Ilipoishia sehemu ya kwanza ya In the name of LOVE
โNdiyo, nilikua napita tu.โย
โKuna harusiโย
โHarusi?โย
โNdiyo, vipi umeshtuka Mzee?โย
โNani anaolewa?โย
โMtoto wa Mwenye nyumba anaolewa, anaitwa Zaylisaโ alisema Kishaย aliondoka zake, hakujua alikua ameupasua moyo Wangu kiasi gani, hakujuaย alikua ameuunguza moyo Wangu kwa kiasi gani. Chozi la pole pole lilianzaย kunitoka, nilihisi kuishiwa nguvu. Endelea
SEHEMU YA PILI
Nilitegemea kusikia vyote lakini siyo kuolewa kwa Zaylisa, sikutarajia. Kwaย jinsi Zaylisa alivyokua ananipenda ilikua ngumu kuyaamini Yale maneno,ย nilihisi ilikua ni njozi ya kutisha niamke. Nilitetemeka mwili mzima, Kilaย kiungo kiliuliza maswali yasiyo na Majibu.ย
Magari ya Kifahari yalikua nje ya Geti, chozi lilinibubujika kama Mtoto.ย Sikutaka kuukubali ule ukweli, sikutaka kuyaamini Yale maneno ya yuleย jamaa. Niliona ni Bora niingie ndani kushuhudia nilichokisikia. Nilitembeaย taratibu kama Mgonjwa wa Miguu.ย ย
Nilisali ili nisione nilichokisikia, nilipofika getini nilianza kusikia muziki waย sauti ya chini, niliingia taratibu Hadi ndani ya Uzio mahali ambapo nilionaย tukio likifanyika. Ndiyo! Alikua akivishwa Pete mbele ya macho yangu,ย ndelemo na vificho vilisikikaย
Kila mmoja alifurahia tukio Hilo isipokua Mimi, nilitoka ndani harakaย sikutaka kuendelea kujiumiza. Zaylisa alikua akiolewa, niliondokaย nikikimbia kurudi nyumbani kwa Sudi huku nikilia kama Mtoto njia nzima.ย Mapenzi yanaumiza, mapenzi yanatesa sana, ni Bora kuyasikia kwa Mtuย lakini usiombe yakukuteย
Sikua na kazi, nilimpoteza Mama yangu, lakini mbaya zaidi ni yuleย niliyemtegemea Angekua kimbilio kwangu alikua akiolewa. Nilihisiย kuchanganikiwa, nilihisi nimeingiwa na wazimuย
Nilikimbia hovyo kukatisha barabara, ghafla niligongwa na gari. Sikuonaย chochote wala kusikia chochote tena, sikuelewa kilichoendelea baada yaย pale.ย
**ย
Niliipata fahamu zangu baada ya ile ajali kutokea. Nilipotuliza akili vizuriย nilitazama ukutani, niliona picha ya Mzee Mmoja mwenye asili ya kihindi.ย Nilikua na maumivu makali sana ya kichwa, hapakua na yeyote mleย chumbani.ย
Niliyoyaona yalinifanya nigundue kua nilikua wodini, palikua na mashineย ya kupima mapigo ya Moyo. Vifaa kadhaa vya matibabu, nilijiuliza nilikuaย wapi na kwanini? Lakini kitu kingine nilichojiuliza na kilicho nisumbua zaidi ni kutaka kujua Nimefikaje paleย
Pale pale aliingia nesi mmoja. Alikua na asili ya Kihindi, alisogea pole poleย huku akitabasamu Kisha aliniuliza ninajisikiaje, sikumjibu chochoteย kwasababu Bado nilikua na maswali chungu nzima.ย
Mara akaingia Mwanamke mmoja mweupe, mrefu kiasi. Alikua amevaliaย gauni Jekundu, alikua akinitazama kwa furaha na tabamu Kisha aliniitaย
โJacobโ nilipomtazama sikumfahamu kabisa, lakini yeye alionekanaย ananifahamu Mimi.ย
โWewe ni Nani?โ nilimuuliza, swali langu lilimpa simanzi, alipoteza Nuruย machoni pake Kisha aliniangalia kwa Mshangao mkubwa halafuย akamtazama yule Nesi.ย
โSubiri nimwite Daktariโ akasema yule Nesi, haraka akaondoka pale.ย
โJacob umenisahau tena? Mimi ni Claraโ alisema, Bado alikuaย akinishangaa kwa kutomfahamu. Kiukweli sikukumbuka kama niliwahiย kumwona popote pale. Niliendelea kumtazama
โUmesahau Mimi nilikua na wewe ule Usiku ulipopoteza Mama Yako? Haukumbuki siku ile nilikesha kwa ajili Yako na Mdogo wako Melisa?โย ย
Alisema, niliona namna alivyokua akipitia wakati mgumu kunieleza mamboย ambayo nilikua siyakumbuki.ย
โMama na Mdogo wangu?โย
โNdiyo, umenikumbuka?โย
โSikumbuki chochote, Nimefikaje hapa?โย ย
