Robert akiwa kwenye gari lake alianza kulia, akashindwa hataย kuendesha akaamua kusimama kando ya Barabara akiwaย anabubujikwa na machozi.ย
Machozi yakawa yanamtiririka Robert huku akizidi kulia kwaย uchungu mkubwa, jua lilikua likiwaka huku Watu wakiendelea naย shughuli zao lakini kwa Robert ilikua tofauti sana, alijikutaย yupo kwenye kisa chenye utata sana.ย
Alikua amevalia Suti nyeusi, kiatu cheusi lakini sura yakeย hofu na hali ya majuto ilikua imetanda sana. Akajikutaย akipiga usukani kutokana na hali aliyokuwa nayo, akageukaย nyuma ya gari.ย
Kulikuwa na Mwili wa Mtu uliokuwa ukivuja damu, mwili huoย hapana shaka ulikuwa ni wa kike kwani ulikuwa na vazi laย Shela.ย
Robert akaliondoa gari pale kando ya ile barabara, sasa akawaย barabarani kuelekea alipokusudia huku ile hali ya kulia ikiwaย imekata. Simu yake ilikua ikiita mno lakini hakutakaย kuipokea, Alipofika mbele akaachana na barabara kuu akaingiaย barabara ya vumbi ambayo ilikua ikielekea ufukweni.ย
Robert alipofika juu ya kilima akaongeza mwendoย akalitumbukiza gari hilo ndani ya bahari na kuzua taharukiย kwa Watu waliokuwa upande mwingine wa ufukwe, kelele naย taharuki vikaamka pale Ufukweni, Watu wa uokozi wakawa tayariย kwa ajili ya kuzama majini kulitoa gari hilo.ย
Kwa muda mfupi lile gari lilikuwa limezama ndani ya yale majiย ya Bahari ambapo kwa upande ule kulikuwa na kina kirefuย ambacho Watu walikuwa hawaendi kuogelea, Punde polisi wakajaย pale huku Watu wakiendelea kupigiana simu kuwa kuna gariย limezama ndani ya Bahari, kilikuwa ni kituko kwa kilaย aliyesikia, kila Mtu akataka kujua ilikuwaje.
Polisi wakazungusha utepe wao kuashiria kuwa eneo hiloย halikuwa salama kwa wakati huo, ziliwachukua zaidi ya dakikaย 45 waogeleaji kuchopoa miili miwili. Moja ilikuwa ni ile yaย kike na nyingine ilikua ni ya Robert, gari ya huduma yaย kwanza ikaichukua miili ambapo yote ilikuwa tayari hainaย uhai.ย
Taarifa hii ikawa na mkanganyiko mkubwa kwa Watu walioisikia,ย haikuhitaji uchunguzi mkubwa sana kugundua kuwa walikuwa niย Wanandoa au watarajiwa, mwili wa Mwanamke ulikutwa na risasiย shingoni.ย
“Ufanyike uchunguzi haraka sana kuhusu hili tukio” Akaagizaย mkuu wa Upelelezi.ย
- โขโขโขโขโขโขโขโขย
Vilio vilikuwa vimetanda ndani ya kanisa moja lililopoย katikati ya Jiji, tayari polisi walikuwa wamefika na kuukutaย mwili mwingine uliokuwa umejeruhiwa kwa risasi, ulikuwa niย mwili wa Mwanaume mmoja ambaye alitambulika kama Bosco, nayeย alikuwa amevalia suti.ย
Polisi wenyewe walipigwa na butwaa kwa jinsi hali ya vilioย ilivyokua imetanda ndani ya kanisa hilo kubwa na lenye hadhi,ย Watu wengi walikuwa wakisimuliana kilichotokea hapo.ย
Mama mmoja alikua akilia kwa uchungu huku akiutikisa mwili waย Bosco uliokuwa umeloa damu, shati jeupe alilovaa lilikuaย limetapakaa damu mno.ย
“Mwanangu mimi! Eeeh Mungu mtihani gani huu umenipa mimi leoย tena mbele ya Kanisa” Sauti ya kilio iliyotoka kwa kwikwiย ilimtoka Mama huyo, mmoja wa Askari akapata shahuku yaย kumfuata huyo Mama.ย
“Pole Mama!” Akasema huku akiwaambia watu wa Huduma ya kwanzaย wauchukue ule mwili kwa ajili ya taratibu za kiupeleleziย zaidi.ย
Lilikua ni pigo lililoamsha kilio chake, Mwili wa Boscoย ulikuwa ukiwekwa kwenye gari maalum kwa ajili ya kuupelekaย Hospitali, mkononi Askari huyo aliyejitambulisha kamaย Inspekta Zola alikua ameshikilia karatasi yenye majina yaย Watu waliopoteza Maisha kwenye kisa kile cha kutisha. Jina laย Robert lilikua la kwanza, la pili ni Sandra na la tatu niย Bosco. Akajiuliza Watu wale walikua kwenye kisa ganiย kilichopelekea vifo vyao.
