Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Fredy Ni Mchezaji Mzuri Akitumiwa Vizuri Ataisaidia SIMBA
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Fredy Ni Mchezaji Mzuri Akitumiwa Vizuri Ataisaidia SIMBA

    MhaririBy MhaririMay 1, 2024Updated:May 1, 20248 Comments2 Mins Read1K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Fredy Kutoka Simba
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Mimi naomba nitofautiane kidogo na wadau wengi wa Kijiweni hasahasa mashabiki wa timu hizi kubwa yaani Yanga pamoja  mashabiki wa Simba ambao  wanadai Fredy Koublan ni garasa ingawa anafunga vizuri tu pale ambapo akipata nafasi japokua huwa kuna makosa baadhi ambayo huwa yanajitokeza pale ambapo anakosa magoli. Huyu mchezaji namfananisha na The Great Khali (kwa walioangalia mieleka miaka ya 2005 watakua wanamjua vilivyo)

    Kwanza ana mwili mkubwa, ni mrefu, ameshiba pia ana nguvu ni kama the great khali ambaye ushindi wake WWE huupata kwa faida ya umbo lake na mwili wake, mbinu na ufundi sifuri, akikutana na beki ambaye ana mwili mdogo huwa ndio utaona balaa lake zaidi.

    Fredy huwa anasumbua sana mabeki akiwa na mpira ni ngumu kumpokonya maana ana nguvu kama kifaru ila hana skills nzuri za kufunga, hupenya kirahisi ndani ya 18 na ni vigumu kumpiga .mtama au kumsukuma akaanguka, ili kuweza kumshinda inabidi akabwe na watu wanne azingirwe pande zote. Beki kitasa BACCA alimshindwa akafunga, magoli mengi anayofunga ni ya kuwashinda nguvu mabeki.

    Ushauri wangu huyu mwamba achezeshwe namba 10 kwa sababu hiyo namba inahitaji mtu mwenye misuri na anayeweza kupenya kirahisi ukuta wa beki zote za kati na pembeni, Atafutwe namba tisa mwingine mwepesi mwenye mbio na Simba itapata matokeo ya haraka

    SOMA ZAIDI: Tukiyafanya Haya Kiwango Cha Mpira Tanzania Kitapanda

    808 kikosi cha simba leo simba sc

    8 Comments

    1. Fredi0 on May 1, 2024 1:35 pm

      Fred ana vigezo vyote vya kuwa striker😎

      Reply
    2. Valence on May 1, 2024 1:36 pm

      Kikubwa ashatufunga wananchi,, lazima awe striker mzuri he he

      Reply
    3. Fred on May 1, 2024 1:49 pm

      Fred ni striker alie kosa mwalimu wakutoa kilicho ndan yake
      Ila kama akipata coach mzr atakapoa kuna wachezaj tunawaona wakawaida lakin wakiwa na mtu sahihi wakua viumbe vngin kbs

      Reply
    4. Mhe.Laizer on May 1, 2024 2:41 pm

      Fredy n staiker mzuri Sema wanasimba wamekosa uvumilivu tu wa kumsubiri wawe vizuri kumbuka Ata Ayoub walimsema sanaaa lakin sahivi kila mtu anamkubali kwahyo nashauri watu wampe saport kubwa naamini atakuja kuwa striker bora zaidi ya alivyokua MK14 alipojiunga simba NI SWALA LA MUDA TU apewe msimu 1

      Reply
    5. T J on May 1, 2024 2:43 pm

      Fredy ni mchezaji mzuri yes. But kwenye timu gan?? Anahitaji kukosea mara nyingi kisha ndo afunge swali ni je, simba wanahitaji mchezaji wa aina hiyo? Jibu ni hapana, jamaa anacheza mpira wa 2000 anasubiri aletewe mali, kukaba uvivu, pressing 0 akienda kukaba unajua ni faulo, for me ni mchezaji mzuri lakini sio kwa simba, ni mchezaji wa timu ndogo, simba watafute mshambuliaji. Fredy ni nyanya za nyongeza (zilizolegea, kwenda kuoza)

      Reply
      • Munta_boe on May 1, 2024 2:53 pm

        Ahahah et nyanya ya nyongeza daah kk umetia folaa😅😅😅

        Reply
    6. Mr dream on May 2, 2024 2:29 pm

      Kinachomponza njaa tu

      Reply
    7. Pingback: Kinachomponza Mgunda Ni 'Rangi Yake Na Utanzania Wake' - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.