Ilipoishia
Angalau eneo Hilo lilikua na taa, nilitembea haraka haraka Hadi nilipofika nyumbani, ila nilikua naogopa sana kuingia ndani, nikapata wazo la kumuamsha Mama Amida nimuombe nilale nyumbani kwake Hadi Asubuhi.
Niligonga mlango wake kwa nguvu huku nikimtaka anifungulie haraka, chozi lilianza kunitoka. Nilikua nageuka huku na kule, mara haraka Mama Amida alinifungulia, nilimsukuma nikaingia Hadi ndani Kisha nikamwambia aufunge mlango haraka, akafanya hivyo haraka bila kujua ni kwanini nilimtaka aufunge mlango, Kisha akanigeukia
“Saida, Kuna tatizo gani?” aliniuliza, chozi lilikua linanibubujika tu. Akanishika mkono na kunipeleka chumbani kwake Kisha akaniambia nikae kwenye kiti.
Hukusoma SEHEMU ZILIZOPITA? Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI , SEHEMU YA TATU Kisha Endelea
SEHEMU YA NNE
“Una shida gani saida mbona unanitisha, Usiku huu umetokea wapi wewe Mtoto?” kiukweli sikuweza kujibu chochote maana nilizidiwa na woga kiasi kwamba hata mdomo Wangu uligoma kusema chochote kile. Alinielewa, istoshe yeye ni Mtu mzima akaniambia nipande kitandani tutaongea Asubuhi, nilipandwa kitandani nikajikaza Chali. Alikua akiishi peke yake baada ya Mume wake kufariki, Mtoto wake alikua akilala chumba kingine na Msichana wa kazi.
Sikupata hata lepe la Usingizi Hadi kulipo pambazuka. Mama Amida aliniambia nimpe majibu ya maswali yake, akili kidogo ilikua imetulia lakini nilifikiria kua siwezi kumweleza chochote kinachoendelea
“Saida, naomba unijibu ulipatwa na Nini?” Aliniuliza kwa msistizo.
“Samahani, nilikua nafukuzwa na wezi” nilimpa jibu la uwongo huku nikiwa Nina aibu machoni pangu kwa kusema Uwongo kwa Mtu ambaye nilikua namchukulia kama Mama yangu.
“Wezi?”
“Ndiyo”
“Ulikua unatokea wapi muda ule?”
“Nilienda kwa rafiki yangu lakini nakuahidi haitajirudia tena” “Mmh! Haya”
“Pia Asante kwa msaada wako”
“Usijali Saida, muda wowote” alisema Mama Amida lakini sura yake ilionesha Wazi kua alikua ameshanishtukia kua nilikua nasema Uwongo lakini hakutaka kukuza mambo, nilimuacha akiwa amekaa kwenye kiti chumbani kwake. Niliondoka nikaelekea nyumbani, safari hii niliingia ndani sababu nilihitaji kubadilisha nguo lakini pia kuvaa viatu.
Nilioga haraka haraka Kisha nikabadilisha nguo nikatoka, nikakaa nje ya nyumba. Nyumba yetu nilikua naiyona kama Kituo Cha Polisi, niliogopa hata kukaa ndani
Nikampigia simu Veronica, akaniambia kua alishaongea na Meneja hivyo niende kwao Mabibo halafu Ndiyo twende kwa Mganga. Katika Hali ambayo nilikua nayo ilikua rahisi kwangu kukubali Kila ninachoambiwa ili tu nipate ahueni, kwa jinsi nilivyoongea na Veronica ilionekana hakupata kashikashi yoyote Usiku hivyo Mlengwa nilikua ni Mimi.
Basi niliondoka nyumbani nikaelekea kituo Cha Daladala, nikaingia kwenye daladala Kisha safari ya kuelekea Mabibo ilianza.
Nilimtazama Kila Mtu kwenye lile daladala kama vile nilikua kondakta, lakini nilikua mwoga sana sababu nilishajua Maisha yangu yalikua hatarini. Nilikua mwingi wa kushtuka shtuka.
Hadi tunafika Mabibo nilikua nimegeuza shingo yangu mara nyingi sana kuangalia huku na kule. Veronica alinipokea akanipeleka Hadi nyumbani kwao, ilikua ni mara ya kwanza nafika kwao pia nakutana na Mama yake. Tuliongea mengi huku Mama yake akitupatia stori za hapa na pale zenye
kufanana na mkasa wetu, akatupatia uhakika kua utapatikana muafaka bila wasiwasi wowote ule
Maneno yake yalikua ni faraja pekee niliyohitaji Maishani mwangu kwa wakati ule, nilihitaji kutiwa moyo kama alivyofanya Mama yake Veronica, akatuandalia chai tukanywa huku tukipiga stori.
