Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 07

    Vilabu Vyamwaga Mabilioni Dirisha La Usajili EPL Likivunja Rekodi

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 06

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-05
    Hadithi

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-05

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJuly 17, 2025Updated:July 23, 202576 Comments8 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya nne

    Wakiwa wanaendelea kujibizana, walianza kusikia sauti ya Bi. Lugumi ikisema 

    “Kufaaaaa‼ kufaaaa‼” kila aliyeisikia sauti hii alianza kutetemeka huku damu nzito  ikimtoka puani kisha walikufa papo hapo, hali ya taharuki iliingia na kufanya kila  mmoja atawanyike anakokujua yeye mwenyewe. Sauti ya Bibi Lugumi ilizidi kusambaa,  ilikua ni sauti ya kunong’ona iliyotoka kwa kuivuta sana. 

    SEHEMU YA TANO

    Kelele za Wanakijiji ziliwashtua Mzee Miroshi na Zahoro wakiwa wamefungiwa ndani ya  chumba kimoja nyumbani kwa Mzee Kova, Zahoro akamwambia Baba yake 

    “Ni lazima tujiokoe kutoka hapa Baba” alisema kisha alitafuta kitu kitakachomsaidia  kuuvunja ule Mlango, macho yake makubwa yalikiona kipanda cha mbao kilichokua  kimeegemezwa ukutani, akakichukua. Kilikua ni kipande kilichotokana na fanicha za  

    zamani, haraka akasogea mlangoni huku akimtazama Baba yake Mzee Miroshi ambaye  tayari alikua ameshaishiwa nguvu huku akitoa hewa nzito 

    “Baba usijali tutatoka salama Hapa” alisema Zahoro, kisha alimsogeza kando Baba yake  ili atakapouvunja mlango Baba yake asiathirwe na vipande vitakavyoruka. Akavuta  nguvu kisha akaukita mlango kwa kutumia kipande cha mbao, mlango ukatikisika 

    Kelele zilizoendelea kusikika huko nje zilimpa nguvu Zahoro ya kuendelea kuuvunja  Mlango ili waondoke kifungoni. Hapakua na Mlinzi hapo nje kwasababu taharuki  ilikuwa imewasomba wote na kuiacha nyumba hiyo yenyewe. 

    Zahoro aliendelea kugonga mlango kwa nguvu zaidi, kila pigo liliufanya mlango  kudhoofika. Jasho lilimtoka huku mikono yake ikianza kuuma, lakini hakuacha. Alijua  kuwa muda ulikuwa hauko upande wao. Baada ya mapigo kadhaa, mlango ulianza  kulegea na hatimaye kupasuka vipande vipande. Haraka akamshika baba yake mkono  na kumsaidia kusimama. 

    “Twende Baba, hatuna muda!” alisema kwa sauti ya dharura. Zahoro alimsaidia Baba  yake kutoka ndani ya chumba kisha wote walisimama huku macho yao yakijawa na  Mshangao. Moshi mkubwa ulikua ukifuka Kijijini, Mlinzi mmoja wa kijiji ambaye  aliachwa kwa ajili ya kuwalinda walimkuta akiwa amelala chini huku Damu nzito  ikimtoka puani na Mdomoni. 

    Mzee Miroshi aligeuza shingo yake kwa uchovu akimtazama Zahoro ambaye aliguswa na  Mtazamo wa Baba yake, macho yao yalipokutana kila mmoja alisubiria kusikia kutoka  kwa mwenzake. Ghafla sauti ya muito wa simu ilisikika kutoka kwenye mfuko wa suruali  wa Zahoro. 

    Mzee Miroshi alikaza macho ya Mshangao, hakuwahi kumwona Zahoro akiwa na simu  hata siku moja. Zahoro alipepesa macho taratibu kumwonesha Baba yake kua alikua  akiitumia simu hiyo kisiri, haraka aliitoa kutoka mfuko wa siri maarufu kama ‘Docho’

    Ilikuwa ni simu ndogo sana. Mzee Miroshi akampa ishara Zahoro aipokee haraka – pengine wangepata msaada wa kutoka hapo kijijini. Zahoro aliweka simu sikioni, lakini  kabla hajaongea chochote, alishtuka kuona kivuli kikisogea mbele yake. 

