Ilipoishia Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 07
“Unajua nini wewe?” Wakati huo Damu nyingi zilikua zikimtoka Mfalme Selasi, akamwambia Anna
“Unaenda kutafuta Pete ya Baba Yako, Mimi naijua ilipo. Namjua anayeitumia huko Duniani, bila Mimi kamwe hutoipata” Anna aligeuka akamtazama Zahoro Kisha Zahoro akamuuliza Mfalme Selasi
“Kama utasema ilipo basi nitakupatia jicho lako. Utajitibia na kupona, ipo kwa Nani?” Mfalme Selasi akaachia Kicheko Cha maumivu huku Damu ikimtoka Mdomoni. Endelea
SEHEMU YA NANE
“Huwezi kuitangaza amani ukiwa umeshika Upanga Kijana, nipatie jicho Kisha nitawaambia ilipo” Haraka kwa hasira Anna akaelekea chini na kumshika shingoni Mfalme Selasi Kisha akamwambia
“Kama unafikiria sitaipata Pete kwa sababu Yako ni Bora ufikirie mara mbili kwasababu tutakuacha hapa na hutopata msaada. Mji wote wa Patiosa utakua chini yetu muda siyo mrefu, ni Bora ufanye maamuzi kwasababu hatuna muda tena” alisema Anna, alimwonesha Mfalme Selasi upande wake wa pili akiwa na hasira.
“Sitawaambia Hadi mnipatie jicho langu. Hakika hamuijui Dunia, hamtaipata na kamwe hamtoiongoza Patiosa bila hiyo Pete” Anna akatikisa kichwa chake Kisha akasimama, akamshika mkono Moana, akasogea naye Hadi mlango wa Kuzimu.
Akamshika mkono Zahoro Kisha akamwambia Mfalme Selasi
“Kwa ajili ya Familia yangu basi huo Mji wa Patiosa si Mali kitu. Tunaondoka na kuifunga Kuzimu, hakuna kitakachoingia wala kutoka. Hadithi ya Maisha Yako itaishia hapa” alipomaliza kusema wote waliangalia mbele na kuiona jinsi Dunia ilivyo nzuri, Dunia ilikua ikilishuhudia jua la Mchana wakati huo Kuzimu ilikua ni Usiku.
Mara Mfalme Selasi akasema kwa kuweweseka.
“Sawa nitawaambia lakini mtunze ahadi yenu kwangu…” Anna na Zahoro waligeuka, Kisha Mfalme Selasi akawaambia
“Pete ipo kwa Mwanasayansi Mkubwa wa Nchi ya Ganza, anayeitwa Steve Mbasa.”
“Una hakika ni yeye ndiye aliyeuwa Wazazi Wangu?”
“Ndiyo Nina hakika, ni yeye ndiye aliyeuwa Wazazi wako hapa. Kisha aliondoka na Pete, yeye ni Mtu Mashuhuri sana, ni tajiri na ana uwezo mkubwa wa Kisayansi kwasababu ya hiyo Pete. Sasa nimeshawaambia Ukweli, nipeni Hilo jicho” Zahoro alimtazama Anna ambaye alianza kububujisha chozi lake pole pole Kisha Anna akamwambia Mfalme Selasi
“Nina hakika na maneno Yako, lakini nikukumbushe Mfalme kua. Ukiuwa kwa Upanga utauawa kwa Upanga, kwakua ulitutelekeza na sisi tunakutelekeza hapa”
“Hapana Usifanye hivyo Binti, sikuwauwa wakati ule. Niliwaacha mwende na Ndiyo maana Hadi Leo mpo hai”
“Sawa, Nami nakuacha uwe hai” alipomaliza kusema hivi. Waliingia Upande wa Pili ambao ni Duniani. Kisha waliufunga mlango wa Kuzimu, walijikuta wametokezea ndani ya godauni Moja lenye kuhifadhi mizigo ya Nafaka.
Mbele Yao walimwona Mzee mmoja ambaye aliwashuhudia Anna, Moana na Zahoro wakitokea Sehemu ya ajabu sana Kisha Sehemu hiyo kujifuta kama vile hapakutokea chochote.
