Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Kumi
“Veronica najua unanisikia, usifanye jaribio la kuondoka tafadhari” Aliongea Joji akiwa anapanda atokee kwenye lile dirisha, nikasema liwalo na liwe pembeni kulikuwa na kipande cha mti uliokauka niliuchukua na kukaa makini nikitazama pale ambapo angetokea, Honi ilipigwa zaidi ya mara saba hatimaye ukimya ulitawala.
Joji alipotokeza kichwa chake nilimpiga na kile kipande cha Mti, nilimpiga tena na tena akiwa hawezi hata kurudi nyuma, nilihakikisha nampiga hadi azimie na ndicho kilichotokea nilimpiga hadi nikamuaribu ile sura yake, damu zikawa zinamtoka kama bomba la maji lililo pasuka, kwakuwa ilikuwa ni nyuma ya nyumba hakukuwa na shida yoyote, nilimuacha akiwa juu ananing’inia. Endelea
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Nilipochungulia niliona geti likisukumwa, Anko Sanga ndiye aliyekuwa akisukuma lile geti, nilimtazama kwa makini sana, kuruka ukuta ilikuwa ni shida nyingine ambayo kwa vyovyote nisingeiweza kwasababu alikuwa ameweka wavu maalumu wenye ulinzi wa umeme, Nilimuona sasa akielekea ndani haraka baada ya kuona Joji hayupo pale kwenye kibanda chake. Nilikaa makini kusikiliza milio ya funguo hadi alipomaliza na kufungua geti, kisha akafungua mlango.
Bahati nzuri kwangu alikuwa ameacha geti wazi, nilikimbia kuelekea getini nikafanikiwa kutoka nje kabisa lakini ilikuwa msituni sana na barabara ilikuwa ya vumbi tena isiyopitisha magari, mvua zilizokuwa zikinyesha zilisababisha madimbwi ya maji, nilianza kukimbia kuifuata ile barabara nikakumbuka kuwa Joji alisema hadi kufika Kwenye makazi ya Watu ingenichukua Kilomita 90 au zaidi.
Nikiwa naendelea kukimbia huku maumivu ya mguu yakiwa juu, nilisikia gari ya Anko Sanga ikija kwa nyuma, ilinibidi niongeze mwendo, nilipofika mbele nilijificha, gari ikapita, nikaona sio salama tena kuendelea kutumia ile barabara nikazama msituni na kuanza kukata nyika.
Nilikimbia na kutembea huku njaa ikianza kunishika, nilikunywa maji yaliyotuama ili niendelee na safari, nilikatiza milima na mabonde kwa tabu sana hadi giza lilipo ingia, nilikuwa naona mwanga wa gari na nilisikia mlio, nilijua tu Anko Sanga alikuwa akiendelea kunitafuta baada ya kugundua kuwa nilikuwa nimetoroka.
Nilitembea usiku kucha ili tu nifike kwenye makazi ya Watu niweze kupata msaada, mwendo ulikuwa mrefu hadi kulipo pambazuka nilijikuta nikiwa juu ya kilele kidogo cha Mlima, niliona jinsi gari ya Anko Sanga ilivyokuwa ikipiga misele yake ya kunitafuta Usiku na Mchana.
Nilisubiria jua litoke ili nipate nguvu kidogo ya kutembea, ule mguu ulio na maumivu ulikuwa ukiendelea kunipa shida sana. Kwa mbali niliona Moshi ukifuka nikajua tu ni lazima kutakuwa na makazi ya Watu, nguvu ikanijia hata kabla jua halijatoka nikawa na nguvu ya kusonga mbele. Kila nilipoitazama picha ya Mtoto wangu nilijikuta napata nguvu ya kwenda mbele.
Nilitembea hadi jua lilipoanza kuwa kali nilikutana na barabara kubwa, ikiwa na mchepuo mdogo ambayo ndio barabara iliyoenda kwenye nyumba ya Anko Sanga, mbele kabisa niliona kibao kikiwa kimeandikwa UNAKARIBIA MPAKA WA KENYA, upande mwingine ulikuwa ukisema UNAKARIBIA MPAKA WA TANZANIA, hivyo
nilikuwa pale katikati, nikaongoza upande wa Tanzania nikiwa ninakimbia. Nilikimbia kwa spidi sana licha ya kuendelea kusikia maumivu ya Mguu hadi nilipokaribia kwenye uzio wenye Askari, nilipogeuka nyuma nililiona gari la Anko Sanga likija, niliongeza mwendo hadi nilipofika walipo Askari.
