Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 06
Nilikua nikihema, Wazazi wangu walikua wamesimama vile vile kama Watu wasiojitambua.Β Yule Bibi aliendelea kunisogelea huku mguu wake mmoja akiwa anauburuza. Ulikua kama unaΒ dosari ya ukilema hivi, nilikua kwenye butwaa ambayo ilihitaji Mtu anitingishe ndiyo nitokeΒ katika ile hali tata.Β
Fumba na kufumbua Macho yule Bibi Kizee alikua amejaa machoni pangu akinimulika naΒ macho yake makali, nilishtuka na kutoka katika ile hali ya Butwaa. Nilipohitaji kukimbiaΒ alinishika mkono na kunivuta kwake lakini alipigwa na shoti kali, niliona moto mkaliΒ uliomsukuma na kumtupa chini.Β Endelea
SEHEMU YA SABA
Alinitazama kwa Mshangao kisha aliniuliza kwa sauti yake kali.Β
βWewe ni Nani?β aliongea huku akitokwa na moshi mdomoni, bado mvua ilikua ikichapa.Β Niliuangalia mkono wangu, niliiuona ule ushanga, ndio ulionisaidia. Sasa kilichobakia kwanguΒ kilikua ni kuokoa Uhai wangu, nilirudi nyuma nyuma tayari kukimbia, yule Jini aliwaamrishaΒ Wazazi wangu wanifukuze.Β
Niliipa miguu yangu mamlaka ya kukimbia, lakini sikufikiria kwenda mbali isipokua kurudiΒ nyumbani mara moja, nilijigonga getini eneo la mguu lakini halikuninyima mwendo, nilijivutaΒ haraka na kukimbilia ndani kisha nilifunga mlango.Β Β
Nilifika ndani nikiwa nimechoka, nimelowa na pia nimetawaliwa na hofu. Haikua hali yaΒ kawaida niwakimbie Wazazi wangu niliowapenda, radi zilikua zikipasua anga halafu sauti yaΒ kucheka ya yule jini ilikua ikisambaa kila kona.Β
Nilisimama nikiwa nina bubujikwa na machozi, Wazazi wangu walikua kama mazombiΒ yasiyoelewa Mimi ni Nani kwao, sijui aliwafanyia nini hadi wakaanza kuniwinda kiasi hiki. BasiΒ nilikua nikiwaona Wazazi wangu kupitia kioo cha mlangoni jinsi walivyokua wamebadilika.
Macho yao yalikuwa hayana kiini cheusi, meupe kama karatasi, walikua wakitokwa na udenda. Niliumia ndani ya moyo wangu kuwaona Wazazi wangu katika hali ile ya ajabu, walikua naΒ nguvu za ajabu kiasi kwamba walikua wakivunja kioo waingie ndani.Β
Nilitamani sana kuwasihi Wazazi wangu wanitambue lakini niliona isingelikua rahisi,Β nikapandisha ngazi huku nikisikia namna walivyokua wakivunja kioo, nilikimbia kwa spidi sanaΒ hadi chumbani kwangu, nikawa naitafuta simu yangu ili niombe Msaada nje.Β
Sijui simu nilikua nimeiweka wapi, niliitafuta kila kona. Nilianza kusikia sauti ya kusukumwaΒ kwa mlango wangu kwa nguvu, walikua wameshafika mlangoni kwangu.Β
Nilikua natetemeka sana maana nafsi yangu ilikosa utetezi tena. Kwa bahati nzuri niliisikia simuΒ yangu ikiita. Sijui ni saa ngapi iliingia uvunguni mwa kitanda, niliinama, ilikua mbali kidogoΒ hivyo ni lazima nikivute kitanda kwanza, nilijivuta nikakisukuma kitanda nikaipata simu yangu.Β Β
Nilikua natetemeka sana, mwili ulikua ukichuruzika maji. Mapigo yangu ya moyo yalikuaΒ yakienda sambamba na pumzi zangu. Mate yalinikauka, kutoa nywira ya simu yangu ilinichukuaΒ dakika nyingi kutokana na wasiwasi uliokua umenivaa. Nilishindwa hata kuifungua simu yangu,Β mlango ulikua katika nyakati za mwisho kufunguka.Β
Nilidondosha simu yangu huku nikiwa nimeutolea macho mlango ukiwa unatikiswa haswa,Β nilihisi harufu ya kifo. Taratibu nilianza kurudi nyuma nikitamani nipate msaada usiotarajiwa.Β HamadβΌ! Mlango ulifunguka, Baba na Mama yangu walikua mbele yanguΒ Β
