Ilipoishia “Kuna kundi linaitwa MAFIA GANG, ni kundi maalum kwa ajili yaย Ugaidi…Mkuu wa kundi hili anaitwa John Brain ni mzunguย anayeishi Uskochi, Kazi yake ni kuratibu mauwaji. Amefanyaย kazi katika Nchi nyingi na sasa yupo hapa Nchini ndiyeย anayeratibu mauwaji ya viongozi kwa maslahi yake binafsi.ย Mwaka 2003 nchini Congo walifanya mauwaji mengi sana,ย nakuamini Zola ndio maana nataka ufanye upelelezi wa kina,ย ukomeshe kabisa kundi hili hapa Nchini” Yalikua ni maneno yaย Mzee Dawson yalitoka na moshi wa sigara.ย
“Kila kitu kipo tayari kwa ajili yako Zola, unahitajiย kuikomboa Nchi yako. Nakufahamu vizuri linapokuja suala laย kesi tata” Akamaliza kwa kumtakia kila la Kheri kwenye jukumuย lake zito la kuliondoa kundi la MAFIA GANG lakini kichwaniย bado alikua anauwaza ule mkasa wa akina Robert, akajiulizaย waliingiaje huko na nini kilipelekea? Endeleaย
SEHEMU YA PILIย
“Oooh! Jesus!” Akasema Zola huku akilikodolea macho gari laย kifahari la Mzee Dawson ambalo lilikua likitokomea, mkononiย alikuwa ameshikilia bahasha nyeusi ambayo ilikua maalum kwaย ajili ya kazi za siri, alijua ni vitu gani vitakuwepo kwenyeย ย Bahasha hiyo.ย
Safari ya Inspekta Zola ilimchukua masaa takribani matatuย kufikia yalipo makazi yake ya siri ambayo alikua akiyatumiaย kwenye upelelezi kila alipopata kazi ngumu mbele yakeย alijificha kwenye makazi hayo ambayo aliyapa jina la HOMEย TOWN.ย
Lilikua ni jumba lililopo karibu na fukwe ya Bahari ya Hindi,ย alichagua eneo hili sababu lilikua tulivu sana, licha ya kuwaย ni eneo ghali sana lakini alimudu gharama ambazo alikuwaย akilipiwa na kitengo cha Siri cha Mzee Dawson ( MPA )ย
Akabandua karatasi zilizopo kwenye ubao maalum, kishaย akabandika karatasi nyeupe akachora kwa kalamu na maandishiย yakapata kusomeka kama MAFIA GANG akimaanisha ndio kwanzaย alikua akiingia kazini kwa ajili ya kupambana na kikosi hichoย hatari cha Bwana John Brain.ย
Ilikua tayari usiku umeshaingia, akapiga simu kwa Waangaliziย wa zile maiti Hospitali kuwa hazipaswi kutolewa hadi paleย upelelezi utakapo kamilika, Hivyo familia zisubirie kwanzaย kabla ya maiti za akina Robert kupatikana kwa ajili yaย mazishi, alikua na lengo lake ndani ya kichwa chakeย kilichojaa nywele za mvi, akakuna kidevu chake baada kuwaย tayari ametoa maelekezo muhimu sana.ย
Inspekta Zola licha ya kuwa umri ulikua umeenda kidogo lakiniย alikua akipenda sana visichana vidogo vidogo, akaondokaย kwenye makazi yale akaelekea Baa kwa ajili ya kupata mvinyoย na kuangalia Mwanamke wa Kustarehe naye usiku huo.ย
Akaagiza White Wine huku akikodolea macho baadhi ya visichanaย vilivyokua ndani ya Baa hiyo, alipomaliza kunywa akawaย ameshapata Msichana wa kustarehe naye usiku huo ambapoย akaelekea Kwenye Hoteli moja iliyopo mita kadhaa kutokaย kwenye makazi yake ya siri. Akastarehe naye kisha akamuondoaย usiku huo huo, akabadili hoteli ambako alilala hadi asubuhi.ย
Aliamka na uchovu kiasi, akapata Kahawa kisha akaondokaย hotelini hapo akaelekea Hospitali, akaagiza iletwe maiti yaย Sandra. Akaanza sasa kuikagua rasmi kwa kutumia jicho lakeย kali la kijasusi, akiwa amevalia miwani yake ya machoย akagundua jambo, akaagiza mkasi na kisu, akavalia glovesย kwanza.ย
Akawaambia Watu wa Maabara waongeze mwanga wa taa, wakafanyaย hivyo. Akaona alama kwenye sura ya Sandra ambayo ilioneshaย kuwa sura ile haikuwa halisi. Akafwatisha ile alama kwa kisuย ndipo akaona sura ikijivua. Wote waliokuwa ndani ya chumbaย cha Maabara wakaingiwa na ganzi, lilikua ni jambo lililoย hitaji umakini wa hali ya juu zaidi.
