Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-05

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Jasusi Sehemu Ya Nne (04)
    Hadithi

    Jasusi Sehemu Ya Nne (04)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaDecember 1, 2024Updated:December 2, 20249 Comments8 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Aaaah Zola” ilisikika sauti upande wa Mzee Dawson, ikioneshaย  alikuwa akijigeuza.ย 

    “Hebu fanya taratibu tuonane ana kwa ana Mzee Dawson, nahisiย  kuchanganikiwa sasa” Zola alikata simu bila kusikiliza sautiย  ya Mzee Dawson, baada ya hapo akapiga simu sehemu nyingineย  ndani ya kitengo cha siri cha Mzee Dawson kinachoitwa MPA,ย  akaomba madaktari waweze kufika eneo la tukio, akawapa Ramaniย  kamili lilipo eneo hilo.ย  Endelea

    SEHEMU YA NNE

    Hakuwa na muda wa kukaa pale, akatoka taratibu hadi nje,ย  akayaangalia vizuri mazingira yale kwa jicho na akili yaย  kipelelezi akajua tu kifo kile kimetokea masaa machacheย  yaliyopita na kwa vyovyote mwenye chumba kilichokuwaย  kinaangaliana na mlango lilikofanyika tukio atakuwa labdaย  amesikia au kuona chochote kile, akakumbuka kuwa mlango huoย  ulifungwa na funguo kuondolewa, akajiuliza haraka akiwaย  analitazama dirisha la Chumba jiraniย 

    “Kama funguo imetolewa maana yake kuna Mtu amefunga mlango naย  kumfungia Mtu ndani, Nani amefanya hivi?” Akapata akili yaย  kusogea chumba cha jirani, alipogonga akatoka yule Msichanaย  ambaye alimuelekeza chumbani kwa Anastanzia, yule Mdadaย  alipomuona Zola akaanza kujishebedua kwa kuhisi kuwa Zolaย  alikuwa akimtaka, alionekana kuvutiwa na Mzee Zola kutokanaย  na muonekana wa kitajiri alionao bila kujuwa kuwa alikuwaย  amesimama mbele ya Mtu hatari kwa upeleleziย 

    “Nilijua tu utakuja kwangu, Anastanzia sio aina ya Mwanamkeย  ambaye anakufaa wewe. Wazee kama nyie mnatakiwa kupetiwaย  vizuri ili msiwe na mawazo ya kufa kufa” Alisema hukuย  akitabasamu mbele ya Zola, kisha Zola akamuuliza yuleย  msichana

    “Mara ya mwisho umemuona Anastanzia lini?” Mdada akaachaย  kujishebedua baada ya Zola kuonesha sura ya mbuziย 

    “Wiki sasa sijamuona ila rafiki yake si umeonana nae? Maanaย  nimekuona ukitoka humo ndani” Zola akatoa kitambulisho chaย  uaskari akamuonesha yule mdada kisha akamuulizaย 

    “Unaitwa nani?” Mdada akawa anatetemekaย 

    “Naitwa Scolastica”ย 

    “Rafiki yake Anastanzia amekufa, naomba uniambie ni naniย  umemuona akiingia au kutoka mle ndani kabla yangu Mimi”ย 

    “Kulikuwa na Mkaka mmoja hivi, aliingia kisha akafunga mlangoย  akatoka, sikumuona tena”ย 

    “Anafananaje?”ย 

    “Mrefu kiasi, mweusi ana rasta”ย 

    “Sikia, watakuja polisi kuchukua mwili wa Marehemu, asanteย  kwa ushirikiano wako” Zola akaingia kwenye gari yakeย  akatokomea eneo hilo, akawasiliana na Mzee Dawson ili wapateย  kukutana na kuzungumza, Mzee Dawson kama kawaida yakeย  akamueleza Zola wakutane sehemu ya siri.ย 