โJacob, ulipata ajaliโฆโ kabla hajasema zaidi, aliingia Daktari pale wodiniย Kisha akamwambia Clara.ย
โTaratibu, alipata ajali mbaya na huwenda kwasasa hakumbuki chochote,ย Jacobโฆ.unajisikiaje?โย ย
โMaumivu ya Kichwa, lakini huyu Mwanamke anasema nini kuhusu Mimi,ย mbona sielewi?โ niliuliza, Daktari akatabasamu Kisha akaniambiaย
โUlipata ajali mbaya Jacob, umekaa bila fahamu kwa Miezi mitatu, upoย India kwa matibabu. Leo Ndiyo unazinduka, usijali utakumbuka taratibuโย alisema , Kila nilichokisikia kilikua kigeni masikioni mwangu. Nilikuaย sikumbuki chochote kile zaidi ya kushangaa nilivyokua ninaambiwa,ย nilipoteza kumbukumbu zangu zote za Maisha yangu.ย
Nilijiuliza kuhusu Mama na Melisa lakini sikuwakumbuka. Sikukumbukaย chochote kuhusu Maisha yangu yaliyopita. Nilijisikia huzuni kubwa, kituย pekee nilichokumbuka kilikua ni jina langu.ย
Basi, niliendelea na matibabu taratibu siku Hadi siku. Nilianza kuimarikaย kadili siku zilivyo songa, Mtu pekee aliyeonesha kunifahamu alikua niย Clara, akaniambia siku tukirudi Tanzania atanipeleka kwa Watuย wanaonifahamu hasa Mdogo wangu Melisa. Nilifurahi pia nilijilazimishaย kukumbuka lakini iliniwia ugumu sana kukumbuka kuhusu Maisha yanguย ya nyuma.ย
Baada ya ajali nilihamishwa kutoka Hospitali ya Muhimbili na kuelekeaย India kwa ajili ya Matibabu.ย ย
โJacob, wewe ni Mtu mzuri sana lakini ulipitia kipindi kigumu sana.ย Najutia kukugonga na gari siku ile, pengine Leo hii ungekua pamoja naย Mdogo wakoโ alisema Clara tukiwa kwenye viunga vya Hospitaliย akinifanyisha mazoezi.
โUsijali, natamani nikukumbuke Clara. Pengine una kumbukumbu nzuriย kwanguโ nilisema, Clara akatabasamu tu Kisha akaniambiaย
โHakuna kumbukumbu nyingi kuhusu Mimi na wewe, Mimi nilikua mtejaย kwenye Mgahawa uliokua ukifanyia kazi. Zaidi ya hapo hakuna nyingineย Jacob, tumekutana mara chache sanaโย ย
โNatamani kukumbuka nilijisikiaje baada ya kumpoteza Mama yangu,ย ilikuwaje kuhusu Mdogo wangu Melisaโย ย
โTartibu Jacob, tukifika Tanzania utaelewa vingiโย
โHakuna Mtu niliyempenda?โ nilimuuliza, alinitazama kwa sekundeย kadhaa Kisha aliachia tabasamu la kupangusa akanijibu taratibu kwa sautiย ya Upole akasemaย
โNasikia ulimpenda Mwanamke mmoja anaitwa Zaylisa. Sijui kuhusu weweย na yeye lakini inaonesha ni Mwanamke anayekupa furaha sanaโ alisemaย Kisha alitabasamu, nilicheka kidogoย
โKwnini hakufika huku kama alikua ananipenda sana?โย
โSidhani kama alikua anajua kua umepata matatizo. Samahani Jacob,ย sikuweza hata kumtafuta Mdogo wako kumweleza kutokana na namnaย nilivyokua nimechanganikiwa. Huko aliko atakua na huzuni sanaโย
โNatamani kumwona pengine nitajikumbuka Clara. Namwomba Munguย nizirejee kumbukumbu zangu, natamani kumwona Zaylisa nijueย anafananaje Hadi tukapendana hivyoโ nilisema tukawa tunacheka naย kupiga stori za hapa na pale, akanifanya nijihisi amani sana Moyoniย mwangu lakini kumbukumbu zilizopotea zilinitesa sana.ย
Kila nilivyofikiria kuhusu Maisha nilijiona nimepoteza vitu vingi muhimuย lakini sikujua ni vitu gani, Maisha yalinifundisha kuishi bila kua naย chochote. Niliendelea na matibabu kwa muda wa wiki mbili zaidi Hadi paleย Madaktari walipoona naruhusiwa kurejea Tanzania.ย
Clara ndiye Mtu pekee niliyekua namwona. Basi, tulirudi Tanzania Kwaย kutumia shirika la ndege la Air Tanzania, Clara alinipeleka kwanzaย nyumbani kwake. Alikua ana uwezo kifedha, alinitendea vizuri sana, alikuaย mkarimu na mwenye kunijali sana. Mara kadhaa aliniuliza kuhusu hisia yaย Upendo, kusema ukweli sikuwahi kua na hisia ya Upendo na sijui kamaย niliwahi kua nayo huko nyuma.
