Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 05
Taratibu nilitembea kuelekea mbele ya gari kumsikiliza yule Mwanaume, alikua mnene kiasi naย pia alikua na ndevu nyingi mfupi wa wastani, alikua ananukia manukato makali sana. Nilitembeaย taratibu huku nikijikwaa jiwe dogo lililonipa mwendo zaidi hadi nilisogea kabisa karibu yake,ย akanipa pole huku akigeuka na kunitazama nikitembea taratibu hadi nilipofika mbele yake.ย
โUsiwe na wasiwasi Celin, usiogope sababu nusura ya Maisha yenu yapo mikononi mwakoโ niliyafinya macho yangu kwa mshangao mkubwa sana, moyo ulilipuka ghafla na kuanza kwendaย mbioย
โUnamaanisha nini?โ nilimuuliza nikiwa na mhemko wa alichoniambia, tayari nilikuaย nimepoteza marafiki zangu wawili.ย Endelea
SEHEMU YA SITA
โNinachomaanisha ni hiki, Sisi tulizaliwa wawili tu. Mimi pamoja na Dada yangu Sabra, Babaย yetu alikua tajiri sana. Mama yetu alifariki muda mrefu, Baba yetu hakutaka kuowa kabisa.ย Alitulea kwa mikono yake hadi tulipokua wakubwaโ alisema huku nikimwona kama Mtuย anayekaribia kulia. Nilimeza mate huku nikiwa na shahuku kubwa ya kusikia alichokusudiaย kukisema. Kisha aliendeleaย
โPesa hugeuza Dunia juu chini, Usiku mmoja. Kaka yake Baba yetu alimuuwa Baba yetuย akimtuhumu kujilimbikizia mali ambazo alirithi kutoka kwa Baba yao. Usiku ule bado unaishiย ndani yangu, Mimi na Dada yangu Sabra tulishuhudia ukatili ule. Baba mkubwa akaagizaย tusakwe mle ndani tuuawe, tulikimbilia chumba cha chini ambacho mara zote Baba alisema kuaย
kama itatokea shida basi tukimbilie humo kujificha, wakati huo Mimi nilikua na Miaka 11 naย Sabra alikua na Miaka 15.โ Alipofika hapa alijiinamia, alikua akilia. Nilitamani kumshika naย kumtuliza lakini alikua Mtu mgeni kwangu istoshe nilikua nikimwogopa. Niliishia kumtazama tuย hata neno la kuongea sikuwa nalo.ย
Aliinua kichwa chake kunitazama, nusura nikimbie. Alikua na macho meupe yasiyo na kiini.ย ย
โUsikimbie, huu ndiyo ukweli pekee unaoweza kunusuru Maisha yenu Celinโ alisema, niliitikiaย kwa kutumia kichwa lakini moyoni nilikua nimejawa na hofu sana, miguu yangu ilitamaniย kukimbia kuliko kusimama mbele ya yule Mwanaume.ย
โJitihada zetu hazifukua dafu, walitukamata. Walituambia tupige magoti, tulifanya hivyo kishaย Baba yetu Mkubwa alifika kule chini kisha alituambia hakukusudia kutudhuru sisi isipokuaย tulishuhudia kifo cha Baba yetu. Aliamuru wale watu watuuwe, walichinja shingo zetu naย kumaliza Uhai wetu kule chiniโ niliachama, hewa ya ghafla iliingia kwa mshangao mkubwa, inaย maana nilikua nazungumza na Mfu? Nilijiuliza ndani yangu lakini cha ajabu alinijibu kama vileย nilizungumza kwa sautiย
โNdiyo, Mimi ni mfu. Msaada wangu ni wewe Celin. Walituzika kule kule chini kisha waliuzibaย mlango wa kuelekea kule chini, sijui kuhusu Baba yetu alienda kutupwa wapi. Lakini kule chiniย tulizikwa Mimi na Dada yangu Sabra. Nasfi zetu zimeishi kwenye ile nyumba kwa miaka mingi,ย ย
