Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya sabaย
Siku iliyofuata, Serikali iliongeza Watu zaidi ili kumsaidia Waziri kazi ya utafiti eneo laย tukio, sio TU wataalam kutokea Ganza bali Afrika nzima pamoja na Mataifa kadhaa yaย
Ulaya. Sayansi ilikataa kutoweka kwa Kijiji hicho lakini shahidi za kimazingira ikiwemoย ramani pamoja na Wakazi wa vijiji jirani zilichagiza uzito wa jambo lenyewe.ย
Pamoja na uwepo wa Sayansi lakini nyuma ya pazia Waziri Majula Majula alikuaย akishirikiana na Mganga aliyemwamini huku akiwa amepoteza Imani na Sayansi yaย Mazingira ambayo ilikua ikiendelea Kuchunguza kupotea kwa Kijiji Cha Nzena.ย ย
SEHEMU YA NANEย
Helikopta zilizobeba maafisa ziliendelea kushuka eneo la Tukio, ulinzi ukazidiย kuimarishwa huku Waandishi wa Habari wakizuiwa kutoa taarifa yoyote ile inayohusuย kupotea kwa Kijiji hicho Hadi pale Serikali ya Ganza itakavyotoa mwelekeo waย Uchunguzi.ย ย
Kwenye mitandao ya Kijamii kama X , Facebook na Instagram paliibuka hoja kua ulikuaย ni Mpango wa Serikali kutengeneza propaganda ili kuchukua Madini na kuuza bila pesaย kuingia Serikalini lakini walio eneo la tukio waliishia kujishika vichwa vyao. Mtu pekeeย ambaye alibeba matumaini Yao alikua ni Zahoro, lakini simu ya Zahoro ilikuaย haipokelewi tena.ย
Hisia zao ziliwaambia pengine Mtu huyo alikua tayari ameshafariki Dunia. Hawakua naย Uwezo tena wa kupata taarifa kutoka ndani ya Kijiji kisichoonekana.ย
***ย
Ndani ya Kijiji Cha Nzena.ย
โAaaahggโผโ ilikua ni sauti ya Kugugumia ya Zahoro, alijikuta ndani ya shimo lenye Gizaย nene kiasi kwamba hakupata nafasi ya kuona chochote. Palikua kimya kuliko kawaida,ย harufu ya uozo ilikua ikipenyeza pua yake ndogo Iliyo chongoka.ย
Alijiinua na kuketi chini, kwa mbali alianza kusikia sauti ya utiririko wa Maji. Aliamuaย kufuata hisia pamoja na sauti hiyo pasipo kuona mbele. Kila alivyojaribu kupiga hatuaย aliona inawezekana kuifikia sauti hiyo, hakujua Upendo alikua wapi. Kichwa lilikuaย kinamuuma, akakumbuka kilichokua kimetokea wakati wanakimbizwa na kile kiumbeย Cha ajabu.ย
Alitumbukia ndani ya shimo Hilo kabla hajanaswa na kile kiumbe Cha ajabu. Pichaย halisi ilikua kichwani pake, akajikuta sasa akiwa na shahuku ya kumtaka kujua alipoย Upendo, alianza kumwita kwa sauti ya chini iliyojaa tahadhari sanaย
โUpendoโผ Upendoโผโ hapakua na mwitikio wowote ule, alijihisi kua peke yake ndani yaย shimo Hilo lililojaa Giza, shimo lililo chimbwa kuelekea mbele mithiri ya handaki.ย
Alipoona ukimya ndio ulikua ukimwitikia aliamua kwenda mbele kufuata mtiririko waย Maji, alitembea taratibu akipapasa Kila Kona ya shimo Hilo ili kuhakikisha anafikiaย lengo lake huku kitendawili kichwani pake kikiwa kama ataweza kutoka nje ya Kijiji Chaย Nzena akiwa salama.ย ย
Alikua amechoka kwa njaa Kali na kiu cha Maji, alihisi koo lake likiwa limekauka hukuย akikiri kua mwili wake ulianza kua dhahifu sana. Hakukata tamaa alizidi kwenda mbeleย bila kuchoka, shimo lilikua na kona nyingi zilizo titia ukimya.ย
