Ilipoishia “Kuna kundi linaitwa MAFIA GANG, ni kundi maalum kwa ajili yaΒ Ugaidi…Mkuu wa kundi hili anaitwa John Brain ni mzunguΒ anayeishi Uskochi, Kazi yake ni kuratibu mauwaji. AmefanyaΒ kazi katika Nchi nyingi na sasa yupo hapa Nchini ndiyeΒ anayeratibu mauwaji ya viongozi kwa maslahi yake binafsi.Β Mwaka 2003 nchini Congo walifanya mauwaji mengi sana,Β nakuamini Zola ndio maana nataka ufanye upelelezi wa kina,Β ukomeshe kabisa kundi hili hapa Nchini” Yalikua ni maneno yaΒ Mzee Dawson yalitoka na moshi wa sigara.Β
“Kila kitu kipo tayari kwa ajili yako Zola, unahitajiΒ kuikomboa Nchi yako. Nakufahamu vizuri linapokuja suala laΒ kesi tata” Akamaliza kwa kumtakia kila la Kheri kwenye jukumuΒ lake zito la kuliondoa kundi la MAFIA GANG lakini kichwaniΒ bado alikua anauwaza ule mkasa wa akina Robert, akajiulizaΒ waliingiaje huko na nini kilipelekea? EndeleaΒ
SEHEMU YA PILIΒ
“Oooh! Jesus!” Akasema Zola huku akilikodolea macho gari laΒ kifahari la Mzee Dawson ambalo lilikua likitokomea, mkononiΒ alikuwa ameshikilia bahasha nyeusi ambayo ilikua maalum kwaΒ ajili ya kazi za siri, alijua ni vitu gani vitakuwepo kwenyeΒ Β Bahasha hiyo.Β
Safari ya Inspekta Zola ilimchukua masaa takribani matatuΒ kufikia yalipo makazi yake ya siri ambayo alikua akiyatumiaΒ kwenye upelelezi kila alipopata kazi ngumu mbele yakeΒ alijificha kwenye makazi hayo ambayo aliyapa jina la HOMEΒ TOWN.Β
Lilikua ni jumba lililopo karibu na fukwe ya Bahari ya Hindi,Β alichagua eneo hili sababu lilikua tulivu sana, licha ya kuwaΒ ni eneo ghali sana lakini alimudu gharama ambazo alikuwaΒ akilipiwa na kitengo cha Siri cha Mzee Dawson ( MPA )Β
Akabandua karatasi zilizopo kwenye ubao maalum, kishaΒ akabandika karatasi nyeupe akachora kwa kalamu na maandishiΒ yakapata kusomeka kama MAFIA GANG akimaanisha ndio kwanzaΒ alikua akiingia kazini kwa ajili ya kupambana na kikosi hichoΒ hatari cha Bwana John Brain.Β
Ilikua tayari usiku umeshaingia, akapiga simu kwa WaangaliziΒ wa zile maiti Hospitali kuwa hazipaswi kutolewa hadi paleΒ upelelezi utakapo kamilika, Hivyo familia zisubirie kwanzaΒ kabla ya maiti za akina Robert kupatikana kwa ajili yaΒ mazishi, alikua na lengo lake ndani ya kichwa chakeΒ kilichojaa nywele za mvi, akakuna kidevu chake baada kuwaΒ tayari ametoa maelekezo muhimu sana.Β
Inspekta Zola licha ya kuwa umri ulikua umeenda kidogo lakiniΒ alikua akipenda sana visichana vidogo vidogo, akaondokaΒ kwenye makazi yale akaelekea Baa kwa ajili ya kupata mvinyoΒ na kuangalia Mwanamke wa Kustarehe naye usiku huo.Β
