Ilipoishia sehemu ya Kumi na moja ya In the name of LOVE
Moyo Wangu na akili yangu vilikua tayari kusikia chochote kile hata kama kitaniumiza kiasi gani lakini Ndiyo ukweli pekee niliouhitaji kuusikia ili nifahamu mengi yaliyokua yakinitatiza.
Nilikua kimya huku moyo Wangu ukinidunda, viti vilipoletwa tuliketi kando ya kile chumba Kisha yule Mzee alishusha pumzi zake akaniuliza
“Ulikua wapi Kijana?” Endelea
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
“Nilipata ajali Baba, ilikua mbaya. Nilikaa Hospitali kwa wiki tatu” nilisema.
“Wiki tatu?”
“Ndiyo Baba”
“Na hizo siku nyingine ulikua wapi Hadi Mdogo wako anafia humu ndani, tunamzika kwa kushirikiana na Watu uliokua ukifanya nao kazi?” nilikaa kimya, kuhusu kifo Cha Melisa nilikisikia, nilikumbushwa machungu yaliyoanza kupoa moyoni mwangu, nikajiinamia huku chozi likianza kunitoka.
“Usilie, wewe ni Mwanaume. Lakini ni Kosa kubwa umefanya kumtelekeza Mdogo wako hapa Hadi rafiki Yako Sudi alipofanya aliyoyafanya. Kwa Miaka mitano nimekifunga hiki chumba nikiamini ungerudi hapa kuchukua kumbukumbu za Mdogo wako” alisema Baba mwenye nyumba, niliinua kichwa changu huku chozi likiendelea kunibubujika.
Nilimtazama kwa macho yenye huzuni huku nikipeleka macho yangu ndani ya chumba Cha Sudi, palikua patupu nikajiuliza hizo kumbukumbu anazozisema zipo wapi.
“Hizo kumbukumbu zipo wapi?” nilimuuliza, alikaa kimya kidogo Kisha akaniambia kwa sauti ya Ubaba.
“Kwa bahati mbaya nimezichoma moto asubuhi ya Leo, nilikata tamaa niliamini usingelirudi hapa. Kijana kwa Miaka yote ulishindwa kurudi hapa
kweli?” aliniuliza swali lile lile lililokua likichanganya akili yangu, nilijiuliza ndani ya nafsi yangu
“Miaka yote? Ni Miaka gani anaizungumzia huyu Baba?” aliponiona nipo mawazoni alinigutua kwa kunishika bega akaniuliza tena
“Ulikua wapi?” Nilivuta hewa kidogo Kisha nilifuta chozi langu halafu nikamtazama yule Baba kwa macho yaliyojaa ukungu wa mchozi laini nikamwambia kwa sauti ya kitetemeshi Cha kulia.
“Kuna kitu hakipo sawa kwangu Baba, sijui kuhusu Miaka unayoisena. Naona ghafla Kuna kitu sikikumbuki, ni wiki tatu tu naona Kila Mtu anaizungumzia kuhusu Miaka mitano iliyopita na mwingine Miaka minne. Nipo gizani Baba naomba unieleze ukweli, Mdogo wangu alifariki lini?”
Nilikua ninalia kwa kuuumia, akili yangu ilifungwa gizani. Kila kitu katika Maisha yangu kilianza upya kabisa, Yule Baba alinitazama Kisha akaniambia
“Nifuate” alinyanyuka na kuingia ndani ya kile chumba, moyo Wangu ulizizima kwa upweke na maumivu. Chumba Cha Sudi kilibeba kumbukumbu zenye kuniumiza sana, niliishi na Mdogo wangu humo lakini kwa Simulizi alifia humo kwa kuuawa na Sudi Kisha Sudi akakimbia.
Nilisimama huku miguu yangu ikiwa mizito sana kuingia ndani ya hicho chumba, yule Baba alikua tayari ameingia akageuka na kunipa ishara kua niingie, nilinyanyua Mguu wangu huku chozi likinibubujika.
Kumbukumbu za Melisa zilipita machoni pangu mithiri ya filamu ya maumivu. Mguu wangu ulikua baridi sana kama Mtu aliyepooza lakini niliusukuma ili niingie ndani pengine ningeona kitu chenye kunikumbusha kitu kuhusu Miaka inayotajwa.
Niliingia ndani ya chumba Cha Sudi, kilikua vile vile, magazeti ya Michezo yalikua yamebandikwa ukutani, nilitembea Hadi ukutani huku yule Baba akiniangalia tu. Niliushika Ukuta, nikapapasa Yale magazeti, yalikua yamejaa vumbi
Moja ya gazeti liliandikwa tarehe, ilikua ni Miaka mitano iliyopita. Palikua na kitanda kilichofunikwa shuka nyeupe, yule Baba akaniambia
“Tulimkuta Mdogo wako akiwa ameharibika hapa” nilianza kulia, akanituliza na kuniambia.
“Nilikitunza chumba hiki niliamini ungerudi japo nilikata tamaa. Kijana, ni Miaka mitano imepita, unapaswa kuwauliza Watu wako wa karibu ni kitu
gani wanakuficha” Alisema yule Baba, chozi lilianza kunibubujika maana hata hao Watu wa karibu hawakuweza kunieleza chochote kile
“Baba, niliambiwa baada ya ajali akili yangu haijakaa sawa lakini nahisi nilidanganywa. Hapa Kuna kitu ninafichwa” nilisema Kisha Niliketi kitandani, yule Baba naye aliketi kitandani pia
“Kijana, hii Dunia ni Uwanja wa Siri, Binadamu wanaweza kuficha Siri Hadi wanaingia kaburini ilimradi tu Siri hiyo isiwe faida kwa mwingine. Inawezekana katika hiyo Siri Kuna jambo muhimu ambalo hawataki ulijue, Kitu pekee kinachoweza kukufanya uijue Siri unayofichwa nayo ni kuwa mdadisi zaidi” alisema yule Baba, maneno yake yaliamsha Hali Fulani ya Ujasiri ndani yangu, nilikubali maneno yake kua kama nitaendelea kulia siwezi kufahamu chochote kuhusu Miaka mitano iliyopita.