    Mzee Kova alikuwa amesimama hapo, uso wake ukiwa na uamuzi usiotikisika. Mikono  yake ilikuwa thabiti, ikishikilia bunduki aina ya Gobole, ambayo sasa ilikuwa  imeelekezwa moja kwa moja kwa Zahoro. 

    “Usithubutu kuendelea,” Mzee Kova alisema kwa sauti nzito, yenye mamlaka. 

    Zahoro alihisi mgongo wake ukilowa jasho, lakini akajitahidi kutokupoteza mwelekeo.  Akatazama moja kwa moja machoni mwa Mzee Kova, akijaribu kutafuta dalili yoyote ya  huruma. “Mzee Kova, hatutaki matatizo. Tunajaribu tu kuondoka hapa,” alisema kwa  sauti tulivu lakini thabiti. 

    Mzee Kova hakutikisika. “Hamna pa kwenda. Mnafikiria mnaweza kutoroka baada ya  yote yaliyotokea?” aliuliza huku akiimarisha mshiko wake kwenye Gobole. 

    Mzee Miroshi aliyekuwa kimya muda wote, alisogea mbele kidogo, akiinua mkono wake  kwa ishara ya utulivu. “Mzee Kova, umetufahamu kwa miaka mingi. Unajua kuwa sisi si  maadui zako. Tafadhali, tuache tuondoke.” 

    Mzee Kova akahamaki huku akihisi pengine Mzee Miroshi alikua anapanga njama ya  kumzubaisha ili waondoke, akaikaza Gobole huku kidole kikiwa tayari kufyatua risasi,  akawa anaiamisha Bunduki kutoka kwa Zahoro kuelekea kwa Mzee Kova 

    “Nipatie hiyo simu vinginevyo nitamuuwa Baba yako” alisema Mzee Kova kwa sauti  iliyoashiria muda wowote anaweza kutenda ikiwa mzaha utatokea. Kwa jinsi Zahoro  anavyompenda Baba yake, alimpatia ile simu Mzee Kova ambaye alikua makini sana. 

    Akamuuliza Zahoro 

    “Hakuna simu inayofanya kazi hapa Kijijini, simu yako imewezaje kuita?” Zahoro  alijawa na hofu huku akitetemeka. Jasho la mgongo lilikua likimvuja 

    “Mzee Kova, Kijana wangu si adui yako. Alikua Mdogo wakati ule, tafadhari sana  hurumia Maisha yake” alisema Mzee Miroshi, akapigwa na Mdomo wa gobole  akaanguka chini.  

    “Hii Biashara haikuhusu kabisa Miroshi, kaa kimya.” Kisha akamgeukia Zahoro,  akakaza Mikono yake kwenye Gobole huku akimtazama kwa jicho kali. 

    “Wewe kosa lako ni kuona laana ikiwa inaingia, nina uhakika unajua njia ya kutoka hapa  Kijijini” alisema Mzee Kova, kelele za WanaKijiji ziliendelea kuongezeka, vilio na Moshi  viliendelea kujaza taharuki.

    Sauti ya Bibi Lugumi ilikua ikiendelea kusikika taratibu ikija nyumbani kwa Mzee Kova,  kila mmoja aliisikia sauti hiyo, ni sauti nyemelezi isiyo na kelele. Sauti ya kunong’ona  inayouwa Mamia ya Wanakijiji wa Kijiji cha Nzena. Mzee Kova akataka kufanya haraka  ili sasa Zahoro aseme njia ya kutoka hapo Kijijini ili awe salama na Laana ambayo yeye  ndiye aliyeisababisha kwa kumuuwa Masumbuko. 

