Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Tatu-03)
    Hadithi

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Tatu-03)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaApril 25, 2025Updated:April 27, 202532 Comments11 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nyumba Juu Kaburi

    Tulipishana Mwaka mmoja wa kuingia chuoni, alinitendea wema kila nyakati. Hata wakati  ambao alipaswa kufurahi alinipa furaha yake na kisha yeye alibakiwa na huzuni yangu.  Nilimwona akiwa anafunguliwa kutoka juu ya feni akiwa amevalia gauni lake jekundu. 

    Hakika maneno ya yule Bibi yalianza kutimia, nilimpoteza mmoja nimpendaye. Nilijiegemeza  ukutani nikilia kwa kwikwi nikiushuhudia mwili wa Zena ukiondolewa na Askari Polisi  waliokua hapo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa.  Endelea

    SEHEMU YA TATU

    Mimi na Caren tulibakia chumbani kwa Zena tukilia, haikua rahisi kuamini kua Zena alikua  amekufa kikatili sana kwa kujinyonga. Mara simu yangu ilianza kuita kutoka kwenye mkoba  wangu niliokua nimeutupia pembeni, nilishtuka sana. Niliacha kulia nikauvuta mkoba kisha  nikaitoa simu yangu ambayo bado ilikua ikiendelea kuita 

    Moyo ulinipiga ‘Paaa‼’ nilipoona ni Mama yangu ndiye aliyekua akinipigia. Sikutaka kusikia  taarifa nyingine mbaya. Niliiacha simu iite hadi ilipo acha kuita, niliirudisha kwenye mkoba  mara moja halafu fikra zangu zikawa nyumbani kwetu. 

    Maneno ya yule Bibi yalikua na nguvu ya kunizunguka kichwani, nilihisi nyumbani kwetu  hapako salama. Niliumia ndani ya moyo wangu huku nikiitupa miguu yangu sakafuni.  

    Sikujua ni Nani alikua anafuata baada ya Zena, yule Bibi ni Nani na kwanini haya mauzauza  yameanza baada ya kuhamia kwenye ile nyumba. Maswali haya yote nilijua ni Nani anapaswa  kuyajibu. Ni yule Mzee wa nyumba jirani, huwenda anafahamu jambo fulani la kutisha kuhusu  nyumba yetu. 

    Nilinyanyuka kutoka sakafuni, nikamtazama Caren aliyekua amelegea kutokana na kukosa  nguvu kwa kile kilichotokea, tulimpoteza rafiki mzuri sana katika mazingira ya kutatanisha.  Nilimwambia Caren 

    “Nataka kupata majibu ya haya yote Caren, siwezi kuruhusu hii hali iendelee” sauti yangu ilitoka  kwa hisia kali ya maumivu, nilifuta chozi langu. Caren naye alisimama. Tulikua wawili tu ndani  ya kile chumba cha Zena.  

    “Ukweli upi, ni kuhusu yule Bibi au kifo cha Zena?” aliniuliza, nilimtazama kwa sekunde  kadhaa kisha nilimwambia 

    “Vyote kwa pamoja, jina la Zena lilikua kwenye ile Barua uliyopewa na yule Bibi wa ajabu.  Sijui, lakini nahisi kuna shida sehemu” Umakini wa Caren uliongezeka, akanitazama kwa  shahuku akaniuliza 

    “Shida Sehemu?”  

    “Ndiyo, baada ya kuhamia kwenye ile nyumba nilianza kupata hisia ya ajabu. Sitaki kuwaambia  Wazazi wangu kuhusu hilo lakini nahisi kuna Mtu anajua jambo kuhusu ile nyumba, Caren  nisikilize Mimi” nilisema kisha nilimshika mabega Caren ili nimueleze zaidi. Nilimfanya Caren  kua Mshirika wangu

    “Kuna Mzee nyumba jirani nina wasiwasi anajua jambo, ile nyumba sio ya kawaida kabisa.  Sitaki Wazazi wangu wajuwe sababu watachanganikiwa. Tunaweza kuutafuta ukweli?”  nilimuuliza, alinitazama kwa tafakari fupi kisha aliniambia  

    “Kama hisia zako zinakwambia hivyo Celin, sina chaguo” nilimkumbatia Caren, angalau nilipata  Mtu anayeweza kunielewa. 

    Nilirudi nyumbani jioni, hofu na mashaka viliendelea kunitafuna hadi nafika nyumbani.  Niliogopa kukuta Watu wengi pale nyumbani, niliogopa kusikia sauti ya Kilio, niliogopa  kupoteza Mtu mwingine. Nilipofika getini kwetu, nilisimama kidogo huku macho yangu  yakielekea nyumbani kwa yule Mzee. 