Baada ya kumaliza akatuambia twende sasa kwa Mganga maeneo ya Mburahati. Tulielekea kituo Cha daladala tukapanda magari ya Mburahati, nilikua najisikia amani sana sababu nilihisi nipo salama zaidi.
Tulipofika Mburahati, akatupeleka nyumbani kwa Mganga. Akatuhakikishia kua ni Mganga kiboko sana kutokea Liwale, ana uwezo mkubwa sana.
“Msijali, hii Dunia isikieni tu ila Ina mambo mengi sana Wanangu” alisema Mama yake Veronica akiwa amesimama mbele ya nyumba Moja ya
kizamani. Namna alivyokua anaongea nasi ni kama vile kapteni wa Timu ya Mpira vile
Tuliachia tabasamu kwa pamoja, nisiseme Uwongo ila nilikua mwenye amani zaidi nilipokua namsikiliza Mama yake Veronica. Alikua amevalia gauni Jekundu na Ushungi.
“Hili limekwisha, twendeni”
“Sawa Mama” tulisema kwa pamoja Kisha tulitazamana halafu tukamfuata Mama Veronica ndani. Namna alivyoingia ni kama vile alikua ni mwenye kuja sana kwa huyo Mganga. Tuliingia Uwani, Kisha tulisogea Hadi mlangoni kwenye chumba kimoja hivi ambacho kilikua na pazia nyekundu iliyokua ikipepea mlangoni.
“Baba Masinde” aliita Mama Veronica huku akigonga Mlango. “Karibu” ilisikika sauti nzito ya kukwaruza.
“Nipo na wageni Baba” alisema tena Mama Veronica.
“Ingieni hakuna shida” alisema, Kisha Mama Veronica alitangulia ndani. Nilianza kuogopa kidogo lakini nilihitaji kua na amani ya Maisha yangu, ili nipate amani ya Maisha yangu ni lazima niyaondoe mauzauza kwenye Maisha yangu, njia pekee ilikua ni kupewa tiba kwa Mganga.
Tulivua viatu pale nje Kisha tuliingia ndani, tulipokelewa na harufu za ajabu ajabu sana, binafsi ilinibidi nivumilie tu kwasababu nilikua Nina shida lakini harufu hii ilinikumbusha Maisha ya Rukwa kule nyumbani kwa Mzee Mwinyi Mkuu.
Mganga huyo alitukaribisha tukae kwenye mkeka, chumba kilikua na mandhari zote za Uganga, hata mavazi ya huyo Mzee yalikua yakiganga pia. Basi tukasalimiana naye lakini Mama yake Veronica alisalimiana naye kwa shahuku kubwa sana.
“Baba, kama nilivyokwambia kwenye simu wakati natoka nyumbani, huyu ni Binti yangu anaitwa Veronica na huyu ni rafiki yake. Chonde Mzee wangu wasaidie hawa Vijana” alisema Mama yake Veronica. Yule Mganga akatuangalia kwa jicho lililo kimya, hakusema chochote.
Ilipofika zamu ya kuniangalia aliniangalia sana tena kwa muda mrefu Hadi nikawa na hofu. Alitumia dakika Moja ananiangalia tu, nilitamani kumuuliza kwanini alinitazama kwa muda mrefu.
“Hebu Mama tuongee nje” alisema yule Mganga Kisha yeye na Mama Veronica walitoka mle chumbani. Nilimsogelea Veronica nikamuuliza kwanini yule Mganga aliniangalia sana?
“Nitajuaje sasa Saida, Mimi sijui haya mambo ni vile tu Mama amesistiza” alisema Kisha aliegemea Ukuta.
“Yaani moyo unanienda mbio sana, naogopa mno” Nilisema, nilijikuta nikiwa mwoga mno.
Baada ya dakika Moja mlango ulifunguliwa Kisha Mganga na Mama Veronica walirudi ndani, nilizidi kutetemeka kwa hofu.
Kilicho chochea hofu yangu ni jicho la Mama Veronica, alikua akiniangalia kwa jicho Kali sana lisilo na Upendo kabisa.
Palikua kimya sana, si Mama Veronica wala Mganga aliyesema chochote. Nilitamani kulia maana niliona Wazi kua Kuna kitu hakipo sawa kwangu, halafu Mganga na Mama Veronica walitazamana Kisha Mganga akajikoholesha Kisha akasema kwa sauti yake kavu.
“Binti” alimtazama Veronica.
“Wewe hauna shida yoyote sababu umeingizwa kwenye Mchezo usioufahamu. Ila wewe Binti….” Alinitazama kwa jicho Kali sana huku akininyooshea kidole.