Akamfwata Mtu mmoja aliyekua amekaa kando, alikua amejitengaย sana na wengine. Kupitia jicho la Kipelelezi Inspekta Zolaย akagundua jambo, alipomfikia akamuulizaย
“Nini kimetokea?” Ilikua ni kama vile ameamshwa kutoka kifo,ย akajikuta akishtuka sana. Naam! alikuwa ni Mdada mwenye suraย ya upole, mweupe mwembamba, kwa jinsi alivyovaa ilikua rahisiย kutambua kuwa hakua miongoni mwa Watu waliofika kwa ajili yaย ile shughuli pale Kanisani.ย
“Unaitwa nani?”ย
“Judith!!”ย
“Huonekani kama mmoja wa Waalikwa hapa, kimekuleta nini?”ย Swali hili likaambatana na jicho kavu la kipeleleziย
“Mimi?”ย
“Ndio wewe kwani naongea na nani?” Mdada akakaa kimya bilaย kujibu chochote huku akionesha kutetemeka, Yule Askariย akamchukua Mdada kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja naย baadhi ya Watu ambao walitambulika kama ndugu wa Bosco ambayeย amefariki kwa kupigwa risasi.ย
Ilikua ni siku ya majonzi sana, vilio vilitanda hadi kituoย cha polisi ambapo baada ya polisi kuwataka watulie ndipoย vilio vilipokoma.ย
“Nini kimesababisha vifo vyao?” Aliuliza Inspekta Zola ambayeย alikua makini, mbele yake kulikua na Ndugu zake Bosco naย wengine ambao walijitambulisha kama ndugu wa Sandra, yuleย Mdada alikua amekaa pembeni akiwa katika hali ya hofu.ย
“Inatisha na kusikitisha Afande, marafiki walioshibana leoย wanauwana” akaongea Mama yule ambaye alifahamika kama Ndiyeย Mama yake na Bosco, kilio kilianza tena ikabidi sasa Inspektaย Zola amuondoe Huyo Mama kwasababu asingeliweza kuzungumzaย chochote zaidi ya kilio.ย
“Nini kimetokea?” akauliza tena Inspekta Zola akiwatazamaย walioko mbele yake, mmoja akatikisa kichwa ishara ya kuwaย hajui hasa kilichosababisha vifo vya Watu watatu, Inspektaย Zola akapata wazo la kumuuliza yule Mdada, akamuitaย
“Nini kimetokea?” Akamuuliza yule Mdada ambaye hata baada yaย kuulizwa alikaa kimya kwa kitambo kidogo kabla ya kuanzaย kuzungumza.ย
Chozi likianza kumbubujika akajikuta akianza kuongea.
