Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 08

    In the name of LOVE – 07

    In the name of LOVE – 06

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » In the name of LOVE – 08
    Hadithi

    In the name of LOVE – 08

    Hamza NgondoBy Hamza NgondoSeptember 24, 2025Updated:September 24, 20254 Comments10 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia sehemu ya saba ya In the name of LOVE

    “Nampeleka Mtoto Arusha, kesho nitarudi. Ubaki salama” alisema Kisha  aligeuka na kuondoka hapo huku Melisa akigeuka geuka mara kwa mara  kuniangalia, sikujua ni kwanini alikua akiniangalia sana lakini hisia  zilinianbia nilikua na uhusiano wa Maisha yaliyopita na Mtoto yule. 

    Nilirudi chumbani, nilianza kujihisi huzuni kiasi. Nilimtazama Zaylisa  aliyekua amelala, nilijiinamia huku kichwa kikiwaka moto kwa mawazo  lukuki, nilitamani kujua kitu ambacho nilihisi kilikua muhimu kukijua  lakini sikujua nitafanya nini. Nilishusha tu pumzi zangu, Usingizi ulikua  umeshaisha. Endelea

    SEHEMU YA NANE 

    Saa ya ukutani iliniambia kua ilikua ni saa 12 asubuhi, nilivaa fulana Kisha  nilitoka chumbani nikaelekea jikoni, nilihisi kuhitaji kitu Cha kupasha  tumbo moto kidogo. Nilipofika jikoni nilikutana na Msichana wa kazi,  aliponiona alinywea sana 

    Haikua mara ya kwanza kua hivyo pindi anionapo, nilimtazama kidogo  nikagundua ni mwenye wasiwasi Fulani uliojaa Siri. Basi nilimsogelea  karibu, nikapata kuuona ule uwoga na hofu ya Siri fulani, alipoteza  kujiamini kabisa 

    Nilimuuliza “Haujambo?” 

    “Sijambo shikamoo” alisalimia kwa wasiwasi. Nilimkazia macho yangu,  akainamia chini.  

    “Kwanini Kila unionapo unakua ni mwenye wasiwasi?” nilimuuliza, sijui  nilijihisi vipi lakini nilihisi kiu kubwa ya kupata majibu ya maswali mengi  yaliyoingia kichwani pangu. 

    Alikaa kimya huku akipata tabu, alipoteza Hali ya utulivu kabisa. 

    “Baby” niliisikia sauti nyuma yangu, sauti ya Zaylisa ilikatisha zoezi langu.  Nilitabasamu Kisha niligeuka 

    “Naam‼” alinisogelea Kisha aliniuliza “Kwanini upo hapa ukaniacha peke  yangu chumbani Baby” 

    “Nilihitaji kitu Cha moto Cha kuingiza tumboni, istoshe nilikuacha umelala  sikutaka kukusumbua”

    “Hapanaa‼ hauwezi kunisumbua Mpenzi, Mimi ni wako” alisema Zaylisa,  yule Msichana wa kazi akaondoka pale jikoni. 

    “Haya niambie nikuandalie nini?” 

    “Chai, weka limao na asali”  

    “Basi?” 

    “Ndiyo babe” sura zetu zilijaa tabasamu kubwa sana, basi Zay alianza  kuniandalia chai. Nikatoka nikaelekea chumbani 

    Nilichohitaji kufanya wakati ule kilikua ni kuingia bafuni kwa ajili ya kuoga  Maji ili nikitoka nipate chai niliyoagiza. Wakati naelekea bafuni, simu ya  Zaylisa ilianza kuita 

    Nilijishauri mara mbili, nimpelekee au nioge. Nilifikiria huwenda ilikua  simu muhimu asubuhi ile, niliona ni Bora nimpelekee jikoni, basi nilikata  shauri nikaielekea ile simu 

    Wakati naifikia ilikua inakata, lakini niliona ni Bora niipeleke tu kama ni  simu muhimu ili awahi kuwasiliana na Mtu huyo, niliichukua nikawa  natoka chumbani, ukaingia Ujumbe 

    Sijui ni kitu gani kilinifanya niangalie kioo, kumbe ilikua haijafungwa kwa  nywila. Meseji ilijionesha pale juu, Meseji hiyo ilitoka kwa Mtu aliyemsevu  kama Mzee wa Mipango.  