Akaagiza White Wine huku akikodolea macho baadhi ya visichanaΒ vilivyokua ndani ya Baa hiyo, alipomaliza kunywa akawaΒ ameshapata Msichana wa kustarehe naye usiku huo ambapoΒ akaelekea Kwenye Hoteli moja iliyopo mita kadhaa kutokaΒ kwenye makazi yake ya siri. Akastarehe naye kisha akamuondoaΒ usiku huo huo, akabadili hoteli ambako alilala hadi asubuhi.Β
Aliamka na uchovu kiasi, akapata Kahawa kisha akaondokaΒ hotelini hapo akaelekea Hospitali, akaagiza iletwe maiti yaΒ Sandra. Akaanza sasa kuikagua rasmi kwa kutumia jicho lakeΒ kali la kijasusi, akiwa amevalia miwani yake ya machoΒ akagundua jambo, akaagiza mkasi na kisu, akavalia glovesΒ kwanza.Β
Akawaambia Watu wa Maabara waongeze mwanga wa taa, wakafanyaΒ hivyo. Akaona alama kwenye sura ya Sandra ambayo ilioneshaΒ kuwa sura ile haikuwa halisi. Akafwatisha ile alama kwa kisuΒ ndipo akaona sura ikijivua. Wote waliokuwa ndani ya chumbaΒ cha Maabara wakaingiwa na ganzi, lilikua ni jambo lililoΒ hitaji umakini wa hali ya juu zaidi.
Sura ilipovuka wakaikuta sura nyingine kabisa, pale paleΒ akavua gloves akachukua simu na kupiga picha kisha akapigaΒ simu kwenye kitengo cha siri cha Mzee Dawson ( MPA )Β
“Nahitaji wataalam wa Maabara haraka sana kwenye Hospitali yaΒ ST. James karibu na chuo cha Biashara” Ilikua ni sauti yakeΒ iliyojaa umakini zaidi, haraka wale wataalam wakawaΒ wamewasili hospitalini hapoΒ
“Chunguzeni maiti mbili za Robert na Bosco, vueni sura zao zaΒ Bandia kisha mpige picha mnitumie” Akawaachia maagizo,Β Inspekta Zola akaondoka pale Hospitalini akiwa na jambo jipyaΒ ndani ya akili yake, sasa ndio akawa na mashaka juu ya wapiΒ walipo Akina Robert wa ukweli na kwanini wale wajitoe muhangaΒ kupoteza maisha yao?Β
“Kuna jambo limejificha sio bure” Akasema Inspekta Zola akiwaΒ kwenye gari yake, alikua akielekea ofisini kwa Mzee DawsonΒ ambaye ni mtaalam wa Taarifa kutoka usalama wa Taifa.Β
“Naam! Zola , kuna jipya umeligundua?” akauliza Mzee DawsonΒ baada ya kukutana ana kwa ana na Inspekta ZolaΒ
“Dawson!! hili jambo lina mchakato wa hatari unaohitajiΒ utulivu zaidi”Β
“Hilo ndilo nililotegemea kulisikia kutoka kwako Zola, hiiΒ sio kazi ya kitoto ndio maana nimeileta kwenye meza yako,Β umekutana na kazi nyingi za hatari na zote umefanikiwa, hiliΒ haliwezi kuwa jepesi pia”Β
“Maiti zile zina sura za Bandia, inaonesha kuna mwamvuli waΒ Kifo uliotumika hapa ili kupumbaza akili za kipelelezi”Β
“Una maana maiti sio halisi kwa sura tambuliwa?”Β
“Ndio, hii moja wapo” Akamuonesha sura iliyokutwa kwenyeΒ maiti iliyotambuliwa kama Sandra.Β
“Wauwaji ni Watu wenye akili kubwa sana na inaonesha niΒ wazoefu wa hii kazi Zola, unatakiwa kuwa makini sana endapoΒ watakugundua hali itakua mbaya, unatakiwa upate sura yaΒ Bandia ili kuficha uhalisia wako” Akasema Mzee DawsonΒ akionesha kuanza kulitazama jambo hilo kwa jicho la tatu.Β
