Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » City yatinga raundi ya 16 Ligi ya Mabingwa
    Biriani la Ulaya

    City yatinga raundi ya 16 Ligi ya Mabingwa

    Brenda UlomiBy Brenda UlomiNovember 9, 2023No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Soccer Football - Champions League - Group G - Manchester City v BSC Young Boys - Etihad Stadium, Manchester, Britain - November 7, 2023 Manchester City's Erling Braut Haaland scores their third goal Action Images via Reuters/Lee Smith
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Man City yatinga raundi ya 16 Ligi ya Mabingwa kwa ushindi mkubwa dhidi ya Young Boys

    City, ambao sasa hawajapoteza katika mechi zao 28 za Ligi ya Mabingwa Ulaya katika uwanja wa Etihad, walidhibiti mchezo kuanzia mwanzo na wangeweza kuongoza mapema dakika sita kupitia kijana mwenye miaka 18 Rico Lewis.

    Mabingwa wa mara tatu walikuwa wakipiga hodi kwa nguvu huku Kyle Walker, ambaye aliongezwa katika kikosi baada ya jeraha la Manuel Akanji wakati wa maandalizi, akipiga mkwaju wa faulo uliopanguliwa vizuri na Anthony Racioppi.

    Foden labda angepaswa kufunga katika nafasi ya pili lakini pia alizuiwa.

    Manchester City 3-0 Young Boys (7 Nov, 2023) Game Analysis - ESPN (UK)

    City ilipata bao lao baada ya Lauper kumchezea rafu Matheus Nunes ndani ya eneo la hatari, na hivyo kumpatia Haaland penalti katikati ya kipindi cha kwanza.

    Mwenye umri wa miaka 23 alimlamba chapuo kipa na kufungua ukurasa wa mabao.

    Guardiola alionekana kuchanganyikiwa wakati City ilipunguza kasi, lakini wenyeji walionekana daima kuwa na udhibiti.

    Foden alimsaidia kocha wake kabla ya mapumziko alipokutana na pasi ya Jack Grealish na kumchana Ulisses Garcia kufunga bao la pili kwa ustadi.

    Haaland aliweka mchezo nje ya uwezo wa Young Boys kwa bao la kushangaza – la pili tu kutoka nje ya eneo la hatari kwa City – muda mfupi baada ya mchezo kuanza tena, akipiga mpira upande wa pili wa lango na kuujaza wavuni.

    Haaland scores twice as Man City clinch Champions League last 16 place |  Reuters

    Sasa ana mabao 67 katika mechi 60 kwa klabu.

    Young Boys walipoteza matumaini yote wakati Lauper alionyeshwa kadi nyekundu ya pili kwa kucheza rafu ya pili dhidi ya Nathan Ake ambayo labda ilistahili kadi nyekundu moja kwa moja.

    Guardiola alimtoa Haaland kabla hajafunga hat-trick kuchagua kumpumzisha mfungaji bora kabla ya safari yao ya Jumapili kwenda Chelsea

    City ilikuwa na nafasi za kutosha za kumaliza na mabao matano, lakini haikuwa na maana kwa Young Boys ambao hawakufanikiwa kufanya mashambulizi yoyote katika mchezo wote.

    City, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, walihakikisha nafasi yao katika raundi ya 16 kwa msimu wa 11 mfululizo na michezo miwili kusalia, na sasa wanakaribia kuchukua nafasi ya kwanza.

    Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa

    city ulaya young boys
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.