Walikua katika fahamu zisizo zao, walisimama wakinitazama. Niliona huo ni muda waΒ kuzungumza nao pengine ningeweza kuwashawishi wakarudi katika hali zao, chozi lilinitoka.Β Sikuwahi kuwaza wala kuota kua siku moja Baba na Mama yangu wangekuwa katika hali kamaΒ hiyo, hali ambayo wasingeliweza kunitambua Mimi binti yao wa pekee Celin.Β
βMamaβΌ BabaaβΌβ nilianza kwa sauti ya kilio cha maumivu sana, niliishiwa nguvu hata manenoΒ niliyohitaji kuyatoa yalikua mazito kutoka mdomoni mwangu. Nilikua na maumivu makali sanaΒ ndani yangu, udenda ulikua ukiwatoka Wazazi wangu.Β
βNi Mimi Celin, najua hamnitambui kama ambavyo ninyi hamjitambui Wazazi wangu. Mimi niΒ Binti yenu, hampaswi kunidhuruβ walikua wametulia kimya wakati naongea, nilihisi walikuaΒ wanaanza kunisikiliza.Β
βOna, furaha yenu ni Mimi hapa, furaha yangu ni ninyi hapo. Hayo siyo Maisha yenu, sijawahiΒ kuwaona mkiwa hivyo naomba wazazi wangu rudini katika halo zenu. Mna mengi ya kuyajuwaΒ kuhusu hii nyumbaβ Nilisema, hapa sasa ndipo nilipoiona dhamira ya yule jini kwangu,Β alichotaka ni kuhakikisha Wazazi wangu wananimaliza.Β
Walinifuata kwa spidi ya ajabu ili wanishambulie lakini kwa bahati nzuri niliweza kuwakwepaΒ nikajigonga ukutani, Mama alikua kama Mbogo kwa jinsi alivyokua akitoa sauti ya hasira kamaΒ Mnyama vile.
βMama ni Mimi Celinβ nilisema, angalau Baba yangu alikua hana hasira kama ambayo MamaΒ yangu alikua nayo, alinivamia tena kunishambulia. Alinijeruhi kwa kucha ndefu, kishaΒ nilimsukuma nikapata nafasi ya kuondoka pale chumbani, nikashusha ngazi haraka huku MamaΒ akiendelea kunikimbiza.Β
Nilifika hadi chini, nilipogeuka Mama yangu alinirukia mithiri ya Ndege tai, alinidondosha chiniΒ kama mzigo halafu akawa ananishambulia vibaya sana usoni kwa kucha, nilijitahidi sanaΒ kupambana naye ili niinuke, nilifanikiwa kumsukuma lakini alikua amenikwaruza usoni vyaΒ kutosha.Β Β
Nilisimama huku Mama akijiandaa tena kunishambulia, nilishaona kua kama sitakua ngangaliΒ basi Mama angeweza kunimaliza, maana alinishambulia usoni bila huruma halafu alinikwanguaΒ shingoni na kuniacha na maumivu makali sana. Nilipaswa kupambana naye bila kujali kuaΒ hayupo katika fahamu zake.Β
Alikua akiunguruma kama Simba mwenye njaa, nilikimbilia jikoni lakini kabla hata sijafungaΒ mlango aliusukuma kwa nguvu, alikua akinifuata taratibu baada ya kuingia jikoni, nilirudiΒ nyuma nyuma nikifikiria nifanye jambo gani. Mama alinisogelea bila haraka, alijuaΒ nisingeliweza kukimbilia popote tena. Nilifika mwisho wa jiko, nikakutakana na meza na ukutaΒ nyuma yangu.Β
Upande wa kushoto palikua na kisu, nilisogea taratibu huku nikiiambia nafsi yangu kuwaΒ nisipojiokoa sitaweza kupona, nilimpenda Mama yangu lakini aligeuka kua adui yangu. Nilipaswa kumshambulia kama alivyokua akinishambuliaΒ
Nilipapasa na kukishika kisu.Β
βMama, ni Mimi Celin, Mwanao hupaswi kunitendea hiviβ nilisema kwa mara ya mwisho, kamaΒ atanisikia na kuacha kunishambulia kwa maelekezo ya yule jini mbaya. Haikusaidia, MamaΒ alikuja tena mithiri ya ndege tai ili anishambulieΒ
Sikujiuliza mara mbili nilipaswa kufanya nini, nilimkita kisu Cha shingo Mama yangu. KilizamaΒ upande mmoja na kutokea upande mwingine. Mama aligugumia kwa mumivu mkali, ile hali yaΒ ushetani ilimtoka ghafla tu akawa Yule Mama niliyempenda kisha alidondoka chini akihema kwaΒ shida.Β