Sura ilipovuka wakaikuta sura nyingine kabisa, pale paleย akavua gloves akachukua simu na kupiga picha kisha akapigaย simu kwenye kitengo cha siri cha Mzee Dawson ( MPA )ย
“Nahitaji wataalam wa Maabara haraka sana kwenye Hospitali yaย ST. James karibu na chuo cha Biashara” Ilikua ni sauti yakeย iliyojaa umakini zaidi, haraka wale wataalam wakawaย wamewasili hospitalini hapoย
“Chunguzeni maiti mbili za Robert na Bosco, vueni sura zao zaย Bandia kisha mpige picha mnitumie” Akawaachia maagizo,ย Inspekta Zola akaondoka pale Hospitalini akiwa na jambo jipyaย ndani ya akili yake, sasa ndio akawa na mashaka juu ya wapiย walipo Akina Robert wa ukweli na kwanini wale wajitoe muhangaย kupoteza maisha yao?ย
“Kuna jambo limejificha sio bure” Akasema Inspekta Zola akiwaย kwenye gari yake, alikua akielekea ofisini kwa Mzee Dawsonย ambaye ni mtaalam wa Taarifa kutoka usalama wa Taifa.ย
“Naam! Zola , kuna jipya umeligundua?” akauliza Mzee Dawsonย baada ya kukutana ana kwa ana na Inspekta Zolaย
“Dawson!! hili jambo lina mchakato wa hatari unaohitajiย utulivu zaidi”ย
“Hilo ndilo nililotegemea kulisikia kutoka kwako Zola, hiiย sio kazi ya kitoto ndio maana nimeileta kwenye meza yako,ย umekutana na kazi nyingi za hatari na zote umefanikiwa, hiliย haliwezi kuwa jepesi pia”ย
“Maiti zile zina sura za Bandia, inaonesha kuna mwamvuli waย Kifo uliotumika hapa ili kupumbaza akili za kipelelezi”ย
“Una maana maiti sio halisi kwa sura tambuliwa?”ย
“Ndio, hii moja wapo” Akamuonesha sura iliyokutwa kwenyeย maiti iliyotambuliwa kama Sandra.ย
“Wauwaji ni Watu wenye akili kubwa sana na inaonesha niย wazoefu wa hii kazi Zola, unatakiwa kuwa makini sana endapoย watakugundua hali itakua mbaya, unatakiwa upate sura yaย Bandia ili kuficha uhalisia wako” Akasema Mzee Dawsonย akionesha kuanza kulitazama jambo hilo kwa jicho la tatu.ย
********ย
Ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa, Six na yule Mdadaย aliyejitambulisha kwa Inspekta Zola kama Judith lakini hukuย alikua akiitwa Malaika walikua wakisubiria ugeni ndani yaย Uwanja huu.ย
Malaika alikua kwenye sura yake halisi, akionekana kama mdadaย mwenye majivuno sana, shingo yake ilikua na tatuu ya maua yaย rangi aina ya Rose, iliwabidi kukaa hapo kwa zaidi ya nusuย saa. Punde wakapata kumuona Mtu waliyekuja kumpokea, alikuaย ni Mzungu mwenye kibegi kidogo.ย
Safari ya kutoka Uwanja wa ndege kuelekea kwenye makazi yaoย ya siri ilianza, Mzungu alipofika kwenye gari akavua suraย bandia. Yes! huyu ndiye John Brain ambaye idara nyingi zaย Usalama Duniani zilikua zikimtafuta lakini ilikua ngumu sanaย kumnasa, licha ya kuwa yeye ndio Bosi wa kundi la MAFIA GANGย lakini pia alikua akipokea oda kutoka kwa Mabosi wake ambaoย walikuwa wa siri sana.ย
“Umefanikisha kuchukua nyaraka?” akauliza John Brain hukuย akiwa anaiweka ile sura ndani ya begi lake dogo ambaloย lilikua na sura nyingine za Bandia ambazo alikua akizitumiaย mara kwa mara ili kuficha utambulisho wake.ย
“Nimefanikisha lakini kuna Mpelelezi mmoja makini anafwatiliaย jambo hili”ย