    Alipofika Zola, Mzee Dawson aligundua ni jinsi gani Zolaย  alikuwa katika nyakati ngumu ambayo hakupata kumuona nayo,ย  akamimina mvinyo kwenye glasi na kumpatia, akapiga funda mojaย  la mvinyo ukawa umeisha kwenye Glasi, kisha akaitua Glasiย  hiyo mezani kama Mtu aliyechoshwa na kinachoendelea.ย 

    “Dawson! Hili jambo ni zito sana, kulifahamu lilipo kundi laย  Mafia Gang, na kuwajua Watu hao inakuwa kazi ngumu sana.ย  Sijui ni mafunzo ya namna gani watu hao wanapatiwa kabla yaย  kutekeleza jambo fulani” Alisema Zola huku akakunja midomoย  yake, akampa Glasi Mzee Dawson ili amuongeze mvinyo,ย  ukamiminwa mvinyo kwenye Glasi ya Zola haraka kisha Dawsonย  akakaa vizuri ili amjibu Zola, kwanza akajikoholesha kishaย  akasemaย 

    “Mauwaji yaliyofanywa na Mafia Gang huko Congo yanatishaย  sana, hapa bado kabisa hawajavuruga kisawasawa! John Brainย  kama lilivyo jina lake ni Mzungu hatari sana Zola, nahisiย  yupo hapa Nchini na kuna mpango wanautekeleza, umejaribuย  kufuatilia ni mafaili gani yaliibiwa na huyo Msichana katikaย  kituo cha polisi” Zola alitikisa kichwa kuashiriaย  hakufuatilia suala hilo, Dawson akapiga tena fundo la Mvinyoย  kisha akabeua kidogo

    “Zola ninayemjua Mimi hawezi kukosa kujuwa mambo kama hayo,ย  akili yako haipo kabisa Zola, John Brain ana akili sana naย  anachezea ubongo wako! Huenda ameshakujua na kukufuatilia,ย  anachofanya ni kukuchezesha, hapa kuna mambo mawili huendaย  yanafanyika kwa wakati mmoja”ย 

    “Mambo gani hayo?”ย 

    “Wananunua Muda wako na muda wa Wapelelezi wengine iliย  watekeleze mipango yao, hata haya mauwaji yanayotokea huwendaย  wanakuhadaa ili usipate muda wa kutuliza akili yako, wanajuwaย  wewe ni hatari kiasi gani, hilo lipo wazi Zola”ย 

    “Hili suala linaninyima usingizi Dawson, nahisi nipo katikaย  chumba chenye giza ambacho siwezi kuona kuna nini ndani yakeย  hata kusikia sauti inayonipa ishara, nahisi kushindwa”ย 

    “Ha!ha!ha! Zola, huwezi kukata tamaa mapema hivi, umekulaย  kiapo cha kulinda Taifa hili ikiwemo kupambana na Watu ainaย  ya John Brain, nafikiri muda unaenda, umekuja na gari yako?”ย 

    “Ndio”ย 

    “Tuitumie sasa hivi”ย 

    “Tunaenda wapi?” Aliuliza Zola huku akimtazama kwa makiniย  Mzee Dawson ambaye tayali alionekana kuwa ameshaanza kulewaย  lakini alimjuwa sawa sawa jinsi alivyo, akilewa huwa anaamuwaย  mambo kwa kutumia akili sana.ย 

    “Tunaenda Hospitali kuruhusu ile Maiti moja iliyosalia kwendaย  kuzikwa”ย 

    “Tutawapa vipi Maiti ambayo si yao, kumbuka ile ni Maiti yaย  Anastanzia na sio Sandra”ย 

    “Tunairudisha sura ya Bandia kama ilivyo Mwanzo, huu sioย  wakati wa wao kujuwa ukweli, acha waamini wanamzika Mtu wao”ย  Waliitumia gari ya Zola hadi walipofika Hospitali, tayariย  maiti mbili zilikuwa zimeruhusiwa kwenda kwa wahusika ambazoย  ni Maiti ya Bosco na Robert.ย 

    Wakasimamia zoezi la kuveshwa sura kwa Mwili wa Anastanzia,ย  dakika chache muonekano ulibadirika,ย 