โClara, naomba unipeleke nikamwone Melisa. Nataka kukumbuka kuhusuย yeyeโ nilimwambia Clara, tulikua mezani tukipata chakula Cha Usiku.ย Alitabasamu kidogo Kisha akaniambiaย
โSiwezi kupasahau, nitahakikisha unamwona Jacob. Natamani upateย kumbukumbu zako tenaโ alisema, mara zote alikua chanya kwangu,ย hakuwahi kunikatisha tamaa.ย ย
โAnafanana na Mimi, au yeye ni mkarimu kama wewe. Nataka kujua nilikuaย nampenda sana Melisa?โ Maswali yangu yalimfanya atabasamu kidogo,ย akapiga funda Moja la juisi kabla ya kunijibu.ย ย
โUnampenda sana, hamjafanana sana lakini kitu pekee kwake ni kuaย anakupenda sana nawe unampenda sana. Siku ile alipopoteza fahamuย baada ya Kifo Cha Mama yenu, ulichanganikiwa sana, haukua hivyo bilaย sababu isipokua Upendoโย ย
Chozi lilianza kunibubujika, nilijihisi ni mwenye hatia japo nilikuaย sikumbuki, Clara alisema Melisa hakua na taarifa ya ajali yangu hivyoย alikua mpweke asijuwe Niko wapi kwa Miezi mitatu. Kipindi hicho kilitoshaย kumfanya apoteze tumaini.ย ย
Iliniumiza sana โUsilie Jacob, kesho utaonana na Mdogo wako. Naaminiย utapata kumbukumbu kuhusu yeye, atafurahi sana akikuona.โ Alisemaย Clara, nilifuta chozi langu Kisha nilimwambia Claraย
โUsinichoke Clara, sikumbuki chochote. Naomba univumilie tafadhaliโย
โUsijali, Ndiyo Maisha Jacob. Kupoteza au kutokupoteza hakuondoi maanaย ya wewe kua Binadamu mzuri sawa?โย ย
โAsante Claraโ nilisema Kisha niliinuka na kuelekea Chumbani, sikuachaย kulia kwasababu nilikua gizani. Kila nilichokiona, Kila niliyemwona alikuaย mpya kwangu. Mazingira, Hali ya hewa vyote nilihisi kama niliviona kwaย mara ya kwanza. Ilitosha kunitesa kiakili, sikubakisha kumbukumbu yoyoteย zaidi ya Jina langu la Jacob.ย
Usiku ulikua mrefu sana, nilipepesa macho yangu Usiku kucha hukuย nilifikiria namna nitakavyo mkumbatia mdogo wangu, namna atakavyoliaย akiniona, namna nitakavyo rejesha kumbukumbu zangu. Hadiย kunapambazuka nilikua sijapata hata lepe la Usingiziย ย
Nilimwamsha Clara kwa kumgongea mlango wake, sikutaka kuchelewaย
โEeh Jacobโ alisema Clara baada ya kufungua mlango, alikua amejawa naย Usingizi.
โZa Asubuhi, Claraโย
โNzuri, vipi wewe?โย
โNipo salama. Pole, nimekatisha Usingizi wako, nimeshindwa kupataย pumzikoโย
โUsijali, naelewa Jacob. Hata kama ningelikua Mimi ningelikua hivyo, sasaย Wacha nijiandae nawe tafadhali jiandae tupate chai Kisha tuondokeโย alisema, nilitabasamu Kisha nilirudi chumbani.ย ย
Sikukumbuka Melisa angependa nini, nilivalia nguo nilizozipenda.ย Nilijiandaa haraka haraka Kisha nilielekea Sebleni, wakati nafika Claraย naye alikua akitoka chumbani kwake. Tukapata chai pamoja, Kishaย tuliondoka kwa kutumia gari la Clara.ย
โHaukumbuki chochote Bado Jacob?โย
โSikumbuki chochote Clara, natamani nikumbuke ili nijuwe tunapoelekeaโย
โHofu ondoa, Kila kitu kinahitaji muda kukifahamu. Jipe muda zaidi,ย usikimbie sana Bali taratibu utakumbuka hatua kwa hatua Jโ ilikua niย safari ya wastani wa saa nzima, Hadi tulipofika mtaani.ย
โGari haiwezi kufika Hadi kule, hivyo tutatembeaโ alisema Clara, tuliachaย gari mahali Kisha tulishuka na kuanza kutembea. Tulikatisha maeneoย kadhaa, nilimwona Clara akinitazama sana ili kuona kama nilikuaย nikiikumbuka mitaa hiyo, sikukumbuka kabisa.ย ย
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya PILI
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xxย
10 Comments
https://shorturl.fm/KnZqN
https://shorturl.fm/Ux12y
https://shorturl.fm/030Bu
https://shorturl.fm/Toiio
https://shorturl.fm/XXKCQ
https://shorturl.fm/GX3yv
https://shorturl.fm/HiO2p
jlaitq
https://shorturl.fm/2ulY0
https://shorturl.fm/euOo2