“Dammn!! niliwaambia mnatakiwa kwanza kusafisha kikosi chaย Usalama wa Taifa ndipo kazi nzito ianze” John Brain akachukuaย nyaraka na kuanza kuzipitia, alifahamu lugha zaidi ya 20ย hivyo hakupata shida pindi alipokuwa akiratibu mpango fulaniย kwenye Nchi tofauti tofauti.ย
- โขโขโขโขโขโขโขโขย
Ndani ya Ikulu, Mzee Dawson alikua akifanya mazungumzo naย Rais wa Nchi ili kujua wamefikia wapi. Ilikua ni lazimaย wadhibiti MAFIA GANG kabla haijaleta mpasuko na taharuki kwaย Wananchi, tayari Watu ambao hawakua Usalama wa Taifa walianzaย kufa, vifo vya Askari 15 ndani ya kituo cha polisi ilikua niย miongoni mwa taarifa zilizomkasirisha sana Rais.ย
“Dawson! Unasifika kwa Ujasusi, tayari kazi hii iko mikononiย mwako na hakuna namna tunaweza kufanya bali kusikilizaย maendeleo yako” Yalikua ni maneno ya Rais, Mzee Dawson alikuaย akichezea karamu kuonesha alikua akitafakari namna yaย kumjibu, Rais akagonga meza kama ishara ya kuhimiza kupataย jibu kutoka kwa Mzee Dawsonย
“Kazi iko kwenye mikono yangu Mkuu, ni lazima nilifyeke kundiย hili kabla halija leta madhara zaidi”
“Madhara zaidi? tayari wameleta madhara na hofu imetanda kwaย watendaji wa Serikali, najiuliza ni Watu wa namna gani hawaย wameweza kuingia kwenye nyumba ya Msaidizi wangu ( Makam waย Rais ) na kufanya mauwaji bila Askari na walinzi wengineย kujua, hali sio shwari Dawson” Rais akapaza sauti iliyoambataย na kukauka kwa koo lake, akahitaji maji ya Baridi kutokaย kwenye friza, Dawson akampatia maji kwenye glasi, yalikua niย maongezi ya siri kati ya Dawson na Rais huyu. Baada yaย kumaliza kunywa glasi moja ya maji baridi, akawa ametulizaย mzuka wake.ย
“Dawson! nakuamini” akasema Rais akiwa anaweka glasi juu yaย meza kisha akavuta tai yakeย
“Sitakuangusha Mkuu ni jukumu langu zito, nimekula kiapoย kuilinda nchi yangu” akasema kwa utii na heshima kubwa mbeleย ya Rais huyu Kijanaย
“Wanataka nini?”ย
“Mapema tutalibaini hilo, kuanzia hapo tutawadhibiti Mkuu.ย Wamefanya mauwaji Nchi nyingi lakini hapa wameingia sehemuย isiyo salama kwao, nakuhakikishia nitawafyeka harakaย iwezekanavyo”ย
“Dawson! Nchi inakuangalia wewe na kitengo chako cha Usalamaย wa Taifa” Akamaliza kwa kumrunusu Dawson akaendelee naย majukumu yake mazito, jasho likiwa linamvuja…Mzee Dawsonย akachukua Lifti kushuka chini, akaingia ndani ya gari yake.ย
Jua lilikua tamu sana siku hii, hali ya ubaridi ikiwaย inachukua nafasi kubwa. Inspekta Zola akaelekea nyumbani kwaย Marehemu Robert, Waombolezaji walikua wengi sana lakini Zolaย akahitaji kuonana na Mama yake na Robert, akaoneshwa mahaliย ambapo Mama huyo alikuwepo.ย
“Pole Mama, Naitwa Inspekta Zola nafikiri unanikumbuka?”ย akaongea baada ya kuketi, akahitaji kuzungumza na Mama yakeย Robert pekee, waombolezaji wengine wakaamriwa kutoka.ย
“Mara ya Mwisho ulionana wapi na Robert?” Mama akafuta choziย lake, akajiweka sawa kuongeaย
“Nilizungumza na Robert kupitia simu, akaniambia nije hukuย kwa ajili ya harusi yake. Nilichelewa kufika huku kutokana naย mazingira yaliyo nje ya uwezo wangu, Alinisistiza sanaย natakiwa kuwepo lakini nilifika siku ya harusi…”ย
“Ulionana na Mwanao baada ya kufika?”