βMamaaβΌβ nilimwita kwa sauti iliyojaa mashaka, kisha nilikaa chini na kukipakata kichwaΒ chake. Mama alikua akitapatapa kwa maumivu, alikua hawezi kusema chochote kutokana na kileΒ kisu nilicho mchoma nacho.Β
Alianza kukosa hewa, nilikua ninalia na kumwomba msamaha Mama yangu. Baba alikuja jikoniΒ akiwa katika hali ya kujitambua kabisa, alikua ameloa nguo zake. Alipotuona alishangaa sanaΒ kisha alikuja haraka pale chini na kuniuliza kilichompata Mama.
Niliishia kulia nikimtazama Mama, Baba akaniambia tumpeleke Hospitali Mama akapateΒ huduma ya kwanza, sikuwa na chaguo isipokua kumsikiliza, sote tulikua tumechanganikiwa ilaΒ Baba alichanganikiwa zaidi maana alionekana kutojua chochote kilichotokea. Muda huo mvuaΒ ilikua imeacha kunyesha, palikua tulivu na wala hapakua na hali yoyote yenye kutia wasiwasi.Β
Baba alimbeba Mama hadi nje, bahati nzuri palikua na Taxi moja iliyokua ikipita.Β Tuliisimamisha kisha tulimpakiza Mama, tulianza safari ya kuelekea Hospitali. Tulipofika,Β Mama alipokelewa kama mgonjwa mahututi anayehitaji huduma haraka sana bila maelezoΒ yoyote yale, aliingizwa chumba cha Upasuaji mara moja.Β
Mimi na Baba tulikaa kwenye Benchi, uso wa Baba yangu uliniambia vingi, kimojaΒ kilichotawala zaidi ni swali la nini kilichotokea hadi Mama akawa katika hali ile, Mimi ndiyeΒ niliyepaswa kumpa majibu Baba lakini atanielewa?Β Β
βCelinβ Baba aliniita, alikua amevalia shati la Mistari myeupe na suruali nyeusi na kiatu cheusiΒ chini. Niligeuka kumtazama maana nilikua nimejiinamia nikilia, chochote kitakachotokea basiΒ Mimi ndiye niliyesababisha. Chozi lilikua linanivujaΒ
Baba alipepesa macho yake akanitazama mara moja kisha akaangalia chini na kuniuliza kwaΒ sauti ya taratibu sana.Β
βMama yako amefikwa na nini, kile kisu Nani amemchoma?β aliuliza Baba, nilibana midomoΒ yangu. Kila jibu nililo lifikiria kua lingekua jibu kwa Baba lingezua maswali zaidi, nilimtazamaΒ Baba ili kusoma sura yake alikua akifikiria nini.Β
Kisha nilimwambia Baba βSijui Baba, sijui nini kimetokea. Nimemkuta Mama katika hali ileβΒ Nililazimika kusema uwongo, Baba alishusha pumzi ndefu. Mtu mzima yeye, alihitaji ushawishiΒ zaidi kuamini nilikua sijui chochote kuhusu Mama.Β
βPolisi watakuja, tutawajibu hatujui?β aliniuliza. Nilizidi kudondosha chozi.Β
βBaba, niamini sijui chochote. Nilimkuta akiwa katika hali ile Mimiβ nikizidi kujitetea mbele yaΒ Baba. Chozi lilikua likinibubujika huku nafsi yangu ikinisuta. Chochote kitakachomkuta Mama,Β wa kulaumiwa ni Mimi hapa Celin.Β
Basi Baba aliniegemeza kwenye bega lake ili kunipa faraja, niliendelea kulia huku tukisubiriaΒ taarifa kutoka chumba cha Upasuaji. Tulikaa kwa zaidi ya masaa mawili, jua lilikua likikimbiaΒ kwa kasi kuelekea kuzama, jioni ilikua imeshaingia, taa ziliwashwa kuonesha kua giza lilikuaΒ linajiandaa kuingia.Β
Nilikua na uchovu wa kukimbizana huku na kule, mwili ulikua na maumivu pia nilikua naΒ majeraha kadhaa ya kucha za Mama. Baada ya dakika kumi kupita, Daktari mmoja alitokaΒ chumba cha Upasuaji, tulikua tunasubiria kwa muda mrefu, tuliposikia mlango ukifunguliwaΒ tulisimama mara moja na kutazama.