“Mapenzi! Najiuliza kwanini yameumbwa, kwanini yanatesa,ย yanafanya Watu wawe maadui, watu wapoteze furaha walizonazo!ย Ni mapenzi” Kila mmoja alikaa kimya baada ya huyo Mdadaย kuanza kuzungumza, Familia zote zilizopo pale polisi zilikaaย kimya kumsikiliza Mtu ambaye hawakumfahamu.ย
“Huyu ni Muongo” Akadakia Dada Mmoja aliyekuwa akibubujikwaย machoziย
“Hebu subiri aongee alafu sisi tutapima maneno yake kamaย yamejaa ukweli au uwongo” akaongea Inspekta Zolaย
“Nawaomba polisi mufanye kazi yenu lakini sio kusikilizaย maneno ya Mtu huyu, Mdogo wangu Sandra hakuwahi kuingiaย kwenye vita ya Mapenzi, anaongea Uwongo Mtupu…”ย
“Mpaka hapa tunapozungumza hakuna aliye hai ambaye anayewezaย akatueleza kilichotokea, ni vema tukamsikiliza huyu Binti”ย
“Una maanisha nini? Mdogo wangu Robert amekufa?” akauliza kwaย Mshituko kuhusu Robert ambaye mwili wake uliopolewa Bahariniย baada ya kulitosa gari lake ndani ya Bahari.ย
“Sandra na Robert wamekutwa wakiwa tayari wamekufa ndani yaย maji, ndio maana nasema tukae kimya kumsikiliza ili kama kunaย ukweli unazungumzwa basi ndio utatupa uelekeo wa kujua chanzoย cha vifo hivi vya Kutisha” Akajibu Inspekta Zola, taarifaย ikaamsha tena vilioย
“Nilijua Robert atakuwa salama jamani”ย
“Nini kimetokea Robert Mwanangu…Nini Babaaa??”ย
“Bosco mlikuwa mnaficha nini kwenye maisha yenu wanangu?”ย Zilikuwa ni sauti zilizojaa vilio hadi Inspekta Zola akaamuruย sasa watolewe nje ili afanye mahojiano na huyo Mdada ambayeย alionesha kufahamu baadhi ya mambo!ย
“Judith sitaki uingie matatizoni, unaonekana sio mtuย mbaya…sura yako inaonesha hujahusika kwenye jambo hiliย lakini unafahamu kitu..lisaidie jeshi la polisi, niniย kimesababisha vifo hivi vya kutisha na ilikuwaje paleย kanisani?” Chozi likaanza kumbubujika Judith akiwa anamtazamaย Inspekta Zola ambaye alikua makini kusikiliza atakachoย kisema.ย
“Judith…unafahamu nini kuhusu Maisha ya Bosco, Sandra naย Robert?” akauliza tena Inspekta Zola lakini bado Judithย aliendelea kulia.
“Mapenzi yamefanyaje Judith? wewe ni sawa na binti yangu naย huwa naumia sana kumuona Binti kama wewe ukiingia kwenyeย matatizo”ย
Judith akajifuta mchozi uliokua ukitiririka kwenye mashavuย yake akavuta hewa kama Mtu mwenye mafua kisha akamkodoleaย macho Inspekta Zolaย
“Tupo mimi na wewe tu, tuongee kama Mtu na Baba yakeย Judith…Nini kimetokea?” Kauli hii ikamfanya Judith avuteย hewa, akajisikia uhuru fulani wa kuzungumza. Macho yaย Inspekta Zola yaliyokomaa Kijasusi yakawa yana Mmulika Judithย ndani ya Chumba kimoja cha mahojiano.ย
“Unawafahamu vipi hawa Watu?” aliuliza tena Inspekta zolaย tena bila kuchokaย
Judith akanyanyua kinywa chake ili aanze kuelezaย kilichotokea, mara mlango ukafunguliwa akaingia Polisi mmojaย aliyevalia sare za kipolisi, akapiga saluti kwa Inspektaย Zola.ย
“Ripoti ya uchunguzi wa miili ya Marehemu wote Watatu”ย Akaongea polisi aliyeingia, akamkabidhi baasha Inspekta Zola,ย akaifungua ili asome ripoti hiyo.ย
Akazisoma ripoti zote lakini ripoti ya mwili wa Sandraย ilimshangaza kidogo licha ya kukutwa kwa risasi sehemu yaย shingo pia Mwili ulikutwa na tatuu ya jina la Bosco upande waย kulia wa paja lake lakini pia upande wa kushoto wa paja lakeย lilikutwa jina la Robert. Inspekta Zola akamtazama yuleย polisi kisha akarudisha macho yake kwa Judith, akawa naย maswali mengi yaliyohitaji majibu ya haraka.ย
“Sandra alikua na mahusiano na Bosco na Robert kwa wakatiย mmoja?”ย
“Ndio”ย
“Je, Robert na Bosco walikua wakijuana kwenye penzi laย Sandra?”ย
“Hapana”ย
“Walikua marafiki walioshibana sasa waliwezaje kuishi kwenyeย penzi la Mtu mmoja?” Akauliza Inspekta Zola, kisha akatazamaย saa yake tayari usiku ulikua umeingia.
