Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Hapa MSUVA Pale MPENJA Ofa Kibao Kutoka LEONBET

    In the name of LOVE – 12

    In the name of LOVE – 11

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Jasusi Sehemu Ya Kumi (10)
    Hadithi

    Jasusi Sehemu Ya Kumi (10)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaDecember 7, 2024Updated:December 9, 202415 Comments12 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Hayo ni majina ya Watu wa siri wa Mzee Dawson, Sande yupoย  hai, moja ya kaburi hapo linaweza kuwa kaburi la Zola,ย  fukueni haraka sana.” Ilisikika sauti ya John Brain, aliaminiย  Dawson ni Mtu mwenye akili sana kwenye mambo yake.ย 

    Mengine yalionekana kuwa ya zamani sana lakini moja lilikuwaย  bado jipya, wakalifukua hilo kwa kutumia chepe iliyo kwenyeย  kona ya chumba hicho chenye makaburi. Kazi hii ilifanywa na Six aliyekuwa amebana rasta zake kwa nyuma. Jasho lilikuwaย  likimtoka, harufu kidogo ilianza kutapakaa pale, haikuwazuiaย  kufanya kazi yao. Endelea

    SEHEMU YA KUMI

    “Oooh Shit!” Alisema Six huku akitema mate, Malaika ilimbidiย  asogee paleย 

    “Duuh! Kweli huyu jamaa alipitia mafunzo makubwa sana”ย  Alisema Malaika, mwili huo ulikuwa umeharibiwa kwa kemikaliย  maalum ambayo iliwafanya akina Six washindwe kuitambuwa suraย  hiyo, wakati wanaendelea kushangaa tukio lile Malaika alionaย  kitu kama redio Call hivi kando ya aliposimama tena ikiwaย  imefukiwa kidogo, akaifuata na kuiokota akakuta redio hiyoย  ikiwa inafanya kazi.ย 

    Haraka Malaika akakimbilia alipoliacha begi lake, akatoaย  Laptop na baadhi ya vifaa fulani kisha akavaa Head Phone,ย  akawasha kitu fulani kutoka katika Laptop yake akaona mawimbiย  ya redio hiyo yakiwa yanatoka kando ya Bahari ya Hindi.ย 

    “Umefanikiwa kugundua chochote?” Aliuliza Six akiwaย  ameshikilia chepeย 

    “Eneo ulipo mtambo wa redio hii ni kando ya Bahari ya Hindiย  upande wa Mashariki”ย 

    “Inaweza kuwa mhusika wa andaki hili yupo huko, kama niย  Dawson basi arobaini yake imefika” Alisema Six kisha kwaย  pamoja wakapanda juu kutoka katika lile andaki wakijiandaaย  kufuata mawimbi hayo. Walipotoka wakakutana na wauminiย  waliokuwa wamesimama nje ya andaki hilo, walionekanaย  kushangaaย 

    “Nani amechimba andaki hili hapa?” Aliuliza Malaika hukuย  akiwa ameshatoa kitambulisho feki walichopewa na Rais iliย  waonekane ni Watu wa Usalama wa Taifa. Macho ya watu haoย  yalionekana kujawa na woga wakawa wanasakiziana kujibu, mmojaย  akasikaka akisemaย 

    “Hatukuwahi kuona wala kuhisi uwepo wa shimo hilo, kwa miakaย  mingi nimeishi hapa lakini hili shimo sijawahi kuliona”ย  Alisema huku akitikisa kichwa chake, alionekana kuwa Mzeeย  sana mwenye mvi nyeupe zisizo na matunzoย 

    “Kanisa hili limejengwa lini?” Aliuliza Sixย 

    “Miaka 15 iliyopita”

    “Nani alihusika na ujenzi wake?” Six aliuliza tena,ย  alichotaka kusikia ni jina la Mzee Dawson likitajwa ili waweย  na uhakika wa wanachoenda kufanyaย 

    “Mfadhili alishafariki miaka mitatu baada ya kanisa hiliย  kukamilika” Alijibu tena yule Mzee ambaye alijibebesha mzigoย  wa kujibu maswali ya Sixย 

