Ilipoishia sehemu ya kwanza ya In the name of LOVE
“Ndiyo, nilikua napita tu.”
“Kuna harusi”
“Harusi?”
“Ndiyo, vipi umeshtuka Mzee?”
“Nani anaolewa?”
“Mtoto wa Mwenye nyumba anaolewa, anaitwa Zaylisa” alisema Kisha aliondoka zake, hakujua alikua ameupasua moyo Wangu kiasi gani, hakujua alikua ameuunguza moyo Wangu kwa kiasi gani. Chozi la pole pole lilianza kunitoka, nilihisi kuishiwa nguvu. Endelea
SEHEMU YA PILI
Nilitegemea kusikia vyote lakini siyo kuolewa kwa Zaylisa, sikutarajia. Kwa jinsi Zaylisa alivyokua ananipenda ilikua ngumu kuyaamini Yale maneno, nilihisi ilikua ni njozi ya kutisha niamke. Nilitetemeka mwili mzima, Kila kiungo kiliuliza maswali yasiyo na Majibu.
Magari ya Kifahari yalikua nje ya Geti, chozi lilinibubujika kama Mtoto. Sikutaka kuukubali ule ukweli, sikutaka kuyaamini Yale maneno ya yule jamaa. Niliona ni Bora niingie ndani kushuhudia nilichokisikia. Nilitembea taratibu kama Mgonjwa wa Miguu.
Nilisali ili nisione nilichokisikia, nilipofika getini nilianza kusikia muziki wa sauti ya chini, niliingia taratibu Hadi ndani ya Uzio mahali ambapo niliona tukio likifanyika. Ndiyo! Alikua akivishwa Pete mbele ya macho yangu, ndelemo na vificho vilisikika
Kila mmoja alifurahia tukio Hilo isipokua Mimi, nilitoka ndani haraka sikutaka kuendelea kujiumiza. Zaylisa alikua akiolewa, niliondoka nikikimbia kurudi nyumbani kwa Sudi huku nikilia kama Mtoto njia nzima. Mapenzi yanaumiza, mapenzi yanatesa sana, ni Bora kuyasikia kwa Mtu lakini usiombe yakukute
Sikua na kazi, nilimpoteza Mama yangu, lakini mbaya zaidi ni yule niliyemtegemea Angekua kimbilio kwangu alikua akiolewa. Nilihisi kuchanganikiwa, nilihisi nimeingiwa na wazimu
Nilikimbia hovyo kukatisha barabara, ghafla niligongwa na gari. Sikuona chochote wala kusikia chochote tena, sikuelewa kilichoendelea baada ya pale.
**
Niliipata fahamu zangu baada ya ile ajali kutokea. Nilipotuliza akili vizuri nilitazama ukutani, niliona picha ya Mzee Mmoja mwenye asili ya kihindi. Nilikua na maumivu makali sana ya kichwa, hapakua na yeyote mle chumbani.
Niliyoyaona yalinifanya nigundue kua nilikua wodini, palikua na mashine ya kupima mapigo ya Moyo. Vifaa kadhaa vya matibabu, nilijiuliza nilikua wapi na kwanini? Lakini kitu kingine nilichojiuliza na kilicho nisumbua zaidi ni kutaka kujua Nimefikaje pale
Pale pale aliingia nesi mmoja. Alikua na asili ya Kihindi, alisogea pole pole huku akitabasamu Kisha aliniuliza ninajisikiaje, sikumjibu chochote kwasababu Bado nilikua na maswali chungu nzima.
Mara akaingia Mwanamke mmoja mweupe, mrefu kiasi. Alikua amevalia gauni Jekundu, alikua akinitazama kwa furaha na tabamu Kisha aliniita
“Jacob” nilipomtazama sikumfahamu kabisa, lakini yeye alionekana ananifahamu Mimi.
“Wewe ni Nani?” nilimuuliza, swali langu lilimpa simanzi, alipoteza Nuru machoni pake Kisha aliniangalia kwa Mshangao mkubwa halafu akamtazama yule Nesi.
“Subiri nimwite Daktari” akasema yule Nesi, haraka akaondoka pale.
“Jacob umenisahau tena? Mimi ni Clara” alisema, Bado alikua akinishangaa kwa kutomfahamu. Kiukweli sikukumbuka kama niliwahi kumwona popote pale. Niliendelea kumtazama
“Umesahau Mimi nilikua na wewe ule Usiku ulipopoteza Mama Yako? Haukumbuki siku ile nilikesha kwa ajili Yako na Mdogo wako Melisa?”
