Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02
    Hadithi

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJuly 12, 20256 Comments9 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya kwanza 

    “Baba” aliita Zahoro, Mzee Miroshi alimtazama Zahoro bila kusema chochote huku sura  yake ikionesha utayari wa kumsikia.  

    “Naogopa Mimi” alisema Zahoro, alijisogeza mwilini mwa Baba yake na kumkumbatia,  haikua hali ya kawaida kwa Mzee Miroshi. Alijua ni kitu gani alichokua akikiota  Mwanaye sababu alimsikia akiweweseka. 

    Alimeza tena funda zito la mate huku akimpiga piga Zahoro Mgongoni katika hali ya  kumfanya ajisikie kupoa. 

    SEHEMU YA PILI

    Zahoro alilala mwilini mwa Baba yake hadi kulipopambazuka, alipoamka alikutana na  sura ya Baba yake. Uso wa Zahoro bado ulikosa nuru kabisa, aliketi vizuri huku akiwa  amejiinamia kimya. 

    Mzee Miroshi hakusema chochote alinyanyuka na kuelekea chumbani kwake, kisha  baada ya dakika mbili alirejea chumbani kwa Zahoro na Kuketi kitandani.

    “Zahoro” alimwita 

    “Baba” 

    “Usije ukazungumzia kuhusu ndoto yako kwa Mtu yeyote yule, jiandae tunaondoka  Kijijini sasa hivi” alisema kisha alihitaji kunyanyuka lakini Zahoro alisema na kumfanya  asite kunyanyuka 

    “Umeijuaje ndoto yangu Baba?” aliuliza huku akimtazama Baba yake, alikaza macho  huku akisubiria jibu. Mzee Miroshi alinywea, akatazama chini huku akiwa amejiinamia 

    “Baba” baada ya kitambo Zahoro alimkumbusha Baba yake. Mzee Miroshi akainua  kichwa chake akamtazama Zahoro kisha akamshika mkono na kumwambia 

    “Ulichokiota nakijua, hii ni siri nzito sana ambayo inakuja kuharibu Kijiji cha Nzena.  Ulikua mdogo Zahoro wakati laana inatolewa na Bibi Lugumi kutokana na kifo cha  Masumbuko, niliamini laana ile haiwezi kupita bure ni lazima ingerudi na kukitesa  Kijiji. Miaka kumi na tatu imepita sasa, ile Laana imeanza kufanya kazi, naamini  kuanzia sasa Nzena itakua sehemu mbaya zaidi Duniani” alisema kwa utulivu Mzee  Miroshi, wakati huo ilikua kama hadithi ya kusadikika kwa Zahoro. 

    Masikio yake yalisikia, akili yake ikamuuliza, Baba yake aliwezaje kujua alichokiota.  Alishusha pumzi kisha akamwuliza Baba yake 

    “Kwani Masumbuko aliuawa?” Kabla Mzee Miroshi hajajibu, ilisikika sauti ya kuita  huko nje. Mzee Miroshi akamwambia Zahoro 

    “Andaa mizigo michache tunaondoka sasa hivi, ngoja niitike wito nje” alisema kisha  taratibu aliondoka chumbani kwa Zahoro. Alipofika nje, alikutana na Mzee mwingine  aliyeegemea ukuta mbovu, akamwambia 

    “Kwanini unataka kuangukia ukuta wangu Mzee Kisugu?” Mzee huyo aliyeitwa kwa jina  Kisugu, alinyanyua macho yake. Alikua amevalia shati jeusi lenye makunyazi, suruali  iliyopasuka kidogo. Juu alikua na baraghashia iliyopoteza rangi yake ya kahawia 

    Alimtazama Mzee Miroshi kwa macho yaliyobeba Ujumbe fulani mzito, walisogeleana.  Tahadhari ilianza kumwingia Mzee Miroshi, aliona uso mfupi wa Mzee Kisugu ukiwa na  Ujumbe wa kutatanisha, akamwuliza tena 

    “Kimetokea nini Kijijini?” Kisha Mzee Kisugu akashusha pumzi, akasema “Msiba Mzee Miroshi” 

    “Msiba?” 

    “Siyo mdogo, Kijiji kina Msiba mzito sana”  

    “Upi huo?”  

    “Watu watatu wamekutwa wakiwa wamejinyonga wenyewe kwenye Majumba yao, wote  ni viongozi wa Kijiji akiwemo mwenyekiti, Makamu wake pamoja na Mzee Ushirika”  Mwili wa Mzee Miroshi ulikua kama umemwagiwa maji, alipoa mwili na roho yake, hata  mdomo wake ulikataa kutoa neno akabakia akiwa amemtazama tu.

    “Jiandae uje Mzee Mwenzangu” alimaliza Mzee Kisugu kisha akageuka na kuondoka  hapo kwa hatua fupi fupi huku mikono ikiwa nyuma, chozi lilianza kumbubujika Mzee  Miroshi, nyuma yake alitokea Zahoro, alikua amesikia kila kitu. 

    Zahoro alisogea hadi mbele kwa Baba yake, akashuhudia chozi likimbubujika Baba yake. “Baba” akaita. 

    “Hupaswi kua hapa Zahoro, Ondoka haraka sana. Mungu akipenda tutaonana wakati  mwingine” alisema Mzee Miroshi, bado masikio ya Zahoro yalikua yakipokea kauli tata  ambazo hakuweza kuzichambua na kuzielewa kabisa.  

    “Baba” 

    “Nimesema ondoka Kijijini hapa, Nenda mbali, hii adhabu isikukute Zahoro.” Mzee  Miroshi alipaza sauti yake, Zahoro hakuwahi kuisikia sauti ya namna hii kutoka kwa  Baba yake hivyo alijua kuna jambo lisilo la kawaida limeanza kutokea Kijijini hapo,  haraka akaingia ndani kisha akatoka akiwa amebeba begi dogo Jeusi 

    Alimtazama Baba yake. 

    “Usiseme chochote, nenda na Usigeuke nyuma. Nenda mbali Zahoro, hii laana isikukute  popote. Kuanzia Sasa usizungumze chochote kile hadi utakapofika mbali na Kijiji hiki”  alisema Mzee Miroshi huku chozi likiendelea kumbubujika. 

    Macho ya Zahoro yalidondosha chozi, hakutegemea kama siku moja angetengana na  Baba yake. Ghafla palitokea wingu la ajabu lililoanza kukifanya kijiji kua giza, Zahoro  akamwambia Baba yake 

    “Kama ninaikimbia laana ziwezi kukuacha hapa Baba yangu. Twende” alisema kisha  alimshika mkono Baba yake, Mzee Miroshi akamwambia Zahoro. 

    “Nenda ndani, kwenye begi langu kuna kitabu. Niletee haraka sana” alisema, haraka  Zahoro alikimbilia ndani huku giza likianza kukizingira Kijiji chote. Ilikua ni hali ya  ajabu ambayo ilishtua wengi, ghafla Asubuhi iligeuka kuwa Giza tupu. 

    Zahoro alipotoka ndani hakumwona Baba yake, alijaribu kuizunguka nyumba kwa  kuamini pengine angekua nyuma ya nyumba lakini haikuwa hivyo, hapakua na dalili ya  uwepo wa Mzee Miroshi popote pale. Hali ya taharuki ilianza pale Kijijini Nzena, watu  walitoka ndani ili kujionea kwa macho namna ambavyo Giza lilikua likiingia kwa kasi ya  ajabu sana. 

    “Babaaa‼ Babaaaa‼” aliita Zahoro huku chozi likimtoka, alimjua Baba yake na  misimamo yake. Hakutaka kuongozana na Zahoro, alihitaji Zahoro pekee aondoke  Kijijini hapo haraka zaidi. Zahoro hakua na chaguo, alianza kukimbia kuondoka kijijini  hapo. 

    Mzee Miroshi alikua amejificha nyuma ya Mti mkubwa akimtazama Zahoro akiwa  anakimbia, akajisemea 

    “Nenda, hukuhusika na chochote Zahoro. Mimi nitawajibika sababu sikupinga mauwaji  ya Masumbuko, hii laana itatumaliza na kulipa kisasi kwa Kifo cha yule Kijana na Bibi  yake” alipomaliza kujisemea aliishika njia ya kuelekea kwenye Msiba.

    Baada ya Masaa matatu, giza liliondoka ghafla sana. Anga likatawaliwa na mwanga wa  jua. Simulizi za hapa na pale zilianza, kila mmoja alielezea namna ambavyo giza lile  liliweza kumwogopesha.  

    Mkaguzi wa Kijiji aliyetumwa na Wazee wa Kijiji aliagizwa kuzunguka kila nyumba ili  kubaini kama giza lile lilileta madhara, alipomaliza kuzunguka alirudisha jibu kua hali  ilikua shwari kabisa Kijiji chote.  

    Mzee mmoja akamtazama Mzee Miroshi kisha akamwuliza 

    “Una hakika?” alikua amemkazia macho, kilikua ni kikao cha dharura huku taarifa ya  Mzee Miroshi kua Kijiji kimepokea laana ikijadiliwa. Mzee Miroshi akatazama chini,  alipoinua kichwa akapepesa kidogo kope zake huku upepo wa wastani ukiendelea  kuvuma 

    “Ndiyo, si habari ya kusadikika bali ni habari ya kweli” alijibu kwa sauti ya utii kwa  Mzee huyo wa Kijiji cha Nzena aliyekua amekunja uso wake, wengi walikua  wakimwogopa kutokana na Uchawi alionao. Yeye ndiye aliyetoa amri ya Masumbuko  kuuawa kwa kile alichokiita kuondoa laana. 

    Kisha akamsogelea Mzee Miroshi, Mzee huyu Mchawi na katili aliitwa Mzee Kova.  Alikua na macho mekundu, alikua amevalia msuli na tisheti nyeusi, akamtazama sana  Mzee Miroshi kisha akamwambia 

    “Namwona Zahoro akikimbia Kijiji, hakuna atakayeondoka hapa Nzena.” Alisema kwa  kujiamini, kikao hiki kilikua kikifanyika nyumbani kwa Mzee Kova. Akaagiza Zahoro  akamatwe haraka sana 

    Askari wa Kijiji walitawanyika kila kona kumtafuta Zahoro. Mzee Miroshi alimwomba  Mzee Kova kwa kupiga magoti kua amwache Zahoro aondoke Kijijini lakini amri hiyo  haikubadilika, yeye pia alikamatwa na kufungiwa kwenye moja ya chumba cha Mzee  huyo hapo nyumbani kwake. 

    Hakuna aliyejaribu kufungua mdomo kuhoji, wala kutetea. Wote walikua kimya  akiwemo Mzee Kisugu.  

    ** 

    Upande wa pili, Zahoro alikua amekimbia umbali mrefu hadi alichoka. Bado alikua  ndani ya Kijiji lakini angalau alikua amefika mbali. Aliamua kupumzika chini ya Mti  mmoja mkubwa, akafungua begi lake dogo akatoa kopo la maji na kuanza kugida ili  kuusaidia mwili kukaa vizuri. 

    Sauti ya Bi Lugumi ilikua ikijirudia masikioni mwake, ilikua ni sauti kali iliyokua  ikimwambia kua Laana ya Kijiji ilikua imeshafika, hakuna Mtu atakayeingia wala kutoka  ndani ya Kijiji hicho, Watu watakufa kwa mpigo, wataandamwa na laana ya vizazi na  vizazi. 

    Sauti hii ilikua ikimfanya Zahoro akimbie zaidi, alinyanyuka na kuongeza mbio akiamini  alikua akikaribia Kijiji jirani, alikua Msituni. Alizidi kukimbia hadi alipoanza kusikia  sauti ya vilio vya Watu. Alisimama kwa mshituko na Mshangao mkubwa.

    “Kwanini wanalia?” alijiuliza Zahoro, alikua akitokwa na jasho. Alimeza funda zito la  mate kisha alianza kutembea huku akiishuhudia njia mbele yake kitu ambacho kilianza  kumshangaza Wakati alikua kwenye Msitu mnene. Aliamua kuifuata huku sauti ya vilio  ikizidi kupaa kuonesha kua alikua ameshafika eneo hilo. 

    Cha ajabu alianza kusikia sauti ya Baba yake Mzee Miroshi, alisimama huku akijiuliza  alikua akiisikia kweli au lilikua wenge lake tu, masikio na akili yake vikamwambia alikua  akiisikia kweli sauti ya Baba yake Mzee Miroshi akiwa anagugumia kwa maumivu.  Hakutaka kuamini kua sauti hiyo ilikua ya Baba yake kwani alikua ameenda mbali zaidi  na Kijiji 

    “Sasa kama ni Baba yangu, amefika saa ngapi huku?” alijiuliza, akili yake ikakumbuka  kua alipotezana na Baba yake wakati giza linaingia, akajipa tumaini huwenda Baba yake  alikua wa kwanza kufika. 

    Kadili alivyokua akipiga hatua alizidi kushangaa Zahoro, alikua akiingia Kijijini kwao,  Ndiyo! Kijiji cha Nzena ambacho alikua amekikimbia kwa zaidi ya Masaa matatu, nguvu  zilimwisha Zahoro. Mbele yake alikua akiitazama nyumba ya Mzee Kova, ndimo sauti ya  Baba yake ilimokua ikisikika. 

    Nguvu zilizidi kumwisha Zahoro, chozi lilianza kumbubujika huku yale maneno ya Bibi  Lugumi yakianza kutimia, akayasikia tena kua 

    “Laana imeshaingia Kijiji cha Nzena, Hakuna atakayeingia wala kutoka. Watu watakufa  kwa Mpigo, laana itadumu vizazi kwa vizazi” sauti hii ilimfanya aamini kua ndoto yake  ilikua ya ukweli ndiyo maana hata alipojaribu kukikimbia Kijiji alijikuta akirejea tena  Kijijini.  

    ** 

    Kijiji cha Nzena kilipotea, hakuna aliyekiona tena. Wageni waliotarajia kuingia Kijiji  hicho siku hiyo walipigwa na Butwaa. Hapakua na Kijiji isipokua pori lenye nyasi fupi,  ndege na Wadudu wadogo wadogo. Mwanzo ilikua kama taarifa ya kuchekesha ilipofika  kwa baadhi ya Watu wakiwemo matajiri wanao miliki migodi ndani ya Kijiji hicho. 

    Masaa mawili baadaye taarifa ilienea Duniani, kauli ya Bibi Lugumi ilizidi kutimia.  Taarifa kila ilipofika ilishangaza sana, haikua rahisi kuamini eti Kijiji kimepotea  hakionekani. Wataalam wa masuala ya Uchunguzi, maafisa wa ardhi, viongozi wa Vijiji  jirani wote walikubaliana kua Kijiji hicho kilikua kimetoweka na kubakia Pori dogo,  eneo hilo ndilo hasa kilipokua Kijiji cha Nzena. 

    ** 

    Kijijini Nzena. 

    Zahoro aliendelea kushangaa, Sauti ya Baba yake kuomba msaada ilizidi kumduwaza.  Hakujua aamini au akatae lakini tayari alikua ameingia tena Kijiji kilicholaaniwa cha  Nzena. 

    Alipiga magoti na kujiinamia huku chozi likimtoka Zahoro, yeye na Baba yake pekee  ndiyo ambao walikua wa kwanza kutambua kua laana ya Kifo cha Masumbuko  iliyotolewa na Bibi Lugumi ilikua imeanza kufanya kazi, lakini ni yeye pekee ndiye 

    aliyegundua kua hakuna anayeweza kuondoka hapo Kijijini kuanzia muda ambao aliiota  Laana ile na kuisikia sauti ya laana ya Bibi Lugumi  

    Akiwa hapo anatokwa na mchozi, mara alivamiwa na walinzi wa Kijiji waliotumwa na  Mzee Kova kumkamata. Dunia yake ilijaa mishangao sana, akawauliza kwa sauti ya  upole huku chozi likimtoka. 

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU Hapa Hapa Kijiweni

     

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

     

    riwaya mpya riwaya za kusisimua riwaya za kusoma mtandaoni

    6 Comments

    1. Rachel Richard on July 12, 2025 6:23 pm

      Duh angetoka hata zahoro tu sio mbaya asa mbona balaa hili

      Reply
    2. Senior on July 12, 2025 7:40 pm

      Fantastic story 👏

      Reply
    3. Ankush on July 12, 2025 10:08 pm

      🔥🔥🔥

      Reply
    4. Jovis .s. Banturaki on July 12, 2025 10:45 pm

      Funzo la liwaya hii tujifunze kutoonea watu Kwa sababu ya rangi kabira sura hata umasikini tukijua kua ukimuua binadam mwenzako utapata utajiri wakati hata ww huna mda dunian Asante kaka mkubwa Kwa mafundisho

      Reply
    5. Jovis .s.Banturak on July 12, 2025 10:49 pm

      Unasitahiri mchango wa kuendereza kazi. Hii tuutumeje ukufukie kaka mkubwa

      Reply
    6. Karim on July 12, 2025 10:55 pm

      Heeh kesi imeshakuwa ngumu 🙆

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 12, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya kwanza  “Baba” aliita Zahoro, Mzee Miroshi alimtazama Zahoro bila…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.