Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Barua Hii Iwafikie Wachezaji Wa Simba Huko Misri
    Africa | CAF

    Barua Hii Iwafikie Wachezaji Wa Simba Huko Misri

    MhaririBy MhaririApril 4, 2024Updated:April 6, 20244 Comments2 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Kikosi Cha Simba
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kwa wachezaji wa Simba,

    Natumaini kwamba barua hii inawapata nyote katika hali njema na hamu kubwa ya kuelekea kwenye mchezo muhimu wa robo fainali dhidi ya Al Ahly huko Misri. Ni mchezo mkubwa lakini naamini kuwa kama ilivyo Nguvu Moja basi kwa pamoja na umoja wenu bila kusahau juhudi zenu Simba inakwenda kufuzu hatua ya nusu fainali na kufikia mafanikio makubwa.

    Mchezo huu ni fursa ya kipekee ya kuthibitisha uwezo wenu kama timu bora kutoka Afrika Mashariki na Kati.Ni nafasi ya kipekee ya kuonyesha ulimwengu wa soka uwezo wenu na kutimiza ndoto za mamilioni ya mashabiki wenu wanaowasapoti kwa moyo wote.

    Nina imani kubwa katika kila mmoja wenu.Najua kuwa Al Ahly ni timu ngumu na yenye uzoefu mkubwa, lakini hilo halipaswi kuwafanya muogope au kupunguza juhudi zenu. Badala yake, ni wito kwnuu kufanya kazi kwa bidii zaidi, kutumia kila uwezo wenu, na kucheza kwa moyo wote.

    Kila mmoja wenu ana jukumu muhimu katika kufanikisha malengo ya klabu ya Simba.Mnahitaji kujituma kila dakika ya mchezo, kuwa na nidhamu ya hali ya juu, na kufanya maamuzi sahihi kila wakati. Mnapojitolea kwa pamoja na kucheza kama timu moja ni rahisi kufikia mafanikio makubwa.

    Maandalizi ni muhimu sana. Kila mmoja wenu anahitaji kujiandaa kikamilifu kimwili na kiakili. Mnahitaji kuwa na imani na ujasiri katika uwezo wenu wenyewe na kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha mnakuwa tayari kwa kila kitu.

    Napenda kuwasihi mjisikie fahari kuvaa jezi ya klabu ya Simba na kuiwakilisha kimataifa kwani hii ni fursa ya kipekee ya kufanya historia na kuandika jina lenu katika soka la Afrika. Ni wakati wenu wa kung’aa na kufikia mafanikio makubwa.

    Msikate tamaa, msikubali kushindwa na naamini kuwa mkicheza kwa moyo wote na kufanya kazi kama timu moja, hatuna shaka kuwa mnaenda kufikia mafanikio makubwa.

    Kama ilivyo nguvu moja basi kwa umoja na ujasiri ni wakati wa kuonesha maana halisi ya neno Nguvu Moja nchini Misri na ninawatakia kila la heri katika maandalizi yenu

    Iwakilisheni Simba kwa heshima na ujasiri, na kwa pamoja mtashinda.

    Kwa heshima kubwa,

    Mhariri

    SOMA ZAIDI: Barua Hii Iwafikie Wachezaji Wa Yanga Huko Afrika Kusini

    al ahly vs simba CAF CHAMPIONS LEAGUE SIMBA SC simba na yanga simba sc leo

    4 Comments

    1. Charles James on April 4, 2024 8:18 pm

      Mlima kwa simba mpaka sasa ni mkubwa sana

      Reply
    2. Maureen on April 4, 2024 8:37 pm

      Mungu afanye muujiza kama siku ya mkate mmoja na samaki wawili wakala maelef ya watu na wakasaza ndivyo navoiombea Timu yangu ‘ msiogope mjiamini tuko nyuma yenu tunawaamini msituangushe plz

      Reply
    3. Michael Julius masaka on April 5, 2024 7:33 am

      Ata mie pia naongezea kwa kusema simba ni timu kubwa nasyo mara ya kwanza kucheza nahao wamisri khyo mnatakiwa kujiamini na kucheza kwa malengo yakuingia nusu fainali ninaiman na benchi la ufundi pamoja na wachezaji pia nawaombea kwa mwenyezi Mungu awajaze nguvu afya njema ili muweze kufanya vizuri nakupata ushindi mkiwa ugenini

      Reply
    4. Charles ally on April 5, 2024 6:32 pm

      Apo kutoboa ni ngumu but everyrhing is possible tunaweza kwenda nusu fainal wote simba&yanga

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.