Mzee huyo aliishiwa Cha kusema alibakia akiwatazama wakiondoka hapo Hadi nje ya godauni. Walijikuta wakiwa wamezungukwa na Maghorofa ya Mji Mkuu wa Nchi ya Ganza, Moana alitabasamu kwasababu aliyaona magari kwa mara ya kwanza, Kila kitu kilikua kipya kwake
Hii pia ilikua ni mara ya kwanza kwa Anna kufika Duniani, naye alijikuta akishangaa sana. Kila kitu kilikua kipya kwake, kuanzia hewa na Kila kitu. Aliachia tabasamu kama Moana, Zahoro hakushangaa sababu yeye alizaliwa Duniani hivyo alishawahi kufika ndani ya Jiji Hilo
“Tunahitaji pesa” alisema Zahoro. Anna aligeuka kumtazama Zahoro, alishangaa kumwona Zahoro ni Kijana wa Miaka 22 kama alivyopotea na Kijiji Cha Nzena, alirudi na Umri ule ule wakati Kule Kuzimu alikua na Umri wa kuanzia Miaka 40. Hata Zahoro alipomtazama Anna alistaajabu kumwona Anna ni Bibi Kikongwe, aliyejawa na mvi na makunyanzi, asiyejiweza kutembea vizuri.
Anna alijishangaa pia kutokana na sauti aliyoitoa, alihisi mwili wake kuchoka sana. Moana yeye alikua mdogo vile vile hakuna kilichobadilika kwake, Anna akajipapasa Uso wake Kisha akamwambia Zahoro
“Mimi si wa Duniani, sistahili kua hapa Zahoro” wakati anaongea hivi, Moana alishangaa kuona mkono wa Mama yake ukiwa na makunyanzi, akainua kichwa kutazama. Aliona mabadiliko ya Wazazi wake akauliza
“Mama, Baba….Mmekuaje?” alikua akistaajabu sana, Zahoro akasema
“Nitakueleza Moana, usijali. Kwasasa tupate mahali pa kufikia kwanza” Anna alimtazama Moana kwa jicho la huzuni sana huku moyo wake ukimwambia kua siku Moja ataachana na Moana na hatomwona Milele sababu Moana amefuata asili ya Baba yake.
Chozi likamtoka lakini akalifuta, Zahoro akaanza kumsaidia Anna kusonga mbele, wakavuka barabara. Wakasimama mbele ya Mgahawa, walikua wakihisi njaa pia hata mavazi Yao yalikua yamechoka sana
Watu waliwatazama kama Ombaomba wasiojiweza, baadhi waliwasaidia pesa. Kwa Moana na Anna pesa ilikua ni kitu kigeni kwao, lakini Anna akamwambia Zahoro kua wanaweza wakapata pesa kama hizo kupitia jicho la Mfalme Selasi
“Tafuta Sehemu tulivu kisha liambie Hilo jicho la Miujiza linaweza kutupatia pesa” alisema Anna, basi Zahoro akawasogeza ndani ya Mgahawa ili wapate chakula Kisha Zahoro akaelekea Chooni
Akatafuta Sehemu ya kutulia Kisha akaomba pesa kupitia jicho. Maburungutu ya pesa yakatijitokeza, Zahoro akayaokota na kuyasweka Mfukoni, Kisha akatoka.
Walikula chakula walichopenda na kulipa pesa Kisha walitafuta Hoteli nzuri wakachukua chumba. Zahoro aliondoka na kwenda Kununua nguo kwa ajili ya Moana na Anna Kisha aliporudi walikaa pamoja.
“Baba, kwanini mmebadilika?” aliuliza Moana. Zahoro alionesha tabasamu kidogo Kisha akamwambia Moana.
“Kwasababu tupo Duniani sasa, tupo mahali ambapo Mimi nilizaliwa na kukua. Mama Yako yeye si Mtu wa huku Ndiyo maana baada ya kuingia hapa amebadilika.”
“Mbona na wewe pia umebadilika?”
“Sijui Moana, lakini wakati nimepotea nilipotea nikiwa na Umri huu. Pengine Maisha yangu Duniani yalisimama, niliporudi Ndiyo yameendelea. Wewe umefuata asili yangu, wewe ni Mali ya huku”
“Kwahiyo Mama ataondoka si Ndiyo?”
“Ndiyo, wakati ukifika. Mengine utayajua Taratibu sawa?”
“Sawa” alisema Moana Kisha alimtazama Mama yake kwa huzuni sana, alikua amelala kitandani akionekana ni Mzee aliye dhahifu sana.