    Walipoona hawawezi kupata walichokuwa wanakitaka waliondokaย  haraka eneo hilo ili kuanza safari ya kuelekea Kando yaย  Bahari ya Hindi upande wa Mashariki, upande huu ndiko ambakoย  nyumba ya siri ya Marehemu Zola ilijengwa.ย 

    Kitendo cha Six na Malaika kuondoka kilimpa mwanya yule Mzeeย  akawaacha wenzake wakiendelea kushangaa uwepo wa andakiย  kanisani, akaenda nyuma kabisa ya kanisa hilo, alihakikishaย  hakuna aliyemuona tena akionekana kuwa mwenye wasiwasiย  Mkubwa.ย 

    Akawa anatafuta kitu ardhini kwa kukita mguu wake, alifanyaย  hivyo kwa dakika kadhaa hadi alipokita mahali aliposikia kamaย  kuna sauti inamuitikia, ilikuwa ni sauti iliyoashiria uwepoย  wa kitu fulani sehemu hiyo, akafukua kwa kutumia mikono yakeย  sababu eneo hilo lilikuwa limeloa kutokana na maji yaliyokuwaย  yakimwagika kutoka katika tanki, akafanikiwa kufukua na kutoaย  sanduku la rangi ya fedha, akapanda juu ya ukuta akiwa naย  sanduku hilo dogo kisha akatokomea zake pasipo kuonwa naย  yeyote yule.ย 

    Turudi kule kwenye Makazi ya siri ya Marehemu Zola, hali yaย  kutafakari ilikuwa imechukua nafasi kubwa sana. Dawson haliย  yake kiafya haikuwa nzuri hasa baada ya kupata mikiki ya hapaย  na pale kwa zaidi ya masaa nane bila kutuliza akili yake,ย  kifua kilikuwa kikimbana mno huku Kisko akimsaidia baadhi yaย  dawa na huduma nyingineย 

    “Asante Kisko! Natamani sana siku moja niwaone mkitoka katikaย  Maisha haya ambayo nahisi yanawapa mateso makubwa sana, hamnaย  uhuru wa kufanya mambo yenu. Nimewalea kwa muda mrefu sana”ย  Alisema Dawson huku akiangalia saa yake mkononi, kiskoย  akamuulizaย 

    “Kwanini unaangalia saa hiyo kila wakati ilhali haioneshiย  chochote?” Mzee Dawson akajilazimisha kucheka kidogoย 

    “Inaonekana kutokufanya kazi ndio lakini Je kama nikikwambiaย  Hii saa ndiyo Mimi utaamini?” Kisko akacheka kisha akasema

    “Hata Mtoto mdogo hawezi kuliamini hilo, Mtu anawezaje kuwaย  saa?”ย 

    “Bahati mbaya au nzuri, nyie mna majina yenu. Majina ambayoย  mlipewa huko mlipotoka, licha ya kupewa majina ya Kijeshiย  lakini hayakuweza kubadili uhalisia kuwa wewe ni Kisko,ย  wenzako ni Jesca na Chande” Akasema kisha akakohoa na kutoaย  damu nzito sana, akapewa maji ya kusukutuaย 

    “Nawaza Jesca atakuwa wapi, ni masaa mengi yamepita bilaย  kuwasiliana naye. Ulifanya kama nilivyo kwambia?” Alihojiย  Dawsonย 

    “Ndio redio Call niliiacha kwenye kile chumba chenyeย  makaburi” Alijibu Kisko huku akionekana kuwa mwnye kiu yaย  kutaka kujuwa mengiย 

    “Hata wewe pia ni mwenye Bahati kama ni hivyo, una jina lakoย  halisi Kama Dawson” Dawson akacheka tena kisha akasemaย 

    “Sababu Mimi ni Afsa wa juu katika Nchi hii ni lazima nitumieย  jina halisi lakini kuna jambo lililo nyuma ya Pazia, utakujaย  kuelewa siku moja endapo Mungu atanijalia uhai mrefu waย  kuishi” Yalikuwa ni maongezi yaliyojaa mafumbo ambayoย  hayakumshibisha Kisko, Muda huo Chande alikuwa kwenye chumbaย  kimoja na Sande Olise wakiwa wanazungumzaย 

    “Tunasubiria nini?” Aliuliza Chande akiwa anamtazama Sandeย  Olise aliyekuwa ameegesha nwili wake kwenye moja ya kioo naย  kujipa fursa ya kutazama chini ya jengo hilo la kifahariย 