“Afande utahakikisha anakua salama huyu binti hadi keshoย asubuhi” akasema Inspekta Zola kisha akaondoka zake paleย kituo cha polisi, Judith akachukuliwa kwa maelekezo maalum yaย Inspekta Zola akapelekwa sehemu ili apumzike ndani ya kituoย kile cha polisi.ย
- โขโขโขโขโขโขโขโขย
Nyumbani kwenye familia ya Robert bado vilio vilikuaย vimetawala kila mmoja akijiuliza Robert alikua amepatwa naย nini hadi akawapiga risasi Sandra na Bosco, wote walishuhudiaย tukio hilo ndani ya kanisa. Ndugu walikua wakifika kwa ajiliย ya mazishi ya Robert, pia upande wa Bosco hali ilikua hivyoย hivyo, pia kwa Sandra hali ikawa hivyo hivyo.ย
Hakuna aliyejua hasa sababu ya Marafiki hawa walioshibanaย kuangukia kwenye kivuli cha Umauti.ย
Baada ya kutoka kituo cha Polisi Inspekta Zola akaelekeaย nyumbani kwake, siku hii hakuwa katika hali ya kawaida baliย kwenye tafakari nzito kuhusu kisa kile kizito ambacho kilikuaย mikononi mwake. Taarifa iliyopo kwenye meza yake ilikua niย Robert kumpiga risasi Bosco, kisha kumpiga risasi Sandra naย kwenda kujitosa ndani ya Bahari.ย
Akiwa kwenye chumba chake maalum kwa ajili ya upeleleziย akaanza kuvuta picha tofauti tofauti ambazo alikuaย akizifikiria lakini hakufanikiwa kupata picha halisi ya tukioย lile, umri wake wa miaka 60 ulitosha kumwambia kuwa kisa kileย kilikuwa na simulizi ya kusisimua ndani yake.ย
Akachukua karamu na karatasi akaandika ” ROMEO NA JULIET”ย kisha akafuta kwa kuamini kuwa visa hivyo ni tofauti,ย akamaliza kwenda kitandani na kujitupa, akajigalagaza hadiย Usingizi ulipomchukua.ย
Asubuhi jua likiwa tayari limetoka akaamshwa na mlio wa simuย yake ya mkononi iliyokua pembezoni mwa Kitanda chake. Akaamkaย na kuipokea, akajua kuwa siku ilikua imeanza. Akajiandaa naย kuelekea kituo cha polisi, akaelekea moja kwa moja chumba chaย mahojiano akamkuta Judith akiwa anamsubiria.ย
Kabla hajaanza na Judith, akaikuta baasha pale mezani, hapanaย shaka ilikua ikimsubira yeye. Alipofungua akakutana na ujumbeย mwingine uliomkata maini yake, Naam! haraka akachomoka paleย na kumuacha Judith akiwa kwenye uangalizi, akachukua gariย yake ndogo na kuelekea Hospitali ambako maiti zilikuaย zimehifadhiwa.