“Anna, tunahitaji kumpata Steve Mbasa haraka sana. Sijui itawezekana vipi lakini ni lazima iwe hivyo, tuipate Pete ya Baba Yako Kisha tutaieleza Dunia juu ya Kijiji Cha Nzena”
“Sawa Zahoro, nahisi baridi naomba nilale” alisema Anna, Zahoro akamfunika Anna shuka gubigubi Kisha yeye akaketi kochini. Moana naye akapitiwa na Usingizi Mzito.
**
Waliitumia siku yote kupumzika, kuzoea mazingira. Siku iliyofuata asubuhi, Zahoro aliwasha televisheni. Alikutana na taarifa ya Mwanasayansi Steve Mbasa aliyekua akifanya mahojiano na kituo Cha Runinga Cha Taifa kua anatarajia kuzindua kifaa kipya Cha kuelekea angani.
Ndipo Zahoro alipoiona sura ya Steve Mbasa aliyetajwa na Mfalme Selasi wa Kuzimu. Akatamani kuiona hiyo Pete inayosemwa, kweli aliiyona Pete nyekundu kidoleni. Pete hiyo haikuonekana kua ya Kisasa, pia ilikua ya kifalme.
Zahoro akamwambia Anna kua alichokisema Mfalme Selasi kilikua sahihi, jinsi ya kuipata Pete hiyo ilibaki kua ndoto ya Mchana.
Watawezaje kumfikia na kuichukua Pete? Zahoro alijiona ni Mtu pekee aliye na nguvu lakini hakua na mamlaka. Akamwuliza Anna
“Nifanye nini angali upo Kitandani?”
“Ili ufike kwake unapaswa kua tajiri, au Mtu mkubwa Zahoro. Msaada pekee ni Pete ya Miujiza. Inaweza kukufanya ukawa hivyo, ukiipata Pete Ndiyo nafuu yangu Mimi.” Alisema Anna. Basi Zahoro alianza kuliomba jicho limpatie pesa nyingi zitakazompa jina kubwa Mjini.
Lakini jicho hilo halikutoa pesa, halikufanya chochote. Zahoro alichukia sana akatamani kulipasua lakini jicho hilo likamwambia
“Hata ukiwa na pesa kiasi gani, hauwezi kuipata ile Pete. Anayepaswa kuichukua Pete ni Anna” wote walishangaa, Anna angewezaje kuipata Pete wakati yeye ni Bibi Mzee aliye kitandani.
“Anna yupo kitandani hajiwezi, atawezaje kuipata Pete?” Zahoro akauliza, lile jicho likasema
“Udhaifu wa Steve Mbasa ni kusikia habari za Kuzimu. Mara nyingi husisimka sana na kuhitaji kujua kuhusu Kuzimu kwasababu hufanya safari za mara kwa mara kuelekea Kuzimu kuonana na Mfalme Selasi” Zahoro alimtazama Anna, Kisha Zahoro akapata wazo akasema
“Tutampigia simu na kumdokeza machache kuhusu Kuzimu, kuhusu Mfalme Selasi na Mji wa Patiosa. Nina uhakika akisikia atahitaji kutufahamu. Hapo ndipo tutakapoweka mtego na kuipata Pete” akaachia tabasamu. Zahoro aliondoka Hotelini na kuanza kuuulizia namna ya kupata mawasiliano ya Mwanasayansi Steve Mbasa
Akafika Hadi kwenye makao Makuu ya Mwanasayansi huyo maarufu Duniani, mahali hapo palikua na Ulinzi wa kutosha lakini hakuogopa sababu alijua nguvu aliyonayo
Taratibu alipandisha ngazi na kufika lango kuu, hapo alikutana na eneo la mapokezi.
“Habari‼” alisalimia Zahoro kwa utulivu sana huku akiachia tabasamu. “Nzuri, Karibu sana.” Mdada aliyepo mapokezi alimjibu. Kisha Zahoro akasema
“Ninahitaji kuonana na Bwana Steve Mbasa” akaachia tabasamu kidogo, yule Mdada akamwuliza
“Una miadi naye?”
“Hapana, Mimi ni Mtu maalum kwake. Sihitaji Miadi” Yule Mdada akacheka kidogo akamwambia Zahoro
“Huwezi kuonana naye bila Miadi, hauonekani kama Mtu maalum. Istoshe yupo Nje ya Bara la Afrika” alisema.
“Ooh! Pengine Mimi ninaweza kumfanya arejee haraka sana kwa ajili yangu, unaonaje?” akasema Zahoro kwa kujiamini sana.
“Sidhani, Kuna jambo unahitaji msaada?”