    “Hatuwezi kukurupuka! Tupo mawindoni Chande, kosa dogoย  unaadhibiwa kifo. Nchi inatutambua kama waasi kutoka masaaย  machache ya kujulikana kama Wazalendo wenye kulipiganiaย  Taifa, Dunia wakati mwingine inaweza isikupe maana halisi yaย  Binadamu”ย 

    “Ha!ha!ha!” Alicheka Chande, muda huo Kisko alikuja mbio naย  kuwaambiaย 

    “Mzee Dawson hali yake ni mbaya sana” Taarifa ikazua taharukiย  pale, wote wakaelekea chumbani kwa Dawson! Wakamkuta akiwaย  ana pumua kwa shida sana.ย 

    “Inabidi tumsaidie!” Alisema Chande akionekana kuwa na wengeย  la kutoshaย 

    “Tulia!! Hatuwezi kufanya hivyo kwa sasa, hatuweziย  kuhatarisha Maisha yetu kirahisi hivyo!!” Alisema Sande kishaย  alimgeukia Dawson

    “Yupo sahihi! Rais anajuwa Mimi naumwa kwa muda mrefuย  simalizagi wiki mbili kabla ya kupelekwa JNI Hospital kwaย  matibabu ya ugonjwa wangu sababu wao ndio speshelist waย  tatizo hili, huu ni mtego mtakamatwa wote. Ni bora mniacheย  nife nyie mbaki kuwa hai” Alisema Dawson kwa sauti iliyojaaย  maumivu mnoย 

    “Baba usiseme hivyo unayo nafasi ya kuendelea kuishi, semaย  unataka nifanye nini Baba” Chande alisema kwa uchungu hukuย  macho yake yakibubujika chozi laini lililolowesha mashavuย  yake madogo, Mzee Dawson kwao alikuwa ndiye Baba yao sababuย  aliwatoa kwenye kituo cha kulea Watoto yatima miaka mingi,ย  akawapeleka mafunzoni, wakapata mafunzo ya kijeshi naย  kijasusiย 

    “Chande anayejuwa mwisho wangu atawapa tumaini endapoย  atanichukua” Alisema Dawson huku hali yake ikizidi kuwaย  mbaya!! Sande Olise akahisi jambo, haraka akaelekea kwenyeย  kioo kutazama chini akaona gari nyeusi ikiwa imesimama nje yaย  uzio wa jumba hilo la siri, walikuwa ni Malaika na Six ambaoย  walikuwa wakifuatilia mawimbi ya Redio Call kutoka kanisaniย  hadi Ufukweni, kifaa chao kiliwaambia kuwa walikuwa wamefikaย  eneo husika.ย 

    “Kuwa makini!” Alisema Six kisha akampatia Bastola Malaika.ย  Sande akarudi kwenye kile chumba akawapa taarifa kuwa Kunaย  hali ya hatari wanapaswa kuokoa Maisha yao harakaย  iwezekanavyo, muda huo Mzee Dawson alikuwa katika hali mbayaย  ya kuumwa.ย 

    Ndani ya msitu mmoja ulio kando na Jiji hili, alionekana Mtuย  mmoja Mzee Akikimbia, mkononi alikuwa ameshikilia sandukuย  lenye kutu, alikuwa ni yule Mzee aliyefukua Sanduku kuleย  kanisani. Alikuwa amechoka baada ya kukimbia kwa muda mrefu,ย  mikono yake ilikuwa ikitetemeka. Akaingiza mkono mfunoniย  akatoa funguo kisha akasimma chini ya Mti mmoja mkubwa,ย  akalifungua sanduku hilo.ย 

    Ndani ya sanduku kulikuwa na kifaa kimoja kilichoonekana kuwaย  cha zamani sana, akakiangalia kisha chozi likawa linamtoka.ย  Akabonyeza kitufe cha kuwasha, kikawaka.ย 