    Zahoro alikua kimya akiisikia sauti hiyo iliyokua ikikaribia hapo, sauti hii ni ile sauti  aliyoisikia ndotoni. Ni sauti iliyomsumbua, hakutaka kuisikia. Akaziba masikio yake 

    “Hutaki kusema si ndiyo? Sasa nakuuwa” akasema Mzee Kova, kitendo bila kuchelewa Mzee Miroshi akaivuta Miguu ya Mzee Kova ili Zahoro akimbie. Mzee Kova akaanguka,  Gobole lake ikadondokea pembeni. 

    Ghafla wote wakasimama huku wakiangalia juu, kitendo kilichomshangaza sana Zahoro,  akajiuliza maswali mengi huku akiwa ameziba masikio yake. Akashuhudia Damu  zikianza kuwatoka. Hata dakika moja haikufika, walianguka chini na kuanza  kutapatapa. Kwa macho yake Zahoro alishuhudia kivuli chenye taswira ya Bibi Lugumi  aliyemwona ndotoni, alikua akitabasamu huku akiongea maneno yake ambayo Zahoro  hakutaka kuyasikia kabisa 

    Macho yalimtoka pima Zahoro, alirudi nyuma huku akijibamiza ukutani. Alihisi hali  isiyo ya kawaida, mwili ulikua mzito akitokwa na jasho jingi huku kile kivuli kikimtaka  Zahoro atoe mikono yake Masikioni aisikie ile sauti ya ajabu inayouwa. Zahoro hakutaka  kuisikia ile sauti hivyo alijitahidi sana kupambana 

    Kadili kivuli kilivyosogea ndivyo ambavyo alikua akipata maumivu makali ya kichwa,  mwisho alipiga kelele yenye sauti kali ya kugumia. Pale pale alipoteza fahamu zake na  kuanguka chini kama mzigo. 

    *** 

    Nje Ya Kijiji. 

    Magari ya Ulinzi na Usalama yalikua eneo ambalo Kijiji cha Nzena kilikuwepo kabla ya  kutoweka kwake. Bado ilibakia kua simulizi ya kushangaza kwa wengi. Waziri wa  Maliasili alikua akifikiria kwa kina ni sayansi ya aina gani ambayo imekipoteza Kijiji  kilichobeba rasilimali kubwa ya Madini, wafanya Biashara na wamiliki wa Migodi  walikua wamepotelea humo. 

    Simu zilikua hazipatikani, akasogea kwa mmoja wa washauri wake akamwuliza 

    “Haihusiani na Uchawi?” aliuliza kwa sauti ambayo ilionesha wazi kuwa alikosa majibu  ya kawaida. Aliongea akiwa anapandisha suruali yake nyeusi, akaweka koti lake vizuri.  Huku nje ilikua ni saa Mbili asubuhi, jua lilikua limechomoza vyema sasa. 

    “Mh! Hili jambo ni gumu sana kulipatia majibu ya haraka, kupotea kwa Kijiji ni hadithi  za kwenye vitabu vya kale lakini leo tumeshuhudia hili jambo la kushangaza” alijibu  Mshauri wa Waziri, akaweka mawani yake vizuri halafu akaendelea 

    “Pengine tunaweza kupata Majibu kwa njia hiyo, hebu tuifanyie kazi” alisema, haraka  Waziri akamjibu kwa sauti ya kishindo

    “Atafutwe na afichwe kwa siri ili hili jambo liwe siri baina yetu.”  

    “Ondoa shaka Mkuu” akasema kisha akapiga simu mahali ili kuhitaji Mganga wa  Kienyeji mwenye uwezo Mkubwa sana wa kuangalia mambo yasiyoonekana kwa macho  ya kawaida.  

    Ilichukua takribani masaa mawili hadi kumpata na kumfikisha kwenye gari ya Waziri wa  Maliasili. Gari hiyo ilikua kubwa yenye nafasi ya kutosha, Mganga akaelezwa ni jambo  gani aliloitiwa hapo. 