kila aliyeamia kwenye ile nyumba alikutana na mikasa ya ajabu kila uchwao, wengiย walikimbia.โย ย
โHakuna aliyepata ujasiri wa kufwatilia chochote kile. Nafsi zetu ziliwasumbua sana, ndipo Babaย Mkubwa alipotafuta Mganga kwa ajili ya kuizindika ile nyumba lakini hata zindiko lakeย halifukufanya kazi isipokua lilitengeneza jini ambalo wewe umekutana nalo mara kadhaa. Jiniย mzee aliyeishi kwenye ile nyumba na kuzidi kuuwa Watu, hata Baba Mkubwa aliuawa na lileย jini, ni jini hatari sana ambalo linaondoa Kila anayeishi ndani ya ile nyumba. Awali Babaย mkubwa aliishi mule lakini aliikimbia nyumba mwenyewe kutokana na mauza uza, aliiachaย nyumba yenyeweโย
โKatika harakati za kupambana na lile jini nilijikuta nikiondoka kwenye kaburi na sijui nawezaย vipi kurudi tena ndani ya ile nyumba. Ujasiri wako, udadisi wako ulinivutia sana Celin, naombaย unisaidie jamboโ alisema, hadi kufikia hapo nilikua na simulizi halisi ya ile nyumba ambayoย niliitilia sana shaka tokea mwanzo.ย ย
โNitasaidia nini, siwezi kupambana na vitu kama hivyo. Sina hiyo nguvu Mimiโ nilisema,ย alinitazama kisha akaniulizaย
โUnajua wazazi wako wanapitia nini ndani ya ile nyumba? Usije ukawapoteza kirahisi hivyoย Celin, Baba na Mama yako wanahitaji msaada na msaada pekee ni wewe kuitoa nafsi ya Dadaย yangu, ikiwa huru tunaweza kupambana na jini linalouwa kila anayeifahamu siri ya ile nyumba.ย Jini hilo ni Bibi Mzee, ameuwa kila Mtu anayehoji kuhusu nyumba ile, nimekuokoa padogo sanaย
lakini bado atakuwinda akumalizeโ chozi lilianza kunibubujika, sikuwaamini Wazazi wanguย lakini niligundua walikua hawana hatia, pengine hilo jini ndilo linalowatumikisha.ย
โUsilie Celin, nitakupa njia ya nini ufanye unapofika ndani ya chumba ambacho huwa unamsikiaย Mwanamke akiimba au kulia, huyo ni Dada yangu Sabra. Amekuwa Mtumwa wa huyo jini katiliย aliyepandikizwa na Baba Mkubwaโ Alisema, nilijaza hewa kifua changu maana niliyoyasikiaย yalikua ni mambo ya kutisha sana.ย
Ilikua ni kama nasoma kitabu cha Riwaya ya kutisha kilichoandikwa kwa mtiririko wa ajabuย sana, mishipa ya kichwa ilinisimama. Nguvu zilikua zikiniondoka taratibu huku nikihema juuย juu, alichokisema ndicho nilichokua nikikitafuta kukisikia lakini baada ya kukisikia nilitamaniย nisingelisikia kabisa.ย
Hadithi ya kuogofya iliyoondoa wapendwa wangu pamoja na Dalali aliyetutafutia nyumba.ย Haikua rahisi kuelewa, sikuacha kumtazama yule Mwanaume ambaye kwa mujibu wa hadithiย yake ni Mtu aliyekufa muda mrefu, ni nafsi inayohangaika kumtafuta Dada yake aliyezikwaย chini ya nyumba yetu tuliyoinunua. Sikutaka kujua nyumba ipo chini ya naniย ย
Kila nilichokisikia kuhusu nyumba yetu kilinipa uhakika wa kile alichoongea, kuhusuย Mwanamke anayeimba na kulia hilo ni jambo dhahiri sana. Nilipata kujua kuhusu jini Mzeeย anayeishi ndani ya nyumba yetu na kufanya Mauwaji.ย ย