“Hapana, yeye ndiye anayehitaji Msaada kwangu. Mpigie Umwambie Kua Mfalme wa Patiosa amefika” alisema Zahoro, yule Mdada akashangaa.
“Mfalme? Dunia ya Sasa Ina Mfalme mweusi? Hata hivyo siwezi kupoteza muda, unaweza ukaondoka au niite walinzi wakuondoe hapa?”
“Kama utampigia na kumwambia kua Mfalme wa Patiosa nimefika Kisha akakwambia hanifahamu unaweza ukawaambia Walinzi wanikamate na kunitupa nje” alisema tena kwa kujiamini. Yule Mdada akamtazama sana Zahoro, Ujasiri alionao ukamsukuma akashika simu akampigia Steve Mbasa.
“Samahani Bosi, Kuna Mtu amekuja hapa amejitambulisha kama Mfalme wa Patiosa. Anasema anahitaji kukuona” Yule Mdada alibakiwa na simu sikioni huku akimtazama Zahoro
Kisha simu ikaondolewa sikioni, akamwambia Zahoro
“Kwanini ameshtuka kusikia upo hapa?”
“Nilikwambia”
“Nenda chumba namba 555, floo ya saba” alisema, Zahoro akatabasamu Kisha akaongoza kuelekea Alipoelekezwa.
Alipofika floo ya saba akazuiliwa na walinzi, akasachiwa Kisha akaruhusiwa kuingia ofisini kwa Steve Mbasa. Hofu ikaanza kumwingia Zahoro huku akijiuliza kama ataweza kukabiliana na Steve Mbasa.
Alikutana na macho ya Steve Mbasa yakimwangalia kwa shahuku kubwa, akayafinya macho yake akimtazama Zahoro. Alikua na tafakari kubwa baada ya kumwona Zahoro, huku akijiuliza maswali mengi sana.
Zahoro akaketi pole pole kitini huku akikikagua chumba Cha ofisi, ilikua ni ofisi kubwa yenye picha nyingi ukutani, Steve Mbasa alikua ameketi kitini akimtazama.
“Wewe ni Nani?” akauliza.
“Mimi ni Mtu ninayekufahamu Steve Mbasa” alisema. Steve Mbasa akaachia Kicheko kidogo Kisha akamuuliza
“Umetumwa na GGB si Ndiyo? Nafikiria nahitaji kukufundisha somo ili ukamwambie aliyekutuma kua Steve Mbasa si Mtu wa kuchezea” alisema Steve Mbasa Kisha akachomoa Bastola na kujiweka vyema tayari kumuuwa Zahoro.
Macho yakamtoka pima Zahoro, akajua fika kua hapaswi kufanya Mchezo kwani Steve Mbasa ni Mtu katili asiyejali utu. Akamwambia
“Kabla hujanimaliza, natamani kukwambia kua kwasasa hutaweza tena kuelekea Kuzimu kwasababu funguo ya huko ninayo Mimi. Mfalme Selasi Hana tena madaraka, najua unaelewa kua ili Pete uliyonayo iendelee kufanya kazi unapaswa kuelekea Kuzimu Kila baada ya Muda Fulani.” Maneno ya Zahoro yalizidi kumfanya Steve Mbasa azidi kupagawa, akajikuta akichanganikiwa.
Aliyoambiwa na Zahoro yote yalikua ni kweli, si mambo ambayo hata GGB alikua akiyafahamu hivyo Zahoro alikua Mtu wa kipekee aliyeijua Siri ya Steve Mbasa.
“Wewe ni Nani?” akauliza.
“Mimi ni Mtu kutoka kuzimu. Nitaonana na wewe, nitakueleza ni wapi tukutane. Usisahau kua Nina funguo ya jicho la Mfalme Selasi” alisema Zahoro Kisha alisimama na kumwambia
“Ni lazima uniache nikiwa hai ili uilinde hii Siri ambayo hutaki Watu waijue, tutaonana Nje ya Mji, Jioni ya Leo. Uje peke Yako nitakupa jicho la Kuzimu” alisema Zahoro Kisha akaongeza
“Makutano ya Mji. Karibu na mnala wa Mashujaa, nitakua hapo kuanzia sasa 12 jioni nikikusubiria” alisema Kisha Zahoro aliondoka ofisini hapo akimwacha Steve Mbasa akiwa amepagawa.
Alijiuliza maswali mengi sana, mgeni huyo aliwezaje kuyajua yote Yale wakati ilikua ni Siri kubwa kati yake na Mfalme Selasi?