Wale Askari waliniweka chini ya Ulinzi wakinitaka nitoe maelezo wakati huo Anko Sanga alikuwa ameshafika pale, nilijielezea kidogo nikataja namba za kitambulisho changu cha Taifa, wakakagua na kuthibitisha kuwa ni Mtanzania, Wakati wote huu Anko Sanga alikuwa kwenye gari lake akinifwatilia kwa makini, kila nilipogeuka nilikutana nae.
Wakamuuliza Anko Sanga alikuwa akielekea wapi akawaambia kuwa anaenda mjini, nami nilishawaambia naenda mjini wakamwambia anipe lifti ya kuelekea Mjini, hakukuwa na gari nyingine zaidi ya ile ya Anko Sanga, wale Askari wakanitaka nifanye haraka niingie kwenye gari, sikuwa na jinsi bali kuelekea kwenye lile gari. Nilijua nilikuwa nikiingia tena kwenye mikono ya Mtu katili,
Sikutaka kusema kuwa alikuwa mbaya mbele ya wale polisi nikihofia zaidi mambo yangekuwa mengi pale, nilichotaka ni kumpata binti yangu tu.
Nilipoingia kwenye gari niliketi siti ya nyuma ya gari yake, nilipomtazama nilimuona alitoa tabasamu la Furaha kuonesha kuwa ilikuwa ni ngumu kuruka mitego yake, ikabidi aanze kuliondoa lile gari, kabla hata hajaondoka wale Askari walimsimamisha.
Kulikuwa na Watu wengine wawili waliotakiwa kupewa Lifti akiwemo Polisi mmoja na Mama mmoja ambaye alikuwa akiuza Chakula pale Mpakani, yule polisi alienda kukaa mbele wakati mimi na Yule Mama tulikaa nyuma, nilimuuliza alikuwa akishuka wapi akaniambia Mjini kabisa nikaona hawezi kuwa msaada hivyo nikasubiria atakaposhuka yule polisi ndio nami nishuke.
Anko Sanga alinitazama kwa sura ya hasira, yule Mama alikuwa akiniuliza maswali kadhaa maana nilikuwa kama nimedhohofu hivi, akanipatia chakula huku safari ikiwa inaendelea. Tulienda kwa mwendo mrefu hadi jioni ilipoingia, Yule polisi alishuka kilomita kadhaa kabla ya kufika Mjini, nilikuwa nikiyafahamu yale mazingira nami nilishuka.
“Nilijua unashuka Mjini?” aliniuliza yule Polisi “Hapana natakiwa nishuke hapa mara moja ili nionane na Mtu
“Haya ndugu una abiria mmoja tu mfikishe salama” aliongea Polisi kisha Anko Sanga aliondoa lile gari, nilijua hawezi kumfikisha yule Mama Mjini ni lazima tu atanirudia hivyo nilikatiza haraka na kuvuka barabara kisha niliingia mtaani, nilitembea kwa haraka kulekea mjini lakini kwa kutumia Njia za mtaani, usiku ulipoingia nami nilikuwa naingia Mjini Arusha ambako nilikuwa nikiishi na Mama yangu siku za nyuma.
Ilipata kama saa 4 kasoro, nilipata wazo la kwenda kule tulikokuwa tunakaa zamani, nilimkumbuka yule jirani aliyenipa tahadhari kuhusu Mama yangu Mzazi, niligonga mlango nikiwa nimechoka sana, alinifungulia kisha alifunga mlango
“Veronica umepatwa na nini?” aliniuliza, nikamwambia ni stori ndefu ningependa nipumzike, nilimtoa hofu sababu nilikuwa nimekonda sana niko hovyo hovyo kama tahira fulani hivi.
Aliniacha nipimzike ili nikitulia ndipo nimpe hadithi ya kilichonikuta, majira ya saa 5 usiku Anko Sanga alikuja pale kwa jirani, akaniuliza kama nilikuwa nimefika pale, sasa yule jirani kwa jinsi alivyoyasoma yale mazingira akajua tu huenda kuna shida akamwambia Anko Sanga kuwa hajaniona kwa zaidi ya miaka miwili, tena akawa anahoji kuna nini kimetokea? ikamfanya Anko Sanga aamini kuwa sikuwepo pale, wakati huo nilikuwa nimelala.
