzi,ย  Mafunzo waliyoyapokea huko Mexico waliambiwa kitu pekeeย  wanachotakiwa kukiepuka ni urafiki sababu usaliti wa Nchiย  huanza kirafiki hatimaye kuwa janga la Taifa, hivyoย  waliheshimu misingi hiyo, ndiyo sababu ya kukaa Miaka mingiย  bila kuwasiliana.ย 

    “Nzuri ndugu yangu Sande, upo wapi siku hizi?” Alihoji Zola “Nipo Botswana uhamishoni, nina kitengo cha siri huku”ย 

    “Pole kwa majukumu! Ulisikia juu ya kifo cha Makam wa Rais naย  Matukio yanayoendelea huku?”

    “Nimesikia Zola, najua Mtaalam wa kazi utakuwa upo mzigoni,ย  lakini hao mnaopambana nao sijui kama ni saizi yenu, walikujaย  huku Miaka mitatu iliyopita lakini balaa lake ni kubwa sana,ย  wameuwa makomando 50, na taarifa nyingine zimefichwa”ย  Yalikuwa ni maelezo ya Sande Oliseย 

    “Sande hali ni tete sana, hili jambo ni zito na hawa jamaaย  wana mtandao Mkubwa sana Duniani, kupambana nao ni sawa naย  kutupa jiwe gizani, wanauwa kama hawana akili nzuri”ย 

    “Ha!ha!ha!” Alicheka Sandeย 

    “Mbona unacheka Sande”ย 

    “Hao jamaa wanamafunzo maalum nasikia Mkuu wao anaitwa Johnย  Brain, huyo Brain ndiyo mwalimu wa Osama Bin Laden,ย  anajihusisha pia na Alqaeda…Ni ngumu kumtambua kwa sura ilaย  alama kubwa ni vidole viwili wanavyoviacha wakiwa wamefanyaย  mauwaji, Mimi nipo Uhamishoni, majukumu yamepungua nakulaย  bata tuu sababu Mimi huku ni Bosi” Alisema Sande, lengo kuuย  la Zola lilikuwa ni kumshawishi Sande arudi Nchini iliย  washirikiane kupambana na Mafia Gang sababu Sande ni Mtuย  pekee anayeweza kumuaminiย 

    “Sande lengo langu la kukupigia na kuhitaji msaada wakoย  katika kazi hii ngumu niliyonayo, kuna uhusiano Mkubwa sanaย  kati ya Rais wa Nchi na hawa Mafia Gang, ni hatari kwa sasa,ย  siwezi kuinusa kwa pua zangu”ย 

    “Unataka nije kufa huko? CCP ina Wanafunzi wengi tulioendaย  Mexico kipindi kile, ni Mimi tu Zola?”ย 

    “Hadi nakupigia wewe nina uhakika kazi hii tutaiweza kablaย  mambo hayajaharibika zaidi, ujio wako utakuwa wa siri sanaย  ili tupeleleze kwa kina ni jambo gani lipo nyuma ya kapeti”ย 

    “Ooh! Zola unajuwa siwezi kukukatalia, nitakujulisha nipeย  siku tatu”ย 

    “Over!”ย 

    “Over!” Simu ilikatika mara moja, Zola akawa na tumaini laย  Ujio wa Sande Olise ambaye waliwahi kumuita Duma wakimaanishaย  ni Mtu mwenye kufanya mambo kwa haraka sana.ย 

    Zola akaelekea kitandani na kujipumzisha huku picha ya Raisย  ikiwa katika macho na akili yake, alimuwazia Rais huyo. Akiwaย  bado hajapata Usingizi Zola alipokea ujumbe wa simu kuwaย  Askari aliyezungumza naye na kumpa taarifa juu ya Mfungwaย aliyefungwa katika Gereza la Ikulu ameuawa kwa kupigwa Risasiย  akiwa ndani ya Kituo hicho, alishtuka kisha aliamka naย  kuwasha taa, muda huo huo simu kutoka kwa Dawson iliingiaย 

    “Zola umeisikia hiyo taarifa?” Aliuliza Dawsonย 

    “Ndio nimeipata muda huu” Alijibu Zola kisha simu ilikatikaย 

    “Uuups!” Zola alivuta pumzi zake, taswira mbili zilimjia kwaย  haraka haraka kuhusu mauwaji yale, upande mmoja ulimwambiaย  kuwa Rais ndiye aliyekuwa akihusika na mauwaji yale lakiniย  upande mwingine ulishindwa kumpa majibu ya kwanini Mafia Gangย  wanafanya matukio yale, Kichwa chake kiliwaka moto.ย 