Alisema, niliona namna alivyokua akipitia wakati mgumu kunieleza mambo ambayo nilikua siyakumbuki.
“Mama na Mdogo wangu?”
“Ndiyo, umenikumbuka?”
“Sikumbuki chochote, Nimefikaje hapa?”
“Jacob, ulipata ajali…” kabla hajasema zaidi, aliingia Daktari pale wodini Kisha akamwambia Clara.
“Taratibu, alipata ajali mbaya na huwenda kwasasa hakumbuki chochote, Jacob….unajisikiaje?”
“Maumivu ya Kichwa, lakini huyu Mwanamke anasema nini kuhusu Mimi, mbona sielewi?” niliuliza, Daktari akatabasamu Kisha akaniambia
“Ulipata ajali mbaya Jacob, umekaa bila fahamu kwa Miezi mitatu, upo India kwa matibabu. Leo Ndiyo unazinduka, usijali utakumbuka taratibu” alisema , Kila nilichokisikia kilikua kigeni masikioni mwangu. Nilikua sikumbuki chochote kile zaidi ya kushangaa nilivyokua ninaambiwa, nilipoteza kumbukumbu zangu zote za Maisha yangu.
Nilijiuliza kuhusu Mama na Melisa lakini sikuwakumbuka. Sikukumbuka chochote kuhusu Maisha yangu yaliyopita. Nilijisikia huzuni kubwa, kitu pekee nilichokumbuka kilikua ni jina langu.
Basi, niliendelea na matibabu taratibu siku Hadi siku. Nilianza kuimarika kadili siku zilivyo songa, Mtu pekee aliyeonesha kunifahamu alikua ni Clara, akaniambia siku tukirudi Tanzania atanipeleka kwa Watu wanaonifahamu hasa Mdogo wangu Melisa. Nilifurahi pia nilijilazimisha kukumbuka lakini iliniwia ugumu sana kukumbuka kuhusu Maisha yangu ya nyuma.
Baada ya ajali nilihamishwa kutoka Hospitali ya Muhimbili na kuelekea India kwa ajili ya Matibabu.
“Jacob, wewe ni Mtu mzuri sana lakini ulipitia kipindi kigumu sana. Najutia kukugonga na gari siku ile, pengine Leo hii ungekua pamoja na Mdogo wako” alisema Clara tukiwa kwenye viunga vya Hospitali akinifanyisha mazoezi.
“Usijali, natamani nikukumbuke Clara. Pengine una kumbukumbu nzuri kwangu” nilisema, Clara akatabasamu tu Kisha akaniambia
“Hakuna kumbukumbu nyingi kuhusu Mimi na wewe, Mimi nilikua mteja kwenye Mgahawa uliokua ukifanyia kazi. Zaidi ya hapo hakuna nyingine Jacob, tumekutana mara chache sana”
“Natamani kukumbuka nilijisikiaje baada ya kumpoteza Mama yangu, ilikuwaje kuhusu Mdogo wangu Melisa”
“Tartibu Jacob, tukifika Tanzania utaelewa vingi”
“Hakuna Mtu niliyempenda?” nilimuuliza, alinitazama kwa sekunde kadhaa Kisha aliachia tabasamu la kupangusa akanijibu taratibu kwa sauti ya Upole akasema
“Nasikia ulimpenda Mwanamke mmoja anaitwa Zaylisa. Sijui kuhusu wewe na yeye lakini inaonesha ni Mwanamke anayekupa furaha sana” alisema Kisha alitabasamu, nilicheka kidogo
“Kwnini hakufika huku kama alikua ananipenda sana?”
“Sidhani kama alikua anajua kua umepata matatizo. Samahani Jacob, sikuweza hata kumtafuta Mdogo wako kumweleza kutokana na namna nilivyokua nimechanganikiwa. Huko aliko atakua na huzuni sana”
“Natamani kumwona pengine nitajikumbuka Clara. Namwomba Mungu nizirejee kumbukumbu zangu, natamani kumwona Zaylisa nijue anafananaje Hadi tukapendana hivyo” nilisema tukawa tunacheka na kupiga stori za hapa na pale, akanifanya nijihisi amani sana Moyoni mwangu lakini kumbukumbu zilizopotea zilinitesa sana.
Kila nilivyofikiria kuhusu Maisha nilijiona nimepoteza vitu vingi muhimu lakini sikujua ni vitu gani, Maisha yalinifundisha kuishi bila kua na chochote. Niliendelea na matibabu kwa muda wa wiki mbili zaidi Hadi pale Madaktari walipoona naruhusiwa kurejea Tanzania.