Alitembea kwa hatua nyingi za kuhesabu Hadi pale alipoanza kuhisi mwanga machoniย pake, hata sauti ya kutiririka kwa Maji ilikua ikisikika kwa ukaribu zaidi. Alianzaย
kupepesa macho yake ili aone mbele zaidi, angalau alianza kuona ni wapi alipotoka naย wapi anakoelekea.ย
Alijikuta akiwa amesimama mwisho wa shimo Hilo, mbele yake palikua na korongoย kubwa linalotiririsha Maji likiwa limepambwa kwa mawe makubwa na miamba mizito.ย Hakuweza kuangalia chini kwa jinsi ambavyo palikua mbali, angehisi kizunguzungu.ย ย
Hapa kua na dalili ya yeye kutoka eneo Hilo hatari ambalo halikua na njia yoyote tenaย zaidi ya kurudi alipotoka. Alijikuta chozi likiwa linambubujikaย
Masikini Zahoro aliketi chini kwa kukata tamaa Kisha alijiinamia huku akitiririsha choziย lake, kushuka kule chini ilikua haiwezekani kabisa sababu palikua na umbali mrefu naย hatari zaidi. Alilia kwa uchungu, alikua amekata tamaa ya kuendelea kuishi.ย
Alikumbuka mambo mengi yaliyopita kwenye Maisha yake, wakati mzuri alioishi naย Baba yake kabla ya Kijiji chao kukumbwa na laana. Aliwakumbuka marafiki, mandhariย nzuri ya Kijiji Cha Nzena ambacho sasa kinateketea.ย
Hakua na Mtu pembeni yake, alihisi upweke ulio ambatana na hofu isiyo mithirika.ย Mapigo ya moyo wake yalitoa ishara kua hapakua na tumaini la uhai wake. Akajiulizaย
โKwanini naendelea kuishi kwenye Ulimwengu wa Giza?โ ilikua ni sauti kuu iliyopitaย kwenye akili yake, nafsi yake ikamwambia kua ni Bora kufa kuliko kusubiria kifo Chaย mateso hapo mbeleni. Masikini Zahoro aliona ni Bora ajitupe korongoni na afie hukoย kuliko kufa taratibu kwa njaa, hofu na kiu.ย
Alipomaliza kutafakari alisimama Kisha alisogea karibu na Mdomo wa Korongo uolikuaย ukimnongโoneza kua ajitupe na afie humo. Alivuta hewa nyingi ili kujiweka sawa,ย akafumba macho tayari kwa kujitosa Korongoni.ย
Mara alianza kusikia sauti kubwa ikija upande wake, sauti hiyo ilimshtua huku masikioย yake yakiisikiliza kwa makini. Alipofumbua macho alikua amepata jibu kua ilikua niย sauti ya mashine. Moja kwa Moja alijua kua huwenda alishafika nje ya Kijiji Cha Nzena.ย Alitabasamu huku chozi likimtoka kwa uchungu na hamu ya kutoka salama.ย
Macho yake yalimwonesha uhalisia wa alichokisia, ilikua ni sauti ya Helkopta ya Kijeshiย iliyobeba Watafiti waliokua waliendelea kukichunguza Kijiji kilichopotea Cha Nzena.ย Helkopta hiyo ilikua mbali kiasi Cha MITA mia mbili lakini ilikua ikisogea taratibu.ย
Zahoro akapaza sauti yake huku akinyoosha Mikono yake akiomba msaada, alipungaย mikono yake.ย ย
Mmoja wa Watafiti alimwona Zahoro, akamwambia rubani asogeze Helkopta hiyoย karibu na Korongo ili waone zaidi kama alikua Mtu. Kadili walivyosogea walishangaaย kumwona Mtu.ย
Chozi likimbubujika Zahoro, Helkopta ilikua imeshafika mbele yake. Akapiga goti hukuย akiwa analia kwa Uchungu na furaha, wale Watafiti walihitaji kumsaidia Zahoroย wakiamini anaweza kua miongoni mwa Wahanga wa Kijiji Cha Nzena.