Tulipomwona Daktari tulisogea aliposimama akituangalia, alikua akitokwa na jasho, alivuaΒ Barakoa kisha akajishika kiuno. Sura yake ilikosa tumaini, nilijikuta nikilegea mwili mzima.Β Baba akamuulizaΒ
βHali ya mgonjwa inaendeleaje?β aliulza Baba kwa shahuku sana, yule Daktari akamtazamaΒ Baba, akashusha pumzi kidogo akasemaΒ
βTumejitahidi sanaβ kisha akatikisa kichwa halafu akaendeleaΒ
βJitihada zimezidi kudra, amefarikiβ sauti ya yule Dakati siwezi kuisahau, yaani ndani ya wikiΒ moja nilipoteza Watu watatu muhimu sana Maishani mwangu. Nilianza kumpoteza Zena, kishaΒ Caren, leo nampoteza Mama yangu Mzazi tena kwa mikono yangu Mimi mwenyewe, nilianguaΒ kilio cha Mtu mzima, nilihitaji nilie kwa uchungu tena kwa sauti kubwa kabisa.Β
Baba alinishikilia maana nilikua ninalia kwa kusaga meno, kilichoniliza zaidi ni kwambaΒ Mikono yangu ndiyo iliyoondoa Uhai wa Mama yangu, nilimuuwa mwenyewe katika hali yaΒ kujiokoa. Baba alitokwa na machozi huku akiwa ameufunga mdomo wake, aliitumia mikono yake kunibembeleza lakini haikusaidia.Β
Daktari akamwomesha Baba chumba kitupu ili tukakae huko kwa muda, Baba alinipeleka hukoΒ na kufunga mlango ili nilie hadi maumivu yaishe, palikua na viti viwili. Baba aliketi na kuniachaΒ sakafuni nilie hadi nimalize, nililia sana Mimi. Hakuna siku nililia sana kwenye Maisha yanguΒ kama siku hii, maneno ya yule Jini Bibi kizee yalitimia, nilitambaa hadi miguuni kwa BabaΒ nikamwambiaΒ
βNisamehe Babaβ nilisema nikiwa ninalia, japo nilikua ninalia lakini niliona maumivu hayaweziΒ kwisha kama sitasema ukweli mbele ya Baba yangu aliyekua hajui nini kilitokea, alikuaΒ akinitazama tu.Β Β
βNisamehe Mimi Baba , ni makosa yanguβ niliendelea kusema, Baba alishangaa inawezekanajeΒ yakawa ni makosa yangu. Aliniyanyua na kuniulizaΒ
βInawezekanaje ukasema ni makosa yako Celin?β nilifuta chozi, nilihitaji ujasiri sasa kumwelezaΒ ukweli Baba. Nilianza kusema βKifo cha Mama ni Makosa yangu, mikono yangu niliyoipendaΒ imeondoa uhai wa Mtu ninayempendaβ Baba alihamaki akaniuliza kwa sauti kavuΒ
βUnasemaje?βΒ
βBaba, sikukusudia. Nimemuuwa Mama kwa bahati mbaya Mimi, nisamehe Baba AaaahβΌβΒ niliendelea kulia, nilimweleza Baba ukweli lakini hakuonekana kuukubali kabisa. Alinilea naΒ kunifundisha tabia njema, akasemaΒ
βSikukuzaa Muuwaji Celin, sitaki kuyaamini maneno yakoβ alisema Baba kwa uchungu sanaΒ kisha alipiga hatua za haraka na kwenda kujiinamia ukutani. Nilisikia kilio cha chinichini chaΒ Baba na manungβuniko, nilielewa ni vita ya ndani kwa ndani ndiyo iliyokua ikiendelea kwake.