“Nenda kautafute ukweli kwa gharama yoyote ile, hakuna kitu kibaya katika Maisha ya Binadamu kama kujipoteza. Usikubali kujipoteza, unapaswa kupambana” alisema tena, maneno yake yalijaa hekima na busara kubwa sana.
Nilifuta chozi langu nikamwambia “Naenda kuutafuta ukweli ulio gizani Baba” Kisha nilinyanyuka na kuondoka pale, nilimwacha yule Baba akiwa amesimama Mlangoni akinitazama nikipotea kwenye Kuta za nyumba yake
Jina Moja lililo kichwani kwangu ambalo niliamini linaweza kunipa majibu ni Clara, ndiye Mtu pekee aliyekua kando yangu siku niliyorudisha fahamu baada ya ile ajali.
Nilimsimamisha dereva wa pikipiki, nilihitaji kurudi nyumbani kwa Clara. Akili yangu haikutaka kutulia kabisa, ilikua ni Mishale ya Alhasiri, nilifika nyumbani kwa Clara
Moja kwa moja nilielekea Chumbani kwangu, Zaylisa alikua hajarudi. Sikujali sana kuhusu yeye, nilichohitaji ni kufika chumbani kwa Clara pengine alikua Mtu muhimu kwenye Maisha yangu niliyoyasahau, akili yangu iliniambia hivyo maana asingeliweza kua pale wakati narudisha fahamu tena akiwa na Mtoto wake Melisa
Nilizunguka chumbani huku nikipanga mkakati wa namna gani nitaingia chumbani kwa Clara, Mtu pekee ambaye angeniwezesha kuingia humo alikua ni Matilda.
Niliufungua mlango Kisha nilienda sebleni, nikamkuta Matilda akiwa anaangalia filamu, nikamtazama kwa sekunde kadhaa Kisha nikafanya
uamuzi wa kukielekea chumba Cha Clara, aliponiona naelekea huko Matilda alinikimbilia
Nilitikisa kitasa Cha mlango nikagundua mlango ulikua umefungwa kama nilivyohisi mwanzo, sasa lile wazo la kumtumia Matilda lilitakiwa kufanya kazi.
“Nahitaji kuingia chumbani kwa Clara” nilisema nikimtazama Matilda kwa jicho Kali, hata yeye alishangaa kwasababu sikuwahi kumtazama kwa jicho lile, akameza funda zito la mate huku akipumua kwa nguvu, alishaanza kuingiwa na woga lakini akaniambia
“Dada amefunga mlango wake, kwanini unataka kufanya hivyo?”
“Nina uhakika ndani ya hiki chumba Kuna kumbukumbu zangu, nataka kujua Clara ni Nani kwangu, kitu gani ambacho hamkisemi nyinyi?” niliuliza kwa Uchungu sana, niliona Wazi kua Watu wale walifanya makusudi kunipoteza kifikra bila kunipa kumbukumbu yoyote ile.
Matilda alirudi kidogo nyuma, alichokisikia kutoka kwangu alionesha Wazi kua alikitarajia. Hata sura yake ilionesha kua alikua ni miongoni mwa Watu walioamua kunificha kuhusu Maisha yangu yaliyopita
“Matilda, Kuna kitu unakijua na hutaki kusema si Ndiyo? Mimi ni Nani nataka kujua Matilda, kwanini najiona sijakamilika Kuna kitu gani nimesahau, nataka kujua ni kitu gani muhimu nimekisahau?” niliuliza, Matilda alikua akinitazama kwa Mshangao tu huku chozi lake likimbubujika
Nilisogea taratibu Kisha nilimwambia kwa sauti ya huzuni huku chozi likinidondoka.
“Nakuomba Matilda, lazima utakua unanifahamu vizuri. Niambie nisichokifahamu, niambie nilichokisahau” nilisema, niliona jinsi ambavyo sura yake ilivyokua ikionesha huruma juu yangu. Nilimshika mabegani nikamwonba aniambie chochote hata kama kilijaa maumivu kiasi gani lakini nilitaka kusikia ukweli, niliona chozi lilikua likimbubujika ni wazi aliguswa sana na maneno yangu.
“Akili yangu imekosa utulivu Matilda, Nilipopata ajali na kurejesha fahamu nilimwona Clara pale Hospitalini, niambie yeye ni Nani kwenye Maisha yangu?” nilimuuliza Matilda. Alikua akinitazama kwa jicho la huruma sana
Matilda hakusema chochote kile japo sura yake ilionesha kua alifahamu jambo fulani.
Nilirudi chumbani kwangu nikiwa na huzuni sana, chozi lilikua likinibubujika. Kilichokua moyoni mwangu ni kama Mzigo mzito nilioshindwa kuubeba. Nilijivuta Hadi nikaketi kitandani, sikua na hamu ya chochote isipokua kujua Siri ya Maiaka Mitano iliyopita.
Usiku ulipoingia ulinikuta nikiwa nimejiinamia, chumba kilikua Giza sababu sikuwasha taa yoyote ile. Nilianza kusikia sauti ya Matilda akigumia
“Mwizi! Mwizi!” nilishtuka, haraka nikapapasia taa halafu nikafungua mlango nikaelekea nje, Matilda alikua ameshafika getini. Kwa Kipindi hicho nyumba ya Clara ilikua Haina Mlinzi
Nilikimbilia getini nikamkuta Matilda akiwa analia, nilimuuliza kimetokea nini, alikua analia akaniambia
“Mwizi aliingia chumbani kwangu”
“Sasa chumbani kwako alikuja kufanya nini?” nilimuuliza, aliendelea kulia bila kusema chochote. Ilinifikirisha kidogo, mwizi kuingia chumba Cha Msichana wa kazi ambaye Hana chochote kile.
“Basi usilie Matilda kwani amefanikiwa kuiba chochote?” “Sijui Mimi, ila nimemkuta chumbani kwangu akanisukuma na kukimbia” “Uliiyona sura yake?”
“Hapana alivaa kofia”
“Basi twende ndani, hawezi kurudi tena. Mimi nipo nitakulinda” nilisema kama Mwanaume. Nilimpeleka Matilda sebleni Kisha nilimpatia Maji ya baridi anywe ili aondoe wenge. Alipomaliza kunywa Maji angalau akili yake ilitulia akanieleza kwa uzuri
“Basi Wacha tukaangalie kama Kuna chochote amechukua” nilisema.