Akaiomba maiti ya Sandra, ikaletwa kwenye chumba maalum kishaย paja la Sandra likafunuliwa, akaiona Tatuu yenye jina laย Bosco kisha akaifungua ile taarifa iliyopo kwenye baashaย akagundua ufanano wa jambo fulani, pale pale simu yakeย ikaita. Akaweka miwani yake vizuri kisha akaipokea hiyo simuย
“Zola! nafikiri umeupata Ujumbe wangu, Haraka sana anza naย upelelezi wa kina…Hawa marehemu watatu huenda wakawaย wanahusika na kifo cha Makam wa Rais” Ulikuwa ni ujumbe tataย sana kwenye kichwa cha Inspekta Zola, jasho likawa linamtoka.ย
“Inawezekanaje? Wauwaji wakauwana wenyewe kwa wenyewe?”ย Akauliza Zolaย
“Zola, fanya upelelezi wako upesi. Idara yangu ya Usalama waย Taifa inakuamini sana ndio maana sijaona Mtu wa Kumpa hiyoย kazi zaidi yako”.ย
“Oooops! sawa Mkuu” Akajibu kwa utiifu wa hali ya juu sana,ย Hofu ikatanda na hali ya tahadhari ikapanda kwenye kichwa chaย Inspekta Zola, akajua sasa alikua kwenye kazi rahisiย iliyogeuka kuwa ngumu kupita maelezo.ย
Kwenye Tatuu ya Jina ka Bosco kulikua na alama ya vidoleย viwili, alama hii ilikua maarufu sana miezi michacheย iliyopita baada ya kutokea kwa vifo vingi vya Watu waย Usalama, na viongozi wa juu wa Serikali, kila aliyeuawaย alikutwa na muuli wa alama ile ya Vidole, hapo ndipo wasiwasiย ulipoibuka baada ya kukutwa kwa Tatuu kwenye mwili wa Sandra.ย
Mara moja simu ya Inspekta Zola ikaanza kuita, ilikua ni simuย kutoka kituo cha Polisi.ย
“Unasemaje?” akauliza Inspekta Zola akiwa amesimama kando yaย maiti ya Sandraย
“Nakuja haraka sana” akasema Zola kisha akachukua gariย kurejea kituo cha Polisi, akasikia Milio ya gari za kubebeaย wagonjwa kutoka kituo cha polisi, maiti zilikua zimezagaaย eneo la kituo cha polisi.ย
Zola hakuamini macho yake, Polisi mmoja akamfwata Zola naย kumwambia kuwa yule Binti aliyekuwa akihojiwa ndani ya kituoย hicho ndiye aliyekuwa amesababisha madhara yaleย
“Inawezekanaje binti dhahifu kama yule awashinde zaidi yaย Askari 15 na kuwauwa wote?” Akauliza Zola huku akiwaย anatazama jinsi maiti zilivyokuwa zikichukuliwa na kuwekwaย kwenye Magari ya kubebea wagonjwa.
“Inspekta, Binti anaonekana kuwa na mafunzo ya kimapigano naย ujasusi wa hali ya juu sana” Baada ya kusikia hivi Inspektaย Zola akaelekea ndani ya kituo, damu zilikua zimetapakaa hukuย matundu ya risasi yakiwa kwenye miili ya askari waliokuwaย tayari wameuawa.ย
“Amechukua baadhi ya nyaraka kwenye masanduku” akaongezaย askari ambaye alikuwa akimfwata Inspekta Zola kwa nyuma,ย akaingia moja kwa moja hadi kwenye kile chumba cha mahojianoย ambacho alimuacha yule Mdada aliyejitambulisha kama Judith,ย akaona kuna ujumbe juu ya meza, akaufungua ukiwa kwenyeย baasha akakutana na ujumbe ulioandikwa “KIVULI CHA UMAUTI”ย alafu alama ile ya vidole ikawa chini ya maneno hayo.ย
“Uuupsss” Akashusha pumzi kisha akaketi kwenye kiti naย kuegemea ile mezaย
“Ngoma hii ni ngumu sana kuicheza” akajisemea kwa sauti kuuย huku akitikisa kichwa chake.ย
- โขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโข
Ndani ya Jengo moja refu zaidi katika Jiji hili, kulikuwa naย jamaa mmoja aliyeitwa Six, alikua ameketi huku akivuta sigaraย yake, mwili wa Six ulikua na tatuu nyingi sana za rangi, simuย yake ilikua bize sana akionekana kupokea na kutoa taarifa.ย