    Kifaa kile kilikuwa kimeunganishwa na vifaa vinne ambavyoย  vilikuwa kwa Watu wanne, Mtu wa kwanza kupata ishara alikuwaย  ni John Brain, Mtu wa pili ni Mzee Dawson, wa tatu ni Malaikaย  na Wanne ni Six ambaye alikuwa akitembea kuelekea kwenyeย  jengo lingine kama kawaida yake kutafuta eneo zuri la kulengaย  shabaha, kitendo cha kuwashwa kile kifaa na yule Mzee kuleย  msituni kilimfanya Six aanguke na kuhisi baridi kali sana,ย vivo hivyo kwa Malaika ambaye alikuwa ameshafika kwenye getiย  la kuingia katika jumba la siri ambalo Mzee Dawson na vijanaย  wake walikuwemo, kwa Mzee Dawson iliwaka ile saa ambayo Kiskoย  alimuuliza Dawson kwanini alikuwa akiiangalia mara kwa maraย  lakini wakati inawaka Mzee Dawson alikuwa ameshapoteza Fahamuย  zake, wote walishangaa kuona saa ya Dawson imewaka ghafla naย  kutoa mwanga wa kijani, katika saa hiyo kulikuwa na kitu kamaย  ramani iliyokuwa ikizunguka ndani yake.ย 

    John Brain alishtuka sana baada kupata ishara kutoka katikaย  moja ya saa yake ndogo ambayo mara nyingi alikuwa akitembeaย  nayo, saa hiyo ilikuwa ikifanana sana na saa aliyokuwaย  akiivaa Mzee Dawson! Akasimama na kutabasamu kisha akajikutaย  mwenye furaha isiyo kifani.ย 

    “Baada ya miaka mingi hatimaye umeonekana, niliweka Maishaย  yangu rehani kwa muda mrefu kukutafuta” Alisema John Brain.ย 

    Muda huo yule Mzee ambaye hakujulikana ni nani na ametokeaย  wapi, alichukua kifaa kingine ndani ya sanduku, kifaa ambachoย  kilikuwa kama simu hivi kisha akapiga mahali. Simu iliitaย  ndani ya Ikulu, ilikuwa ni katika ofisi ya Raisย 

    “Mimi ni P55 Mbaga” ilikuwa ni sauti komavu kutoka kwa Mzeeย  huyo, Rais alishtuka sana kusikia jina hilo yaani P55 Mbaga,ย  akakata simu haraka sana baada ya kusikia hivyo kishaย  akanyanyua simu kumpigia John Brain ambaye alikuwa katikaย  hali ya furaha sanaย 

    “Mimi ni mfu John!!” Alisema Rais kwa sauti iliyooneshaย  alikuwa kwenye butwaaaย 

    “Kivipi?” Alihoji Brainย 

    “P55 Mbaga amejitokeza!!”ย 

    “Imarisha ulinzi haraka, Naingia kazini kupambana naye”ย  Alisema John huku tabasamu likiwa limeimarika katika suraย  yake.ย 

    Muda huo yule Mzee ambaye ni P55 Mbaga alikuwa akitoka kuleย  Msituni na kufunga safari ya kufuata uelekeo wa saa ya Mzeeย  Dawson, alikuwa na kifaa chake alichokiamini sana, alionekanaย  kuwa mtaalam wa kifaa hicho, Dakika tano baada ya vifaaย  vilivyofungwa katika miili ya Six na Malaika kuwaka,ย  iliwafanya wabadili maamuzi yao. Mpango ulikuwa ni kuwauwaย  Sande na Mzee Dawson, haraka wakaingia kwenye gari naย  kuondoka eneo lile, huku maswali yakiwa mengi vichwani mwao.

    Yule Mzee alifika hadi eneo la Mashariki ya Bahari ya Hindi,ย  kifaa kikamwambia kuwa alikuwa amefika eneo ambalo saa hiyoย  ilikuwepo, muda huo Mzee Dawson alikuwa akirejea kwenyeย  fahamu zake!! Alipoamka alishangaa kuona saa yake imewaka,ย  akashtuka kisha akaulizaย 

    “Imeweka saa ngapi?” Aliwatumbulia macho vijana wake ambaoย  walikuwa wamesimama mbele yake, alikuwepo Kisko na Chandeย 

    “Nusu saa iliyopita” alijibu Chande huku akimtazama Mzeeย  Dawson aliyekuwa kitandaniย 

    “Na Sande yupo wapi?”ย 

    “Nafikiri yupo kwenye korido, unamuhitaji?”ย 

    “Hapana!! Nipe Maji ya kunywa” Alisema tena Mzee Dawson kishaย  alikohoa na kutoa damu.ย 