“Hapana Kaka, hakuchukua chochote hata usijali” alisema, lakini ndani ya sauti yake nilihisi Kuna kitu hakikua sawa. Mara Mlango ulifunguliwa, aliingia Zaylisa
“Eeeh mmetulia wenyewe hapo mnapiga stori” alisema, haraka akili yangu iliniambia napaswa kujifanya hakuna nilichokiona kuhusu yeye ili niweze kumchunguza vizuri, nilitabasamu kidogo tu nikamwambia
“Umepishana kidogo na mwizi” Nilisema, akashtuka
“Mwizi?”
“Ndiyo, aliingia chumbani kwa Matilda lakini bahati nzuri hakuiba chochote kile” Zaylisa akasogea taratibu Kisha akamshika bega Matilda
“Pole Binti, pole sana iwe funzo siku nyingine usiache mlango Wazi sawa?” alisema kwa sauti ya kujali iliyojaa Udada ndani yake. Matilda akaitikia kwa kichwa Kisha akanyanyuka na kuondoka akaelekea chumbani kwake.
Nilitabasamu kidogo, Zaylisa aliniangalia kwa jicho la mapenzi. Nikashusha pumzi nikamuuliza
“Za utokako?”
“Ahh‼ hivyo hivyo Mpenzi, Hali ya Baba siyo nzuri sana yaani napata wakati mgumu sana” alisema, kwa mara ya kwanza nilimwona Zaylisa akiongea uwongo mbele yangu, nilihisi kuumia sana. Hakujua kua niliifahamu Siri aliyoificha kua Mzee Paulo alifariki siku nyingi
“Jamani, pole sana my love. Kua na Imani Baba Yako atapona”
“Asante, Ndiyo maana napenda kua karibu Yako Jacob. Najihisi amani na furaha sana niwapo kando Yako” alisema Kisha alilala begani kwangu. Nafsi yangu ilizidi kutapa tapa, hakuna kitu kinaumiza moyo kama kugundua Mtu unayemwamini na kumpenda anafanya mambo gizani, nilijiuliza alikua ana lengo gani la kusema uwongo
“Usijali, Mimi ni wako Zay. Basi twende ukaoge ili uweke mwili safi” nilisema Kisha nilibeba mkoba wake, tukaongozana Hadi chumbani, akabadilisha nguo akavalia taulo Kisha akaelekea Bafuni. Nilisubiria Hadi pale nitakaposikia Maji yakimwagika
Niliutazama Mkoba wake, simu yake ilikua humo. Nilipata wazo la kuipekua simu yake maana mara nyingi alikua haweki Nywila. Taratibu na kwa umakini mkubwa sana niliuchukua mkoba Kisha nikafungua zipu pole pole bila kelele huku macho na masikio yangu vikiwa makini sana.
Nilipomaliza kufungua zipu ya mkoba wake niliiyona simu yake. Nilishusha pumzi zangu, huku nikiamini simu hiyo itanifungulia njia ya kujua ni mpango gani wa Siri ambao Zaylisa alikua nao na huwenda alikua anaifahamu Siri ya Miaka mitano nisiyoikumbuka na pengine hakutaka nikumbuke.
Basi niliichukua simu taratibu na kwa umakini, Kisha nilibonyeza mahali, mwanga ukawaka. Nilijaribu kuifungua lakini ilidai Nywila yaani namba ya siri, nilihisi kupandwa na hasira maana nisingeliweza kufanikiwa chochote kile. Iliongeza Hali ya Wasiwasi kua alikua na mpango Fulani, kwanini aweke namba ya siri bila kuniambia
Niliirudisha simu na kufunga zipu Kisha niliuweka mkoba pale pale nilipoutoa halafu, nikatulia kitandani nikiendelea na tafakari, Kila nilichofanya hakikunipa mwanga
Zaylisa aliporudi kutoka Bafuni alikua mwingi wa tabasamu, alinitazama kwa tabasamu Kisha alinifuata na kuanza kunipiga mabusu. Sikua na hisia naye tena, ghafla tu hisia zilihama kwake licha ya Upendo mwingi niliowahi kua nao kwake
Tulifanya mapenzi huku nikijitahidi kuigiza kua nilikua na hisia Kali sana juu yake, sikutaka aujue mpango wangu kama ambavyo nilihisi alikua akiuficha mpango wake kwangu.
Baada ya kumaliza alijilaza kifuani kwangu, alikua mwingi wa kubadilisha stori za hapa na pale. Ilichochea wasiwasi wangu kua lipo jambo zipo alilokua akilificha
Basi, tulilala Hadi asubuhi kulipo pambazuka. Kama kawaida yake aliniaga kua anaenda kumhudumia Baba yake Mgonjwa, nami nilikua mwepesi wa kumruhusu ili nyuma nifanye Uchunguzi wangu.
Nilimfuatilia tena nyuma nyuma kwa kutumia Bodaboda, safari zake zilikua zile zile. Alipofika Mwenge aliingia kwenye gari nyeusi iliyopanda juu iliyoonekana kua ya gharama sana Kisha walielekea kwenye ile Hoteli
Nikapata wazo kua ndani ya Hoteli hiyo Kuna jambo Fulani ambalo yeye pamoja na yule Mwanaume anayevaa kofia walikua wakilipanga au kulifanya.
Sikutaka kuendelea Kuchunguza zaidi, nilirudi nyumbani. Nilimwita Matilda, Kuna kitu nilitaka kumuuliza, alipofika alinisalimia maana nilipotoka sikuonana naye
“Hivi ile siku ambayo Zaylisa na Clara walizozana ilikuaje? Naomba usinifiche chochote” nilimuuliza kwa sauti kavu ambayo ilimfanya aone kua sikutaka utani.
“Dada Zay, alimwambia Dada Clara kua…..” alisema Kisha alisita, nikamkazia macho yangu kwa ukali
“Alimwambia hataruhusu Melisa awe karibu na wewe” nilishtuka sana, kwanini aseme hivyo kwani Mimi na Mtoto Melisa tuna uhusiano gani?
“Kwanini aseme hivyo?” nilimuuliza, nilikua makini kusubiria jibu la Matilda.
“Mimi sijui Kaka, niliyasikia hayo tu ndipo wewe ulipokuja”
“Matilda sura Yako inaonesha una jambo la ziada la kuniambia, niambie tuu tafadhali” nilisema kwa sauti ya Unyonge.