Jirani hakulala hadi kulipo pambazuka, nilipoamka ndipo akaniambia kuwa Anko Sanga alikuwa akiniulizia, nilimsimulia jinsi ilivyokuwa, kuanzia mwanzo hadi mwisho alisikitika sana,
“Lakini nilikwambia Veronica kuwa Mama yako na Kaka yake wanaskendo ya ushirikina, wamevuma sana hadi Mama yako akahama hapa”
“Imeshatokea Jirani, namuwaza Mtoto wangu na Mume wangu sijui wako wapi, sijui Mama anaishi wapi”
“Kwasasa Veronica unatakiwa utulize akili kwanza, ukitumia haraka unaweza ukajikuta umepoteza kila kitu kwenye Maisha yako, cha msingi uko hai hilo ndio jambo muhimu kuliko yote, kwanza jiimarishe kiafya, unaonekana una Umwa kabisa”
“Nashukuru kwa kunijali Jirani, kila nikikumbuka jinsi nilivyopona kutoka kifo najikuta nalia tuu” Nilisema
“Nakushauri kwa sasa rudi Dar kwanza kisha Afya yako ikikaa vizuri ndio urudi hapa Arusha, kule ni salama zaidi lakini hapa watakuwa wanakutafuta, hili jambo linahitaji ushahidi hata kama utaenda polisi, je unao? Nilitafakari alichokisema niliona kina busara ndani yake nilimuomba anipe nauli ili niweze kuondoka Arusha.
Alinipatia nauli kisha niliondoka siku iliyofuata Alfajiri, nilipofika Dar nilienda hadi tulikokuwa tunaishi, nyumba ilikuwa imekaa bila Mtu kwa miaka miwili, ilikuwa ya hovyo tuu. Nilimtafuta Mama Sofia, aliponiona alinishangaa sana.
“Umepatwa na nini Veronica?” ilinibidi nimsimulie kila kitu, alinipa pole kwa kila kilichotokea. Alimtafuta fundi akavunja mlango na kuutengeneza kisha alimtafuta Mtu wa usafi akasafisha nyumba.
“Asante Mama Sofia”
“Usijali Veronica, kilichobakia na Afya yako, Mara ya mwisho Jonas aliniambia anaenda Arusha kumchukua Mtoto ndio hajarudi tena”
“Ndio hivyo Mama Sofia” Mama Huyu alihakikisha naenda hospitali kupimwa maradhi yote, nilikutwa na virusi vya Ukimwi, nililia sana.
“Usilie Sofia ndio Maisha, cha msingi unatakiwa kuimarisha Afya yako kwanza” alinitia moyo mno maana nilikuwa katika dimbwi la mawazo, kukutwa na virusi vya Ukimwi kuliniumiza na nilijua ni Anko Sanga ndiye aliyenipa Ugonjwa.
“Sijui kama Mtoto wangu Moyo atakuwa mzima Mama Sofia, ameniharibia Maisha yangu. Mama yangu nimemkosea nini Mimi?” nililia kwa uchungu lakini sikuwa na cha kufanya zaidi ya kupokea matibabu ya magonjwa mengine, nilianza dozi ya ARV
Nilirudi nyumbani, nikawa nakula vizuri nafanya mazoezi kila siku hadi hali yangu ilipoanza kutengemaa.
Wema wa Mama Sofia utabaki kwenye kumbukumbu za Maisha yangu, alihakikisha Maisha yangu yanarudi, alinitia moyo nilipoonekana kukata tamaa, alinifanya nijihisi sina tatizo lolote
“Veronica, sasa unaweza kwenda kutafuta haki yako ilipo. Afya yako sasa iko sawa” Alisema Mama Sofia baada ya miezi mitatu ya kuishi Dar, ni kweli hata nilipojitazama niliona nimeimarika kiakili na Kiafya
“Asante Mama Sofia, sijui bila wewe ingekuwaje kwa haya yote niliyoyapitia. Nakushukuru sana kwa ukarimu na wema wako! Mungu akujaze tumaini” Nilimwambia
“Mpaka sasa nashangaa ni kwanini Mama yako ameamua kuwa hivyo alivyo, nenda kamchukue Mtoto wako na Mume wako Jonas, mrudi kuishi Maisha yenu. Naamini umejifunza katika haya uliyoyapitia”
“Nitajaribu kuhakikisha Mama yangu haingii matatizoni, pamoja na yote alinitendea bado atabaki kuwa Mama pekee kwangu!”