“Ni kweli hua naenda Kuzimu Kila baada ya Miezi kadhaa. Aliwezaje kuyajua yote haya, Ina maana ni kweli ametokea Kuzimu, kama ni hivyo napaswa kuipata hiyo funguo iwe yangu Milele. Nitaweza kwenda Kuzimu na kurudi Duniani nitakavyo Mimi” alijisemea Steve Mbasa
**
Jioni ilipofika, gari ndogo ya kifahari iliongoza kuelekea Makutano nje kabisa ya Mji, Kisha gari Hilo likaegesha karibu na Mnara wa Mashujaa, palikua tulivu, kimya. Ni eneo la kihistoria ya Mashujaa wa zamani waliopigana vita.
“Nitakuuwa Kisha nitakuchukua jicho bila sharti lolote lile” alisema Steve Mbasa huku akiweka sawa Bastola yake Kisha aliisweka kiunoni. Akashuka kwenye gari na kuiruhusu miguu yake kusogea taratibu Hadi eneo la Makaburi ya Mashujaa.
Alipofika hapo aliangaza huku na kule, kwa mbali akamwona Mtu akiwa ameketi. Alisogea taratibu Hadi alipomfikia, Mtu huyo alikua ameketi kwenye kiti Cha walemavu. Alipofika karibu alimwona Anna, hakumfahamu sababu hakuwahi kumwona popote lakini alishangaa kumwona Mzee eneo Hilo badala ya Zahoro.
Akaangaza huku na kule Kisha akamuuliza Anna
“Nilipaswa kuonana na wewe hapa?” Anna akamtazama Steve Mbasa kwa sekunde kadhaa Kisha akamwambia
“Ndiyo, nimekusubiria hapa kwa kitambo kidogo” alisema kwa sauti ya Uzee iliyojaa mikwaruzo.
“Iko wapi hiyo funguo?” aliuliza.
“Kabla sijakupa, nataka makubaliano.”
“Enhee‼ makubaliano gani?”
“Naitaka Pete” alisema Anna. Steve Mbasa akaangua Kicheko Kisha akasema
“Oooh kwahiyo unahitaji Pete ili unipe funguo ya Kuzimu. Nisipokupa utafanya nini?”
“Nitaichukua kama ulivyoichukua mikononi mwa Baba yangu Kisha ukamwua” alisema Anna, Steve Mbasa akajua sasa alikua akiongea na Mtoto wa Mfalme wa zamani wa Patiosa ambaye ndiye mmiliki wa Pete hiyo, akahamaki akachomoa Bastola yake
“Huwezi kuichukua Pete kutoka kwangu kamwe, hii Pete Ndiyo maana halisi ya Maisha yangu. Pete hii ni Uzima Wangu, ni utajiri Wangu hivyo siwezi kukupatia. Kwanza siwezi kukuacha ukiwa hai, ninakuuwa”
“Kama unaona ni rahisi kufanya hivyo basi niuwe Steve Mbasa, nimeishi Maisha yangu nikiwa na kisasi juu yako. Niliusubiria huu wakati kwa muda mrefu sana” alisema Anna, pale pale Steve Mbasa akafyatua risasi ya ghafla kuelekea kwa Anna.
Risasi ikapenya na kumrarua eneo la kifua, Damu nzito ikaruka. Anna akatoa Mchozi Kisha akamwambia
“Nimekuja kulipa Kisasi Steve Mbasa” Akapigwa risasi nyingine, Kisha akapigwa nyingine, akapigwa Risasi nyingi Hadi Bastola ya Steve Mbasa ikaishiwa na risasi. Jasho lilikua likimtoka Steve Mbasa huku akimtazama Anna aliyekua ameinamisha kichwa chake.
Baada ya kuona alikua amemwua Anna, aligeuka ili aondoke lakini ghafla alikutana na Sura ya Zahoro. Akapigwa na nyundo kichwani, akaangukia pembeni. Damu nzito ikawa inamtoka, Zahoro akamfuata na kuanza kumpiga na nyundo kichwani Hadi akahakikisha amemmaliza.
Akauvuta mwili wa Steve Mbasa kuelekea kwa Anna, Kisha akaukamata mkono wa Anna na kuutumia kuivua Pete, Kisha Pete hiyo akamvisha Anna. Ghafla polisi wakafika hapo kutokana na zile risasi zilizo sikika.