    Palikua kimya, hapakua na dalili ya Mtu. Nilijiweka sawa kiakili ili Wazazi wangu wasigundue  lolote, sikutaka wajuwe kuhusu kifo cha Zena wala jambo lolote lile lenye utata. Nilipoingia  Bustanini niliitazama sana nyumba yetu, nafsi yangu iliniambia kuna jambo lisilo kawaida  kuihusu hii nyumba lakini sikua na ushahidi wa kuthibitisha hilo. 

    Nilipata amani nilipowakuta Wazazi wangu wakiwa wameketi sebleni wanaangalia taarifa ya  Habari, angalau moyo wangu ulipata kupumzika. 

    Niliwasalimia kisha nilipandisha ngazi nikaelekea chumbani kwangu. Nilisimama kando ya  dirisha nikiitazama nyumba ya yule Mzee, bado ilikua kimya. Palikua na majani mengi sakafuni  kuashiria kua eneo hilo halikufanyiwa usafi kwa muda mrefu. 

    Baada ya kusimama kwa muda kidogo nilirudi na kuketi kitandani nikiwa nakumbuka matukio  ya siku nzima, chozi lilinitoka tena. Kusema ukweli kifo cha Zena kiliniumiza sana, kuna namna  nilijiona Mimi ni Mkosaji. Basi nilijiegesha kidogo, nikajikuta nikipitiwa na Usingizi. 

    Nilishtuka, bado palikua na giza. Mwili ulikua umechoka sana, hisia ya kua nililala muda mrefu  ilinijia. Nilijinyoosha kidogo kabla ya kuchukua simu na kuangalia saa 

    Niliona ilikua ni saa 7:11 Usiku, nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani kisha nikasogea pale  dirishani na kuangalia nyumbani kwa yule Mzee. Bado palikua kimya, hapakua na dalili yoyote  ile, Mbwa walikua wakibweka sana. 

    Nilifungua mlango taratibu kisha kwa mwendo wa kuchoka nilishusha ngazi, taa zilikua tayari  zimezimwa kuashiria kua Wazazi wangu walikua wameshalala, swali pekee nililojiuliza 

    “Inawezekanaje Wazazi wangu walale bila kuniamsha?” Sikupata jibu la haraka, nilitembea  taratibu baada ya kufika sebleni kisha niliwasha taa, kisha nililielekea friji nikachukua maji ya  Baridi na kuyanywa. Angalau niliusikia mwili wangu ukiwa umepoa 

    Nilifikiria kuwagongea mlango wazazi wangu lakini niliona nitawasumbua, badala yake niliketi  kwenye sofa. Bado taswira ya kifo cha Zena ilikua ikiendelea kunisakama.

    Nikiwa hapo nilianza kuhisi mwili wangu ukisisimka sana kama vile nilikua napandwa na  sisimizi, kichwa kilianza kua kizito huku nikianza kuisikia sauti fulani ya ajabu. Nilisikia sauti  ya kugonga, ilisikika ikigongwa kwa utaratibu sana 

    “Mh‼ hii sauti inatokea wapi?” nilijiuliza, nilisimama taratibu huku sauti ya kochi ikisikika  wakati nanyanyuka. Niliisikilizia vizuri ile sauti niligundua ilikua ikitokea kwenye chumba  kimoja pale eneo la chini.  

    Chumba hicho tulihifadhia baadhi ya vitu ambavyo hatuvitumii mara kwa mara, mfano wa stoo  hivi. Woga ulianza kunijia kisha nilianza kusikia sauti ya Mwanamke akiimba, sikujua alikua  akiimba nyimbo gani lakini sauti ilikua ikitoka mule mule chumbani.  

    Ilikua ni sauti laini inayoimba kwa umaridadi sana, mapigo ya moyo wangu yaliongezeka sana,  yalikua yakidunda kama ngoma. Hata pumzi ziliongezeka, woga ulinishika sana, mwili  uliendelea kusisimka kwa kasi huku nikihisi kama nina hali ya kuchanganikiwa. Nilipiga hatua  za taratibu sana kuelekea nilipoisikia sauti ile, korido ilikua tupu isipokua Mimi pekee. 