Walisogeza zaidi Helkopta. Mmoja akajaribu kumwambia Zahoro kwa sauti ya Juu kua,ย ajiandae kurukia kwenye Helkopta. Wakaisogeza zaidi ili iwe rahisi kwake kuingia ndaniย ya Helkopta.ย
Ghafla Upepo Mkubwa ukaanza kuvuma na kusababisha rubani ashindwe kuimuduย Helkopta, upepo ukaishinikiza Helkopta ianguke lakini Rubani alikua akipambanaย kuhakisha wanaondoka hapo haraka sana.ย
Tumaini lilianza kufifia kwa Zahoro, alikua akiushuhudia Upepo katili ukiishinikiza kwaย nguvu sana Helkopta hiyo, alijua upepo huo haukua wa kawaida ulikua ni ule upepo waย ajabu. Sauti ya Bibi Lugumi ilianza kusikika na kuzima kabisa ndoto za Zahoro.ย
Helkopta ilianza kuyumba Kisha iliangukia Korongoni na kuwaka Moto. Hapakua naย msaada tena kwa Zahoro lakini alitambua kua alikua ameshafika nje ya Kijiji Cha Nzena,ย shimo Hilo ilikua NDIYO njia ya kuondoka Kijijini hapo.ย
Taswira ya sura ya Bibi Lugumi ilionekana katikati ya Upepo huo, Bibi Lugumi hakutakaย Mtu yeyote atoke Kijijini hapo. Zahoro alianza kutetemeka huku akirudi nyuma nyumaย huku akiushuhudia Upepo huo ukianza kumfuata taratibu.ย
Alianza kukimbia kuelekea ndani zaidi ya shimo Hilo lenye Giza nene, alikimbia bilaย kuona mbele huku akiusikia upepo ukivuma nyuma yake. Aliendelea kukimbia kwa Kasiย huku akijigonga gonga huku na kule ndani ya shimo Hilo.ย
Alikimbia bila tahadhari huku akisukumwa na hofu iliyotanda akilini mwake, alikimbiaย Hadi alipofika mwisho wa shimo. Juu yake akaona Pana mizizi mikubwa akajishikizaย hapo Kisha akatokea kwa juu.ย ย
Akajikuta ndani ya Kijiji Cha Nzena, maiti zilikua Kila mahali. Aliuwona utofautiย mkubwa sana wa alipotoka na alipo, alihisi alikua amerudi Kuzimu. Sauti za ajabuย zilikua zimetawalaย
Akiwa hapo alisikia sauti ya Mtoto mchanga kwa mbali, alijikuta akiwa na shahuku yaย kuifuata, taratibu alianza safari ya kuifuata sauti hiyo ambayo ilisikika Mita kadhaย kutoka alipo. Alitembea taratibu na kwa tahadhari kubwa sana Hadi alipofika eneo Hilo,ย hakuyaamini macho yakeย
Sauti aliyokua akiisikia haikutoka kwa Mtoto Bali ilikua imetoka kwa Mwanaumeย mmoja aliyetapakaa Damu, alimwonesha Zahoro tabasamu la kuashiria kua alikuaย amemnasa kwenye mtego wake.ย
Mwanaume huyo alikua ameshikilia Upanga mkononi mwake, alikua akimtazamaย Zahoro kwa jicho la roho mbaya. Alikua tumbo Wazi, Zahoro alianza kurudi nyumaย huku akijihadhari na hatari ya Mwanaume huyo wa ajabu.ย
Basi yule Mwanaume akaanza kumfukuza Zahoro kwa Kasi ya ajabu sana, alionekanaย Wazi kua alikua na nguvu za Kichawi zisizo za kawaida. Alikua na Kasi sana kulikoย Zahoro aliyezorota kwa njaa na kiu, Kijana Zahoro alijitahidi sana kukimbia kwa Kasi iliย aokoe Maisha yake
Kila alipogeuka aliziona hatua za yule Mwanaume aliyetapakaa Damu huku Upangaย wake ukiwa mkono wa kulia tayari kumshambulia pindi atakapomnasa. Ulikua mtihaniย mzito kwa Zahoro, bahati mbaya akajikwaa kwenye kisiki na kuanguka.ย
Hakuweza kunyanyuka kwa haraka, alikua chini akigalagala kwa maumivu makali yaย Mguu wake hasa eneo la Goti. Fumba na kufumbua, Alikua amekamatika na yuleย Mwanaume. Mwanaume huyo alikua akikoroma mithiri ya Simba Dumeย
Zahoro alikua akitetemeka mwili mzima, aliiona pumzi ya Maisha yake ikikatishwa naย Mwanaume huyo wa ajabu sana aliyekua akichecheza kwa Madaha. Zahoro alianzaย kujiburuza kwa kutumia makalio yake lakini haikumsaidia kufika mbali na kujiokoa.ย ย