    “Baba kwanini hii saa ni muhimu sana kwako umeamka hujaliย  afya yako unauliza kuhusu saa?” Alihoji Kiskoย 

    “Nilikwambia hii saa ndiyo Maisha yangu, Mimi ni hii saa,ย  niliisibiria kwa miaka mingi na jambo hili lilibakia kuwaย  siri ambayo sina budi kuwaeleza mkiwa pamoja” Muda huo Chandeย  alirejea akiwa na glasi yenye maji ya vuguvugu ambayo maraย  nyingi Mzee Dawson alikuwa akiyatumia. Ghafla, Sande aliingiaย  chumbani bahati nzuri Dawson alikuwa ameshapata fahamuย  akasemaย 

    “Kuna Mtu anakuja upande huu, anaonekana kuwa anafuatiliaย  jambo maana yupo bize na kitu mkononi, nafikiri ana GPS”ย  Alisema Sande, Mzee Dawson akanyanyuka na kwenda kuangalia,ย  alipofika dirishani alimuona Yule Mzee ambaye mara nyingiย  alikuwa akishinda kule kanisani akajiuliza alikuwa amefuataย  nini paleย 

    “Unamfahamu?” Aliuliza Sandeย 

    “Ndio….huyu Ni Miongoni mwa Wazee wa kanisa letu, najiulizaย  amepajuaje hapa” Akajibu Mzee Dawson huku akionekana kujawaย  na mshangaoย 

    “Niachie Mimi” Sande alisema kisha akashusha ngazi kuelekeaย  chini, akafungua mlango kisha akatoka. Akakutana yule Mzeeย 

    “Wewe ni nani?” Alihoji Sande lakini kwa tahadhari sababuย  Mzee huyo alikuwa makini kumtazama Sande na jinsiย  alivyomtazama Sande aligundua Mzee huyo alikuwa na machoย  makini kuliko maelezo.

    Punde ikasikika sauti ya Dawson ikisemaย 

    “Mruhusu aje ndani” alipogeuka alikutana na macho ya Dawson,ย  Mzee huyo akaruhusiwa kuingia ndani lakini tayari kila mmojaย  alikuwa na umakini mno. Tembea ya Mzee huyo bado ilikuwaย  makini sana, alionekana kutafuta kitu lakini alipoingia humoย  kifaa chake chenye GPS kilizimika sababu nyumba hiyo ilikuwaย  maalum kwa ajili ya kazi za kipelelezi hivyo ilikuwa ni ngumuย  kwa baadhi ya vifaa kupenyeza.ย 

    Alipewa kiti akakaa kisha akaulizwaย 

    “Umefikaje hapa?” Aliuliza Mzee Dawson, yule Mzee akawatazamaย  kisha akasema bila kujibu swali la Dawsonย 

    “Nimekuja kwa ishara yako Dawson, nimetoka mbali, nimesubiriย  kwa miaka mingi kukuambia kuwa Dunia ilikuwa ikikutafuta kwaย  miaka hiyo, nilikuficha kwa muda mrefu sana” Alisema Mzeeย  huyoย 

    “Wewe ni nani hasa?”ย 

    “P55 Mbaga” Alijibu Mzee huyo na kusababisha mshangao kwaย  Mzee Dawson ambaye alionekana kulifahamu jambo hiloย 

    “Haiwezekani, wewe ni Mzee wa kanisa umeijuaje siri hiyoย  niliyoificha kwa muda mrefu!”ย 

    “Hukuificha siri hiyo, siri hii inajulikana ila kuwaka kwaย  saa hiyo ni ishara kuwa mapambano yanaanza upya! Mapambano yaย  kung’oa mizizi ya utawala huu wa Mabavu”ย 

    “Una maana gani?”ย 

    Mzee huyo alisimama kisha akasemaย 

    “Naitwa Mbaga, nilikuwa rafiki mkubwa wa Baba yako japoย  alinizidi umri lakini alinipenda sana. Baba yako alikuwa niย  miongoni mwa Askari wa ngazi ya juu, wakati huo, akatoroka naย  nyaraka za siri ambazo alianza kuzisambaza kuhusu Urais waย  Nchii namna unavyo rithishwa, uozo na ufedhuli uliokuwaย  umejaa serikalini, aliishia kuuawa huku Taifa likiambiwa kuwaย  Baba yako alikuwa ni muasi” Alimeza mate kisha akaendeleaย  Mzee Mbagaย 