    “Yes! Acha wamzike wanayemuamini huku sisi tukiwa bizeย  kufuatilia” Alisema Dawson kisha alikohoa kama kawaida yake,ย  Zola akampa kitambaa akawema mdomoni lakini alipokitoaย  ilionekana damu katika kitambaa hicho cheupe kuashiria kuwaย  mapafu ya Mzee Dawson yalikuwa katika hali mbaya

    “Usijali” akasema Dawson, kisha Zola akapiga simu kwenyeย  familia ya Mama Sandra ili waende kuuchukuwa mwili walioaminiย  ni wa Sandra ili wakauzike.ย 

    “Naingia kazini sasa Zola, tuna muda mchache sana kuhakikishaย  Nchi inakuwa shwari” alisema Dawson na kumfanya Zolaย  atabasamu maana mzigo ulikuwa ukimuelemea sana. Sikuย  iliyofuata Mazishi ya Sandra yalifanyika, Zola alikuwaย  miongoni mwa waliohudhuria lakini uwepo wa Zola msibaniย  ulikuwa na melengo makuu mawili, moja kuhakikisha familiaย  haitambui kama anayezikwa si Sandra, jambo la pili aliaminiย  kama Mpango ule ulisukwa basi wasukaji wangefika pale Msibaniย  kwa ajili ya kufuatilia, lakini Pia Zola alimtilia shaka Babaย  yake Sandra akiamini anajuwa jambo fulani.ย 

    Akiwa ameketi alivalia miwani nyeusi na sura ya Bandia kamaย  alivyoambiwa na Mzee Dawson kuwa Huenda Mafia Gangย  wameshamjuwa ndio maana walitaka kumuuwa katika jaribio laย  bomu, hakutambuliwa na yeyote pale lakini alionekana kuwaย  miongoni mwa waliokuja Msibani, Watu walikuwa wengi mno. Kifoย  kile kilishika mioyo ya wengi.ย 

    Naam!! Zola alikuwa bize sana kuhakikisha anazungusha machoย  yake kila kona, macho yake yakajikuta yametua kwa jamaa mmojaย  ambaye naye alikuwa bize sana kuzungusha macho yake, Zolaย  hakufanikiwa kugundulika baada ya kubadilisha sura kishaย  kuvaa miwani, ingehitaji utaalam mkubwa sana kumtambua.ย  Kilikuwa ni kipindi ambacho Msemaji wa Familia alikuwaย  akiwashukuru Watu waliokuja pale kwa ajili ya maziko yaย  Sandra ambaye alizikwa pale pale nyumbani kwao, Zola hapoย  ndipo akajithibitishia kuwa familia ya Sandra haikusanukaย  kuwa walikuwa wakizika Maiti ya Mtu mwingine, lakini hakusitaย  kukubali uwezo wa Maadui zao ambao walifanikiwa kuuhadaaย  ulimwengu wa vipofu ambao macho yao hayakuweza kuona mbaliย  zaidi ya Jicho la kipelelezi lenye mafunzo ya kijeshi ambaloย  Zola alikuwa nalo.ย 

    Kwa mantiki hiyo, Maadui walifanya tafiti zao kabla yaย  kumtumia Anastanzia kuvaa sura ya Sandra maana miili yaoย  ilifanana sana ndio maana hawakuweza kuhisi kama kuna tatizo,ย  akashusha pumzi zake, alijuwa ilitumika akili kubwa sana paleย  hadi Anastanzia akaingizwa kwenye mwanvuli ule wa Umauti,ย  swali lililomjia akilini mwake haraka ni wapi alipo Sandraย  mwenyewe?. Aliporejesha macho eneo la yule jamaa aliyekuwaย  akimfuatilia, aliona kiti kikiwa kitupu kabisa, akaangazaย  huku na kule bila mafanikio yoyote ndipo akaona ni bora atokeย  nje ili apeleleze yule jamaa ni nani na kwanini alikuwaย  akichezesha yale macho ya kipelelezi, akamkubuka sawasawaย  jamaa huyo mwenye upara na ndevu nyingi.