Wakamweka chini ya Ulinzi Zahoro. Mtu pekee aliye hai hapo alikua ni Zahoro, akakamatwa na Polisi kwa Kosa la Kumwua Mwanasayansi Steve Mbasa. Lakini Zahoro akawaambia
“Ni kweli Mimi ni Muuwaji lakini nimeuwa ili kuiokoa Dunia yetu dhidi ya Watu kama Steve Mbasa” Polisi walistaajabu Kauli ya Zahoro, wakatamani kumwuliza zaidi
“Ndiyo, Steve Mbasa amekufa akiwadanganya kuhusu Sayansi yake lakini ukweli ni kwamba yeye ni Mtu mbaya aliyejificha gizani, amefanya Mauwaji mengi ili kuificha Siri yake. Hakuna anayenijua Mimi lakini naweza kuwaeleza ukweli kua niliishi Kuzimu kwa muda mrefu, Mimi ni miongoni mwa Wakazi wa Kijiji Cha Nzena kilichopotea Duniani, mnakijua hiki kisa si Ndiyo?” Polisi wakatazamana, Kila mmoja akapata shahuku ya kusikia kuhusu kisa Cha Kijiji Cha Nzena kilichoibua maswali mengi yasiyo na Majibu.
“Mimi ni Mhanga wa kile Kijiji ambacho Hadi Leo kipo Kuzimu, Kijiji kile kilikumbwa na laana. Ndiyo sababu ya Kupotea kwake na hakiwezi kurudi tena Duniani, siyo Kijiji kile tu Bali Kuna Miji Mingi ipo kule, Nani anajua kuhusu Pete ya Steve Mbasa?” aliuliza, kuhusu swali hili wala hapakua na Siri sababu GGB aliwahi kuwaambia Watu kuhusu Sayansi feki ya Steve Mbasa akiitumia Pete ya Kuzimu.
“Nipo tayari kupokea adhabu lakini naomba mniruhusu nimrudishe Kuzimu huyu aliye kitini” wote waligeuka kumtazama Anna, walipigwa na Butwaa wakajikuta wakimwachia Zahoro Kisha Zahoro kwa kutumia Jicho akafanikiwa kuifungua njia ya Kuzimu pale pale, akamsukuma Anna kuelekea huko. Baada tu ya Anna kukanyaga ardhi ya Kuzimu akaonekana akibadilika na kua Mwanamke mrembo kama zamani, tena akiwa hai kabisa. Wote walistaajabu Kisha Anna akanyanyuka kutoka kitini na kuwaambia Polisi
“Hii Ndiyo Dunia iliyojificha, Dunia iliyobeba Siri na Miujiza Mingi. Kuanzia sasa naifunga hii njia na hakuna atakayeweza kufika huku. Zahoro naomba umtunze Moana” alisema Anna huku taratibu ile njia ikijifunga.
Chozi la Anna lilimfanya Zahoro aangue Kilio, alikua anaachana na Anna Milele. Hadi mlango unajifunga polisi wote walikua wanashangaa, Waandishi wa Habari walikua hapo wakionesha tukio Hilo Moja kwa moja. Rais wa Nchi ya Ganza akahitaji kuzungumza na Zahoro, akachukuliwa na kupelekwa Ikulu, akaeleza kuhusu Kijiji Cha Nzena.
Akawa ni shuhuda pekeee aliyepotea na kurejea Duniani. Serikali ikamwachilia huru Zahoro, vikaaandikwa vitabu vingi juu ya mapenzi ya Anna na Zahoro, juu ya Mwanasayansi Steve Mbasa. Miongoni mwa waliotajwa kuwa Mashujaa basi GGB naye alikua miongoni mwao sababu alisema huu ukweli Miaka Mingi lakini hakusikilizwa.
Zahoro aliendelea kumlea Moana kama Binadamu wa kawaida, Kisha Mji wa Patiosa ukawa chini ya Anna na Alice ambaye alishinda vita na kuurudisha Mji chini ya Himaya Yao, Mji wa Patiosa ulipata Nuru tena baada ya utawala wa Damu kukoma. Anna na Alice wakaanza kutafuta Watu waliokwama kwenye Miji mingine na kuwaingiza Patiosa ili waishi.
MWISHO.
Unatamani Riwaya Inayofuata Iwe Na Maudhui Gani? Mapenzi au Ujasusi au Maisha?
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx
3 Comments
Iwe ya ujasusi
Ujasusi
https://shorturl.fm/upwy1