“Kaka Mimi sijui chochote kile nakuapia”
“Mimi ni Mtu mzima, ninapoitazama sura Yako naona inakusuta kwa unachokisema. Matilda, usiwe Sehemu ya Watu wanaohitaji niishi gizani Milele, naomba nikuulize. Mimi ni Nani kwa Clara, kwanini siku ile alikua Hospitalini, Nina uhuasiano gani na yeye?”
Matilda alinitazama, uso wake ulinyongea, chozi likaanza kumbubujika.
“Samahani Kaka Jacob, siwezi kusema Kila kitu” alisema Matilda huku chozi likitiririka machoni pake. Nilimshika mabega yake nikamwambia
“Naelewa ni jinsi gani unajizuia kuniambia Matilda lakini huu ndio wakati sahihi wa kunieleza, nateseka kwa kuishi kama kivuli kwenye Maisha yangu” nilisema, Matilda alinishika mkono akanipeleka chumbani kwake Kisha akaufunga mlango.
Akafungua Begi Moja kubwa halafu akatoa picha Moja, akanipatia. Nilihisi upepo Fulani ukikatiza usoni pangu, picha hiyo nilipiga Mimi, yeye na Clara.
Nilipomaliza kuangalia niligundua hakuna kilichobadilika kwangu kwani Bado nilikua sikumbuki chochote hata hiyo picha sikukumbuka ilipigwa lini.
“Hii picha?” niliuliza huku mdomo Wangu ukiwa mzito lakini wenye kuhitaji kuendelea kuongea, Matilda akadakia kwa hisia ya huzuni sana huku chozi likimdondoka akaniambia
“Hiyo Ndiyo siku ambayo ulikua na furaha kuliko siku yoyote uliyowahi kuishi hapa Duniani Kaka Jacob” alisema kwa hisia Kali sana, jicho langu Moja likaanza kudondosha chozi, picha ilikua ikining’inia mkononi huku kope za macho yangu zikicheza kwa muwasho wa chozi.
“Kwanini nilikua na furaha Matilda?” nilimwuliza Kisha niliitazama tena ile picha, ni kweli nilionekana kua mwenye furaha sana, siyo Mimi tu hata Matilda na Clara walionekana kua na furaha, picha ilisadiki maneno ya Matilda lakini sikujua ni kwanini furaha ilitawala kiasi hicho.
Matilda aliibana midomo yake kwa Uchungu huku akizuia sauti ya kilio isimtoke, moyo Wangu ulikua ukidunda sababu nilijua jibu ambalo Matilda angenipatia lingetoa mwanga halisi wa Kila swali nililokua nikijiuliza, akasema
“Hiyo Ndiyo siku ambayo Melisa alizaliwa” alisema, chozi lilimtoka kama alikua amewekwa pilipiki machoni mwake, nilitazama tena ile picha Kisha nilimtazama yeye.
“Nilikuwepo siku ambayo Melisa alizaliwa?”
“Ndiyo”
“Hiyo Miaka mitano iliyopita?”
“Ndiyo, Kaka Jacob wewe ni Mume wa Dada Clara pia ndiye Baba wa Melisa” alifunguka Matilda, ni kama alikua amerusha bomu la anga. Lilitua chini na kupasua Kila kitu, nilistaajabu sana lakini sikukumbuka chochote Bado
Macho yalinitoka, nilirudi nyuma hatua ndogo ndogo. Japo nilihitaji kuambiwa ukweli lakini sikutegemea kusikia nilichokisikia, niligeuka na kutembea taratibu kama Mtu aliyechoka sana, nilitembea na kutoka mle chumbani. Nilifika sebleni nikiwa hoi, chozi na jasho vilikua vikishindana kumwagika kama Maji.
Nilisimama mbele ya sofa huku Bado nikiwa kwenye Butwaa.
“Huo ndio ukweli Kaka Jacob” niliisikia sauti ya Matilda nyuma yangu, haikua sauti ya kawaida Bali ilijaa kilio. Niligeuka na kumtazama Kisha nikamkazia sauti nikamwambia
“Wewe ni mwongo Matilda, unajua kua unasema uwongo. Sijawahi kuyaishi hayo Maisha, sikuwepo na wala hakijapita hicho kipindi Cha Miaka mitano” nilisema, Kisha akanipa picha nyingine
Niliitazama huku chozi likidondokea kwenye ile picha, ilikua ni picha tuliyopiga kanisani Mimi na Clara siku ya ndoa, nilikua nimevalia suti nyeusi, Clara alikua amevalia gauni jeupe na shela. Nilizidi kuchoka, majibu ya maswali yangu niliyapata kikatili sana
“Sasa kwanini sikumbuki, kwanini Clara hakusema chochote?” nilipaza sauti, nilikua katika Hali mbaya sana kisaikolojia, niliambiwa vitu vyenye ushahidi lakini sikukumbuka chochote kile.
Matilda akanisogelea huku akifuta chozi lake akaniambia
“Daktari alisema usikumbushwe Bali asubirie Hadi utakapokumbuka mwenyewe. Hiyo Ndiyo sababu ya kwanini hakusema chochote, Ndiyo maana alimleta Zaylisa tena kwenye Maisha Yako. Wewe ni Msomi, wewe ni Mtendaji Mkuu wa kampuni zote za Dada Clara” alisema Matilda, nilihisi mwili ulikua ukitetemeka kwa uzito wa maneno ya Matilda.
“Kwahiyo nilimpenda Clara?”
“Ndiyo, mlikua na furaha kwa Miaka mitano mliyoishi pamoja kama Mume na Mke. Furaha yenu ilikatishwa Usiku ule ulipopata ajali, ilikua ni siku ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Melisa, ulipata mtikisiko wa Ubongo na kupelekea kupoteza kumbukumbu zako.” Aliposema Kauli hii nilihisi maumivu makali sana ya kichwa huku nikiona baadhi ya picha zikipita kwenye ufahamu wangu
Nilianza kuona baadhi ya kumbukumbu, nilishikilia kichwa changu na kujikuta nikiwa nimeanguka sakafuni, nilipoteza fahamu.
Matilda alihangaika na Mimi, akanipeleka Hospitali.