    Asubuhi mapema aliamka na kueleka kituo cha polisi, akakutaย  hali ya huzunii ikiwa imetanda miongoni mwa polisi, Zolaย  akauliza ni Nani aliyefanya Mauwaji yale, cha ajabu alikuwaย  ni mmoja wa polisi ndiye aliyemuuwa yule polisi, Zolaย  akashika kiuno chake kwa mshangao, akapelekwa alipohifadhiwaย  Askari Muuwaji, hakutaka kuzungumza na Askari huyo akamwambiaย  polisi mmoja amletee Mafaili ya kesi iliyowahusu Robert,ย  Sandra na Bosco sababu ndio chanzo cha kuingizwa yeye katikaย  majukumu yale mazito, akaondoka kituoni na kurudi katikaย  Makazi yake ya siri, akayachoma moto mafaili hayo hukuย  akiamini kuwa matukio yote yale yalifanywa kwa lengo laย  kupumbaza jeshi la polisi ili wasijikite zaidi, walifanikiwaย  kuwapoteza lakini Zola aliinusa hatari hiyo huku akijiulizaย  Mafia Gang wanataka nini katika Nchi yao.ย 

    Muda huo huo Hekeheka ndani ya Kichwa Cha Zola iliongezeka,ย  alijikuta akiwa katika hali ambayo ilihitaji matumizi makubwaย  ya akili kuliko chochote kile. Kijasho chembamba kilikuwaย  kikimtoka kwenye paji lake la uso, picha ya askari aliyeuawaย  ilizunguka katika akili yake huku akijiuliza ni nani alitoaย  maagizo ya Askari yule kuuawa, alijuwa fika kuwa askariย  aliyemuuwa Askari mwenzake alishinikizwa kufanya hivyo, badoย  aliamini Rais alikuwa mhusika namba moja wa mauwaji yale,ย  akatoka nje huku akiwa anatazama taswira ya jua lilivyokuwaย  likichangamsha bustani yake ndogo katika Makazi yake,ย  pembezoni kulikuwa na njiwa waliokuwa wakiruka na kulia kwaย  kupokezana.ย 

    Zola akaingia kwenye gari yake, akaelekea kituo cha polisi,ย  safari hii alihitaji kumbana askari yule aliyemuuwa mwenzake,ย  akaelekea chumba ambacho alihifadhiwa askari huyo kishaย  akaomba polisi wote waondoke, wakabakia wawili tuu.ย 

    Zola alimtazama askari aliyekuwa akimtazama Zola kwa suraย  kavu iliyojaa umakini, hakuonekana kujuta kwa kitendo kileย  hata kidogo, Zola akamshika kichwa Askari huyo akamuuliza

    “Nani amekuagiza umuuwe Askari mwenzako?” Aliuliza Zola hukuย  akizidi kuvuta nywele za Askari huyo aliyefungwa pinguย  mikononi kwa nyumaย 

    “Nani yupo nyuma ya tukio hili? Sababu najuwa huwezi kufanyaย  hivi pasipo agizo maalum, huyu Askari alinieleza siriย  aliyoijuwa….Nina imani hata wewe unaijuwa hiyo na ndiyoย  sababu ya kumuuwa Askari mwenzako!!” Aliuliza tena Zola baadaย  ya kuona swali la kwanza halikujibiwaย 

    “Fanya uliwezalo Zola, fanya tuu lakini siwezi kukwambiaย  chochote zaidi tu ya kusema, nimemuuwa bila kuagizwa na Mtuย  yeyote” Zola akachukua rungu la polisi akawa anampiga polisiย  huyo sehemu za mbavu ili kuhakikisha anasema ni naniย  aliyemtuma kufanya mauwaji ndani ya kituo hicho cha polisi.ย  Askari huyo alikuwa akipiga kelele za maumivu, Zolaย  aliendelea kumpiga hadi akawa anatema damu mdomoni, Zolaย  alionekana kujawa na jazba sana. Muda huo simu yake iliita,ย  ikawa auheni kwa Askari huyo ambaye alikuwa akipunguza sautiย  ya kulalamika.ย 