    Yule Mganga akacheka kidogo kama ilivyo kawaida ya waganga, kisha akatulia na  kuwaambia 

    “Niliona kuhusu Kijiji hiki, hakipo. Kukiona ni Mjaaliwa” alisema kwa kujiamini, kwa  sauti ya upole sana iliyojaa huzuni. Waziri akashtuka kisha akamwuliza 

    “Unamaanisha nini?” alihoji akiwa ameshupaza shingo yake huku makunyanzi yakiwa  yamefunga uso wake. Mganga akameza mate kidogo halafu akasema 

    “Kijiji hiki, kimepokea laana ya Miaka mingi kwa kifo cha Kijana Masumbuko aliyekua  mlemavu wa ngozi. Tangu hapo Bibi yake alikilaani Kijiji hiki kisha alijichoma Moto na  kufa, sasa ile laana imekifanya Kijiji hiki kupotelea kuzimu. Laiti kama mgepata japo  nafasi ya kusikia sauti za vilio, mateso na maumivu wanayo kutana nayo mgelia machozi  ya Damu.” Alisema kisha alisikitika kwa kichwa chake 

    “Hakuna anayeweza kwenda huko wala kutoka huko. Historia itafutika, Kijiji cha Nzena  kimeshapotea. Msihangaike sababu hakuna atakayetoka hai na kurudi Duniani”  alisema, Waziri na Mshauri wake walitazamana. Walielezwa kila kitu na hawakuwa na  swali lolote lile, Mganga akarudishwa walipomtoa. 

    Ukimya ukatawala, kila mmoja alikaa kimya baada ya kujua kuwa hakuna chochote  wanachoweza kukifanya ili kukipata Kijiji hicho tajiri. Agizo la Rais lilikua ni  kuhakikisha wanapata ufumbuzi wa Kisayansi lakini hadi muda huo Sayansi haikutoa  majibu, majibu pekee ambayo waliyapata ni ya kiganga. 

    Waziri akajitupa kitini huku akifumba macho yake, hakujua atamweleza vipi Rais wa  Ganza, utajiri uliopotea kwenye Kijiji cha Nzena ni utajiri mwingi sana wa Madini. 

    Mara mlango wa gari ulifunguliwa haraka sana, Waziri na Mshauri walishtuka. Mtu  mmoja kutoka kwenye timu yake alikuja ghafla na kumwambia kua kuna Mtu kutoka  Kijiji cha Nzena amepiga simu. Macho yalimtoka Waziri wa Maliasili, ingewezekanaje  kua simu itoke kuzimu? Alikua kama Mtu aliyezinduliwa kutoka usingizi wa Pono,  akatupa swali moja ngangari 

    “Unasemaje?”  

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU Hapa Hapa Kijiweni

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    riwaya riwaya mpya riwaya za kusoma mtandaoni

    76 Comments

    1. Kingmbinga on July 17, 2025 5:29 pm

      Good job 🔥🔥🔥🔥

      Reply
      • Yudra on July 17, 2025 5:53 pm

        Tamu

        Reply
    2. Eunice Timba on July 17, 2025 5:55 pm

      Aloooooo hii mambo ni 💥💥💥💥Afu nikukumbushe ni sehemu ya Sita ndo inafata na si sehemu ya tatu kama ulivosema

      Reply
    3. G shirima on July 17, 2025 6:19 pm

      Bonge la move

      Reply
    4. Maestro05 on July 17, 2025 8:00 pm

      Simulizi nzuri Sana sema imekuwa fupi

      Reply
    5. Karim on July 18, 2025 10:12 am

      Mbna kama zahoro atapona🤔

      Reply
    6. [email protected] on July 18, 2025 8:47 pm

      Good story

      Reply
    7. Shelby4467 on July 19, 2025 5:02 pm

      Boost your income effortlessly—join our affiliate network now! https://shorturl.fm/m2tJf