********Β
Ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa, Six na yule MdadaΒ aliyejitambulisha kwa Inspekta Zola kama Judith lakini hukuΒ alikua akiitwa Malaika walikua wakisubiria ugeni ndani yaΒ Uwanja huu.Β
Malaika alikua kwenye sura yake halisi, akionekana kama mdadaΒ mwenye majivuno sana, shingo yake ilikua na tatuu ya maua yaΒ rangi aina ya Rose, iliwabidi kukaa hapo kwa zaidi ya nusuΒ saa. Punde wakapata kumuona Mtu waliyekuja kumpokea, alikuaΒ ni Mzungu mwenye kibegi kidogo.Β
Safari ya kutoka Uwanja wa ndege kuelekea kwenye makazi yaoΒ ya siri ilianza, Mzungu alipofika kwenye gari akavua suraΒ bandia. Yes! huyu ndiye John Brain ambaye idara nyingi zaΒ Usalama Duniani zilikua zikimtafuta lakini ilikua ngumu sanaΒ kumnasa, licha ya kuwa yeye ndio Bosi wa kundi la MAFIA GANGΒ lakini pia alikua akipokea oda kutoka kwa Mabosi wake ambaoΒ walikuwa wa siri sana.Β
“Umefanikisha kuchukua nyaraka?” akauliza John Brain hukuΒ akiwa anaiweka ile sura ndani ya begi lake dogo ambaloΒ lilikua na sura nyingine za Bandia ambazo alikua akizitumiaΒ mara kwa mara ili kuficha utambulisho wake.Β
“Nimefanikisha lakini kuna Mpelelezi mmoja makini anafwatiliaΒ jambo hili”Β
“Dammn!! niliwaambia mnatakiwa kwanza kusafisha kikosi chaΒ Usalama wa Taifa ndipo kazi nzito ianze” John Brain akachukuaΒ nyaraka na kuanza kuzipitia, alifahamu lugha zaidi ya 20Β hivyo hakupata shida pindi alipokuwa akiratibu mpango fulaniΒ kwenye Nchi tofauti tofauti.Β
- β’β’β’β’β’β’β’β’Β
Ndani ya Ikulu, Mzee Dawson alikua akifanya mazungumzo naΒ Rais wa Nchi ili kujua wamefikia wapi. Ilikua ni lazimaΒ wadhibiti MAFIA GANG kabla haijaleta mpasuko na taharuki kwaΒ Wananchi, tayari Watu ambao hawakua Usalama wa Taifa walianzaΒ kufa, vifo vya Askari 15 ndani ya kituo cha polisi ilikua niΒ miongoni mwa taarifa zilizomkasirisha sana Rais.Β
“Dawson! Unasifika kwa Ujasusi, tayari kazi hii iko mikononiΒ mwako na hakuna namna tunaweza kufanya bali kusikilizaΒ maendeleo yako” Yalikua ni maneno ya Rais, Mzee Dawson alikuaΒ akichezea karamu kuonesha alikua akitafakari namna yaΒ kumjibu, Rais akagonga meza kama ishara ya kuhimiza kupataΒ jibu kutoka kwa Mzee DawsonΒ
“Kazi iko kwenye mikono yangu Mkuu, ni lazima nilifyeke kundiΒ hili kabla halija leta madhara zaidi”
“Madhara zaidi? tayari wameleta madhara na hofu imetanda kwaΒ watendaji wa Serikali, najiuliza ni Watu wa namna gani hawaΒ wameweza kuingia kwenye nyumba ya Msaidizi wangu ( Makam waΒ Rais ) na kufanya mauwaji bila Askari na walinzi wengineΒ kujua, hali sio shwari Dawson” Rais akapaza sauti iliyoambataΒ na kukauka kwa koo lake, akahitaji maji ya Baridi kutokaΒ kwenye friza, Dawson akampatia maji kwenye glasi, yalikua niΒ maongezi ya siri kati ya Dawson na Rais huyu. Baada yaΒ kumaliza kunywa glasi moja ya maji baridi, akawa ametulizaΒ mzuka wake.Β