    Alinyanyuka kutoka kitini kama Mtu aliyemaliza tukio laย  mazishi, hakutaka kuonesha dalili zozote kuwa alikuwaย  akifuatilia chochote maana aliamini Maadui walikuwepo paleย  Msibani, akiwa anatoka aligongana na Mwanamke mmoja mrefu,ย  mweupe na mwenye nywele nyingi.ย 

    “Samahani?” Alisema Mwanamke huyo ambaye alikuwa na uzuri waย  kutosha, macho ya Zola yakautalii mwili wa Mwanamke huyo bilaย  staraย 

    “Usijali!” Akasema Zola kisha akatoka pale taratibu bilaย  kugeuka nyuma.ย 

    Yule Mwanamke alimtazama sana Zola hadi alipozama, kishaย  akaketi kitini. Zola alipofika nje alimuona yule jamaaย  akizungumza na simu kisha akaingia kwenye gari, Zolaย  hakuchelewa naye akaingia kwenye gari na kuanza kumfuatiliaย  jamaa huyo ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote uleย  maana hata alivyoendesha gari hilo ilionesha wazi kuwaย  alikuwa katika hali ya kawaida, akaingia Barabara ya tanoย  kisha akashika barabara kuu ambayo ilikuwa ikitoka Uwanja waย  ndege kuelekea eneo ambalo lilikuwa na Hoteli nyingi za nyotaย  tano.ย 

    Bila kupoteza muda Zola alimpigia Dawson simu, akamuelezaย  hali ilivyo kisha akasubiria jibu la Mzee huyo.ย 

    “Washa GPS ya Gari” ilisikika sauti kutoka upande wa pili,ย  ikampa ishara Zola kuwa Mzee Dawson alikuwa na maelekezoย  maalum ya nini cha kufanya.ย 

    “Nakuona!” Alisema Dawson kisha alikata simu mara moja, baadaย  ya dakika tano akampigia tena na kumwambiaย 

    “Fuata maelekezo yangu, kuwa makini hao Watu wana akili yaย  ziada sana wakati mwingine Watu hawaamini kama Huyo Mzungu niย  Binadamu, wana akili iliyozidi…unaweza kuwa umetegwa, kablaย  ya kutoka Msibani hakuna ishara tata?” Alimpa wakati waย  kufikria, Zola akasemaย 

    “Nilikuwa makini kuliko kawaida, hakuna aliyeniona ila wakatiย  natoka…” Ukimya ukatawala, Mzee Dawson akamuuliza Zolaย 

    “Enhee ilikuwaje?” Zola akafikiria alipokuwa akitoka paleย  aliparamiana na Mwanamke mmoja mzuri sana, hakutaka kulisemaย  hilo akiamini sio ishara ya kumueleza Mzee Dawsonย 

    “Sio ishara!”ย 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TANOย  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย 

    ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx

    jasusi riwaya za kijasusi

    9 Comments

    1. Calvin paul on December 1, 2024 6:14 pm

      Ukalii umepamba moto

      Reply
    2. Deogratias on December 1, 2024 6:17 pm

      Jasusi anajasusiwa. Noma sana

      Reply
    3. Verena on December 1, 2024 6:52 pm

      Aiseeeee hatar

      Reply
    4. Charz jr๐Ÿ˜Ž on December 1, 2024 9:27 pm

      โœŒ๏ธโœŒ๏ธ

      Reply
      • GUEVARA on December 1, 2024 10:06 pm

        Thank a lot, kazi nzuri

        Reply
    5. Cathbert on December 2, 2024 5:39 pm

      Iko poa xnaaa

      Reply
    6. Afrasia on December 2, 2024 11:29 pm

      Zola!ยก!!

      Reply
      • Ramadhan Kisalawe on December 9, 2024 2:32 pm

        Ni ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

        Reply
    7. Fawziya Hassan on December 6, 2024 11:56 am

      ZOLA AKIWA KAZINI

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 17, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-05

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya nne Wakiwa wanaendelea kujibizana, walianza kusikia sauti ya Bi.…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.