    Zola akatupa lile rungu chini kisha akasogea ukutaniย  akaipokea simu hiyo ambayo ilimfanya Zola kwanza awe mtii,ย  mwenye kufuata maagizo, simu hiyo ilitoka ikulu, Zola alikuwaย  akizungumza na Rais aliyeitwa Jacob Zagamba.ย 

    “Nakuja Mkuu” Alisema Zola kisha simu ilionekana kukatika,ย  kijasho kilichokuwa kinamtoka Zola kilimwagika hadi kwenyeย  singlendi yake nyeupeย 

    “Shiti!!” Akasema kisha akamtazama yule Askari ambaye alikuwaย  akicheka kwa maumivu makali, Zola akachukua shati lake kishaย  akaondoka pale mara moja. Safari hii Zola alikuwa akielekeaย  Ikulu kuitika wito wa Rais wa Nchi hiyo, akiwa kwenye gariย  akawasha Intaneti kisha akampigia simu ya Video Sande Oliseย  aliyeko Botswana, bahati nzuri simu ilipokelewa haraka sanaย  na Sande Oliseย 

    “Sande!! Mkuu wa Nchi ameniita, naelekea Ikulu sasa” Alisemaย  Zola huku akiendelea kukanyaga mafuta kuelekea Ikulu.ย 

    “Nayaamini maneno yako, kuna mawili unaweza itiwa hapo, mojaย  kuhamishwa kwenda Nchi nyingine au kuonywa”ย 

    “Kwa vyovyote Rais ni mhusika nambari moja wa Matukio yote,ย  hajui kama ninafanya kazi na Dawson” Alieleza Zolaย 

    “Safi sana! Mchezo umeisha hapo, soma kauli yake kishaย  jiongeze Zola….Kifo chako kinaweza kutokea leo baada yaย kukoswa sana Miaka mingi tulipokuwa tukifanya Operesheniย  Upepo, ulikuwa Simba usiyejulikana unayelipigania Taifa lako,ย  Dawson anahitaji pongezi kwa kuwaficha Askari tunao tumikaย  kwenye idara kwa siri sana vinginevyo tungekuwa tunakufa kamaย  Kuku huku tukizungukwa na siasa Chafu” Ilikuwa ni sauti yaย  Sande Olise akizungumza kwa unakini mkubwa.ย 

    “Kama Maisha yangu yatakoma leo Ikulu, Sande uje kufanya hiiย  kazi kuliokoa Taifa mara moja” Alisema Zola kisha choziย  lilimtoka, akakata simu hiyo. Visa vya baadhi ya Askariย  kupotea vilikuwa vingi katika Taifa hilo, Zola baada ya Masaaย  mawili alikuwa akikaguliwa kwa ajili ya kuingia Ikulu,ย  ilikuwa ni mara ya kwanza Zola kuitwa na Rais huyo, si Raisย  huyu Pekee bali Zola hakupata kujulikana na Rais yeyoteย  aliyepita, hii ilimpa shaka sana Zola kwanini Rais ampigieย  simu wakati ambao alikuwa akimbana yule Askari amwambieย  ukweli kuwa Nani anafanya Mauwaji yale.ย  Comments zikiwa nyingi naachia ya 7 leoleo

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABAย  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย 

    ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx

    jasusi riwaya za kijasusi

    43 Comments

    1. Lucy on December 3, 2024 3:05 pm

      Inazid kuwร  ya moto

      Reply
      • Deogratias on December 3, 2024 3:14 pm

        Admin leta no 7 kabisaaa

        Reply
        • Cesilia Nkunga on December 3, 2024 9:41 pm

          Aisee ni ya moto balaa, admin big up!

          Reply
      • Deogratius on December 4, 2024 4:42 pm

        Riwaya tamu mno

        Reply
    2. KingSam4321 on December 3, 2024 3:05 pm

      Oyaaaa Hii Kali Sana Kaka๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅleta ya saba leoleo tuendleee ku-enjoy KIJIWENI

      Reply
    3. DIzzoh on December 3, 2024 3:08 pm

      Mkuuu ni kali balaaa aseee ww wa dunia ingineeeee

      Reply
    4. Hamisi halidi on December 3, 2024 3:08 pm

      Aaa adimin tuma chengne bx mana tamu san iih story

      Reply
    5. Classic loverz on December 3, 2024 3:11 pm

      Achia bampa

      Reply
    6. Ramso on December 3, 2024 3:23 pm

      Aiseee unajua ku2shika.hii story balaaaa

      Reply
    7. Anuar on December 3, 2024 3:31 pm

      Admin lete kituu ..stor imefkia patamu kabisa

      Reply
    8. Charz jr๐Ÿ˜Ž on December 3, 2024 3:42 pm

      ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ 7,8 alooooh!!! Hauchoki kusomaa

      Reply
      • wittie on December 3, 2024 7:02 pm

        Aloohh matukio yamepangiliwa vizurii sanaa….hongera mwandishi

        Reply
    9. Charz jr๐Ÿ˜Ž on December 3, 2024 3:42 pm

      Drop!! Drop it bro!!!