“Dawson! nakuamini” akasema Rais akiwa anaweka glasi juu yaΒ meza kisha akavuta tai yakeΒ
“Sitakuangusha Mkuu ni jukumu langu zito, nimekula kiapoΒ kuilinda nchi yangu” akasema kwa utii na heshima kubwa mbeleΒ ya Rais huyu KijanaΒ
“Wanataka nini?”Β
“Mapema tutalibaini hilo, kuanzia hapo tutawadhibiti Mkuu.Β Wamefanya mauwaji Nchi nyingi lakini hapa wameingia sehemuΒ isiyo salama kwao, nakuhakikishia nitawafyeka harakaΒ iwezekanavyo”Β
“Dawson! Nchi inakuangalia wewe na kitengo chako cha UsalamaΒ wa Taifa” Akamaliza kwa kumrunusu Dawson akaendelee naΒ majukumu yake mazito, jasho likiwa linamvuja…Mzee DawsonΒ akachukua Lifti kushuka chini, akaingia ndani ya gari yake.Β
Jua lilikua tamu sana siku hii, hali ya ubaridi ikiwaΒ inachukua nafasi kubwa. Inspekta Zola akaelekea nyumbani kwaΒ Marehemu Robert, Waombolezaji walikua wengi sana lakini ZolaΒ akahitaji kuonana na Mama yake na Robert, akaoneshwa mahaliΒ ambapo Mama huyo alikuwepo.Β
“Pole Mama, Naitwa Inspekta Zola nafikiri unanikumbuka?”Β akaongea baada ya kuketi, akahitaji kuzungumza na Mama yakeΒ Robert pekee, waombolezaji wengine wakaamriwa kutoka.Β
“Mara ya Mwisho ulionana wapi na Robert?” Mama akafuta choziΒ lake, akajiweka sawa kuongeaΒ
“Nilizungumza na Robert kupitia simu, akaniambia nije hukuΒ kwa ajili ya harusi yake. Nilichelewa kufika huku kutokana naΒ mazingira yaliyo nje ya uwezo wangu, Alinisistiza sanaΒ natakiwa kuwepo lakini nilifika siku ya harusi…”Β
“Ulionana na Mwanao baada ya kufika?”
“Hapana, alipofika kanisani hakupata hata kunitazama. NdioΒ tukio likatokea…”Β
“Mwanao alikua anafanya kazi gani?”Β
“Robert alikua na duka la kuuza Maua mjini, ndio biasharaΒ yake ya muda mrefu”Β
“Unamfahamu vipi Bosco?” Mama akaanza kulia, Zola akajitahidiΒ kumtulizaΒ
“Bosco ni kama Mwanangu, walikuwa wakija pamoja kunitembelea,Β sijui wamepatwa na nini hadi wakauwana” Inspekta ZolaΒ alipomaliza kuzungumza na Mama Robert, akaelekea kuonana naΒ Mzee Dawson ambaye alimpigia simu kuwa kuna ujumbe kutoka kwaΒ RaisΒ
Ndani ya mkoba wa Inspekta Zola kulikua na sura za bandiaΒ ambazo alikua amepewa na Mzee Dawson ili kuficha uhalisiaΒ wake, alipofika kwenye gari akaivaa kisha akaelekea kuonanaΒ na Dawson.Β
Kama kawaida yao walikutana sehemu iliyojificha huku wakipataΒ pombe ambayo kwao waliita kama kifungua kinywa, sura ya MzeeΒ Dawson ilikua imekosa neema ya furaha, tabasamu lakeΒ halikuonekana hata chembe na kumfanya Zola atamani kusikiaΒ kutoka kwa Mzee Dawson ( Google )Β