โKuna Mzee nyumba jirani, unamfahamu?โ nilimuuliza.ย
โNdiyoโผ Unachokiona ni fikra zako na jinsi ambavyo jini yule mbaya anataka uone. Hakunaย uhalisia kwani Mzee yule alifariki Miaka mingi, nyumba yake iko tupu, inakaliwa na huyu jiniย ambaye ndiye aliyemuuwa huyo Mzeeโ nilipepesa macho yangu, kila kitu kilikuwa kipyaย masikioni mwangu.ย
Chozi lilinitoka, alinipa nafasi ya kumuuliza nisichokijua. Alikua akinitazama huku akisubiriaย swali langu.ย
โKuhusu wazazi wangu?โ japo sikutaka kusikia sana kuhusu Wazazi wangu, nilihisi ingeniumizaย sana. Yule Mwanaume alinitazama akaniambiaย
โNi watumwa, unapaswa kuwakomboa kabla hawajatoweka. Kwakua ameshajua wewe unajuaย kuhusu siri ya ile nyumba unaweza ukawa na muda mchache sana wa kuwasaidia.โ Alisema,ย nilizidi kuumia ndani ya nafsi yangu. Baba yangu aliniumiza zaidi sababu alitumia pesa zake zaย kustaafu kununua nyumba ya ndoto zake lakini nyumba hiyo ndiyo chanzo cha Matatizo yote.ย ย
โCelinโ aliniita na kuniondoa kwenye fikra za kuogofya. Nilimtazama, nilimwona kamaย Mkombozi wangu ambaye anaweza kuyarudisha Maisha yangu ya furaha ya huko nyuma.ย
โAbee!โ niliitika kwa utuo, chozi lilikua likinibubujika tu.
โKulia hakuwezi kuokoa Wazazi wako na wapendwa wengine. Vaa Ujasiri, ukiweza kumalizaย hili nitakupa shukuraniโ alisema, niliyatafakari maneno yake. Ni kweli nilihitaji kuuvaa Ujasiriย wa hali ya juu sana lakini haiwezi kuondoa huzuni iliyojaa ndani yangu. Niliitikia kwa kutumiaย kichwa kisha akaniambiaย
โNitakua nawe bega kwa bega hadi mwisho, ikiwa utashindwa nitashindwa pia, ukishindaย nitashinda na weweโ kisha aliingiza mkono mfukoni na kunipatia ushanga mwembambaย uliotungwa vizuri.ย ย
โNipe mkono wa kuliaโ kisha alimalizia na ishara ya Kichwa huku akinyoosha Mkono kuuombaย mkono wangu, alionesha kuhitaji kunivisha ule Ushanga wenye rangi nyeupe. Japo bado nilikuaย namwogopa lakini nilimpatia mkono wangu. Halafu akanifunga ule Ushanga mkononi kamaย kembe hivi.ย
โHuo ndiyo Ulinzi wako Celin. Rudi nyumbani ishi kama kawaida lakini nitakua nawasilianaย nawe mara kwa mara kukwambia nini cha kufanyaโ alisema huku nikiwa nautazama uleย ushanga, nilipoinua kichwa changu sikumwona tena yule Mwanaume hata lile gari halikuwepoย tena. Nilijikuta mwenyewe msituniย
Nilianza kuhangaika kutafuta pa kutokea, niliongoza ile barabara tuliyokuja nayo, nilikuaย ninahema huku nikiwa nina hofu sana. Nilianza kukimbia, nilipojikwaa nilinyanyuka hadiย nilipofika Barabara kuu iliyokua ikielekea Mjini.ย
Nilipunga Mkono wangu kuomba msaada, hatimaye nilipata msaada wa โliftiโ. Gari moja ndogoย iliyobeba wanafamilia ilinisaidia hadi nikafika Mjini. Niliwashukuru kwa msaada wao,ย nilitazama juu palikua na jua kali, saa yangu iliniambia kua ni saa sita Mchana. Niliufunguaย mkoba wangu, nikaitoa simu na kumpigia Mama yangu. Niliposikia sauti yake nilishusha pumziย zangu maana aliniambia wapo salama, nami nilimwambia kua ndiyo nimetoka chuoni narudiย nyumbani.ย