    “Zay nakupigia simu hupokei. Nakusistiza usijisahau, upo huko kwa  mpango maalum” Nilishtuka kidogo, nilijikuta nikipotea kiakili kidogo 

    Nilisimama huku nikichezesha macho yangu huku na kule kama nilikua  natafuta kitu kilichopotea, niligeuza shingo yangu kuelekea chini huku akili  yangu ikiniambia kua ujumbe ule ulikua na maana zaidi ya ulivyoandikwa,  niliufungua Hadi ndani ya Boksi la jumbe. 

    Niliurudia kuusoma tena, hakuna kilichobadilika. Hapakua na Meseji  nyingine kutoka kwa Mtu huyo, pengine walikua wakiwasiliana zaidi kwa  kupigiana simu au zilikua zinafutwa. 

    Moyo ulinienda mbio kidogo, meseji ilikua na Fumbo gumu sana.  Nilitafakari kwa dakika tatu bila Majibu, niliurudia mstari aliposema “Upo  huko kwa mpango maalum”  

    Nilijiuliza “ Upo huko Ina maana ni hapa, sasa kama ni hapa amekuja kwa  mpango gani wakati ni Mpenzi wangu au ulikua ni ujumbe usio wake.?”

    Nilishusha pumzi zangu, kwakua simu ilikua mkononi niliona niufute ule  ujumbe maana asije ona kua nimefungua simu yake, sikutaka kuichunguza  tena ile simu, niliirudisha nilipoitoa 

    Ilianza kuita tena, huku mpigaji akiwa yule yule Mzee wa Mipango.  Nikaelekea Bafuni kuoga, Nilioga nikiwa ninaiwaza sana ile simu, sijui hata  kwanini nilipata wasiwasi Fulani  

    Nilipomaliza kuoga nilitoka bafuni, macho yangu yalikua na shahuku sana,  Moja kwa moja yalielekea kitandani, Bado simu ya Zaylisa ilikua hapo.  Wakati najifuta Maji mwilini, simu ilianza kuita tena 

    “Kwanini huyu Mtu anapiga sana simu?” nilijiuliza, mara Mlango  ulifunguliwa haraka, Zaylisa alielekea Moja kwa moja kuchukua simu yake.  Nilimdadisi kwa umakini sana nikijifanya naendelea kujifuta Maji kama  vile nilikua sijui chochote. 

    “Imeita muda mrefu” nilisema, alinitazama kidogo huku akionekana kua na  wasiwasi Fulani usoni pake baada ya kuona ni Nani aliyekua akimpgia. Kisha akaachia tabasamu la kuzuga, tabasamu nililo ligundua haraka sana  kua halikutoka moyoni pake 

    “Dakika Moja baby, naongea na Baba” alisema Kisha aliondoka chumbani,  moyo Wangu uliripuka kwa mshituko. Nilijiuliza kama alikua Baba yake,  kwanini aliingiwa na wasiwasi au ndio kusema aliyepiga safari hii hakua  yule Mzee wa Mipango?  

    Aliniacha njia panda, akili yangu iligawanyika vipavipande nisijue kipi ni  sahihi na kipi si sahihi. Nilifunika kombe ili mwanaharamu apite lakini akili  yangu iliniambia napaswa kumchunguza Zaylisa 

    Haikuchukua hata dakika tano alirudi akiwa mnyonge sana, nilishtuka  kumwona akitembea pole pole huku sura yake ikionekana kutokua sawa.  Nilimsogelea na kumwuliza  

    “Upo sawa?” alinitazama kwa jicho lililojaa huzuni sana Hadi nilishtuka  huku nikijiuliza alikua ameambiwa nini na aliyempigia simu. 