Ukweli unaoumiza.
Masaa Matatu baadaye nilipata fahamu, nilijikuta nipo kitandani. Macho yalikua mazito yakitokwa na Machozi, nilikumbuka niliwahi kuamka kama hivi na kumwona Clara na Melisa mbele yangu, safari hii ilikua tofauti
Matilda alikua ameketi kando amejiinami, hakujua kua nilikua nimeamka. Nilipovuta hewa nzito ndipo aliposikia na kunitazama.
Alitoa tabasamu lenye huzuni ndani yake huku chozi jepesi likimtoka, aliniangalia Kisha akaniuliza
“Unajisikiaje Kaka Jacob?” chozi lilinidondoka nikiwa ninamtazama, niliamka nikiwa Jacob niliyetimia. Kumbukumbu zangu zote zilikua zimerudi. Nilikumbuka Kila kitu kuanzia kifo Cha Mdogo wangu kipenzi Melisa, kifo Cha Mama yangu, nilimkumbuka Clara na Mtoto Wangu Melisa
Nilitikisa kichwa kuashiria kua nilikua sawa, lakini Matilda akataka kutoka kwa ajili ya kwenda kumwita Daktari, nilimzuia kwa kumshika mkono Kisha nikamwambia
“Nipo salama Matilda, nakushukuru sana” nilisema, Matilda aliketi taratibu huku akiniangalia kwa kunishangaa
“Ndiyo, nimekumbuka Kila kitu kuhusu Mimi” nilisema kwa sauti ya taratibu iliyosindikizwa na huzuni. Matilda aliachia tabasamu huku chozi likiendelea kumbubujika.
“Usilie Matilda, Kila kitu kitakua sawa. Umewasiliana na Clara na kujua yupo wapi?” nilimuuliza, akafuta chozi lake Kisha kwa sauti iliyojaa kubana kwa mafua aliniambia
“Kaka, nimejaribu sana lakini simpati. Sijui yupo wapi, natamani awe hapa na wewe akifurahia kumbukumbu zako” Alisema Matilda, alionesha Wazi kua alikua amejawa na Upendo sana juu yetu, aliyabeba matatizo yetu kama matatizo yake, hakua tu Msichana wa kazi Bali ndugu aliyetimia.
“Nakuomba Matilda, usimwambie yeyote kua kumbukumbu zangu zipo sawa” nilisema, aliitikia kwa kutumia kichwa chake Kisha aliniambia
“Mimi ni mtiifu kwako Kaka, sitathubutu. Nitajifanya kama vile sijui chochote kile” basi nilitabasamu, nikafuta chozi lililobakia machoni pangu.
Nilihisi nimeshusha mzigo mzito mabegani kwangu, nilihitaji kujua mambo mawili, ni wapi alipo Clara na Mwanangu Melisa lakini pia nilihitaji kujua kuhusu Zaylisa, alikua na mpango gani kwenye Maisha yangu.
Baadaye jioni niliruhusiwa kurudi Nyumbani, baada ya kushuka kwenye Bajaji nilisimama na kuitazama nyumba ya Clara, nilikumbuka Maisha mazuri tuliyoyaishi kwa Miaka mitano iliyopita. Kila Kuta ilikua na historia nzuri ya Upendo
Nilihisi kusikia sauti za Kicheko Cha Clara na Mtoto wetu Melisa, Kila nilichokitazama kilinipa kumbukumbu zisizofutika Maishani mwangu. Matilda alinielelewa akanishika bega kua nisiwe na wasiwasi.
Tulipoingia ndani ya Uzio, nilitazama Kila kitu. Kulikua na kumbukumbu nyingi sana, macho yangu hayakuacha kulitazama eneo ka maegesho, hapo palikua na gari tatu lakini Moja ilikua imefunikwa kwa turubai ikionekana kua ilikua haitumiki.
Nilisogea pole pole huku Matilda akiwa nyuma yangu, nilipepesa macho taratibu huku upepo wa pole pole ukiwa unanipiga, nilisogea na kufungua turubai. Nililiona gari langu ambalo nilikua nikilitumia, nililipapasa taratibu huku nikigusa vumbi jepesi
Chozi lilinitoka, gari Hilo lilikua na kumbukumbu ya ajali yangu, halikutengenezwa Bali lilikua vile vile kama ambavyo nilipata nalo ajali, lilikua na mbonyeo upande wa Kushoto huku vioo vikiwa vimevunjika.
“Kaka Jacob” aliniita Matilda, aliguswa sana na Mimi.
Niligeuka kumtazama
“Najua ni jinsi gani umeumia Kaka, lakini Kila kitu kwenye hii Dunia hutokea kwasababu. Namshukuru Mungu umerudisha kumbukumbu zako muhimu” alisema, niliitikia kwa kutumia kichwa kwani kinywa changu kilikua kizito sana hakikuweza kutoa neno lolote lile
Matilda akalifunika tena lile gari sababu tulikubaliana kua Kila Siri itabakia kama ilivyo. Nilipoingia ndani nilizidi kukumbuka kuhusu Familia yangu, Kila hatua niliyopiga ilinipa kumbukumbu nzito sana.
Sikua na swali la kuuliza sababu majibu yote yalikua Wazi, nilikitazama chumba Cha Clara, ndicho chumba chetu lakini napaswa kuishi kama sikifahamu chumba hicho, ulikua ni uamuzi mgumu sana lakini wenye maana. Basi nilikipita chumba kama sikijui Kisha nilielekea Chumbani kwangu na kujilaza kitandani huku macho yangu yakitazama Dali.
Usiku, Zaylisa alirudi kama kawaida yake akijifanya alikua bize sana na kumuuguza Baba yake, aliniletea stori nyingi huku akiamini Mimi nilikua Bado sijapata kumbukumbu zangu, akaingia bafuni kuoga Kisha akarudi tukaketi na kuanza kuzungumza.
Safari hii nilimtazama kwa jicho la tofauti sana, sio mapenzi Bali umakini wa kujua alikua na mpango gani na huyo Mtu anayejiita ‘Mzee wa MIPANGO’
“Kidogo sasa hivi Hali ya Baba inaendelea kuimarika. Hua najisikia vibaya sana kukuacha mpweke Mpenzi wangu” alisema Zaylisa kwa sauti iliyojaa Ulaghai, niliikumbuka sauti hii ilikua ikimtoka Kila siku lakini nilikua gizani sikuweza kuitambua.