Nilijiuliza nimwambie nini Baba yangu aniamini, nilimfuata alipo, hali ilibadilika na mimi ndiyeΒ niliyekua namtuliza Baba baada ya Baba kunituliza MimiΒ
βBabaβΌβ nilimwita, alikua amejiinamia. Hakutaka nilione chozi lake kabisa. Nilimwita tenaΒ akaniambiaΒ
βCelin, wewe siyo Muuwaji Mwanangu tena huwezi kumuuwa Mama yako Mzazi. Sitaki kusikiaΒ hizo hadithi, niambie nini kimemkuta Mama yako?β alisema Baba akiwa ameuficha uso wakeΒ ukutani, macho yangu yalikua hayakauki chozi hata kidogo, niliendelea kububujisha choziΒ Β
βBaba, Mwanao nimepitia Mazingira magumu sana tena kwa siri msijue nyinyiβ nilisema, kilioΒ kilianza upya. Baba aligeuka kunitazama. Macho yake yalikua yamejawa na chozi, alihitajiΒ kusikia nilichotaka kukisema. Nilimtazama.Β
βChanzo cha yote ni ile nyumba Baba, ina majini na kaburi ambalo ndugu wawili wamezikwaΒ mle. Hakuna aliyeweza kuishi ndani ya ile nyumba salama, hata kifo cha Mama ni matokeo yaΒ usiri wanguβ Nilisema jambo ambalo lilimfanya Baba ashangae sanaΒ
βUmetoa wapi hayo unayoyasema Celin?β aliniuliza Baba kwa Mshangao mkubwa sana, nilifutaΒ chozi langu nikaivaa roho ya Ujasiri ili nimsimulie Baba kila kitu. Nilimsimulia kila hatua, kilaΒ jambo. Hadi namaliza kumweleza Baba alikua ameketi kitini akinitazama kwa uzito sana. SuraΒ ya majonzi ilimtawala Baba yanguΒ
βKwanini ulificha jambo kubwa namna hiyo Celin, siri yako imeharibu Maisha yetu, siri yakoΒ imeondoa uhai wa Mama yako Celinβ alinilaumu Baba, nilikua tayari kupokea lawama zoteΒ maana tayari maji yalinifika shingoni, nilikua naangamia.Β
βUnafikiria Polisi wataelewa haya?β aliniuliza Baba, tayari kitengo cha Polisi kilipokea taarifaΒ ya shambulio la Mama yangu. Walikua wameshafika, mlango ulikua ukigongwaΒ
Baba alinisogelea akaniambiaΒ
βKama unaweza kumaliza kila kitu basi maliza Celinβ alisema, kabla hata sijamjibu chochote Baba alielekea mlangoni na kufungua mlango, polisi walikua wamesimama mlangoni.Β
Baba aligeuka na kunitazama kisha alinipa ishara ya tumaini kwa kuniachia tabasamu.Β
βSisi ni maafisa wa Polisi, tunahitaji kuondoka na ninyi kwa ajili ya mahojianoβ alisema PolisiΒ mmoja, Baba akasemaΒ
βHaina haja ya kuondoka na sisi, peke yangu nitathibitisha kila kitu. Binti yangu hakuwepo eneoΒ la tukioβ alisema Baba, kauli yake ya ghafla ilionesha kua alikua ameubeba msalaba wangu.Β Polisi walinitazama kwa sekunde kadhaa huku nikiwa mwoga maana Mimi ndiye Muuwaji,Β kisha waliondoka na Baba yangu. Nililia sana, sikuwa na Mtu karibu yangu wa kuniambiaΒ maneno ya faraja.