“Hali ni mbaya Zola, Mkuu amewaka sana leo anahitaji kaziΒ iishe ndani ya muda mfupi vinginevyo anaweza akaajili WatuΒ kutoka nje ya Nchi kwa ajili ya upelelezi wa kina kuhusuΒ MAFIA GANG” akasema kwa sauti iliyotoka kwa vituo vituo hukuΒ akiwa anameza funda za pombeΒ
“Dawson! umenipa kazi ndani ya masaa 24, ndani ya UpeleleziΒ huu kuna visa tata sana ambavyo vinahitaji umakini wa hali yaΒ juu sana vinginevyo tutakuja kupoteza kila kitu”Β
“Kuna Mtu nitakuunganisha naye, ni rafiki yangu wa muda mrefuΒ anaitwa Pacho…atakusaidia baadhi ya mambo ili kuendana naΒ muda”Β
Punde simu ya Mzee Dawson ikaanza kuita, akaisikilizia kwaΒ miito mitatu kisha akaipokea na kuiweka kwenye sikio lakeΒ lililojaa Usikivu wa kupokea taarifa, alichokisikiaΒ kilimshtua sana mara simu ikakatika.Β
“Barabara namba 8 kuna mauwaji yametokea ya Afisa wa UsalamaΒ akiwa anatoka kanisani” Ilikua ni sauti ya Mzee DawsonΒ iliyotawaliwa na utulivu sana
“Ooh God”Β
“Ndio hivyo Zola, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa wiki hiiΒ na kuendelea”Β
“Ngoja nielekee eneo la tukio” Inspekta Zola akajikusanya naΒ kuondoka pale akimuacha Mzee Dawson akiendelea kugida pombeΒ kali.Β
Yalikua ni majukumu yake ya kazi, akafika eneo la tukio naΒ kuukuta mwili wa Afsa aliyeuwa ukiwa juu ya daraja, gari yaΒ Afsa huyo ikiwa imesimama katikati ya Barabara na kusababishaΒ msongamano.Β
Taratibu za kiusalama zikaanza mara moja huku mwiliΒ ukichukuliwa na kupelekwa Hospitalini, mara simu ya ZolaΒ ikaingia ujumbe kutoka kwa wataalam wa Maabara kutoka kwenyeΒ kitengo cha Siri cha Mzee Dawson kilichoitwa MPA, akapewaΒ taarifa juu ya Maiti ya Robert na Bosco.Β
Milii ile ilikuwa ndio pekee yenye sura halisi tofauti naΒ Maiti ya Sandra ambayo ilikutwa na sura bandia, akajikutaΒ akiwa njia panda hajui aanze na lipi amalizie lipi, simu yakeΒ ikaingia ujumbe mfupi kutoka kwenye namba ambayo ilikuwa yaΒ siriΒ
“ZOLA TOKA ENEO HILO HARAKA SANA” Ujumbe ulisomeka hivyo,Β akajaribu kutafakari kwa kina lakini hakupata majibu kwaΒ haraka, akajaribu kuujibu ujumbe huo lakini hakufanikiwaΒ kupata majibu. Kwa akili yake ya kipelelezi akajuwa mara mojaΒ yupo Mtu anayemuona pale, haraka akaondoka pale na kuelekeaΒ kwenye gari lake ambalo lilikuwa kando na eneo lile, maraΒ akasikia mlipuko mkubwa. Alipogeuka akaona gari moja ikiwaΒ inawaka moto, ndio gari ambalo alikuwa karibu nalo paleΒ alipokuwa amesimama eneo la tukio.Β
Hapo akafanikiwa kujua kuwa kuna Watu wanamfuatilia kwaΒ karibu sana lakini akawa na maswali mengi kuwa ni naniΒ aliyemuokoa kwenye ile hatari? Mlipuko ulisababisha majeruhiΒ wengi sana ambao walikuwa ni Askari na wapita njia.Β