Mara akaingia Judith Mdada ambaye alikua kwenye kile kituoย cha polisi, alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo. Akafikiaย kuketi kwenye sofa karibu na Six, Six akatikisa rasta zakeย
“Mbona uko juu juu sana?” Akauliza huku akizima sigara yake,ย akatoa moshi mwingi mdomoniย
“It’s a bit Strange ( Inatisha kidogo )”ย
“Kumetokea nini?”ย
“Walinishtukia ikabidi nipambane kujiokoa pale”ย
“Oooh! Shit” Six akaongea kwa hasira sana, Mdadaย aliyejitambulisha kwa polisi kama Judith akavua sura yaย bandia.ย
“Hawajafanikiwa kukufahamu?”ย
“Yes! hawajanifahamu”
“Ok! Malaika usiye na dhambi” akaongea huku akiwa anapokeaย nyaraka zilizoibwa ndani ya kituo cha polisi.ย
Nje kidogo ya Jiji hili, Inspekta Zola alikua akipokea kaziย kamili ya kuwasaka waliokuwa wakifanya mauwaji ikiwemo kifoย cha Makam wa Rais ambaye alipigwa risasi akiwa nyumbani kwakeย na kuzua taharuki kubwa.ย
Mbele yake alikua amesimama Mtu mmoja mwenye umri sawa naย wake, wote walikua Wazee wenye utaalam wa upelelezi, Mzeeย huyu alijulikana kama Dawson maarufu kama Google. Jina hiliย la utani alipewa sababu ya taarifa nyingi alizonazo ndani yaย kichwa chake, licha ya Mzee Dawson kuwa Mtu wa Usalama waย Taifa pia alikua ana kitengo chake cha Siri alichokipa jinaย la MPA ambacho kilikua kikidili na masuala ya Upelelezi waย kesi kubwa kubwa ndani na nje ya Nchi.ย
Walifanana sana tabia zao, walikua walevi wa sigara naย nyakati fulani walikua wakitumia pombe kali, ilikua niย kawaida kwao tangu wakiwa vijana kwani kazi waliyokuaย wakiifanya iliwafanya watumie akili nyingi ili kupambana naย uharifu,ย
“Kuna kundi linaitwa MAFIA GANG, ni kundi maalum kwa ajili yaย Ugaidi…Mkuu wa kundi hili anaitwa John Brain ni mzunguย anayeishi Uskochi, Kazi yake ni kuratibu mauwaji. Amefanyaย kazi katika Nchi nyingi na sasa yupo hapa Nchini ndiyeย anayeratibu mauwaji ya viongozi kwa maslahi yake binafsi.ย Mwaka 2003 nchini Congo walifanya mauwaji mengi sana,ย nakuamini Zola ndio maana nataka ufanye upelelezi wa kina,ย ukomeshe kabisa kundi hili hapa Nchini” Yalikua ni maneno yaย Mzee Dawson yalitoka na moshi wa sigara.ย
“Kila kitu kipo tayari kwa ajili yako Zola, unahitajiย kuikomboa Nchi yako. Nakufahamu vizuri linapokuja suala laย kesi tata” Akamaliza kwa kumtakia kila la Kheri kwenye jukumuย lake zito la kuliondoa kundi la MAFIA GANG lakini kichwaniย bado alikua anauwaza ule mkasa wa akina Robert, akajiulizaย waliingiaje huko na nini kilipelekea wauwane.ย
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA PILIย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
ย ย
18 Comments
Narudi tena kusoma hadithi baada ya kusoma riwaya ya MSALA aina hii ya stories ndo napenda mim
Nimependa nimependa
Kitu kitamu sana
Tambara kama hili nikipewa Scene nauwa sana yani sema ndo ivo hatuna nyenzo huku kwetu๐
Tam saaana hiiii
Imekaa poa sana
Naisi hii hii itakua kali kama…MSALA…maana ile ilikua kali kuliko zote๐
Mambo ni ๐ฅ
Asante Mtunzi na Admin
More Love from Kenya โค๏ธ
Aaha kubandika na kubandua
๐๐
Tamuuuu
https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J
Tunasubiri nyungine mkuu
SAWA sawaa
Tunaomba t mwendelezo Admin unatucheleweshea utamu
Tunaomba muendlezo admin adi tutasahau story sasa dah
Very nice
Kitu fire..