    Nilimeza funda zito la mate ili kujipa utulivu ambao kwa hali ilivyo ulihitajika sana, hatua zangu  zilikua za kusuasua sana huku nikitembea kama Mtu nsiye na uhakika wa kufika ninapohitaji.  Nilizidi kutembea taratibu sana kuuelekea mlango, mara nilisikia sauti nyuma yangu 

    “Celin?” ilikua ni sauti ya Mama yangu aliyeonekana kusimama kwa sekunde kadhaa  akinitazama kwa kunishangaa, uso wake haukuwa na hofu kama wangu, jasho lilikua likinitoka. Kwa mara nyingine tena nilijiapiza kua siwezi kumweleza chochote kile Mama yangu. 

    “Mamaa‼” nilimwita kwa sauti ya mshituko kidogo, sikutegemea angekua akinitazama.  Mkononi alikua ameshikilia glasi yenye maji ya Baridi. Taratibu alisogea akionesha kuwa alikua  na maswali ya kuniuliza, aliponifikia aliniuliza 

    “Kuna nini mbona unaonekana kama ni Mtu unayevizia Usiku huu?” swali la Mama lilinifanya  nigundue kuwa alikua hajasikia chochote kile. Ile sauti haikusikika tena 

    “Hakuna Mama, sio kitu” nilisema kisha nilitaka kuondoka lakini Mama akanisimamisha 

    “Kuna jambo unanificha Celin, nakujua nje na ndani, wewe ni Binti yangu ukisema ukweli najua  na ukisema uwongo vile vile najua. Nieleze, ulikua unavizia nini?” nilimshika Mama bega  nikamwambia 

    “Mama usijali, hakuna jambo lolote lile. Nipo sawa” nilisema kisha nilipandisha ngazi nikarejea  chumbani, nilijuwa nyuma yangu Mama alikua na maswali mengi ambayo sikutaka kuendelea  kuyasikia. Nilipofika Chumbani, haraka nilichukua simu yangu na kumpigia Caren lakini  hakuipokea 

    Niliitupa simu kitandani, kisha nilisogea dirishani. Niliitazama tena nyumba ya yule Mzee,  niliamini alikua na majibu mengi ya maswali yangu, nilisimama kwa dakika kama tatu hivi kisha 

    nilikata tamaa, nikataka kufunga dirisha lakini ghafla nilihisi kama kuna Mtu amesimama  dirishani kwenye nyumba ya yule Mzee akinitazama. 

    Nikishtuka sana, nyumba yake ilikua ya kawaida sio ya ghorofa. Dirisha moja lilikua likiwaka  taa, hapo ndipo nilipomwona Mtu akinitazama. Ilionesha wazi kua alikua anajua kua nina tabia  ya kuichunguza nyumba hiyo, nikajificha kidogo na kuanza kuchunguza kwa siri. 

    Nilishtuka sana, niliyemwona akinitazama alikua ni yule Bibi niliyepanda naye kwenye Treni,  ndiye aliyenitamkia maneno ya ajabu na ndiye aliyempa Caren bahasha yenye karatasi yenye  jina la Zena. Kwa namna yoyote ndiye anayehusika na kifo cha Zena, moyo ulilipuka mithiri ya  Volkano nikiwa nimejibanza, niliipa mgongo nyumba ya yule Mzee 

    Mapigo ya moyo wangu yaliongezeka kasi, nilifumba macho ili kuvuta nguvu ya kirejea  kumtazama tena, nilipopeleka tena macho yangu yule Bibi hakuwepo, isipokua ile taa iliyokua  ikiwaka kwa mwanga mkali ilikua ikiangaza. 

    Japo nilikua mwoga sana Maishani mwangu lakini nilipata ujasiri wa kutaka kuelewa zaidi,  nilipata wazo la kwenda kwenye ile nyumba. Usiku ulizidi kuwa mwingi, sikutaka Mtu yeyote  yule ajuwe kuwa ninatoka. Nilichukua koti langu kisha nikalivaa, nilivuta pumzi nikiwa  nimesimama tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa yule Mzee.  

    Simu yangu ilinidokeza kua ilikua imeshapata saa Nane kasoro za Usiku. Nilijiambia kuwa  liwalo na liwe lakini ni lazima niujuwe mzizi wa yote, nisingeliweza kukubali kupoteza  wapendwa wangu, nilifungua mlango taratibu huku nikiisikia sauti ya Baba yangu akikoroma. 

    Sikua na shaka yoyote kua alikua amelala, hofu yangu ilikua kwa Mama yangu. Nilihakikisha  nakua makini sana, nilizichunga hatua zangu za taratibu hadi nilipofika chini, kisha nilifungua  mlango ambao ulinitii bila kupiga kelele zozote zile, nilipiga hatua za haraka baada ya kutoka nje  hadi nilipoondoka ndani ya Uzio wa nyumba yetu. 