Mama yangu alikua amefariki, Baba alikua mikononi mwa Polisi kwa makosa yangu Mimi. Nilijiinamia baada ya kulia kwa muda mrefu, baadaye nilitoka kwenye kile chumba. NilipataΒ Ujasiri wa kuuliza namna ya kuipata Maiti ya Mama kwa ajili ya Maziko. Utaratibu ulikua niΒ lazima tulipie pesa kidogo ndipo watupatie maiti, sikua na pesa nilimwambia Daktari natakiwaΒ kurudi nyumbani kuchukua pesa. Akaniangalia kisha akaniambiaΒ
βUsijali Msichana, tayari maiti imelipiwaβ nilishangaa sana, ni Nani anayeweza kuilipia maiti yaΒ Mama yangu ili itoke Hospitalini. Nilimtazama kwa Mshangao halafu nikamuulizaΒ
βHivi nimekusikia ipasavyo?βΒ Β
βNdiyo, Mjomba wako amelipiaβ alipomaliza kusema nikamwona Mjomba Mgina akiwaΒ anakuja tulipokua tumesimama na Daktari. Huzuni iliniingia Upya kabisa, nilimkimbiliaΒ Mjomba na Kumkumbatia kwa Uchungu sana.Β
βPole Celin, pole sana Mjombaβ alisema huku akinipiga piga taratibu mgongoni katika hali yaΒ kunipoza machungu. Chozi lilinibubujika tena, kwakua tayari nilikua nimemueleza kila kituΒ Baba yangu sikutaka kuleta tena Mkanganyiko.Β
βInaniuma Mjomba, Mama amekufa kikatili sanaβ nilisema, maumivu yaliyokua yamejaaΒ moyoni mwangu yalikua yakinichoma mithiri ya sidano.Β
Basi, tuliitoa Maiti Hospitalini na kuipeleka nyumbani kwa Mjomba Mgina. Palitawala MajonziΒ na vilio, maswali yasiyo na Majibu. Uvumi kua Baba yangu alikua amemuuwa Mama yanguΒ ulianza kusambaa miongoni mwa waombolezaji, kila Mtu alimwita jina baya Baba yangu.Β
Nilizidi kuumia ndani ya Nafsi yangu, Baba yangu aliitwa Muuwaji kwa sababu ya kunisaidiaΒ Mimi. Alijivesha ngozi yangu kunificha Muuwaji halisi, nililia kwa mambo mengi yasiyo naΒ Majibu. Macho yalinivimba, kesho yake tulimzika Mama kwenye Makaburi ya Jiji.Β
Hatimaye Mama yangu aliungana na Zena na Caren kwenye makazi ya milele. KilichokuaΒ kimebakia kwangu kilikua fumbo kubwa, hakuna aliyejua kuhusu ile nyumba yenye kaburi naΒ jini anayeuwa.Β
Sikutaka kumwambia yeyote, moyo wangu ulijawa na kisasi. Sikuuona umuhimu wa kuendeleaΒ kuishi ikiwa nimepoteza Wapendwa wangu kwa usiri wangu. Baba alifikishwa Mahakamani sikuΒ Nne baada ya kumzika Mama, alikiri mbele ya Mahakama kua alitenda Mauwaji hayo kwaΒ mikono yake kwa kile alichokiita wivu wa Mapenzi.Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE
COMMENTS ZIWE NYINGI SASAΒ
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
18 Comments
Good https://is.gd/N1ikS2
Awesome https://is.gd/N1ikS2
Good https://is.gd/N1ikS2
Very good https://is.gd/N1ikS2
Aisee admin story timu kinomaaaaaa shusaa ya 8
ishiii mbna marudioo mzee
Admin mm ndy wa kwanza hii st0ry ip0 0n π₯ asee
Good https://is.gd/N1ikS2
Aisee story timu admin yaan leta ya 8
Tunasubiri sehemu ya 8
Marudio hii admin
Marudio hii umetufowadia ya tarehe 1 .
ishiii mbna marudioo mzee
Story ni π₯π₯ sanaa,,tupe ya 8 bhas
Admin umenikamata aiseee story tamuuu
π₯
Naomba group
yp2bmc