Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Barua Kwako Mo Dewji Rais Wa Heshima Simba Sc
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Barua Kwako Mo Dewji Rais Wa Heshima Simba Sc

    MhaririBy MhaririApril 15, 2024Updated:April 17, 202428 Comments2 Mins Read8K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Mo Dewji
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kwako Mo Dewji

    Natumai barua hii inakufikia wewe na familia yako katika afya njema na ustawi wa kiroho na kimwili. Napenda kutumia fursa hii kuelezea mawazo yangu na kufikisha ombi muhimu kuhusu uwekezaji ndani ya klabu ya Simba.

    Hakuna ambaye hafahamu kuwa Simba ni mojawapo ya klabu kubwa na ya kihistoria katika soka la Tanzania. Klabu hii imekuwa ikileta furaha na shauku kwa mamilioni ya mashabiki wa soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Hata hivyo, ili klabu iendelee kustawi na kufikia viwango vipya vya mafanikio, inahitaji uwekezaji mkubwa zaidi katika miundombinu, vifaa vya michezo, na maendeleo ya vijana.

    Kupitia uzoefu wako na ujuzi wako katika uwekezaji, ningependa kuwasilisha ombi la kuzingatia uwekezaji ndani ya klabu ya Simba na wala sipingani na jinsi ambavyo umekua na mchango mkubwa katika mafanikio y klabu hii,lakini tambua kuwa uwekezaji mkubwa zaidi utasaidia kuboresha miundombinu imara na kuweza kuanzisha programu sahihi za maendeleo ya vijana, na kuimarisha kikosi cha Simba ili iweze kushindana kikamilifu katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

    Kwa ninayoyaona niwazi niseme kuwa mashabiki wamekosa imani kubwa kwa Try Again na Mangungu kwani wanaamini kuwa hawaujui mpira na fitina zake na ndio maana sasa hivi Simba imekuwa katika kipindi hiki cha kupata matokeo kwa shida. Na inaonekana kama vile watu wanaojua mpira Simba na wanaoweza fitina za mpira wakina Magori na Kaduguda japo bado wapo Simba lakini ni kama vile wamekaa pembeni wanatazama jahazi linavyozama. Hata Simba kumaliza nafasi ya tatu kwenye ligi mwaka huu ikiwa chini ya uongozi wa Try Again na Mangungu kwa kweli itakuwa ni bahati sana.

    Mwisho kwa nini Try Again na Mangungu wasiwe waungwana tu wakajiuzulu ili waingie watu wengine wenye uwezo wa kuivusha Simba itoke hapo ilipo. Wanang’ang’ania nini kuongoza Simba wakati toka waingie kwenye uongozi Simba imepoteza makombe yote chini yao na hakuna dalili ya kupata hata moja msimu huu.

    SOMA ZAIDI: Mashabiki SIMBA Wanahitaji Mabadiliko Makubwa Sio Propaganda

     

     

    simba leo simba vs yanga YANGA LEO

    28 Comments

    1. jacques on April 15, 2024 2:32 pm

      Try again na huyo mangungu wanatakiwa kuchomoka haraka sana bila kupepesa macho.

      Reply
      • Alhaji bakari on April 15, 2024 5:21 pm

        Hatumtaki mangungu na Salim try again

        Reply
      • Master on April 16, 2024 10:25 am

        Akika ata mm mm ni ninaumga mkono

        Reply
      • Kingprayer on April 17, 2024 4:50 pm

        Nakuunga mkono asilimia ๐Ÿ’ฏ

        Reply
    2. Jamary on April 15, 2024 2:32 pm

      Mo asa awaambie wajiuzul au

      Reply
    3. Fredy on April 15, 2024 3:01 pm

      Waondoke wte ad wachezaj walotuletea kina saido,boko, fredy,jobe tuletewe wachezaj wa maana simba ni tim kubwa sio ya kuwa na wachezaj wa viwango kam fred

      Reply
    4. Kibasa on April 15, 2024 3:11 pm

      Endeleeni kushikana uchawi sisi yetu macho tarehe 20 msipokaa sawa 8 ili sisi tuwasimulie wanetu kizazi kijacho๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

      Reply
    5. Daniel cupa official on April 15, 2024 3:30 pm

      Wasijihuzuru wasubiri kichapo cha tarehe 20. Watajiua kwa aibu๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

      Reply
      • Mwita on April 15, 2024 5:40 pm

        Hao hawawezi jiuzuru kiwepesi zaidi ya wanachama na mashabiki kuwang’oa kilazima yaani watate wasitake ikiwezekana kipigo kiwepo tofauti na hapo hakuna kitu.