Alipofika kwenye gari yake akapata shahuku ya kutakaΒ kumfahamu aliyemuokoa kwenye kifo, akachukua simu yake naΒ kujaribu kuujibu ule ujumbe lakini hakupata majibu mengine,Β akamtafuta Mzee Dawson na kumtaarifu juu ya tukio hilo laΒ mlipukoΒ
“Aliyekuokoa anaitwa Pacho, ndiye msaidizi wako kwenyeΒ majukumu”
“Oooh! niliona kifo changu pale”Β
“Kuwa makini sana, Watu wa Usalama wanauawa sana….” yalikuaΒ ni maneno ya mwisho ya Mzee Dawson kisha simu ilikatika,Β ikampa wasaa Inspekta Zola kuelekea kwenye makazi yake yaΒ Siri karibu na ufukwe.Β
Masaa mawili baadaye yalimkuta Inspekta Zola akiwa amekaliaΒ kiti kwenye makazi yake ya siri, mbele yake kulikuwa na mezaΒ nyeusi ngumu iliyotengenezwa kwa kioo. Alionekana kuzamaΒ kwenye lindi la mawazo, akafikiria namna Muuwaji alivyokuwaΒ akifanya mauwaji kila kukicha, bado alitakiwa kujuwa ni wapiΒ alipo Sandra wa Ukweli kama Bosco na Robert ni Watu halisi,Β presha ya Rais ya kulazikisha kazi ifanyike upesiΒ ilimkasirisha sana.Β
*****************Β
Anga lilibadilika kuwa jeusi machoni pa Idara za usalama waΒ Taifa, Mauwaji ya Polisi na Maafisa yalitaarifiwa kila konaΒ ya Jiji, Hofu ikachukua nafasi kubwa kila mmoja akijiuliza niΒ nani atafuata Kufa. Ujio wa John Brain Nchini ulikuwa naΒ lengo moja kubwa, akakutana na Vijana wake wawiliΒ aliowatumainia sana mmoja aliyeitwa Six na mwingine aliyeitwaΒ Malaika akawaambiaΒ
“Wakati Polisi wanahangaika kutafuta ufumbuzi wa vifo hiviΒ vya utata sisi tutakuwa bize kumalizia mpango wetu hapaΒ Nchini, Rais wa Nchi hii alitutuma kazi na tumeimaliza sasaΒ kwanini idara yake inamshikilia Jamaal?” Alihoji John BrainΒ
“Huyu Kenge anayeitwa Zola atakuwa kikwazo kikubwa sanaΒ kwenye mpango huu, lazima aondoke kwanza” Alisema MalaikaΒ akakumbuka jinsi Inspekta Zola alivyo makiniΒ
“Udhaifi wa Zola ni Wanawake, kilevi chake kitamuuwa mudaΒ mchache ujao” Alisema John Brain aliyeonekana kujaza mamboΒ mengi kichwani pakeΒ
“Kazi hiyo niachieni mimi” Six akaomba apewe huo mpango waΒ kuondoa uhai wa Inspekta ZolaΒ
“Unatakiwa kuwa makini sana sababu kwa namna alivyo huyo MtuΒ si rahisi akamuamini Mtu kwa Mara ya kwanza, unapaswa piaΒ kujuwa kuwa ukibainika basi kila kitu kitaharibika. Zola niΒ Jasusi mbobezi, kabla hujampeleleza anakuwa tayariΒ amekupeleleza.” Alisema John Brain, kisha Malaika kasema
“Zola anatumika kama Mwanvuli wa Serikali katika kutekelezaΒ mipango ya siri, najiuliza aliwezaje kukwepa mtego wa Bomu”Β
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATUΒ USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Β Β
Β Β
9 Comments
First one
Huna Baya Mwanangu
βοΈβοΈ
Waaahπ
Doooh mambo mengi kwel
Imekaa poa sana
β₯οΈ
cn3qob
kg2pk7