      Reply
    10. Charz jr๐Ÿ˜Ž on December 3, 2024 3:42 pm

      โœŒ๏ธโœŒ๏ธ

      Reply
      • VERONICA on December 3, 2024 9:26 pm

        Story nzuri sana hii, hongera sana Mtunzi

        Reply
    11. Chris wa Maria on December 3, 2024 3:57 pm

      Utamu kunoga

      Reply
    12. Neema on December 3, 2024 4:06 pm

      Safi tunaomba ya Saba

      Reply
    13. Buruhani on December 3, 2024 4:07 pm

      Achia Mzee baba tutililike nayooo

      Reply
    14. Buruhani on December 3, 2024 4:08 pm

      Achia kitu iyomzeebaba turuke nayo

      Reply
    15. Abdul on December 3, 2024 4:10 pm

      Nakubbal mamb ni moto ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ
      Admin usizingue sas

      Reply
    16. Suhayla Ahmad on December 3, 2024 4:15 pm

      Nzuri mno jaman

      Reply
    17. Joven on December 3, 2024 4:30 pm

      Admin eeh ya 7

      Reply
    18. miss tesha on December 3, 2024 4:36 pm

      watu tumejitoa๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

      Reply
    19. JACKZ on December 3, 2024 4:59 pm

      Duu I like to read books like that one โœŒโœŒโœŒโœŒโœŒ

      Reply
    20. Jlucky on December 3, 2024 5:10 pm

      Nilisoma hii story naona kama muv mubasharaaa leta ya 7

      Reply
    21. DAUD DEOGRATIAS on December 3, 2024 5:11 pm

      Adimn achia mzigo wa 7 huo twende kati duuh

      Reply
    22. DAUD DEOGRATIAS on December 3, 2024 5:11 pm

      Mzigo wa moto

      Reply
    23. Angel on December 3, 2024 5:13 pm

      Imefikia pazur sana…admin achia ya 7 leo tafadhali

      Reply
    24. รŸumble_รŸee on December 3, 2024 5:21 pm

      ni tamu

      Reply
    25. Emmanuel LAZARO on December 3, 2024 5:29 pm

      Kaliii sanaaa hiyoo blood

      Reply
    26. GUEVARA on December 3, 2024 5:35 pm

      Imekaa poa sana

      Reply
    27. Elsolo on December 3, 2024 5:49 pm

      Achia mpaka ya kumi

      Reply
    28. Irene Mwapinga on December 3, 2024 5:51 pm

      ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    29. Kadoo on December 3, 2024 6:38 pm

      Achia kamanda

      Reply
    30. G shirima on December 3, 2024 7:44 pm

      Comenti nyingi kabisa fanya kweli admin

      Reply
    31. daredajr on December 3, 2024 8:28 pm

      Achia chuma cha 7

      Reply
    32. Dorah on December 3, 2024 9:49 pm

      Daaaaa ni balaaa yaani nasoma sitamani iishe inazidi kunoga

      Reply
    33. Hamis on December 4, 2024 12:26 am

      Admin umetisha

      Reply
    34. Tina on December 4, 2024 10:10 am

      Motoooo

      Reply
    35. Junior Mtata on December 4, 2024 12:23 pm

      Actually siasa sio kitu Cha kuingilia pili kuna mambo ukiona sio size yako usiyafanye kwa mfano Zola Leo kaitwa hatujui Nini kina mkuta huko

      Reply
    36. David on December 4, 2024 1:34 pm

      Achia tu ya saba mkuu

      Reply
    37. Cathbert on December 6, 2024 5:18 am

      Imekaa poa sanaaaa

      Reply
    38. Fawziya Hassan on December 6, 2024 12:25 pm

      Jamani ZOLA

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 15, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya tatu Mke alipoisoma ile karatasi aligeuza macho kumtazama Mume…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.