        Reply
    6. Yusuph shilla on April 15, 2024 3:38 pm

      Simba ni timu yangu lkn kusema ukwel wanaboa kinomaaa an,,, wanatuumiza sana

      Reply
    7. Contawa on April 15, 2024 3:46 pm

      Timu ya simba inabidi ifumuliwe ianzishwe na upwa na kusajili vyuma pia hao try again na kaduguda waondolewe ili kuijenga simba bora
      “SIMBA NGUVU MOJA๐Ÿ’ช๐Ÿ’ช๐Ÿ’ฏ๐Ÿ’ฏ”

      Reply
    8. Mavugo on April 15, 2024 3:51 pm

      Toa Fredy,saido,jobe,kramo,babacar bila kusahau Baba ester shomy the way sarr Leta wa watu wa maana kina Fiston mayele ayoub aletewe msaidizi anaweza kumpa challenge msimu ujao tuta eshimiana tu

      Reply
    9. Allen on April 15, 2024 3:51 pm

      Sasa me sielewi kwani mo ndo anatakiwa kuwachomoa hao jamaa au aende tu akawaambie
      Ila for sure simba saiv inaboa hatuwezi kuihama nyie hawajui mapenzi ya mpiraa wao wanatake easy tu sababu wao wanapata wanachotaka ila mashabiki hatupati haki yenu ya kuona timu yetu inafanya vizurii

      Reply
    10. Ally Ally on April 15, 2024 4:00 pm

      Kiukweli try again na mangungu na imani kajula wangependwa na Simba milele kama watajiuzulu wenyewe kuliko kungโ€™angโ€™ania uongozi ambao hawauweziiโ€ฆ.

      Reply
    11. Amiri magobole on April 15, 2024 4:30 pm

      Waondoke wachzaji wote ambao hawana viwango vya kuchezea Simba Ili tupunguziwe mateso.

      Reply
    12. Joh on April 15, 2024 4:55 pm

      Me naomba wangalie kama tatizo lipo kwa viongoz na baadh ya wachezaji Raisi wa simba awatoe tunaumia sana na tunapoteza matumaini kwa timu yetu tunaumia ๐Ÿ˜ญ

      Reply
    13. Michael on April 15, 2024 5:04 pm

      shida huwenda sio wachezaji ,kwani timu walizotoka si waliwaka il mbona baada ya kuja tu uku viwango vyao vimeshuka , Cha msingi ni kuangalia kwanini wakija simba hawachezi Kam uko waliko Toka. SHIDA n nini haswa