      Reply
    8. Cameron878 on July 19, 2025 7:53 pm

      Drive sales, earn big—enroll in our affiliate program! https://shorturl.fm/xYLqR

      Reply
    9. Ada2323 on July 21, 2025 6:12 am

      https://shorturl.fm/UdQFq

      Reply
    10. Zane601 on July 21, 2025 6:33 am

      https://shorturl.fm/1eb7S

      Reply
    11. Eleanor1932 on July 21, 2025 9:19 am

      https://shorturl.fm/gUgcb

      Reply
    12. Dallas312 on July 21, 2025 5:09 pm

      https://shorturl.fm/RHot4

      Reply
    13. Mia1531 on July 21, 2025 8:06 pm

      https://shorturl.fm/u2mR6

      Reply
    14. Coraline3817 on July 21, 2025 9:18 pm

      https://shorturl.fm/6Ij8t

      Reply
    15. Kathryn3363 on July 22, 2025 1:46 am

      https://shorturl.fm/n18PQ

      Reply
    16. Asia1406 on July 22, 2025 2:55 pm

      https://shorturl.fm/lLCPQ

      Reply
    17. Geoffrey2867 on July 23, 2025 2:53 pm

      https://shorturl.fm/VDFz4

      Reply
    18. Felix2154 on July 23, 2025 4:50 pm

      https://shorturl.fm/YSHok

      Reply
    19. Levi4990 on July 24, 2025 7:52 pm

      https://shorturl.fm/qMyW8

      Reply
    20. Chad2680 on July 24, 2025 10:46 pm

      https://shorturl.fm/QPd5u

      Reply
    21. Jill4614 on July 24, 2025 11:08 pm

      https://shorturl.fm/8z1AV

      Reply
    22. Alberto2683 on July 25, 2025 4:20 am

      https://shorturl.fm/mU0Th

      Reply
    23. Gage1724 on July 25, 2025 12:54 pm

      https://shorturl.fm/o6Pa2

      Reply
    24. Roger222 on July 25, 2025 2:39 pm

      https://shorturl.fm/W8CvZ

      Reply
    25. Loren4904 on July 25, 2025 3:13 pm

      https://shorturl.fm/DZT98

      Reply
    26. Brandi3566 on July 25, 2025 4:06 pm

      https://shorturl.fm/dun6S

      Reply
    27. Bethany199 on July 26, 2025 5:16 am

      https://shorturl.fm/sYo2L

      Reply
    28. Clarence5000 on July 26, 2025 11:48 pm

      https://shorturl.fm/45riq

      Reply
    29. Amy532 on July 27, 2025 1:28 am

      https://shorturl.fm/ibdka

      Reply
    30. Alejandro3226 on July 27, 2025 1:43 am

      https://shorturl.fm/QpYwV

      Reply
    31. Jim1211 on July 27, 2025 8:35 pm

      https://shorturl.fm/93dBl

      Reply
    32. Weston3537 on July 28, 2025 1:33 am

      https://shorturl.fm/BZcIn

      Reply
    33. Camryn3915 on July 28, 2025 6:14 am

      https://shorturl.fm/i5ly7

      Reply
    34. Paisley1250 on July 28, 2025 10:00 am

      https://shorturl.fm/ptVVr

      Reply
    35. Christina2132 on July 28, 2025 11:04 am

      https://shorturl.fm/LbsZr

      Reply
    36. Clarence537 on July 28, 2025 12:15 pm

      https://shorturl.fm/yhxOF

      Reply
    37. Catherine736 on July 28, 2025 12:53 pm

      https://shorturl.fm/6o3Jf

      Reply
    38. Roger4037 on July 28, 2025 10:02 pm

      https://shorturl.fm/rB0xk

      Reply
    39. Arabella773 on July 29, 2025 4:44 am

      https://shorturl.fm/fEb6q

      Reply
    40. Aisha4959 on July 29, 2025 6:17 am

      https://shorturl.fm/kCC0O

      Reply
    41. Nicole1954 on July 29, 2025 11:42 am

      https://shorturl.fm/NR2u3

      Reply
    42. Carolina2009 on July 29, 2025 3:09 pm

      https://shorturl.fm/p9E8w

      Reply
    43. Isaiah1239 on July 30, 2025 2:56 pm

      https://shorturl.fm/tbLWx

      Reply
    44. Scott167 on July 30, 2025 5:26 pm