“Hapana, alipofika kanisani hakupata hata kunitazama. Ndioย tukio likatokea…”ย
“Mwanao alikua anafanya kazi gani?”ย
“Robert alikua na duka la kuuza Maua mjini, ndio biasharaย yake ya muda mrefu”ย
“Unamfahamu vipi Bosco?” Mama akaanza kulia, Zola akajitahidiย kumtulizaย
“Bosco ni kama Mwanangu, walikuwa wakija pamoja kunitembelea,ย sijui wamepatwa na nini hadi wakauwana” Inspekta Zolaย alipomaliza kuzungumza na Mama Robert, akaelekea kuonana naย Mzee Dawson ambaye alimpigia simu kuwa kuna ujumbe kutoka kwaย Raisย
Ndani ya mkoba wa Inspekta Zola kulikua na sura za bandiaย ambazo alikua amepewa na Mzee Dawson ili kuficha uhalisiaย wake, alipofika kwenye gari akaivaa kisha akaelekea kuonanaย na Dawson.ย
Kama kawaida yao walikutana sehemu iliyojificha huku wakipataย pombe ambayo kwao waliita kama kifungua kinywa, sura ya Mzeeย Dawson ilikua imekosa neema ya furaha, tabasamu lakeย halikuonekana hata chembe na kumfanya Zola atamani kusikiaย kutoka kwa Mzee Dawson ( Google )ย
“Hali ni mbaya Zola, Mkuu amewaka sana leo anahitaji kaziย iishe ndani ya muda mfupi vinginevyo anaweza akaajili Watuย kutoka nje ya Nchi kwa ajili ya upelelezi wa kina kuhusuย MAFIA GANG” akasema kwa sauti iliyotoka kwa vituo vituo hukuย akiwa anameza funda za pombeย
“Dawson! umenipa kazi ndani ya masaa 24, ndani ya Upeleleziย huu kuna visa tata sana ambavyo vinahitaji umakini wa hali yaย juu sana vinginevyo tutakuja kupoteza kila kitu”ย
“Kuna Mtu nitakuunganisha naye, ni rafiki yangu wa muda mrefuย anaitwa Pacho…atakusaidia baadhi ya mambo ili kuendana naย muda”ย
Punde simu ya Mzee Dawson ikaanza kuita, akaisikilizia kwaย miito mitatu kisha akaipokea na kuiweka kwenye sikio lakeย lililojaa Usikivu wa kupokea taarifa, alichokisikiaย kilimshtua sana mara simu ikakatika.ย
“Barabara namba 8 kuna mauwaji yametokea ya Afisa wa Usalamaย akiwa anatoka kanisani” Ilikua ni sauti ya Mzee Dawsonย iliyotawaliwa na utulivu sana
“Ooh God”ย
“Ndio hivyo Zola, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa wiki hiiย na kuendelea”ย
“Ngoja nielekee eneo la tukio” Inspekta Zola akajikusanya naย kuondoka pale akimuacha Mzee Dawson akiendelea kugida pombeย kali.ย
Yalikua ni majukumu yake ya kazi, akafika eneo la tukio naย kuukuta mwili wa Afsa aliyeuwa ukiwa juu ya daraja, gari yaย Afsa huyo ikiwa imesimama katikati ya Barabara na kusababishaย msongamano.ย
Taratibu za kiusalama zikaanza mara moja huku mwiliย ukichukuliwa na kupelekwa Hospitalini, mara simu ya Zolaย ikaingia ujumbe kutoka kwa wataalam wa Maabara kutoka kwenyeย kitengo cha Siri cha Mzee Dawson kilichoitwa MPA, akapewaย taarifa juu ya Maiti ya Robert na Bosco.ย
Milii ile ilikuwa ndio pekee yenye sura halisi tofauti naย Maiti ya Sandra ambayo ilikutwa na sura bandia, akajikutaย akiwa njia panda hajui aanze na lipi amalizie lipi, simu yakeย ikaingia ujumbe mfupi kutoka kwenye namba ambayo ilikuwa yaย siriย
“ZOLA TOKA ENEO HILO HARAKA SANA” Ujumbe ulisomeka hivyo,ย akajaribu kutafakari kwa kina lakini hakupata majibu kwaย haraka, akajaribu kuujibu ujumbe huo lakini hakufanikiwaย kupata majibu. Kwa akili yake ya kipelelezi akajuwa mara mojaย yupo Mtu anayemuona pale, haraka akaondoka pale na kuelekeaย kwenye gari lake ambalo lilikuwa kando na eneo lile, maraย akasikia mlipuko mkubwa. Alipogeuka akaona gari moja ikiwaย inawaka moto, ndio gari ambalo alikuwa karibu nalo paleย alipokuwa amesimama eneo la tukio.ย