Kila nilivyomtazama nilihisi alikua ana Maisha ya tofauti sana kwa Miaka mitano iliyopita, sikujua ni Maisha ya namna gani lakini hayakua Yale niliyomwacha nayo wakati ule. Niliishia kutabasamu kana kwamba nilikua Jacob yule aliyekua akimchezea, hata chembe ya Upendo haikuwepo. Moyoni mwangu
“Pole sana, Mungu atamfanyia wepesi ataimalika zaidi” nilisema huku nikimtazama, japo tulikua tumekaa tunaongea lakini niliona alikua bize sana na simu yake. Akanipa mwanya mzuri sana wa kuitazama upya sura yake.
**
Zilipita siku Nne, hakuna aliyempata Clara kwenye simu. Mwanzo ilionekana kua kawaida lakini tulianza kupata hofu, Kila mara Simu ya Mezani ilipoita ilitufanya tuwehuke sana.
“Au ni kawaida yake?” aliuliza Zaylisa, tulikua tumekaa sebleni. Niligeuka kumtazama, moyoni mwangu nilijua kabisa haikua kawaida kwa Clara, niliishi naye Miaka mitano ya furaha na amani, ni Mke wangu wa Ndoa. Nilipandwa na hasira lakini niliificha
“Mh! Nitajuaje wakati Mimi hapa si mwenyeji Mpenzi, lakini hata Matilda anamshangaa inaonesha sio kawaida” nilisema, alitabasamu kidogo tu
“Lakini Jacob, unajua yeye hataki wewe uendelee kuwa hapa hasa na Mimi hivyo usiwaze sana kuhusu yeye sababu huwezi kujua akirudi atakua na mpango gani dhidi yetu” alisema Kisha alinisogelea akasema tena
“Niangalie Mimi, unanijua na nimekubali kuachana na Mume wangu kwasababu Yako wewe Jacob, Clara asiitumie fimbo ya kukusaidia kukuchapia” Nilitikisa kichwa kukubaliana na Zaylisa huku nikiwa nayaelewa maneno yake kua yalijaa mizizi ya Uwongo, sura yake ilionesha kua alikua akiifahamu Siri ya Miaka Mitano iliyopita lakini swali nililojiuliza nikiwa ninamtazama
“Kwanini Clara alikubali kumleta tena kwenye Maisha yangu ikiwa alikua anajua Mimi ni Mume wake, waliongea nini?” Majibu ya maswali yote yalikua kwa Clara ambaye Hadi sasa hatujui yupo wapi na anafanya nini.
“Ni kweli, sasa tutafanya nini Mpenzi ili kuhakikisha huyu Clara hatuchapi tena? Unajua tatizo Sina mahali pa kukupeleka, Hali yangu kiuchumi unaijua Zaylisa” nilisema kwa Uchungu sana kama vile nilikua mbele ya Kamera nikiifuata Script iliyoandikwa na Mwandishi Nguli. Hata moyo Wangu uliniambia kua kama nikigeukia Uigizaji basi nitaweza kuigiza vizuri sana.
Nilikua nikimtazama kwa uhakika wa uthabiti wa kumaanisha, sikuruhusu hata chembe ya Uwongo ijulikane. Mara akapita Matilda akielekea jikoni, Zaylisa akamwita Matilda kama Kijakazi tu
“Nimekutuma unileteee juisi Hadi sasa haujaleta, una dharau sana wewe Mtoto” alisema Zaylisa, hii Tabia sikuwahi kuiona kwake isipokua wakati huu aliporudi kwenye Maisha yangu upya. Nilimtazama Matilda kwa jicho la hasira Kisha nikamwambia
“Acha dharau Mdogo wangu haya Maisha tu, kipi kinakufanya uoneshe dharau wakati wewe ni Msichana wa kazi tu. Lete juisi hapa” nilikaza sauti
Kisha nilimkonyeza jicho Matilda, sikutaka Kuonesha Wazi nipo Upande wake nilijiegemeza Upande wa Zaylisa ili kuivuna Imani yake kwangu.
“Samahani, nilisahau hata hivyo naenda kukuchukulia” alisema Matilda kwa adabu sana Kisha aliondoka zake pale.
“Jacob, unanifanya nazidi kukupenda maana licha ya kua hauna mamlaka hapa ila unasimama na Mimi” alisema.
“Usijali Kipenzi, nisiposimama na wewe nitasimama na Nani tena maana Sina familia nyingine zaidi Yako wewe” nilimwambia Zaylisa na ikaonekana kumpatia furaha sana
Basi, Baada ya dakika Moja juisi ilikua tayari na Matilda aliileta ikiwa kwenye glasi ndefu Pana, kama nilivyokwambia nyumba ya Clara ni nyumba ya kitajiri hivyo hata vyombo vyake vilikua vya thamani sana. Wakati anampatia kwa bahati mbaya akateleza na kumwagikia Juisi kwenye gauni la Zaylisa
Taharuki ikatokea, hasira ikampanda sana Zaylisa akatamani kumpiga Matilda lakini sikuruhusu litokee nikaingilia kati, nikamtandika Kofi Mimi Matilda, halikua Kofi sawa na lile ambalo Zaylisa angempiga
“Mshenzi sana wewe, kwakua umelazimishwa kuleta Juisi ndio unafanya hivi si Ndiyo?” nilisema kwa kufoka Hadi misuli ya shingo ilinitoka, nilifanya kwa ajili ya kumwaminisha Zaylisa kua nilikua Upande wake muda wote na hakuna nilichokumbuka. Matilda alidondosha chozi huku akiomba msamaha
“Nenda ukatupe vipande vya glasi Kisha uje ufute hapa haraka sana” nilisema, haraka Matilda aliokota vipande vya glasi akaondoka. Nilimgeukia Zaylisa kwa jicho la kujali nikamshika magebani nikamwambia
“Pole Babe, yule mshenzi sana amefanya makusudi ila dawa yake ipo jikoni. Hizi dharau zimefika mwisho sasa” Nilisema huku Zaylisa akipepesa macho yake aliyobandika kope, alikua na hasira sana akaniambia
“Nimechukia sana Jacob, hizi ni dharau na siyo Bure huyu ametumwa na Bosi wake, sasa nitamwonesha” alisema kwa hasira akiwa anatetemeka sana.