Macho yalimtoka Zahoro akiushuhudia Upanga wenye Damu ukishuka kuelekea mwiliniย mwake, alifumba macho asiwe shuhuda wa mateso yake. Damu nzito ikamrukia Zahoroย usoni, alihisi pumzi zake zikikataย
Lakini alijishangaa kujihisi si mwenye maumivu ya Upanga isipokua Damu pekeeย iliyomrukia usoni, akapata hamu ya kufumbua macho yake. Akakutana na sura yaย Mwanamke akiwa amesimama mbele yake, Mwanamke huyo alivalia suruali na tishetiย ya Bluu, chini alikua amevalia kiatu aina ya buti nyeusi. Mkononi alikua ameshikaย Upangaย
Zahoro alistaajabu sana kwa msaada aliokua ameupata, ulikua ni msaada asioutarajia.ย Kando palikua na mwili wa yule Mwanaume wa ajabu ukivuja Damu. Midomo yaย Zahoro ikatamani kumuliza maswali mengi lakini yule Mwanamke wa Makamoย aliyemzidi kidogo umri Zahoro akampa mkono ili kumnyanyua Zahoro.ย
Japo kwa kusita lakini Zahoro aliutoa Mkono wake akampatia Mwanamke huyo. Kishaย akainuliwa juuย
โNaitwa Anna, Mimi ni mwokozi. Nimekuja kukuokoa hapaโ alisema Mwanamke huyoย kwa kujiamini sana, Upanga wake Bado ulikua ukitiririsha Damu, Zahoro aliuangaliaย Upanga Kisha kamjibu kwa hofuย
โNaitwa Zahoroโย
โNakufahamu Zahoro, wewe ndiye jibu la Laana hii. Uliiona kabla haijaingia pia utaionaย ikiondoka, huwezi kunielewa kwasasa lakini nitakueleza zaidi. Nifuateโ alisemaย Mwanamke huyo, Bado aliacha maswali mengi sana kichwani kwa Zahoro. Taratibuย Zahoro alianza kutembea kwa kuchechemea kutokana na majeraha ya Mguu aliyoyaptaย
Alitembea kidogo Kisha alianguka tena kutokana na kizunguzungu kilichosababishwaย na njaa Kali na kiu. Anna akambeba Zahoro na kuondoka naye hapo.ย
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TISA Hapa Hapa Kijiweni
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
73 Comments
https://shorturl.fm/dctKr
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
https://shorturl.fm/0n5Z8
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
https://shorturl.fm/bkQi3
Kumeshaanza kichangamka๐คฆ๐ป๐คฆ๐ป
https://shorturl.fm/8sxMw
https://shorturl.fm/X6uUY
https://shorturl.fm/kNXNF
https://shorturl.fm/r9O4W
https://shorturl.fm/nPm57
https://shorturl.fm/TX5Xn
https://shorturl.fm/02Kqc
https://shorturl.fm/STEG5
https://shorturl.fm/I8rFz
https://shorturl.fm/9v47u
https://shorturl.fm/3tswR
https://shorturl.fm/baRVh
szw4of
https://shorturl.fm/uSVGc
https://shorturl.fm/4dOTW
https://shorturl.fm/4M1nB
7yb1ws
https://shorturl.fm/I2nbg
https://shorturl.fm/9idfJ
https://shorturl.fm/B2Ilh
https://shorturl.fm/hGQ7Q
https://shorturl.fm/dRZZi
https://shorturl.fm/bOxc1
https://shorturl.fm/5wPf7
https://shorturl.fm/oKCFb
https://shorturl.fm/eQRQp
https://shorturl.fm/CoOAH
https://shorturl.fm/ELXLW
https://shorturl.fm/1o6So
https://shorturl.fm/AG6RN
https://shorturl.fm/UozrM
https://shorturl.fm/7CwxL
https://shorturl.fm/Ly7JW
https://shorturl.fm/I215V
https://shorturl.fm/TBImU
https://shorturl.fm/HhfXe
https://shorturl.fm/5hRiw
yglu82
https://shorturl.fm/w42jA
https://shorturl.fm/ubfmE
https://shorturl.fm/tFqIw
https://shorturl.fm/n1yIN
3096o7
https://shorturl.fm/4mfaI
https://shorturl.fm/LAmlz
https://shorturl.fm/rr2v0
https://shorturl.fm/mfI4Q
https://shorturl.fm/LYvtl
https://shorturl.fm/qNNqJ
https://shorturl.fm/dQdsy
pwl9j8
https://shorturl.fm/d1ZVj
https://shorturl.fm/CSaKo
https://shorturl.fm/aPD1X
https://shorturl.fm/tPGPT
dtobo7
https://shorturl.fm/XVBlw
c2s82s
h7b9lb
https://shorturl.fm/BI9Sf
ylx7l4
https://shorturl.fm/h3ckO
https://shorturl.fm/J0QCo
https://shorturl.fm/Vbq3I
https://shorturl.fm/K2myW
https://shorturl.fm/QVEGY
https://shorturl.fm/Onmem