“Mimi?” niliuliza huku nikigusa kifua changu.
“Ndiyo….wewe ni mchafu sana” alisema yule Mganga, hata Veronica alishangaa. Alinitazama kwa Mshangao sana huku akionekana kua na kiu ya kutaka kujua sababu ya maneno Yale makali kutoka kwa Mganga.
Mganga alikua akiongea huku mate yakinirukia kutokana na mkazo wa maneno aliokua nao.
“Kwanini unasema hivyo?”
“Wewe ni Mchawi, wewe Binti ni Malkia wa wachawi.” Alisema yule Mganga, Jamani moyo ulinidunda kwa Kasi sana Hadi nikahisi kuchoka mwili mzima, pua zilikua kama zinauma kwa Kila pumzi niliyoivuta.
Maneno ya Mganga yalikua yakiuchona sana moyo Wangu, nilihisi kabisa sindano ndogo ikipita na kuniumiza ndani ya Moyo Wangu, Hadi chozi lilinilenga, sikuwahi kuambiwa Mimi Mchawi hata siku Moja tangu Kuzaliwa kwangu
Wakati ambao nilihitaji msaada Ndiyo wakati ambao nilianza kuitwa Mchawi, nawezaje kua Mchawi bila Mimi mwenyewe kujua? Tena Nina cheo Cha Umalkia?
“Usijilize hapa, wewe Ndiyo chanzo Cha kumuingiza Mwanangu kwenye Giza. Umeharibu Maisha ya Binti yangu Mjaa Laana wewe” alisema Mama yake Veronica kwa sauti Kali sana, alipaza sauti kwa hasira dhidi yangu. Shutuma hizi zote ziliniacha njia panda maana akili yangu haikuweza kuelewa lolote lile.
Nilimeza mate kwa Uchungu huku chozi likitiririka mashavuni mwangu, nilijiinamia nikiwa ninalia kwa sauti ya Ukimya. Haki ya Mungu nilimkumbuka sana Mama yangu, yeye ndiye Mtu pekee ambaye angeweza kunishika bega na kuniambia nisiwe na wasiwasi lakini hakuwepo kwenye Dunia yangu.
“Mama Veronica, hebu subiri kwanza” alisema yule Mganga akimtuliza Mama Veronica, kwa jinsi ambavyo alikua amekasirika angenishika na kunigalagaza, nilisogea pembeni kwa kujiburuza kwa kutumia Makalio yangu. Muda wote huo Veronica alikua kimya akinitazama kwa Mshangao
mkubwa sana, licha ya kumwonesha sura yangu ya hatia lakini alionekana kutaka kusema jambo zito sana ambalo lilikua limemkaa moyoni.
“Kwanini mnanituhumu kwa kitu ambacho sikijui Mimi?” niliuliza huku nikiwa ninalia, nilikua nimepandwa na hisia ya hasira na huzuni kwa wakati mmoja.
“Usichokifahamu ni kipi? Sasa chochote kinakachomkuta Veronica kuanzia sasa ni juu Yako. Utalipa nakwambia” alisema Mama Veronica Kisha aliondoka pale chumbani kwa hasira akiliburuza gauni lake kuelekea nje
“Yanayosemwa ni kweli Saida?” aliniuliza Veronica huku naye akisema kwa sauti iliyojaa kilio. Nilimtazama nikatikisa kichwa Kisha nikamwambia
“Ningewezaje kuigiza wakati wote ikiwa nafahamu Kila kitu Veronica. Sijui chochote kinachosemwa hapa, nipo njia panda sielewi” nilisema, Veronica alitikisa kichwa chake. Hakua na imani tena na Mimi, alisimama Kisha chozi likawa linamdondoka akaniambia
“Ikiwa Maisha yangu yataharibika kwasababu Yako sitakusamehe Saida” alisema Kisha naye aliondoka zake pale ndani, walituacha Mimi na Mganga.
“Ondoka hapa sitaki Matatizo” alisema yule Mganga, alikaza macho yake kwangu. Msaada uliokua karibu kwangu ulianza kwenda mbali, nilikua na
maswali mengi sana kichwani kama nitawezaje kuishi kwenye Dunia isiyo na Majibu, Dunia inayobadilika kwa haraka sana kwangu
Nilipepesa kope zangu, ni kama niliyaambia machozi yangu yamwagike. Yalimwagika bila hata kizuizi, kulia pekee ndicho kitu nilichoweza kufanya Mimi Saida
“Kwanini unasema Uwongo?” nilimuuliza yule Mganga, akakaza sura yake kwangu Kisha akaniambia
“Ondoka hapa haraka sana sitaki Matatizo na wenyewe”
“Wenyewe, ni akina Nani hao?” nilimuuliza huku chozi likinibubujika. Akanyanyuka haraka Kisha akanishika mkono na kunitoa pale chumbani.