“Usijali, nenda kabadilishe nguo zako” nilisema, aliondoka zake kwa hasira akaelekea chumbani, ile nageuka na Matilda alikua akifika. Nusura chozi linitoke nilimwangalia kwa huruma, sikupenda kumpiga Kofi ila nilifanya vile ili kumkinga na hasira ya Zaylisa.
MWISHO
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love

184 Comments
9k7htg
Sijaelewa hapa maana ya neno MWISHO.
Mwisho gani tena sijaelewa samahani
Mbona mmeandika mwisho ko ndio imeishaje xx
https://shorturl.fm/C8X07
Daaahh bonge moja la story nzuri Sana nimeipenda hakika ndugu mwandishi Mungu azidi kukuongezea ufahamu kwenye hii kazi yako
Natumaini kutakuwepo na season two
Mbona mmeandika mwisho ko ndio imeishaje xx
83jqa4
Nimeipenda sana story jaman
Mwisho?? Inaishaje hivi na ww
Mbona mwisho tena Clara yupo wapi
Bhana inaisha kama muvi za kibongo jaman😭😭😭
Bhana inaishaje ivo kam muvi la kibongo
Admin mwisho kvp
Hatujaelewaaa 🤔😳😒
Tamu sana admn ila neno mwisho limenichanganya samahan lakin
Riwaya nzuri sana ila neno [MWISHO] lanichanganya
https://shorturl.fm/Uj3im
https://shorturl.fm/S0VtW
Nimeipenda sana ila sijapenda ulivyo imaliza Yani bado Kuna visa viwili bado Kuna mama na mtoto
Bado Mzee wa mipamgo atajua kama ndo mume wake au n mchati tu umemaliza kiasara kweli
https://shorturl.fm/sUu0X
https://shorturl.fm/2y40s
Mwisho kivipi Tena hapo2 ndo mnapo alibu vp kuhusu Clara atajuaj kama kacobo kaludisha kmbkmb vp kh zayls n mipng yake 😭
https://shorturl.fm/xK5hp
https://shorturl.fm/R4NZ9
https://shorturl.fm/brQB0
https://shorturl.fm/D3KP7
https://shorturl.fm/Tncwf
Admin kiukweli hapo umefail mwisho gani sasa hujasema maisha yaliendelea vipi baada ya kumbukumbu kurudi upya, Je Jacob aliendelea na Zaylisa au Clara na muda huo wote Clara alikuwa wapi na mwanae na akiwa anafanya nini?Tunaomba muunganiko mzuri wa visa na matukio plz
https://shorturl.fm/nE80q
https://shorturl.fm/8JBgr
https://shorturl.fm/drPl5
https://shorturl.fm/zFeL0
https://shorturl.fm/UDuRb
https://shorturl.fm/JcNQF
https://shorturl.fm/gD1ea
https://shorturl.fm/8lfzs
https://shorturl.fm/nQGXA
https://shorturl.fm/NghYj
https://shorturl.fm/0tT9p
https://shorturl.fm/YjieY
78sd8c
https://shorturl.fm/uVrBU
https://shorturl.fm/ZaNfi
https://shorturl.fm/a3Fw4
https://shorturl.fm/i4Dkd
https://shorturl.fm/rYRBp
t0o3hp
https://shorturl.fm/oE8oh
https://shorturl.fm/yqUh5
6xby2y
https://shorturl.fm/dS0nY
https://shorturl.fm/ReVIg
https://shorturl.fm/Xhc0Y
https://shorturl.fm/AX5uN
esn5fo
https://shorturl.fm/TSRiC
https://shorturl.fm/tqyNt
https://shorturl.fm/Pg3mo
https://shorturl.fm/LQZdg
https://shorturl.fm/ENTJx
https://shorturl.fm/YnmbE
https://shorturl.fm/ZT56P
https://shorturl.fm/XVaZa
https://shorturl.fm/HWPH6
https://shorturl.fm/mrsNP
https://shorturl.fm/4qoXD
Clara yu wapi????
Mapenzi ya Jacob na Zaylisa yaliishia wapi baada ya Jacob kurudisha kumbukumbu??
Mzee wa mipango alikuwa nani na alikuwa na mipango gani?
haahir
https://shorturl.fm/lafTz
https://shorturl.fm/J6WAC
https://shorturl.fm/8zpt5
https://shorturl.fm/e9KsE
gkthqvhysjopgwjftyehhqdqeldzzs
loqmppnvzedojpysuqflpdfxzfukyv
**mindvault**
mindvault is a premium cognitive support formula created for adults 45+. It’s thoughtfully designed to help maintain clear thinking
https://shorturl.fm/sJhBP
https://shorturl.fm/dQ6cP
https://shorturl.fm/U8JDr
https://shorturl.fm/tkv5X
https://shorturl.fm/yblMZ
upcfrg
https://shorturl.fm/BUEc9
https://shorturl.fm/me54m
https://shorturl.fm/PFXZN
房中秘术、泡妞把妹、丰胸美体、奇淫巧技!价值十万电子书下载网址:https://www.1199.pw/
https://shorturl.fm/qCu5t
Bulk commenting service. 100,000 comments on independent websites for $100 or 1000,000 comments for $500. You can read this comment, it means my bulk sending is successful. Payment account-USDT TRC20:【TLRH8hompAphv4YJQa7Jy4xaXfbgbspEFK】。After payment, contact me via email (helloboy1979@gmail.com),tell me your nickname, email, website URL, and comment content. Bulk sending will be completed within 24 hours. I’ll give you links for each comment.Please contact us after payment is made. We do not respond to inquiries prior to payment. Let’s work with integrity for long-term cooperation.
https://shorturl.fm/wAqhF
https://shorturl.fm/APkY8
https://shorturl.fm/NyF6T
https://shorturl.fm/6cElk
https://shorturl.fm/gRzqz
https://shorturl.fm/9WnK9
https://shorturl.fm/h7NIV
https://shorturl.fm/GOH3x
https://shorturl.fm/t00lL
https://shorturl.fm/vjWZ7
https://shorturl.fm/4FvxH
**prostadine**
prostadine is a next-generation prostate support formula designed to help maintain, restore, and enhance optimal male prostate performance.