Nilielekea kituo cha treni, kisha nilipanda treni hadi mitaa ya nyumbani, nikatembea kidogo hadiย nilipofika nyumbani, nilisimama getini nikiiangalia nyumba yetu. Chanzo cha yote ni hiyoย nyumba. Ilikua ni nyumba nzuri iliyojaa utulivu kwa nje lakini ndani ilikua na vibweka vyaย kutisha, masikio yangu yalianza kupiga kelele mithiri ya filimbi za sungusungu.ย
Sikujua ilikua ni ishara gani, sijui ni kitu gani kilinifanya niangalia pembeni ule upande waย nyumba ya yule Mzee, nilimwona yule Mzee akiwa amesimama akinitazama bila hata kupepesaย macho. Sasa nilikua na siri ya huyu Mzee kua si Mtu halisi bali ni mzimu wa Mzee aliyeuawa naย yule Jini Mzee.ย
Alikua kimya sana, akinitazama bila kupepesa macho yake. Ghafla akatoweka katika mazingiraย tata, nilishtuka sana nusura nizimie. Hayakua mambo ya kawaida, nilizoea kuyatazama kwenyeย filamu na tamthilia za kizungu. Kisha nilisikia geti likitoa sauti ya maumivu ya Bawaba kamaย
vile lilikua likisukumwa na Upepo hivi. Ile sauti ilikua ndiyo sauti pekee iliyotawala masikioย yangu.ย
Niliingiwa na shahuku na kusogea, bado masikio yalikua yakipiga kelele sana. Nilianza kupigaย hatua za taratibu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee ili nione geti hilo lilikua likipiga keleleย kwasababu ya upepo gani wakati palikua tulivu sana, nikakumbuka siku ile niliona geti hiloย likiwa limejaa kutu, inawezekana vipi likapiga kelele hivyo?ย
Nilijiuliza nikiwa ninazidi kupiga hatua za kuhesabu, moja mbili, moja mbili nikiwa nazidiย kutembea mwili nao ulikua ukisisimka sana kuashiria nilikua naikaribia hatari. Katika hali isiyoย ya kawaida kabla hata sijafika getini, nilikua ubavuni naelekea nikaona kitambaa kikipepea paleย getini, hakikua kitambaa kidogo kilikua kikubwa na jinsi macho yangu yalivyoniambia nilionaย gauni jeupe, ilikua ni ishara kua palikua na Mtu aliyejibanza getini ili anishambulie.ย
Nilisimama, ghafla nilianza kusikia sauti ya ajabu iliyojaa ushawishi sana. Sauti hiyo ilikua niย sauti ya kizee ikiniambiaย
โCelin, njoooooโผ njoo Binti, unakaribiaโ ni sauti ya taratibu sana iliyotoka kwa kunongโoneza,ย sauti hiyo ilikua ikisikika kila sehemu, ilikua inazidi kunivuta katika hali ya ajabu sana nizidiย kuelekea getini. Vitu viwili vilitokea, mwili wangu ulikua unakataa lakini akili ilikua inatakaย kwenda, niliharibiwa kisaikolojia nikajikuta nikijivuta kusogea.ย
Namna nilivyoyaona mazingira ilikua kama vile nipo Dunia ya peke yangu, isiyo na Mtuย mwingine. Niliona giza la ajabu na mwanga hafifu, kipande cha gauni kiliendelea kupepea. Sautiย ya yule Bibi Kizee jini iliendelea kuniangamiza kisaikolojia, jasho lilikua likinitoka. Nilikuaย naendelea kupiga hatua za mvutano, kumbe wakati yote yanaendelea Mama yangu alikuaย ghorofani akinitazama kwa Mshangao.ย