    “Babe‼”  

    “Baba..” alisema Kisha aliketi kitandani, Nami Niliketi. 

    “Baba amefanya nini?” 

    “Jacob, Hali ya Baba siyo nzuri. Nimepigiwa simu na Mama, natakiwa  kwenda” 

    “Pole sana, basi Wacha tuongozane” nilisema huku nikiweka taulo pembeni  ili nipake mafuta na kuvaa nguo.  

    “Hapana, siku nyingine Jacob. Kwa Leo Wacha Mimi niende kwanza,  taratibu atakufahamu sawa Mpenzi wangu?” alisema, ilinibidi niwe Mpole  ukizingatia ni kweli Wazazi wake walikua hawanifahamu. 

    Nilihisi Kuna uwongo usio dhahiri lakini sikuweza kuuthibitisha, Niliketi  kitandani nikimtazama Zaylisa akijiandaa haraka haraka lakini uso wake  ulikua na ukakasi mwingi sana, alikua akinitazama Kila dakika. Alipomaliza  kujiandaa alinisogelea na kunipa busu Kisha akaniaga 

    “Bye Babe” niliitikia kwa kutikisa kichwa changu, nahisi aligundua kua  sijafurahia.  

    “Basi nisindikize Hadi getini my love” nilitabasamu kidogo, tukatoka Hadi  getini. Alikua tayari ameshaita taxi akaingia na kuondoka zake huku  nikimsindikiza kwa kutumia macho yangu pekee. Nilishusha pumzi zangu  baada ya gari kupotea machoni pangu, mkono mmoja ukiwa umeshikilia  geti na mwingine ukiwa Mfukoni 

    Moyo Wangu uliingiwa na Hali ya Wasiwasi sana. Nilirudi ndani taratibu  nikaketi kwenye Bembea Moja ndani ya Bustani kando ya Eneo la  maegesho. 

    Nilihitaji kutulia zaidi na kuwaza mambo mengi yaliyokua yamepita.  Dakika tano zilipita nikiendelea kufikiria, ghafla nilikatishwa na sauti ya  kugongwa kwa geti, niliuangalia mlango wa kuingilia ndani hapakua na  dalili ya Msichana Wakazi kutoka, nikaona ni Bora nikafungue 

    Nilipofungua nilimwona Msichana mmoja, alisimama kwa matege ya  kurudi nyuma, alikua na nywele ndefu nyeusi zilizoshuka Hadi mabegani.  Alikua amevalia mawani nyeupe huku midomo yake ikiwa imekolea  ‘Lipstiki’ nyekundu. 

    Alikua akitabasamu baada ya kuniona, haraka niligundua alikua  hajanifananisha na yeyote isipokua Mimi nilikua ni Mtu aliye mtarajia.  

    ‘‘Habari Bosi Jacob” alisema huku akili yangu ikiniambia kua Kuna Siri  kwenye jina la Bosi, yeye hakua Mtu wa kwanza kunita jina Hilo lakini  sikuacha kujiuliza ilikua ni Siri gani nzito iliyojificha? Niliachia tabasamu la  kusita, huku nikimpa sura isiyo tabirika. 

    “Nimeleta mzigo uliopaswa kuupokea siku uliyopata ajali” alisema, Kisha  alielekea kwenye gari akatoka na boksi dogo Jekundu. Nilikua katika  Bumbuwazi, Kisha alinipatia Boksi na kuniambia

    “Nakutakia mapumziko Mema pia nakuombea urejee kazini haraka kuliko  ilivyopangwa” aliondoka aliniacha nikiwa kimya kama Bubu, mkononi  nilikua na Boksi Jekundu 

    Macho yangu yalilizunguka Boksi na kugundua palikua pameandikwa jina  langu MR. JACOB.  

    Nilihisi kua nilishawahi kuyaishi Maisha Fulani niliyoyasahau,  kumbukumbu zangu zote zilinianbia kua Mimi Jacob ni Kijana masikini  asiye na kazi lakini kwanini Watu walikua wakiniheshimu kama Mtu  mkubwa mwenye utajiri. 