    Nyumba ya jirani, mbwa alikuwa akiendelea kubweka tena alibweka kwa kasi sana, sauti ya  Bundi ilikua ikiendelea kusikika pia, ulikua ni Usiku mwingi kiasi kwamba hapakua na yeyote  nje isipokua Mimi na shahuku yangu. Upepo wa hapa na pale ulikua ukiendelea kuvuma taratibu,  ulifanya hali ya Ubaridi iongezeke. 

    Nilipofika nje kabisa, niliitazama nyumba yetu. Akili na nafsi yangu viliniambia haikua nyumba  ya kawaida, basi nilishupaza shingo yangu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee, nilikua na  uhakika wa kupata Majibu ya maswali yangu usiku huu. Taratibu niliendelea kupiga hatua 

    Nilipofika mbele ya nyumba ya yule Mzee nilisimama kwanza huku nikijiuliza mara mbili mbili  kama nilikua tayari kufanya nilichokua nataka kukifanya. Nilijiambia ndani yangu kwa sauti  isiyo na mawimbi ya nje 

    “Ni lazima niwe jasiri, vinginevyo naweza kupoteza kila nikipendacho” ilikua ni sauti iliyojaa  ujasiri mwingi ndani yangu. Macho yangu yaliendelea kuitazama ile nyumba kisha nilisukuma 

    geti, halikua geti kubwa, geti dogo lililozungushiwa na uzio wa Miti fulani yenye miiba ndogo  ndogo 

    Urefu wa geti iliishia kifuani pangu, nilipolisukuma nilipokelewa na sauti ya Bawaba za geti hilo  ambazo zilipiga kelele fulani ya maumivu ya kufunguliwa mithiri ya nyumba isiyo kaliwa na  yeyote yule. Sauti hii ilinipa maswali mengi, nilichukua simu na kuwasha tochi nione kama hisia  zangu zilikua sahihi.  

    Macho yangu yalishuhudia kile ambacho nafsi yangu iliniambia, geti lilizungukwa na kutu,  Bawaba zilifichwa na kutu. Hapana shaka geti hili halikufunguliwa kwa muda mrefu, sasa  nilijiuliza nikiwa nimesimama pale pale getini. 

    “Inawezekanaje? Ina maana walio ndani wanapitia wapi kama geti hili halifunguliwi?” Lilikua  swali la kwanza la Msingi, bado nilikua njia panda. Sikutaka kurudi nyuma, niliazimia ni lazima  niichunguze nyumba pamoja na wanaoishi ndani ya hii nyumba.  

    Nilipiga hatua za kunyata, nikafanikiwa kufika mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumba  hii. Nilipofika hapa niliwaza kidogo, jibu nililolipata ni kulielekea dirisha lile ambalo nilimwona  yule Bibi wa ajabu, basi taratibu nilianza kutembea kwa mwendo wa kunyata hadi nilipolifikia  dirisha. 

    Bado palikua panawaka taa, taratibu nilianza kuchungulia ndani, sikumwona yeyote yule lakini  mazingira yote yaliniambia kua ndani ya nyumba palikua na Mtu au Watu kama ambavyo  nilimwona yule Bibi nikiwa chumbani kwangu. 

    Nilisimama hapo kwa dakika kadhaa, palikua kimya sana. Bado upepo wa taratibu ulikua  ukiendelea, nilipata wazo la kuuelekea mlango hivyo nilirudi hadi mlangoni. Nilisimama kwa  sekunde kadhaa, kisha nilijaribu kutekenya kitasa cha mlango 

    Cha ajabu, Mlango ulifunguka kirahisi sana. Baada ya kufungua mlango niliweza kuangaza kwa  ndani ya nyumba hiyo, nilikutana na sebule inayowaka taa kali, palikua na Kochi moja jekundu  lililo chakaa sana, niliona sahani juu ya meza, nilimuona paka akiwa ameketi kando ya meza. 

    Paka huyo alikua ametulizana sana, alikua akinitazama kwa macho yake makali ya kung’aa.  Uwepo wa Paka ilikua ni ishara nyingine kua nyumba hii inakaliwa na Mtu, paka hawezi ishi  mahali ambapo hakuna chakula. Nilishusha pumzi zangu huku moyo ukiendelea kunigonga sana. 

    Bado kichwa changu kiliendelea kugonga kwa maswali yasiyo na majibu ya Uhakika, wazo la  kuingia ndani ya nyumba hiyo lilinijia, moyo haukuacha kudunda kwa nguvu, kijasho  chembamba kilikua kinanitoka, nilipoanza kupiga hatua niliingiwa na Ubaridi, kwa nguvu sana  nilivutwa nje na kuzibwa mdomo wangu kisha nikasogezwa pembeni, nikafichwa nyuma ya Ua  moja. 