“Ole wako urudi hapa, nisikuone” alisema kwa hasira yule Mganga Kisha alifunga mlango. Nilijiinamia na kuanza kulia kwa Uchungu sana, sikua na Cha kufanya tena zaidi ya kuvaa viatu vyangu na kuondoka pale.
Hapakua na yeyote pale nje si Veronica wala Mama yake. Nilifuta chozi langu, nikavaa viatu vyangu Kisha pole pole niliondoka pale Uwani Hadi nje, nilipofika nje nilisikia sauti za yowe
Hazikua mbali kutoka niliposimama, nilipozisikiliza vizuri hazikua yowe za Mwizi Bali ni tukio la Kusikitisha kwa namna ambavyo sauti zilikua zikisema. Nilitembea haraka kwenda kuangalia maana nyumba ya Mganga ilikua kando ya Barabara.
Nilipofika niliona Watu wengi sana, baadhi walikua wamejishika vichwa vyao. Nilijiuliza mwenyewe bila kupata majibu, nikamalizia kufuta chozi langu Kisha nikamuuliza Mtu mmoja aliyekua amesimama kando
“Eti Kuna nini pale?”
“Ajali, wewe acha tu hujaona”
“Ajali?”
“Ndiyo, Kuna Watu wameangukiwa na Kotena. Sura zao hata hazitamaniki” nilishtuka sana huku moyo ukinienda mbio, nikasogea karibu. Ndiyo kwanza walikua wakiiondoa Miili, nilipepesa macho yangu kwa Mshangao mkubwa sana, japo sura zao hazikutambuliwa ila nguo zao zilikua machoni pangu
Nilitamani nikae chini maana hata nguvu ziliniisha, Veronica na Mama yake walikua Ndiyo walioangukiwa na Kontena. Chozi lilinitoka kama
mwendawazimu, nikatikisa kichwa changu Kisha nikatimua mbio kuelekea kwa yule Mganga kumpa taarifa.
Hata kama hakunihitaji tena ila alipaswa kujua kua Mama Veronica na Mwanae walikua wamesha fariki. Niliusukuma mlango wa kuingilia Uwani Kisha niligonga sana mlango wa yule Mganga.
Sikukaribishwa, nikahisi labda atakua amenuna. Nikafikiria kuondoka lakini nikaona ni Bora nimwambie tu.
“Mama Veronica na Mwanaye wamepata ajali hapo nje” nilipaza sauti Kisha nilisubiria jibu lake lakini palikua kimya kabisa. Nikaona ni Bora niusukume ule Mlango, nilivuta nguvu lakini niliposukuma ulikua rahisi kufunguka. Nikajikuta nimeingia ndani ya chumba Cha Mganga
Hapakua na yoyote yule, niliangaza huku na kule lakini sikumwona, ila wakati nataka kuondoka niliona kitu Cha kushangaza sana. Nilisogea taratibu nikachuchumaa ili nikiangalie kitu nilichokiona kikanishangaza
Kilikua ni Picha yangu, nikiwa nimevalia gauni JEUSI, nakumbuka picha hiyo nilipiga baada ya kufunga ndoa na Salehe Miaka mitano iliyopita. Nilipigwa nyumbani kwetu wakati tunajiandaa kuondoka kuelekea Hotelini kulala ili kesho yake tuanze safari ya kuelekea Rukwa
Mtu pekee aliyekua na picha hii alikua ni Salehe, ndiye aliyenipiga picha kwa kutumia simu yake. Tokea kipindi kile sikuwahi kuiona hii picha, sasa nikajiuliza iliwezaje kufika pale kwa yule Mganga? Aliyeipeleka ile picha alikua ni Nani?
“Ina maana Salehe yupo na ananifuatilia?” nilijiuliza. Nilishagundua pale hapakua salama kwangu, nikageuka ili niondoke lakini ghafla mlango ulijifunga wenyewe. Pakawa na kigiza Fulani hivi
“Nani wewe unanifungia? Fungua mlango..” nilipaza sauti yangu. Niligonga na kuvuta mlango lakini sikuambulia chochote, hakuna aliyejitokeza lakini nakumbuka ule Mlango haukufungwa kikawaida, zilitumika nguvu nisizoziona. Kufungiwa ndani ya kile chumba kulinifanya nirejeshe kumbukumbu zangu nyumbani kwa Mzee Mwinyi Mkuu.
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TANO Sasa ( Comments ziwe nyingi)
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx


