Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)

    Ratiba Kamili Ya FIFA CLUB WORLD CUP 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nne-04)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nne-04)
    Hadithi

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nne-04)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 30, 2025Updated:May 31, 202517 Comments8 Mins Read810 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia sehemu ya tatuย 

    “Ndio, ni Mwanangu! Miaka mingi sasa tangia Martinย  alipofariki kwa ajali ya gari akiwa anaelekea Mjini, tanguย  siku hiyo sikuwahi kuamka na kukaa tena hata ongea yanguย  ilikuwa ya shida, Martin alikuwa ndiyo Mwanangu wa pekeeย  niliyempenda, tumaini la Maisha yangu lilikuwa kwa Kijanaย wangu Martin baada ya Baba yake kufukiwa na kifusi hukoย  Merelani akiwa anafanya kazi za mgodi” Alisema Mama huyo,ย  kisha alimuomba Mjukuu wake amsindikize mahali.ย 

    “Nifuateni” Alisema Mama huyo ambaye alijitambulisha kamaย  Mama yake Martin Gimbo ambaye alikuwa akitajwa kama gaidiย  kiongozi wa kundi la ESS. Endelea

    SEHEMU YA NNE

    Walizunguka nyuma ya nyumba, aliwaonesha kaburi la Martinย  Gimbo, kaburi hilo lilikuwa dogo tu kuashiri kuwa Martinย  alifariki akiwa bado Kijana Mdogo, hii iliwashangaza Faudhiaย  na Mohd ambao ndimi zao zilikuwa kimya sana, Faudhia aliketiย  juu ya tofali moja akionesha kuchanganywa na maelezo ya Huyoย  Mamaย 

    “Hakuna aliyewahi kuja kumuulizia Martin Gimbo, nimeshtukaย  baada ya miaka mingi nyie kuja kumuulizia Martin, kwaniniย  mmekuja kumuulizia?” Alihoji Mama huyo.ย 

    “Mama una hakika Martin amefariki?” Alihoji Mohdย 

    “Ndiyo! Martin alizikwa hapa! Ilikuwa ni siku ngumu sanaย  kwangu. Siku ambayo siwezi kuisahau katika Maisha yangu”ย  Aliendelea kuelezea Mama Martin Gimbo, Faudhia alitoa pichaย  ya Martin Gimbo kisha alimpatia Mama huyo ili kuona kamaย  naweza akamtambuaย 

    Mama huyo aliiangalia picha kwa umakini sana, kishaย  aliwatazama Faudhia na Mohdย 

    “Mnamaanisha nini?” Aliwaulizaย 

    “Mama, sisi ni Undercover kutoka kitengo cha Usalama waย  Taifa, kama unavyojuwa sasa hivi tunakabiliwa na ugaidi hapaย  Nchini, huyo pichani ni mshukiwa namba moja, umemfahamu?”ย  Alisema Mohd huku akiamuachia swali Mama huyoย 

    Mama huyo aliirudia kuiangalia tena ile picha kisha alitikisaย  kichwa chake na kusemaย 

    “Anafanana na Martin! Lakini mbona Martin wangu alifarikiย  miaka mingi iliyopita na alizikwa hapa” Alisema Mama huyoย  ambaye hali yake ilianza kubadilika baada ya kuanzaย  kushtushwa na taarifa alizokuwa akizisikiaย 

    “Kifo cha Martin wako kilitokeaje?” Alihoji Faudhia harakaย  baada ya kutambua kuwa Mama huyo alikuwa kwenye hali mbayaย  ambayo ingepelekea kushindwa kuzungumza baada ya dakikaย  kadhaa. Mama huyo alianza kusimulia ilivyokuwa siku ya kifoย  cha Mwanaye japo alikuwa akisimulia kwa shida

    “Martin alipomaliza elimu ya sekondari, aliniaga kuwa anaendaย  kwa Baba yake Mkubwa huko Tabora, lakini majira ya mchanaย  nilipokea taarifa kuwa gari alilopanda Martin lilipata ajaliย  mbaya na kusababisha Mwanangu apoteze uhai, mwili wa Martinย  uliharibika mno ila kwasababu alipata ajali hapa hapa Arushaย  ilibidi aletwe kwa ajili ya maziko” Alisema Mama huyo hukuย  akikohoa, chozi lilikuwa linambubujikaย 

    “Nani alitoa taarifa ya Kifo cha Martin?” Alihoji tenaย  Faudhia kwa umakini sana, Mama huyo alikuwa na picha ambayoย  alipiga yeye na Mtu aliyetoa taarifa ya kifo cha Martinย 

    “Huyu ndiye aliyenipigia simu, aliongozana na Watu wa Gari laย  kubebea maiti kuja hapa” Aliitoa picha iliyomuonesha Mtuย  aliyeenda na maiti ya Mwanaye Martin ikiwa imeharibika, Mohdย  aliiangalia picha hiyo kisha alimpatia Faudhiaย 

    Kilichomshtua Faudhia ni huyo Mtu aliyeleta maiti ya Martinย  Gimbo, hakuamini macho yake hadi presha ilimpanda, Mohdย  akamuulizaย 

    “Unamfahamu huyo Mtu?” Aliuliza Mohd, Faudhia alimtazama Mohdย  kisha alisemaย 

    “Ndio namfahamu huyu Mtu, ni miaka mingi sana imepita sasa.ย  Siamini kama baada ya makosa yale aliachiwa mapema hivyo”ย  Alisema Faudhia, huku akirejea kuiangalia tena picha hiyo,ย  alionekana Mzee Shomari ambaye alikuwa ni Baba wa kambo waย  Faudhia akiwa amepiga picha na Mama yake Martinย 

    “Huyu Mtu alikuja tena hapa?” Aliulizaย 

    “Sikupata kumuona tena, hakuna aliyekuja hata kunipa pole,ย  nilibakia Mimi na Dada yake Martin ambaye naye alifariki naย  kuniachia huyu Mjukuu” Alisema Mama yake Martin Gimbo.ย 

    “Mama una hakika kuwa huyu Mtu alikuja na Maiti hapa?”ย 

    “Ndio” alijibu Huyo Mama huku akianza kutetemeka kutokana naย  maradhi yaliyokuwa yakimsibu.ย 

    “Faudhia, unahisia gani?” Alihoji Mohdย 

    “Kwa jinsi nilivyoishi na Mzee Shomari, simulizi nilizosikiaย  kuhusu yeye na matukio aliyoyafanya, napata mashaka kuwaย  huwenda yeye ndiye aliyemtengeza Chogo kuwa gaidi, sinaย  uhakika na ninachokihisi lakini hisia zangu zinaweza kunipaย  majibu kutokana na picha hii, mwaka ambao Martin amefariki niย  miezi michache baaada ya Mzee Shomari kufungwa kwa kosa laย 

    Mauwaji huko Mbeya, najiuliza aliweza vipi kutoka? Kwaย  vyovyote yupo mfadhili katika haya yote, hayupo peke yake”ย  Alisema Faudhia.ย 

    โ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขย 

    Jioni ilikuwa imeshangia, Chogo alikuwa ndani ya Benki hiyo,ย  aliagiza Diana aende ndani ya Benki kuu. Muda huu alikuwaย  ndani ya chumba cha kuhifadhia pesa, chumba hicho kilikuwa naย  mateka wawili, Gavana na Mke wake ambao walikuwa wamefungwaย  kamba kwenye mikono yao.ย 

    Chogo alikuwa akiweka risasi kwenye Bastola yake, Mwanaumeย  huyo alikuwa mweusi mwenye kipara, Gavana alimuuliza Chogoย 

    “Mnataka nini?” Chogo hakujibu swali la Gavanaย 

    “Nakuuliza wewe, kwanini mmetuteka mnataka pesa?” Aliulizaย  tena Gavana wa Benki kuuย 

    Chogo alikasirika kisha alimfuata Gavana kwa hasira akamshikaย  shingoniย 

    “Hata ukijuwa sababu huwezi kulipa kwa chochote, thamani yaย  nilichokipoteza haiwezi kufananishwa na pesa yenu chafuย  iliyojaa damu” Alisema Chogo kisha alimuachia Gavana ambayeย  alianza kukohoaย 

    “Ukirudia tena kuuliza maswali ya kipuuzi nitakata shingoย  yako” Chogo alisema kisha alinyanyuka na kurudi alipokuwaย  amekaa, kisha alipomaliza kuweka risasi kwenye Bastolaย  aliondoka chumbani hapo, Gavana alimsogelea Mke wake ambayeย  alikuwa akilia tu huku akisemaย 

    “Naogopa sana sijui hatma itakuwaje, sijui kesho itakuwaย  vipi!” Alisema maneno yaliyomfanya Gavana asemeย 

    “Sesilia huna sababu ya kulia maana hata kama ukifanya hivyoย  huwezi kubadilisha chochote kile, cha msingi ni kuangaliaย  tunafanya kitu gani” alisema Gavanaย 

    “Tutafanya nini mbele ya hawa Watu walioizidi akili Serikali?ย  Sisi wawili hatujapitia hata mafunzo ya ujeshi hata mgamboย  tutafanya nini mbele yao?” Alisema Mke wa Gavanaย  aliyejulikana kama Sesilia, Gavana alijisogeza kwa Mke wakeย  akamwambiaย 

    “Unaiona ile meza ndogo?” Alisema Gavana huku akimuonesha Mkeย  wake

    “Ndio naiona” alijibu Mke wa Gavanaย 

    “Nyuma yake kuna Chemba ndogo ambayo kama ukiifikia naย  kubonyeza basi chumba hiki kitazungukwa na ngao ya Umeme,ย  hawataweza kuingia humu tena kisha hapo hapo kuna swichiย  ambayo ukiibonyeza inazibua ukuta sababu pale kuna mlango waย  siri sana” Alisema Gavana kisha Mke wake alimtazama Mume wakeย  sehemu ya Mguu na kuona jinsi damu ilivyokuwa ikimmwagikaย  Gavana.ย 

    “Mguu wangu una maumivu makali sana, unapaswa kufanya hivyoย  Sesilia vinginevyo tutafia humu” Alisema Gavana lakiniย  alitambuwa kuwa Mke wake alikuwa mwenye woga sana, alikuwaย  akitetemeka na kulia, kabla hawajazungumza chochote aliingiaย  Mlinzi kwa ajili ya kuwaangalia Gavana na Mke wake, maongeziย  yalikoma hapo baada ya kumuona Mlinzi.ย 

    Upande wa pili, ndani ya Ghorofa la China plaza maeneo yaย  Karume, floo ya mwisho kabisa, alionekana Mzee mmoja mwenyeย  mvi nyeupe na kitambi, Mzee huyo alikuwa akizungumza na simuย 

    “Hakikisha taarifa inatoka sasa hivi” Alisistiza Mzee huyoย  kisha alikata simu, alipogeuka nyuma yake alikuwepo Dianaย  rafiki wa Faudhia, Mzee huyo alikuwa ni Mzee Shomari. Dianaย  alionekana kutaka kusema jambo, Mzee Shomari alimkaribishaย  akae kwanza kisha alimpatia kinywajiย 

    “Vipi mpango umeenda sawa?” Aliuliza Mzee Shomariย 

    “Faudhia amekwepa mtego wa kifo, yupo Arusha anamfuatiliaย  Martin Gimbo” alisema Dianaย 

    “Shit!!” Alisema Mzee Shomariย 

    “Wameenda hadi shule aliyosoma Martin lakini Mkuu wa Shuleย  alifanya kama tulivyomwambia lakini walimuuwa” Alielezea tenaย  Dianaย 

    “Hakikisha Utambulisho wa Chogo haufahamiki, tuma Watuย  wamuuwe Mama yake Chogo, endapo Chogo atafahamu kuwaย  tumemdanganya basi ngoma itakuwa ngumu sana, ni lazimaย  tufanikishe mpango ulio mbele yetu haraka sana” Alisema Mzeeย  Shomari, haraka Diana alinyanyua simu na kumpigia Mtuย 

    “Uwa panya bila kelele” Alisema Diana, Mzee Shomari akiwaย  amekaa kwenye kiti cha walemavu alitabasamu sana kishaย  alisema

    “Nakuaminia sana Mtoto wangu, hakika wewe ni simba jikeย  unayewinda kimya kimya” Alisema Mzee Shomariย 