    “Kabla ya kuuawa kwake alinipa kifaa maalum, akaniambiaย  unatakiwa kuvaa saa mkononi mwako na wakati wa ukomboziย  utakapofika mimi nitakuja kukusaidia. Teknolojia hiiย  iligunduliwa huko Ujerumani, mmoja wa Watu wa siri wa Baba yako walimwambia Rais juu ya Mpango wetu Mimi na Baba yako,ย  nilitafutwa kila kona bila mafanikio yoyote yale, ndipo Babaย  yako akapiga simu ukiwa masomoni ukabadilishwa Ubin wako iliย  usitambulike, akakuandaa ukawa Mwanajeshi lakini Alipouawaย  ulikuwa bado hujamaliza Mafunzo ya Kijeshi Nchini Cuba, Baadaย  ya Teknolojia kugundulika wao wakatengeneza ya kwao iliย  kujuwa muda na mahala ambapo nitawasha kifaa nilichopewa naย  Baba yako kama ishara ya uhuru na ukombozi” Aliendelea kusemaย  Mzee Mbaga na kuwaacha akina Dawson kinywa waziย 

    Machozi yalimtoka Dawson akakumbuka jinsi Mama yakeย  alivyomwambia mpango huo, kuanzia kipindi hicho aliivaa saaย  hiyo katika Maisha yake yote hadi anafikia uzee wa Makamo,ย  alimkumbatia Mzee Mbaga. Taarifa hii ilikuwa ni ajendaa kuuย  kwa kila Rais aliyetokea katika ukoo wa kurithi nafasi yaย  Urais, alitafutwa sana Mbaga bila mafanikio na Marais Kadhaaย  waliopita.ย 

    Comments ziwe nyingi apa KESHO itoke EPISODE NDEFU YA 11

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABAย  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย 

    ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xxย 

    ย ย 

    jasusi riwaya za kijasusi

    15 Comments

    1. Anuar on December 7, 2024 6:07 pm

      Daah kitu inazidi kuwa pana kama vle inaisha kumbe nd kwanza inaanza

      Reply
    2. Egibeth on December 7, 2024 6:11 pm

      Admin unazid kunfurahisha

      Reply
    3. Charz jr๐Ÿ˜Ž on December 7, 2024 6:11 pm

      Kwisha kwisha ka mkubwaa

      Reply
    4. Deo on December 7, 2024 6:14 pm

      Mambo yanazidi kunoga

      Reply
    5. John on December 7, 2024 6:36 pm

      Hii kitu noma sana lete ingine

      Reply
    6. BENEDICT on December 7, 2024 6:47 pm

      Hatar

      Reply
    7. Hamisi halidi on December 7, 2024 7:06 pm

      Aaha jamaa anakatisha yan utamu

      Reply
    8. Fawziya Hassan on December 7, 2024 7:54 pm

      ๐Ÿ”ฅ
      โค๏ธ

      Reply
    9. Moderich on December 7, 2024 10:17 pm

      Mambo yanazidi kua moto

      Reply
    10. Frankdanford on December 8, 2024 12:35 am

      Yes hadithi ni tamu sana

      Reply
    11. Frankdanford on December 8, 2024 12:36 am

      Yes hadithi ni tamu sana acha moto uwake

      Reply
    12. yahaya on December 8, 2024 8:41 am

      hiz ndo Hadith sasa

      Reply
    13. KingzJeelay on December 8, 2024 9:29 am

      So nice story

      Reply
    14. [email protected] on December 8, 2024 10:24 pm

      Mambo yanzidi kunoga

      Reply
    15. [email protected] on December 8, 2024 10:26 pm

      Tupe. Ya. 11 Admin wetu

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Odds za Moto November 8, 2025

    Hapa MSUVA Pale MPENJA Ofa Kibao Kutoka LEONBET

    Kampuni ya michezo ya kubashiri LEONBET Tanzania imezidi kudhihirisha ubunifu wake katika kukuza michezo na…

    In the name of LOVE – 12

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.