      Reply
    14. Sir. Walter Winstone on April 15, 2024 5:26 pm

      Listen very careful and with all the attention, Simba imeacha kuwa football club imeanza kua business club, why? Hatukatai kila club ina nyakati za kupanda na kushuka hata vilabu vikubwa duniani tunaona.. kwa upande wa Simba sio kwamba tunashuka kwasababu ya nyakati hapana Bali ni sababu baadhi ya watu wamefanya club kuwa chanzo Cha mapato.. wachezaji na team husika wameacha ku focus na mpira wanawaza biashara.. mchezaji hawezi waza kufanya mazoezi na matangazo ya wadhamini wao at the same time hiyo ni point no 1. (Kwanini wasiajiriwe watu special kwa ajili hiyo?. Point no 2. Uuzaji na ununuaji wa wachezaji, kumekuwa na wimbi la kiswahili la ununuaji wa wachezaji ili ku washtua wapinzani kua sisi ni Bora sana na tuna Hela badala ya kuchukua wachezaji wenye ubora na kuruhusu wachezaji hao kupata nafasi ya kuonyesha walichonacho kwa wakati sahihi.. swali, naomba ufafanuzi wa Moses phiri kwanzia usaliji wake, malengo yake kabla ya kuja Simba, kwa kiwango gani ameitumikia Simba na muhimu zaidi aliemuona Moses phiri hadi akamsajili ni nani na kwanini aliuzwa. Point 3. Ununuaji wa makocha. Tumeona uongozi mwingi sana na tumekua mashahidi wa matokeo ya coaches hao, Simba ni club ya Tanzania uzalendo kwanza, tuliona uongozi wa Juma Mgunda kama head coach simba ambapo timu ilikua katika kiwango kizuri mmno, ufungaji, chemistry, accuracy, fitness, good communication skills among leaders na wachezaji.. swali, kwanini Juma Mgunda hakuaminika apewe head coach aendelee na strategies zake kuisogeza Simba mbele? Kwanini tumekua walimbukeni na raia wa kigeni?
      Okay tumempata benchika ameikuta Simba Iko hoi na kaikuta nusu msimu, angalia Benchika ni kocha, ana strategies zake.. anajaribu kutengeneza kikosi kwa njia zake mwenyewe.. ambacho anajua ni kua Simba Iko builded tayari na ina watu specific ndo mana anajaribu kutu prove wrong na kila akijaribu matokeo ni -ve( kinamkost).
      Cha msingi Tuupe muda wakati usogee.. tufikiri kabla ya kutenda.. Simba ina kikakitu kinachotuponza ni pressure kutoka nnje.. tunaweza tusisajili yeyote na tukachukua ubingwa wa African inshallah, ebu tujitafakari alafu.
      1.Tusafishe magugu yote bila kujali tutaonekanaje.
      2.Tuache biashara kwanza tufanye mpira.
      3.Tuwe wavumilivu wa nyakati kwa kutumia akili.
      UJUMBE
      Kila kitu kizuri ni matokeo ya kitu kibaya. Let’s think before doing anything.

      Reply
    15. Lenkai junior on April 15, 2024 6:39 pm

      mm naomba club ya simba kupitia management yake,,ivunje kabisaa utawala uliopo madarakani kwa sasa na kuleta viongozi mahiri ambao wataweza kuifikisha club panapotakiwa na ndio kiu yetu mashabiki zaidi ya hapo tutakuwa uvumilivu in short

      Reply
      • Joshua on April 15, 2024 7:29 pm

        Hapo baadhi ya viongozi wajiuzuru, uwekezaji uongezeke na wamuamini Juma Mgunda kwamba anaweza

        Reply
        • Jux on April 15, 2024 8:33 pm

          ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

          Reply
    16. Pingback: Ligi Kuu Bara Iko Kwenye Vita Ya Mfungaji Bora Kiungo - Kijiweni

    17. Smartkid on April 16, 2024 5:00 pm

      Tuna uchungu na Tim yetu ๐Ÿ˜‘โœ…๏ธfanyeni mabadiliko jamani tuone matunda sio figisu figisu tu

      Reply
    18. Pingback: Barua Nzito Ya Shabiki Kwa Viongozi Wa Simba Kuhusu Inonga - Kijiweni

    19. Nuhu on April 17, 2024 3:50 pm

      Mangungu asitoke wananchi tufurahi

      Reply
    20. Michael on April 17, 2024 7:36 pm

      Admin mbona leo sijaona apdate za mechi zinazoendeleaaaaaaaa au leo tumekaushiwa hapa kijiweni

      Reply
    21. Dastani pascal on April 18, 2024 1:29 am

      Kiukwer hatuitaji propaganda kwasababu Sisi mashabiki ndo tunaoumia na sio wawo maana wawo wanajali masilai Yao tu.

      Reply
    22. Sha'ib Ghalib on May 3, 2024 8:02 am

      Vizuri hata mm nakuunga mkono

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneย  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.