“Uungwana ni kulipa mabaya kwa mazuri Veronica, usishawishike wala usijaribu kuupoteza utu wako. Dunia tunapita tu Mungu ndio mlipaji wa kila jambo” Maneno ya Mama Sofia yalichangia kwa kiasi kikubwa nijione kama nimezaliwa upya, tulienda benki akanipatia pesa kwa ajili ya safari ya kurudi Arusha Kumtafuta binti yangu Moyo
Nilisafiri kurudi Arusha siku iliyofuata, niliwasiliana na yule jirani yetu tukakutana hotelini ili anisaidie zoezi la kumpata Mtoto wangu Moyo.
“Eeh Veronica umebadirika, umerudi kuwa Veronica yule wa miaka mingi, ninayemfahamu mimi” Alisema baada ya kuniona
“Ha!ha! Jirani unajua kila jambo lina wakati wake, kama nilivyo kwambia nahitaji unisaidie kufahamu anapoishi Mama maana ndiye mwenye Mtoto wangu”
“Anhaa! sasa itabidi tumpate aliyenunua nyumba yenu atupatie mawasiliano ya Mama yako!”
“Kabla ya yote nahitaji kwanza kwenda kanisani, nguvu ya Mungu ni kubwa kuliko nguvu wanazozitumia” Tuliongozana hadi kanisani, Baba Mchungaji alishangaa kuniona
“Eeeh! Veronica za miaka mingi?”
“Salama Baba Mchungaji”
“Mama yako nae hajaonekana kwa zaidi ya miezi mitano sasa, lakini tunashukuru kwa nguvu ya Yesu iliyomo ndani yake amesaidia ujenzi wa kabisa hili na baadhi ya miundo mbinu” Alisema, sikutaka kumharibia Mama mbele ya Watu wa Mungu
“Anhaa!! yupo na safari zake za kibiashara”
“Basi Mungu aendelee kumtia nguvu popote alipo” “Amina Baba Mchungaji”
Tulizungumza tukiwa tunatembea tembea kwenye viunga vya kanisa, nikamwambia nahitaji maombi yenye nguvu
“Kwanini Veronica?”
“Naona kama napoteza imani iliyo ndani yangu Baba Mchungaji” “Oooh! sawa hilo halina shida, vipi ndoa yako?”
“Namshukuru Mungu Baba Mchungaji” Siku hiyo aliniombea akanipa na mafuta ya baraka, nilihitaji sana nguvu ya Mungu katika kufanikisha jambo lililo mbele yetu, baada ya maombi tulirudi hotelini.
“Sasa niko tayari Jirani”
“Haya Veronica”
Siku iliyofuata tulienda kwenye nyumba tuliyokuwa tukiishi zamani, tulikutana na aliyeinunua akatupatia namba ya Mama yangu Mzazi, nikajaribu kupiga, akapokea lakini niliposikia sauti ya Mama yangu nilishindwa kujizuia nilijikuta nikilia kwa uchungu sana.
Jirani alinisaidia kuongea nae, akajifanya ni mfanya biashara, Mama akampatia anuani ya alipo tukafanikiwa kujua anapoishi. Tukamtafuta Mtu mwingine ambaye alijifanya ni Mfanyabiashara maana Mama alikuwa akimfahamu jirani huyo, yule Mtu akaenda kule kwa lengo la kuangalia vitu viwili, kwanza uwepo wa Jonas na Mtoto.
Nilimpatia pesa kisha akaenda zake, alipofika pale alimuona Jonas lakini akiwa kwenye kiti cha walemavu na jinsi alivyoelezea alikuwa kama amepooza viungo vyake, alimuona pia Mtoto mdogo ambaye ni Moyo.
“Asante kwa msaada wako” Nilimpatia ujira wake kwa kazi aliyoifanya kisha tukapanga jinsi ya kuingia na kuwakomboa wale wote, Jirani alinishauri twende polisi lakini sikutaka kumtia matatizoni Mama yangu
“Tukienda huko Mama yangu atapotea, ninachotaka ni kuichukua familia yangu tuu” Kutokana na ramani tuliyopewa tulifika hadi pale Mchana, tukamkuta msichana wa kazi tu.
