Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » AL AHLY Moto Kombe La Dunia Klabu
    Kombe la Dunia

    AL AHLY Moto Kombe La Dunia Klabu

    MhaririBy MhaririDecember 16, 2023No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Wachezaji wa klabu ya Al Ahly.
    Wachezaji wa klabu ya Al Ahly wakishangilia baada ya kumfunga Al Ittihad bao 3:1
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Klabu ya Al Ahly kutoka nchini Misri imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa klabu  baada ya ushindi mzito wa bao 3-1 dhidi ya Al Ittihad ya Saudi Arabia.

    Al Ittihad kutoka Saudi yenye Mastaa kama Benzema, Ngolo Kante na Fabinho walikumbana na kipigo hicho pasi na huruma huku mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid anayekipiga katika kikosi cha Ittihad Karim Benzema akikosa penati kwa kazi nzuri ya Mohammed El Shenawy, penati ambayo ingewasaidia kusawazisha bao la Ali Maâloul aliyefunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 21.

    Kazi nzuri sana ya Mohammed El Shenawy iliendelea kuwaweka salama Al Ahly na kipindi cha pili Ahly walicharuka na kufunga mabao mawili kupitia kwa Hussein El Shahat dakika ya 59 na Emam Ashour dakika ya 62 na kwenye dakika za fidia Karim Benzema aliipa Ittihad bao la kufutia machozi.

    Huenda ukawa mwisho wa mshambuliaji Anton Modeste wa Al Ahly ambaye ameoneshwa kadi nyekundu na hajawa kwenye kiwango bora tangu ajiunge na timu hiyo huku tetesi zikidai Januari hii huenda akatemwa na mabingwa hao mara nyingi wa bara la Afrika.

    Urejeo wa Mohammed Abdelmonem ulikuwa muhimu sana kwenye safu ya ulinzi lakini pia kiwango bora zaidi kutoka kwa Mahmoud Kahraba aliyetoa asisti ya bao moja kiwango bora zaidi ndani ya miezi miwili ya karibuni kwa Ahly.

    Mchezo wa mapema zaidi Club Leon walifungwa na Urawa kutoka Japan bao 1:0 goli la Schalk dakika ya 76 ya mchezo.

    Baada ya kutinga nusu fainali Al Ahly anakutana na bingwa wa bara la Amerika kutoka nchini Brazil , Fluminese huku nusu fainali nyingine ikiwakutanisha Urawa Red Diamonds kutoka nchini Japan dhidi ya mabingwa wa bara la Ulaya Manchester City. Unadhani kwa kiwango walichokionesha leo Al Ahly wana nafasi ya kuwa bingwa wa dunia kwa vilabu?

    Endelea kufuatilia habari zetu kuhusu kombe la dunia kwa klabu kwa kusoma zaidi hapa.

    fifa club world cup 2023
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.