    “Siku zote nimeishi na kisasi ndani ya moyo wangu, kifo chaย  Mama yangu ni lazima Faudhia akilipie, nafanya yoteย  kuhakikisha Mama yangu anafurahi huko alipo” Alisema Dianaย 

    “Na siku zote Muuwaji hawezi kuishi, ndiyo maana nilikutoaย  gerezani ili uje kuitafuta haki iliyoporwa na Faudhia”ย  Alikazia Mzee Shomari kisha alimruhusu Diana kuelekea ndaniย  ya Benki, mpango wa Mzee Shomari ulikuwa ni Kumuuwa Faudhia,ย  kisha kuiba pesa za kimarekani ambazo zilihifadhiwa ndani yaย  Benki hiyo katika chemba ya siri, ilikuwa ni zaidi ya Dolaย  Bilioni 900 , alimtumia Chogo kama ngao ya kufanya mambo yakeย  huku akiweka ubia na rafiki yake wa zamani ambaye alikuwaย  akiishi Uholanzi, ndiye aliyemtoa jela na kumfadhili pesa zaย  kufanya ugaidi Tanzania, hivyo Mzee Shomari alikuwa ndiyeย  Gaidi aliyekuwa akiratibu mipango yote, alikusanya vijana naย  kuwapatia silaha nzito, akiwemo Diana na Martin Gimbo maarufuย  kama Chogoย 

    Jinsi alivyowapata Diana na Chogo utakuja kufahamu mbele,ย  hebu tosonge..ย 

    Usiku ulikuwa umeingia, ndani ya Jiji la Arusha, Faudhiaย  alikuwa akimlaumu Mohd kwa kosa la Kumuuwa Mama yake naย  Martin Gimbo.

    Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA NNE

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย 

    riwaya mpya riwaya za kijasusi

    17 Comments

    1. Kรฎรฑgzjรฉรจlรฃy on May 30, 2025 10:10 pm

      Ya 5๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ

      Reply
    2. Samwel mkangi on May 30, 2025 11:01 pm

      Nouuuuumaaaa

      Reply
    3. Chid boy on May 30, 2025 11:45 pm

      Duuuh kwa hyo mohd nae ni mmoja wa magaidi au next plz

      Reply
    4. James Gebhard on May 31, 2025 5:42 am

      aaaaaah! muongeze kdg hii ni ๐ŸŒค๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    5. yasini Tawakali on May 31, 2025 6:34 am

      Mbona fupi ila ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    6. Leynecy Omary on May 31, 2025 1:02 pm

      ๐‘ฑ๐’๐’Ž๐’๐’๐’Š ๐’š๐’‚ 5 ๐’Š๐’”๐’Š๐’„๐’‰๐’†๐’๐’†๐’˜๐’†,,,,๐’Š๐’˜๐’† ๐’๐’…๐’†๐’‡๐’– ๐’๐’…๐’†๐’‡๐’–

      Reply
    7. Alison3943 on May 31, 2025 6:04 pm

      https://shorturl.fm/eAlmd

      Reply
    8. Toby594 on June 1, 2025 1:22 am

      https://shorturl.fm/MVjF1

      Reply
    9. Celeste1133 on June 1, 2025 3:11 am

      https://shorturl.fm/PFOiP

      Reply
    10. Lynn160 on June 1, 2025 5:08 am

      https://shorturl.fm/PFOiP

      Reply
    11. Edgar83 on June 1, 2025 11:59 am

      https://shorturl.fm/DA3HU

      Reply
    12. VERONICA on June 1, 2025 2:46 pm

      Iko fire sana

      Reply
    13. Cathbert on June 1, 2025 6:08 pm

      Good

      Reply
    14. Everett208 on June 1, 2025 8:29 pm

      https://shorturl.fm/YZRz9

      Reply
    15. Leia4366 on June 2, 2025 9:02 am

      https://shorturl.fm/PFOiP

      Reply
    16. Andy1014 on June 2, 2025 10:47 am

      https://shorturl.fm/I3T8M

      Reply
    17. Kennedy491 on June 2, 2025 2:02 pm

      https://shorturl.fm/uyMvT

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 1, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nne “Na siku zote Muuwaji hawezi kuishi, ndiyo maana…

    Ratiba Kamili Ya FIFA CLUB WORLD CUP 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nne-04)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tatu-03)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.