Hakunipa presha hata kidogo, nilimchukua binti yangu, Jirani akanisaidia kumkokota Jonas, tukaingia kwenye gari tukaelekea Hotelini. Ilikuwa ni siku yenye faraja kwangu lakini Jonas alikuwa kama zuzu tu, yaani hajielewi wala hajitambui, alikuwa akivuja udenda.
Nilimkumbatia Moyo wangu, aliyekuwa akilia, hata jirani nae alikuwa akilia, Kilio cha Moyo kilinishangaza sana
“Mbona kama Mtoto anaumia Veronica?” aliniuliza jirani, kwa jinsi ambavyo Moyo alikuwa akilia alikuwa kama vile anaumizwa na jambo fulani ndani ya mwili wake.
Ikabidi nimtoe nguo zote, Masikini ya Mungu Moyo alikuwa na vidonda kwenye Papa yake, alikuwa kama amekatwa hivi, nilitoa bandeji ili niangalie nilijikuta moyo wangu ukiuma hadi mchozi ulinitoka, alikuwa amekatwa mashavu ya Papa yake yote mawili
“Masikini ya Mungu! hivi Mama yako ni Binadamu kweli?” aliniuliza yule jirani nikiwa namtazama binti yangu, ikabidi niende Hospitali nilimuacha Jirani akiwa anamuangalia Jonas, nilipata wazo la kumpima Ukimwi Mwanangu!
“Amepatwa na nini huyu?” aliuliza Daktari baada ya kumuona “Nilisafiri nilimuacha na dada wa kazi sijui hata amekuwaje” “Itabidi kwanza uende polisi ndipo atibiwe”
“Daktari, naomba atibiwe tu kwasababu kwenda huko kote kutachukua muda mrefu wakati Mtoto wangu anateseka tu”
“Ok! nitakusaidia sababu ni Mtoto”
“Naomba pia apimwe Ukimwi”
“sawa!”
Nilikaa kusubiria majibu ya Moyo, Mtoto alikutwa na maambukizi ya Ukimwi, alianza dozi akiwa mdogo kabisa jambo hili liliniumiza sana sikuweza kuvumilia nilijikuta nikitokwa na machozi, Moyo alitibiwa tukarudi Hotelini, kwa mara ya kwanza nililala na binti yangu na mume wangu usiku tukiwa na amani, japo wao walikuwa na maumivu lakini kuwa hai ilinipa moyo sana.
Nilimwambia jirani arudi tu nyumbani, asubuhi aje anisindikize Uwanja wa ndege ili niondoke na familia yangu.
“Ubaki salama Veronica” Aliondoka zake, Tulilala pale nikiwa nimewakumbatia bila kujali kuwa Jonas alikuwa zuzu kama tahira hawezi kuongea wala kujua chochote kile.
Usiku Majira ya saa 7, nilianza kuota ndoto mbaya sana, niliota Mama na Anko Sanga wamekuja pale Hotelini wakiwa katika mazingira ya kichawi, wakawa wanalazimisha kumchukua Jonas, nilijitabidi sana kumng’ang’ania ili wasimchukue, nilipiga na maombi ya nguvu nikiwa ndotoni, niliposhtuka nilimkuta Jonas akiwa anatetemeka sana.
Nilijitahidi kumuita Jonas, alikuwa ametoa macho yake, povu lilianza kumtoka nikamsikia akiniita jina langu, nilipoitika ndio ikawa mazima. Jonas akatulia kabisaa nilipomuangalia vizuri niligundua alikuwa akipoteza joto la Mwili wake.
Nilichukua simu yangu na kumpigia Mama usiku ule ule, baada ya kupokea aliniuliza mimi ni nani
“Mimi ni Veronica, binti uliyemzaa na kumlea kwa shida, binti uliyemtesa na kumnyima uhuru, binti uliyemsababishia maumivu ndani ya Moyo wake! nipo Arusha kwa ajili ya Binti yangu, nipo na Moyo lakini Jonas Umeshamchukua tena kutoka kwangu! Naomba MAMA NIACHIE MUME WANGU” yalikuwa ni maneno mazito niliyoyaongea nikiwa ninalia kwa uchungu sana
Hakujibu kitu alikata simu, nilimtazama Moyo nilimuona akiwa amelala, nilipigia simu jirani aje Hotelini, baada ya kumaliza kuongea nae nilitoka usiku ule ule. Sikuwa na woga wa aina yoyote ile nilienda hadi nyumbani kwa Mama yangu, bahati nzuri wakati nafika ndio geti lilikuwa lilifunguliwa, niliingia mazima.