Clara ndiye Mtu pekee niliyekua namwona. Basi, tulirudi Tanzania Kwa kutumia shirika la ndege la Air Tanzania, Clara alinipeleka kwanza nyumbani kwake. Alikua ana uwezo kifedha, alinitendea vizuri sana, alikua mkarimu na mwenye kunijali sana. Mara kadhaa aliniuliza kuhusu hisia ya Upendo, kusema ukweli sikuwahi kua na hisia ya Upendo na sijui kama niliwahi kua nayo huko nyuma.
“Clara, naomba unipeleke nikamwone Melisa. Nataka kukumbuka kuhusu yeye” nilimwambia Clara, tulikua mezani tukipata chakula Cha Usiku. Alitabasamu kidogo Kisha akaniambia
“Siwezi kupasahau, nitahakikisha unamwona Jacob. Natamani upate kumbukumbu zako tena” alisema, mara zote alikua chanya kwangu, hakuwahi kunikatisha tamaa.
“Anafanana na Mimi, au yeye ni mkarimu kama wewe. Nataka kujua nilikua nampenda sana Melisa?” Maswali yangu yalimfanya atabasamu kidogo, akapiga funda Moja la juisi kabla ya kunijibu.
“Unampenda sana, hamjafanana sana lakini kitu pekee kwake ni kua anakupenda sana nawe unampenda sana. Siku ile alipopoteza fahamu baada ya Kifo Cha Mama yenu, ulichanganikiwa sana, haukua hivyo bila sababu isipokua Upendo”
Chozi lilianza kunibubujika, nilijihisi ni mwenye hatia japo nilikua sikumbuki, Clara alisema Melisa hakua na taarifa ya ajali yangu hivyo alikua mpweke asijuwe Niko wapi kwa Miezi mitatu. Kipindi hicho kilitosha kumfanya apoteze tumaini.
Iliniumiza sana “Usilie Jacob, kesho utaonana na Mdogo wako. Naamini utapata kumbukumbu kuhusu yeye, atafurahi sana akikuona.” Alisema Clara, nilifuta chozi langu Kisha nilimwambia Clara
“Usinichoke Clara, sikumbuki chochote. Naomba univumilie tafadhali”
“Usijali, Ndiyo Maisha Jacob. Kupoteza au kutokupoteza hakuondoi maana ya wewe kua Binadamu mzuri sawa?”
“Asante Clara” nilisema Kisha niliinuka na kuelekea Chumbani, sikuacha kulia kwasababu nilikua gizani. Kila nilichokiona, Kila niliyemwona alikua mpya kwangu. Mazingira, Hali ya hewa vyote nilihisi kama niliviona kwa mara ya kwanza. Ilitosha kunitesa kiakili, sikubakisha kumbukumbu yoyote zaidi ya Jina langu la Jacob.
Usiku ulikua mrefu sana, nilipepesa macho yangu Usiku kucha huku nilifikiria namna nitakavyo mkumbatia mdogo wangu, namna atakavyolia akiniona, namna nitakavyo rejesha kumbukumbu zangu. Hadi kunapambazuka nilikua sijapata hata lepe la Usingizi
Nilimwamsha Clara kwa kumgongea mlango wake, sikutaka kuchelewa
“Eeh Jacob” alisema Clara baada ya kufungua mlango, alikua amejawa na Usingizi.
“Za Asubuhi, Clara”
“Nzuri, vipi wewe?”
“Nipo salama. Pole, nimekatisha Usingizi wako, nimeshindwa kupata pumziko”
“Usijali, naelewa Jacob. Hata kama ningelikua Mimi ningelikua hivyo, sasa Wacha nijiandae nawe tafadhali jiandae tupate chai Kisha tuondoke” alisema, nilitabasamu Kisha nilirudi chumbani.
Sikukumbuka Melisa angependa nini, nilivalia nguo nilizozipenda. Nilijiandaa haraka haraka Kisha nilielekea Sebleni, wakati nafika Clara naye alikua akitoka chumbani kwake. Tukapata chai pamoja, Kisha tuliondoka kwa kutumia gari la Clara.
“Haukumbuki chochote Bado Jacob?”
“Sikumbuki chochote Clara, natamani nikumbuke ili nijuwe tunapoelekea”
“Hofu ondoa, Kila kitu kinahitaji muda kukifahamu. Jipe muda zaidi, usikimbie sana Bali taratibu utakumbuka hatua kwa hatua J” ilikua ni safari ya wastani wa saa nzima, Hadi tulipofika mtaani.