Nilikua namsikia akiniita lakini nguvu ya ile sauti ya yule Bibi ilinizidia kiasi kwamba nilitamaniย kupaza sauti kumwambia Mama kua anisaidie lakini nilishindwa, hata kugeuka kumtazamaย Mama kilikua kipengeleze kizito sana. Shingo yangu ilikaza ikitazama mbele, udenda ulikuaย ukinitoka.ย
Hakika huyu Jini alikua na nguvu za ajabu sana. Alikua akiniita huku akicheka kanakwambaย alikua na uhakika kua ameniweza, nilijitahidi sana kupambana na nafsi yangu lakini sauti yakeย ilikua na nguvu ya ajabu sana.ย ย
Nilisogea karibu kabisa na geti, hatua moja ndiyo iliyobakia kufika alipo yule jini, gauni lakeย lilikua likipepea huku sauti yake ikizidi kuwa karibu zaidi. Niliweka mikono yangu masikioni,ย nilijua nateswa na ile sauti lakini sikua na nguvu ya kupambana nayo.ย
Nilikua natetemeka, nilijaribu kujizuia kwa nguvu lakini nilikua sina hiyo nguvu zaidi yaย kunyanyua mguu ili nifike alipo yule Jini. Ghafla nilishikwa na kuvutwa nyuma, fahamuย zilinirudia, hali ya hewa ilitulia, sauti ilikatika sikuisikia tena.ย
Mbele yangu alikua amesimama Mama pamoja na Baba yangu, macho yalinitoka pima kamaย fundi cherahani anayetungisha uzi kwenye zindano, udenda ulikua ukinitoka nikawahi harakaย kuufuta lakini tayari Baba na Mama walikua wameshaniona katika hali ile ya uzezeta.ย
Walikua kimya wakiniangalia nilivyokua najihangaisha kujiweka sawa kanakwamba kila kituย kilikua vizuri. Mama aliniambiaย
โTumeona kila kitu, unajaribu kuficha nini?โ sauti ya Mama yangu ilinisuta, alizungumza kamaย Mama aliyegundua Uwongo wa Binti yake, macho ya Baba yangu yalikua kwangu piaย akiniangalia kwa mshangao pia.ย
Niliinamia chini, aibu ilikua imenishika vibaya sana. Baba akaniulizaย
โMkononi umevaa nini Celin?โ macho yangu nikayapeleka mkononi, nikagundua alikuaย akiuongelea ule Ushanga niliopewa kama Ulinzi na yule Mwanaume nisiyemjua jina.ย
Nilimtazama Baba kisha Mama, halafu nikasema โNi urembo tu huu Babaโ sauti yangu naย matendo yangu yaliwaambia uhalisia wangu kua kuna jambo nalificha. Haikuishia hapo, Mamaย alienda mbali zaidi akasemaย
โHii siyo mara ya kwanza nakuona unanyata kuelekea kwenye nyumba jirani, Celin unafichaย nini ambacho huwezi kuzungumza na Sisi? Umepoteza marafiki wawili kwa mpigo, kuna niniย kinachoendelea?โ Maswali ya Mama yangu yalikua kama Mshale ulionichoma kooni,ย nilikaukwa mate na maneno ya kujibu.ย ย
Niliishia kuwatazama, mara radi zilisikika. Wingu zito hata lilikotokea hakuna aliyejua, papoย hapo mvua ilianza kunyesha, hakuna aliyetaka kuikimbia mvua. Sote tulisimama tukitazamana,ย Wazazi wangu walihitaji majibu kutoka kwangu.ย
โMama, tutaongea ndani mvua inazidi kua kubwaโ nilisema kisha nilikimbilia ndani nikiwaachaย wazazi wangu wakiwa wamesimama. Nilipanda ghorofani hadi chumbani kwangu, niliwatazamaย Wazazi wangu pale nilipowaacha lakini sikuwaona, nikahisi huwenda nao wamekimbilia ndani.ย