https://shorturl.fm/2Ficl
https://shorturl.fm/qqClv
尖端资源,价值百万,一网打尽,瞬间拥有!多重收益,五五倍增,八级提成,后劲无穷!摸币网,最嚣张的上线替下线赚钱网站:https://1925.mobi/
https://shorturl.fm/76oPp
https://shorturl.fm/XebMH
https://shorturl.fm/RiRjB
**sugarmute**
sugarmute is a science-guided nutritional supplement created to help maintain balanced blood sugar while supporting steady energy and mental clarity.
npwyhkxjxntjxoxqpuylljforsfjmk
nnokntlwfexsdxmhgvdqsnvimszrvv
https://shorturl.fm/1J3Tl
https://shorturl.fm/iv7OG
**glpro**
glpro is a natural dietary supplement designed to promote balanced blood sugar levels and curb sugar cravings.
https://shorturl.fm/Hh5Cy
https://shorturl.fm/eYkUn
**zencortex**
zencortex contains only the natural ingredients that are effective in supporting incredible hearing naturally.
**mitolyn**
mitolyn a nature-inspired supplement crafted to elevate metabolic activity and support sustainable weight management.
**yusleep**
yusleep is a gentle, nano-enhanced nightly blend designed to help you drift off quickly, stay asleep longer, and wake feeling clear.
**prodentim**
prodentim an advanced probiotic formulation designed to support exceptional oral hygiene while fortifying teeth and gums.
**synaptigen**
synaptigen is a next-generation brain support supplement that blends natural nootropics, adaptogens
**vitta burn**
vitta burn is a liquid dietary supplement formulated to support healthy weight reduction by increasing metabolic rate, reducing hunger, and promoting fat loss.
**nitric boost**
nitric boost is a dietary formula crafted to enhance vitality and promote overall well-being.
**glucore**
glucore is a nutritional supplement that is given to patients daily to assist in maintaining healthy blood sugar and metabolic rates.
https://shorturl.fm/CxJNa
**wildgut**
wildgutis a precision-crafted nutritional blend designed to nurture your dog’s digestive tract.
**pineal xt**
pinealxt is a revolutionary supplement that promotes proper pineal gland function and energy levels to support healthy body function.
**energeia**
energeia is the first and only recipe that targets the root cause of stubborn belly fat and Deadly visceral fat.
**boostaro**
boostaro is a specially crafted dietary supplement for men who want to elevate their overall health and vitality.
**prostabliss**
prostabliss is a carefully developed dietary formula aimed at nurturing prostate vitality and improving urinary comfort.
https://shorturl.fm/YbBfL
**potentstream**
potentstream is engineered to promote prostate well-being by counteracting the residue that can build up from hard-water minerals within the urinary tract.
**hepato burn**
hepato burn is a premium nutritional formula designed to enhance liver function, boost metabolism, and support natural fat breakdown.
**breathe**
breathe is a plant-powered tincture crafted to promote lung performance and enhance your breathing quality.
https://shorturl.fm/5EeRO
**hepato burn**
hepato burn is a potent, plant-based formula created to promote optimal liver performance and naturally stimulate fat-burning mechanisms.
https://shorturl.fm/NFQE2
https://shorturl.fm/ODAyi
**cellufend**
cellufend is a natural supplement developed to support balanced blood sugar levels through a blend of botanical extracts and essential nutrients.
**prodentim**
prodentim is a forward-thinking oral wellness blend crafted to nurture and maintain a balanced mouth microbiome.
https://shorturl.fm/iHsrj
**neurogenica**
neurogenica is a dietary supplement formulated to support nerve health and ease discomfort associated with neuropathy.
**revitag**
revitag is a daily skin-support formula created to promote a healthy complexion and visibly diminish the appearance of skin tags.
**flowforce max**
flowforce max delivers a forward-thinking, plant-focused way to support prostate health—while also helping maintain everyday energy, libido, and overall vitality.
https://shorturl.fm/hqUCY
**sleep lean**
sleeplean is a US-trusted, naturally focused nighttime support formula that helps your body burn fat while you rest.
https://shorturl.fm/4pUXn
https://shorturl.fm/ppR0s
**memorylift**
memorylift is an innovative dietary formula designed to naturally nurture brain wellness and sharpen cognitive performance.
https://shorturl.fm/chmHo
https://shorturl.fm/IfzZR
https://shorturl.fm/FfdVh
https://shorturl.fm/Zhph1
https://shorturl.fm/pl0tL
真免费!价值万元资源,不要一分钱,网址:https://www.53278.xyz/
https://shorturl.fm/cctIg
https://shorturl.fm/QuD8x
https://shorturl.fm/ZXve3
https://shorturl.fm/5WXxP
https://shorturl.fm/JPLbr
https://shorturl.fm/3XmVb
https://shorturl.fm/76eA4
https://shorturl.fm/MbkNg
https://shorturl.fm/ZMd7o
https://shorturl.fm/ZMd7o
https://shorturl.fm/2Mvt8
Turkey sightseeing tours Rebecca W. – İzlanda http://www.tecnoac.com/?p=56090
Turkey historical tours Wonderful Turkey tours! Professional organization from airport pickup to final goodbye. Flawless experience. https://evolvff.com/?p=3712
https://shorturl.fm/kmfje
https://shorturl.fm/kzwSH
https://shorturl.fm/cNHtp
https://shorturl.fm/oEYt3
https://shorturl.fm/m9D3C
https://shorturl.fm/uv9z9
https://shorturl.fm/uv9z9
https://shorturl.fm/SMgyt
https://shorturl.fm/wBpUO
https://shorturl.fm/bFmmt
https://shorturl.fm/gMcyd
https://shorturl.fm/whWw4
https://shorturl.fm/yyG2n
益群网:终身分红,逆向推荐,不拉下线,也有钱赚!尖端资源,价值百万,一网打尽,瞬间拥有!多重收益,五五倍增,八级提成,后劲无穷!网址:1199.pw
https://shorturl.fm/0nzPH
https://shorturl.fm/NspyJ
https://shorturl.fm/X1dHU
https://shorturl.fm/C3JkN
https://t.me/s/Top_BestCasino/135