“Veronica!” Mama aliita baada ya kuniona
“Kimekuleta nini hapa?” aliongea tena akiwa anafungua furushi alilolishika mkononi, nilimfuata nikamsukuma lile furushi likaangukia pembeni, nilimkamata na kuanza kumgongesha kwenye kioo cha gari, nilimgongesha kichwa chake hadi damu zilipoanza kumtoka.
Msichana wake wa kazi akaanza kupiga kelele akiomba msaada ndipo alipokuja mlinzi akiwa amebeba begi kutokea ndani, alipomulika tochi alimkuta Mama akiwa amechanika sehemu ya kichwa chake, dimbwi la damu likiwa limejaa chini alipoangukia
Akanifuata na kunikamata, kisha wakapiga simu polisi, Muda ule ule polisi walifika na kumichukua.
Tukio lile lilizua tahamaki kubwa sana, waliotufahamu walisema Mtoto amemuuwa Mama yake, ikawa ndio stori kubwa, kesi ikawa na mlolongo mzito, walinitesa nikamtaja Anko Sanga, walimtafuta na kumkamata.
Kesi iligubikwa na mambo ya kushangaza sana ambayo yalifanya kesi ihamishiwe Mahakama ya Kisutu Jiji Dar, Mama Sofia alipokuja kuniona nilimwambia amlee Mtoto wangu, aliwasiliana na yule jirani akamchukua Sofia, mwili wa Jonas ulizikwa Arusha.
Nilikuwa namalizia kuwasimulia wale Mawakili wa ile kesi, wote walikuwa wakitokwa na machozi!
Nilirudishwa tena Mahakamani, Mawakili wakaelezea tukio zima lilivyo, Wakati huo Anko Sanga alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali hasa Ukimwi alikuwa Hospitali.
Hakimu aliamuru nifungwe kifungo cha miaka 10 jela huku ikitajwa kuwa nimeua bila kukusudia, lakini ripoti ya Afya yangu ilifanya kifungo kipungue hadi miaka 5.
Hii ilikuwa ndio Haki pekee niliyokuwa nikiisubiria kwenye ile kesi!
•••Mwisho•••••
INAFUATA YA KIJASUSI COMMENTS ZIKIFIKA 100 Naachia Kesho MAPEMA SANA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
28 Comments
Vero bye byee🥲
Oyyy uwiiiii mm ningeanza na huyo anko sanga aseeee sijui mm jmn ila hyo hadithi is too much kali knm yaan
Duh ama kwel dunia ina mengi ya ajabu kikubwa kumuomba mungu tu bas
Ahsante Saana Story Ni Tamu Saana Ila Daaah inatufundisha Mengi Saana Kwenye Maisha
Nmeipenda sanaaa hii story hakika mtunz unahitaj pongez🙌
Jaman Jonas😭😭😭😭
Asante
Duuuu ataliii
Asante Sana story Ina mengi ya kuj8funza
Story nzuri Asante sana
Daaah
Stori ilikuwa ya Moto Admin apewe maua yake
Oyyy uwiiiii mm ningeanza na huyo anko sanga aseeee sijui mm jmn ila hyo hadithi is too much kali knm yaan
Duuuuuuu
Super https://shorturl.fm/6539m
Ila mbona veronica ameteseka sana ata kisas chake kama ni kidogo
Pole Veronica kwa uliyopitia Mungu akutie wepesi mambo yako yaende sawa naww uwe sawa kabisa ,,,, admin hongera kwa kazi nzuri
Pole Veronica kwa uliyopitia Mungu akutie wepesi mambo yako yaende sawa naww uwe sawa kabisa ,,,, admin hongera kwa kazi nzuri
Cool partnership https://shorturl.fm/XIZGD
Very good https://shorturl.fm/TbTre
Very good https://shorturl.fm/bODKa
Cool partnership https://shorturl.fm/XIZGD
Duuh
Hatari sana
Cool partnership https://shorturl.fm/XIZGD
Top https://shorturl.fm/YvSxU
Awesome https://shorturl.fm/oYjg5
https://shorturl.fm/TbTre