Niliiangalia nyumba jirani, kichwani nilikua na majibu kua nyumba ile ilikua ikikaliwa na yuleย jini Muuwaji. Cha kushangaza niliwaona wazazi wangu wakiwa wamesimama getini, ni kamaย vile walihitaji kujua nilikua nafuatilia kitu gani, moyo ulinilipuka mithiri ya Volkano kali yaย moto.ย
Mvua ilikua ikiwapiga, kibaya zaidi mbele yao alikua amesimama Yule Bibi Kizee akiwaย amevalia gauni jeupe akiwaita Wazazi wangu kwa kutumia mkono wa kushoto huku akirudiย nyuma nyuma. Kilichowakuta Wazazi wangu ndicho kilichokua kinanivuta na Mimi,ย niliwashuhudia Wazazi wangu wakiwa kama mazombi.ย
Hawajitambui, walikua wakilifungua lile geti huku macho yao yakiwa kwa yule Bibi Kizee, tenaย walikua na haraka sana wamfikie. Walikua wakiielekea hatari ile ile ambayo wao waliniokoaย
nayo, sasa ulikua ni wajibu wangu kuwasaidia. Haraka nilifungua mlango na kuanza kushushaย ngazi niwawahi wazazi wangu wasiingie mikononi mwa yule Bibi kizeeย
Niliteremka ngazi haraka haraka hadi nikafika chini, moja kwa moja nikakimbilia getini,ย nikalifungua geti haraka Halafu nikakimbilia getini kwa yule Mzee. Nilipofika niliwaona Wazaziย wangu wakiwa wamesimama nyuma ya yule Bibi Kizee Muuwaji. Walikua wameinamishaย shingo zao, mvua bado ilikua ikinyesha, geti lilikua wazi.ย
Walikua wakitazama chini, yule Bibi alikua akinitazama halafu aliangusha kicheko kikubwa.ย Alikua na sauti mbaya mithiri ya radi, ghafla alianza kutokwa na kucha ndefu, sura yake ilikuaย ndefu, nywele ndefu zilizo dhohofika, macho yake yalikua mekundu, meno yalichomoka.ย
Alikua na sura mbaya ambayo ilitosha kuniambia kua ni kweli ndiye Jini Muuwaji. Alikua kamaย amewateka Wazazi wangu kifikra. Nilianza kuogopa, alikua akinisogelea taratibuย
Nilikua nikihema, Wazazi wangu walikua wamesimama vile vile kama Watu wasiojitambua.ย Yule Bibi aliendelea kunisogelea huku mguu wake mmoja akiwa anauburuza. Ulikua kama unaย dosari ya ukilema hivi, nilikua kwenye butwaa ambayo ilihitaji Mtu anitingishe ndiyo nitokeย katika ile hali tata.ย
Fumba na kufumbua Macho yule Bibi Kizee alikua amejaa machoni pangu akinimulika naย macho yake makali, nilishtuka na kutoka katika ile hali ya Butwaa. Nilipohitaji kukimbiaย alinishika mkono na kunivuta kwake lakini alipigwa na shoti kali, niliona moto mkaliย uliomsukuma na kumtupa chini.ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SABA
COMMENTS ZIWE NYINGI SASAย
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
10 Comments
Admin wa kwanza apa ntagi mm sehemu inayofuata ๐nzur sana nmeipenda
Awesome https://is.gd/N1ikS2
Familia ya Celin ina kumbwa na majanga
Very good https://is.gd/N1ikS2
Good https://is.gd/N1ikS2
Awesome https://is.gd/N1ikS2
๐๐๐
Awesome https://is.gd/N1ikS2
Dah๐ฎ admin endelea7๏ธโฃ
Admin ya 7 admin