      https://shorturl.fm/TBImU

      Reply
    45. Jonas4460 on July 31, 2025 8:12 am

      https://shorturl.fm/us6pn

      Reply
    46. Gwendolyn48 on July 31, 2025 8:29 am

      https://shorturl.fm/643Zb

      Reply
    47. Franklin207 on July 31, 2025 5:50 pm

      https://shorturl.fm/RT29D

      Reply
    48. Agnes3571 on July 31, 2025 7:09 pm

      https://shorturl.fm/Os806

      Reply
    49. Deirdre4091 on August 1, 2025 2:36 pm

      https://shorturl.fm/FYm24

      Reply
    50. Lila485 on August 1, 2025 2:41 pm

      https://shorturl.fm/JkkWy

      Reply
    51. Lynda4372 on August 1, 2025 3:31 pm

      https://shorturl.fm/Ge56k

      Reply
    52. Dane577 on August 1, 2025 7:47 pm

      https://shorturl.fm/PnAnI

      Reply
    53. Colby1345 on August 2, 2025 2:35 am

      https://shorturl.fm/pK2t7

      Reply
    54. Nikita244 on August 2, 2025 3:05 am

      https://shorturl.fm/ocsH9

      Reply
    55. Dana3469 on August 2, 2025 4:39 pm

      https://shorturl.fm/mos1j

      Reply
    56. Haley3588 on August 3, 2025 2:41 pm

      https://shorturl.fm/HfmZn

      Reply
    57. Elsa1793 on August 3, 2025 4:21 pm

      https://shorturl.fm/qqf35

      Reply
    58. Allison1512 on August 3, 2025 4:42 pm

      https://shorturl.fm/mfI4Q

      Reply
    59. Blair3851 on August 3, 2025 8:53 pm

      https://shorturl.fm/gwE4n

      Reply
    60. Robert1964 on August 4, 2025 1:33 am

      https://shorturl.fm/3Nb4c

      Reply
    61. Esme2947 on August 4, 2025 6:50 pm

      https://shorturl.fm/KwpEn

      Reply
    62. Khloe369 on August 7, 2025 1:19 am

      https://shorturl.fm/YGoz4

      Reply
    63. Jake2521 on August 8, 2025 8:08 am

      https://shorturl.fm/IegeZ

      Reply
    64. Jim526 on August 9, 2025 2:35 pm

      https://shorturl.fm/Nll2t

      Reply
    65. Dorothy3158 on August 12, 2025 1:31 am

      https://shorturl.fm/ZmiSh

      Reply
    66. Chase4333 on August 12, 2025 8:28 am

      https://shorturl.fm/E0888

      Reply
    67. Julian2203 on August 14, 2025 4:48 pm

      https://shorturl.fm/Gg3yo

      Reply
    68. Alaina4720 on August 19, 2025 3:08 am

      https://shorturl.fm/Y3zyG

      Reply
    69. Brian2234 on August 19, 2025 10:15 am

      https://shorturl.fm/PZWoO

      Reply
    70. Karina499 on August 21, 2025 8:13 am

      https://shorturl.fm/n7iyP

      Reply
    71. Theo1421 on August 22, 2025 9:21 pm

      https://shorturl.fm/JtN4E

      Reply
    72. Liam2160 on August 24, 2025 1:39 pm

      https://shorturl.fm/HdajW

      Reply
    73. Cassidy826 on August 25, 2025 6:31 am

      https://shorturl.fm/LXJF8

      Reply
    74. Lachlan594 on August 25, 2025 8:58 am

      https://shorturl.fm/hYYqX

      Reply
    75. Jed1620 on August 25, 2025 10:39 pm

      https://shorturl.fm/RfKcn

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 2, 2025

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 07

    Ilipoishia Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 06  Walipofika shangwe liliibuka kwa Wananchi waliamini kua kumwaga Damu …

    Vilabu Vyamwaga Mabilioni Dirisha La Usajili EPL Likivunja Rekodi

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 06

    Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 05

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.