Hapo akafanikiwa kujua kuwa kuna Watu wanamfuatilia kwaย karibu sana lakini akawa na maswali mengi kuwa ni naniย aliyemuokoa kwenye ile hatari? Mlipuko ulisababisha majeruhiย wengi sana ambao walikuwa ni Askari na wapita njia.ย
Alipofika kwenye gari yake akapata shahuku ya kutakaย kumfahamu aliyemuokoa kwenye kifo, akachukua simu yake naย kujaribu kuujibu ule ujumbe lakini hakupata majibu mengine,ย akamtafuta Mzee Dawson na kumtaarifu juu ya tukio hilo laย mlipukoย
“Aliyekuokoa anaitwa Pacho, ndiye msaidizi wako kwenyeย majukumu”
“Oooh! niliona kifo changu pale”ย
“Kuwa makini sana, Watu wa Usalama wanauawa sana….” yalikuaย ni maneno ya mwisho ya Mzee Dawson kisha simu ilikatika,ย ikampa wasaa Inspekta Zola kuelekea kwenye makazi yake yaย Siri karibu na ufukwe.ย
Masaa mawili baadaye yalimkuta Inspekta Zola akiwa amekaliaย kiti kwenye makazi yake ya siri, mbele yake kulikuwa na mezaย nyeusi ngumu iliyotengenezwa kwa kioo. Alionekana kuzamaย kwenye lindi la mawazo, akafikiria namna Muuwaji alivyokuwaย akifanya mauwaji kila kukicha, bado alitakiwa kujuwa ni wapiย alipo Sandra wa Ukweli kama Bosco na Robert ni Watu halisi,ย presha ya Rais ya kulazikisha kazi ifanyike upesiย ilimkasirisha sana.ย
*****************ย
Anga lilibadilika kuwa jeusi machoni pa Idara za usalama waย Taifa, Mauwaji ya Polisi na Maafisa yalitaarifiwa kila konaย ya Jiji, Hofu ikachukua nafasi kubwa kila mmoja akijiuliza niย nani atafuata Kufa. Ujio wa John Brain Nchini ulikuwa naย lengo moja kubwa, akakutana na Vijana wake wawiliย aliowatumainia sana mmoja aliyeitwa Six na mwingine aliyeitwaย Malaika akawaambiaย
“Wakati Polisi wanahangaika kutafuta ufumbuzi wa vifo hiviย vya utata sisi tutakuwa bize kumalizia mpango wetu hapaย Nchini, Rais wa Nchi hii alitutuma kazi na tumeimaliza sasaย kwanini idara yake inamshikilia Jamaal?” Alihoji John Brainย
“Huyu Kenge anayeitwa Zola atakuwa kikwazo kikubwa sanaย kwenye mpango huu, lazima aondoke kwanza” Alisema Malaikaย akakumbuka jinsi Inspekta Zola alivyo makiniย
“Udhaifi wa Zola ni Wanawake, kilevi chake kitamuuwa mudaย mchache ujao” Alisema John Brain aliyeonekana kujaza mamboย mengi kichwani pakeย
“Kazi hiyo niachieni mimi” Six akaomba apewe huo mpango waย kuondoa uhai wa Inspekta Zolaย
“Unatakiwa kuwa makini sana sababu kwa namna alivyo huyo Mtuย si rahisi akamuamini Mtu kwa Mara ya kwanza, unapaswa piaย kujuwa kuwa ukibainika basi kila kitu kitaharibika. Zola niย Jasusi mbobezi, kabla hujampeleleza anakuwa tayariย amekupeleleza.” Alisema John Brain, kisha Malaika kasema
“Zola anatumika kama Mwanvuli wa Serikali katika kutekelezaย mipango ya siri, najiuliza aliwezaje kukwepa mtego wa Bomu”ย
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATUย USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
ย ย
ย ย
8 Comments
First one
Huna Baya Mwanangu
โ๏ธโ๏ธ
Waaah๐
Doooh mambo mengi kwel
Imekaa poa sana
โฅ๏ธ
cn3qob