“Gari haiwezi kufika Hadi kule, hivyo tutatembea” alisema Clara, tuliacha gari mahali Kisha tulishuka na kuanza kutembea. Tulikatisha maeneo kadhaa, nilimwona Clara akinitazama sana ili kuona kama nilikua nikiikumbuka mitaa hiyo, sikukumbuka kabisa.
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya PILI
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx

51 Comments
https://shorturl.fm/KnZqN
https://shorturl.fm/Ux12y
https://shorturl.fm/030Bu
https://shorturl.fm/Toiio
https://shorturl.fm/XXKCQ
https://shorturl.fm/GX3yv
https://shorturl.fm/HiO2p
jlaitq
https://shorturl.fm/2ulY0
https://shorturl.fm/euOo2
Tuendelee
https://shorturl.fm/PBOeI
https://shorturl.fm/ATM11
https://shorturl.fm/B7C4w
https://shorturl.fm/h7pCU
https://shorturl.fm/4Tp4W
https://shorturl.fm/d6K5g
https://shorturl.fm/1fX40
https://shorturl.fm/tdpDU
https://shorturl.fm/ZiLNl
https://shorturl.fm/M5rGY
https://shorturl.fm/LdDeC
https://shorturl.fm/R4hMD
**mindvault**
mindvault is a premium cognitive support formula created for adults 45+. It’s thoughtfully designed to help maintain clear thinking
**prostadine**
prostadine is a next-generation prostate support formula designed to help maintain, restore, and enhance optimal male prostate performance.
**sugarmute**
sugarmute is a science-guided nutritional supplement created to help maintain balanced blood sugar while supporting steady energy and mental clarity.
**gl pro**
gl pro is a natural dietary supplement designed to promote balanced blood sugar levels and curb sugar cravings.
**zencortex**
zencortex contains only the natural ingredients that are effective in supporting incredible hearing naturally.
**mitolyn**
mitolyn a nature-inspired supplement crafted to elevate metabolic activity and support sustainable weight management.
**yusleep**
yusleep is a gentle, nano-enhanced nightly blend designed to help you drift off quickly, stay asleep longer, and wake feeling clear.
**prodentim**
prodentim an advanced probiotic formulation designed to support exceptional oral hygiene while fortifying teeth and gums.
**synaptigen**
synaptigen is a next-generation brain support supplement that blends natural nootropics, adaptogens
**vittaburn**
vittaburn is a liquid dietary supplement formulated to support healthy weight reduction by increasing metabolic rate, reducing hunger, and promoting fat loss.
**nitric boost**
nitric boost is a dietary formula crafted to enhance vitality and promote overall well-being.
**glucore**
glucore is a nutritional supplement that is given to patients daily to assist in maintaining healthy blood sugar and metabolic rates.
**wildgut**
wildgutis a precision-crafted nutritional blend designed to nurture your dog’s digestive tract.
**pinealxt**
pinealxt is a revolutionary supplement that promotes proper pineal gland function and energy levels to support healthy body function.
**energeia**
energeia is the first and only recipe that targets the root cause of stubborn belly fat and Deadly visceral fat.
**boostaro**
boostaro is a specially crafted dietary supplement for men who want to elevate their overall health and vitality.
**prostabliss**
prostabliss is a carefully developed dietary formula aimed at nurturing prostate vitality and improving urinary comfort.
**potent stream**
potent stream is engineered to promote prostate well-being by counteracting the residue that can build up from hard-water minerals within the urinary tract.
**hepato burn**
hepato burn is a premium nutritional formula designed to enhance liver function, boost metabolism, and support natural fat breakdown.
**breathe**
breathe is a plant-powered tincture crafted to promote lung performance and enhance your breathing quality.
**hepato burn**
hepato burn is a potent, plant-based formula created to promote optimal liver performance and naturally stimulate fat-burning mechanisms.
**cellufend**
cellufend is a natural supplement developed to support balanced blood sugar levels through a blend of botanical extracts and essential nutrients.
**prodentim**
prodentim is a forward-thinking oral wellness blend crafted to nurture and maintain a balanced mouth microbiome.
**neurogenica**
neurogenica is a dietary supplement formulated to support nerve health and ease discomfort associated with neuropathy.
**revitag**
revitag is a daily skin-support formula created to promote a healthy complexion and visibly diminish the appearance of skin tags.
**flowforce max**
flowforce max delivers a forward-thinking, plant-focused way to support prostate health—while also helping maintain everyday energy, libido, and overall vitality.
**sleeplean**
sleeplean is a US-trusted, naturally focused nighttime support formula that helps your body burn fat while you rest.
**memory lift**
memory lift is an innovative dietary formula designed to naturally nurture brain wellness and sharpen cognitive performance.