    Nilikua nimesimama huku Boksi likiwa mkononi mwangu, nilipepesa  macho yangu huku nikitafuta kumbukumbu ambazo sikua nazo, lakini akili  yangu iliniambia huwenda ndani ya Boksi Kuna kitu muhimu sana,  nilifanya haraka nikaingia ndani, Moja kwa moja Hadi chumbani kwangu 

    Nililiweka lile Boksi kitandani, nilijishika kiuno huku nikiendelea  kupambana na Giza nene kichwani kwangu. Niliinama na kulishika tena,  hamu ya kufungua na kuona kitu kilichomo ndani ya Boksi ilinijia, taratibu  nilianza kulifungua huku moyo Wangu ukiwa unadunda sana 

    Mara mlango uligongwa, nilijiuliza ni Nani anayegonga wakati Clara na  Zaylisa hawakuwepo nyumbani, kitu Cha kwanza nilipata wazo la  kuhifadhia Boksi, nikaliweka chini ya Uvungu wa Kitanda Kisha nikaelekea  mlangoni 

    Nilipofungua mlango nilikutana na sura ya Msichana wa kazi. Aliponiona  alinitazama sana kama Mtu ambaye alikua anataka kusema kitu lakini  alikua akiogopa kufanya hivyo.  

    “Hey‼” nilimshitua, kweli alikua mbali kifikra.  

    “Abee‼ samahani, Dada Clara anataka kuongea nawe, simu iko hewani  sebleni” alisema, nilimtazama kidogo. Sikutaka kumwuliza chochote tena 

    Nilielekea Sebleni nikimwacha Msichana nyuma yangu, kweli nilikuta simu  iko hewani, niliiweka simu sikioni  

    “Jacob, nilitaka kukujulisha kua nimefika salama Arusha.” Niliisikia sauti  ya Clara.  

    “Sawa” nilimjibu kwa Mkato Kisha nilisikiliza kama alikua na jambo la  kusema tena.  

    “Haya, kesho nitarudi. Uwe na siku njema” alisema, sikuitikia Bali nilikata  simu. Kuna kitu kuhusu Clara kilikua moyoni mwangu, kitu hicho kilijificha 

    lakini kilianza kuonekana taratibu, kitu chenyewe ni chuki ndogo.  Nilipomaliza, niliirudisha kisikilizio eneo husika Kisha nikageuka  nilikutana na Yule Msichana wa kazi anayeitwa Matilda, alikua akinitazama  na ilionesha alikua akisikiliza maongezi yetu.  

    Nilimvuka na kuelekea Chumbani kwangu. Nikaufungua na kufunga  mlango kwa nguvu sana, Hali ya hasira ilinijaa hasa nilipokumbuka  maneno ya Zaylisa kua Clara hapendi kuniona pale kwake.  

    Nilikumbuka kuhusu Boksi nililolisukumiza Uvunguni, basi niliinama na  kuanza kupapasa pale nilipoamini lile Boksi lilikua limetulia lakini  sikulipata. Niliinama na kuchungulia, palikua peupe, Boksi halikuwepo  mahala pale 

    Ilinishangaza sana, Nani atakua amelichukua na kwanini alichukue.  

    “Au Matilda atakua amelichukua? Kama amelichukua atakua amelionaje,  kwanini alichukue?” nilishusha pumzi, harufu ya utata ilikua imejaa puani  kwangu 

    Jasho lilianza kunitoka kama Mtu aliyekua chumba Cha joto, haraka  nilielekea kugonga chumbani kwa Matilda. Nilikua nahitaji majibu ya  maswali yangu 

    Alipofungua mlango alinitazama kama vile alikua akiniona kwa mara ya  kwanza. Nilimtazama kwa sekunde kadhaa bila kusema chochote kile Kisha  nilimuuliza kwa sauti kavu iliyokua imejaa mamlaka sana 

    “Umechukua Boksi chumbani kwangu?” swali hili liliambatana na kufunga  ndita zangu, sikutaka mzaha kwasababu niliamini lile Boksi lilikua na  Fumbo kuhusu Mimi, akili yangu iliniambia Kuna Sehemu ya Maisha yangu  ilikua imeondoka. Alinitumbulia macho kama vile alikua hajasikia  nilichomuuliza, nilimsogelea huku nikiwa nimemtolea macho ya hasira 

    “Boksi ulilolichukua chumbani kwangu lipo wapi?”  

    “Boksi?” aliniuliza huku mdomo wake mwekundu wenye upana kiasi  ukijiminya kwa kukosa neno la kuongeza 

    “Ndiyo” nilisema kwa hasira Hadi chembe za mate zilimrukia usoni,  alimeza funda zito la mate nililiona likipita kooni pake kama Nyoka  aliyemeza panya mnene, jasho likianza kumtoka huku hofu na wasiwasi  vikimtawala. 

    “Naongea na wewe Matilda, umechukua Boksi” nilimshitua tena baada ya  kuona akili yake ilikua imelala kwa tafakari ya kina, alipepesa kope za 

    macho yake, huku akizungusha macho kama kinyonga. Alipata kigugumizi  Cha sekunde kadhaa Kisha alikuja na jibu kavu huku akiondoa wasiwasi  aliouonesha awali. 

    “Sijui hata unauliza kuhusu Boksi gani, Mimi sielewi” sikuacha kumtazama,  niliona kuendelea kumuuliza ningepoteza muda mwingi zaidi. Niliondoka  nikimwacha amening’inia mlangoni kama konda wa daladala anayedaiwa  chenji. 

    Nilifunga mlango kwa nguvu, sauti ya kuubamiza ikavuma kuashiria  nilitumia nguvu nyingi kuufunga. Nilijiuliza lile Boksi lilikua na kitu gani  kilichokua maalum, kitu ambacho yule Mtu alidai nilipaswa kupokea siku  niliyopata ajali. 

    “ Alisema nilipaswa kupokea Boksi siku niliyopata ajali? Mbona ile siku  nakumbuka nilienda nyumbani kwao Zaylisa, hapa katikati Kuna Siri gani  kuhusu Mimi, kwanini Watu wananipa heshima Mimi masikini nisiye na  chochote?” nilijiuliza huku nikibadilisha mikao pale chumbani. 

    Ghafla tu, wazo la kumpigia simu Zaylisa lilinijia, nilihitaji kujua kama  alikua amefika kwa Baba yake. Nilipopiga niliambiwa simu ya Zaylisa ilikua  haipatikani, nilipatwa na hasira sana 

    Niliketi nikitafakari zaidi, hamu ya kuendelea kua ndani iliniisha. Niliona  ni Bora niende mgahawani ambako nilikua nikifanya kazi, japo nilikua  nimefukuzwa lakini niliamini huko ningepata mwanga zaidi wa Maisha  yangu  

    Niliondoka, nikaita Taxi. Safari ya kuelekea mgahawani ilianza. Nafsi yangu  ilikua kwenye Giza nene, hapakua na mwanga mithiri ya Handaki.

    Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya TISA

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love 

    riwaya riwaya ya koti jeusi riwaya za kijasusi

    4 Comments

    1. Elinor183 on September 24, 2025 5:15 pm

      https://shorturl.fm/sFDZF

      Reply
    2. Reese1981 on September 24, 2025 7:27 pm

      https://shorturl.fm/kY1h4

      Reply
    3. Hmc on September 24, 2025 8:14 pm

      Fupi sana

      Reply
    4. Halinga23 on September 24, 2025 9:12 pm

      Toa na ya 9 Kaka story tanu kweli

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 24, 2025

    In the name of LOVE – 08

    Ilipoishia sehemu ya saba ya In the name of LOVE “Nampeleka Mtoto Arusha, kesho nitarudi.…

    In the name of LOVE – 07

    In the name of LOVE – 06

    In the name of LOVE – 05

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.