    Hata nilipojaribu kufurukuta sikuweza kisha nikaisikia sauti ya Caren

    “Shii‼ ni Mimi” aliongea kwa sauti ya kunong’oneza. Aliniachia, hapo hapo kabla sijamuuliza  alifikaje, sote tulimwona Yule Mzee akiwa ameshikilia tochi, alikua akichungulia pale mlangoni  nilipotaka kuingilia, kwa namna nilivyomwona ni kama alihisi uwepo wa Mtu. Alimulika tochi huku na kule lakini hakufanikiwa kutuona kisha aliufunga mlango wa Nyumba yake. 

    Hapo tuliachia pumzi ndefu maana tulikua tumezibana kuhofia asije akatushtukia. 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATU 

    COMMENTS ZIWE NYINGI SASA 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

    riwaya mpya Riwaya Nyumba Ya Majini Kijiweni riwaya za kijasusi riwaya za kusisimua

    32 Comments

    1. Fau the boss on April 25, 2025 4:52 pm

      Firee🔥

      Reply
    2. GLIMENT TWEVE on April 25, 2025 6:46 pm

      Ni nzur saana

      Reply
    3. Hank4749 on April 25, 2025 7:20 pm

      Very good https://lc.cx/xjXBQT

      Reply
      • Sospiter Paulo Samwel on April 25, 2025 11:59 pm

        It is so very good and attractive

        Reply
        • Nailaty on April 26, 2025 10:38 am

          Nasoma naogopa mwenyewe

          Reply
      • Sagent on April 27, 2025 12:44 am

        Dah n 🔥

        Reply
    4. Piana on April 25, 2025 7:47 pm

      👌👌👌

      Reply
      • Karimu on April 25, 2025 10:00 pm

        Hakika ipo vyema 🤗

        Reply
    5. Karimu on April 25, 2025 10:00 pm

      Hakika ipo vyema 🤗

      Reply
    6. Calvin paul on April 25, 2025 10:49 pm

      Hii ni motoo

      Reply
    7. KingzJeelay on April 25, 2025 11:06 pm

      Alooooooo mambo ni🔥🔥🔥 kaka mkubwaaa

      Reply
    8. KingzJeelay on April 25, 2025 11:08 pm

      KAKA MKUBWA EEEEE…
      TUANDALIE NA STORY ZA UJASUSI💂🏽‍♂️💂🏽‍♂️🥷🏽🥷🏽🥷🏽NAZIKUBARI MNOOOO NA NAZITAMANI SANAAAAA💪🏽💪🏽💪🏽💪🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽

      Reply
      • Sumaiya on April 30, 2025 5:51 pm

        Nzurii jmn lkn inanitishaaaaa mpk watu tunamalizaaa bando

        Reply
    9. Jorge2482 on April 26, 2025 5:06 am

      Awesome https://lc.cx/xjXBQT

      Reply
    10. Rebecca1468 on April 26, 2025 3:37 pm

      Very good https://short-url.org/10VGf

      Reply
    11. Hamisi halidi on April 26, 2025 6:14 pm

      Duh💥💥

      Reply
    12. David ben on April 26, 2025 6:43 pm

      Nzuri sana

      Reply
    13. Susana nicholas abely on April 26, 2025 7:44 pm

      .

      Reply
      • Susana nicholas abely on April 26, 2025 7:44 pm

        💯

        Reply
    14. Susana nicholas abely on April 26, 2025 7:44 pm

      ase ni balaa💯

      Reply
    15. Jackson Wasokye Ramazani on April 26, 2025 8:10 pm

      Usiku wa manane huo Caren katokea wapi, kajuaje kama Celin yupo kwenye nyumba jirani ?

      Hii ya moto kwelikweli.

      Reply
    16. Damian170 on April 26, 2025 9:30 pm

      Good https://t.ly/tndaA

      Reply
    17. cathy on April 26, 2025 10:15 pm

      Jmn woiiiiii ya mot san

      Reply
    18. Alhaji Kising'a on April 26, 2025 11:24 pm

      Twende kazii master

      Reply
    19. Trinity921 on April 27, 2025 4:30 am

      Good https://t.ly/tndaA

      Reply
      • Brown on April 27, 2025 8:10 pm

        Type muendelezo

        Reply
    20. Leonel4053 on April 27, 2025 1:55 pm

      Awesome https://t.ly/tndaA

      Reply
    21. hottest trans porn on April 28, 2025 7:22 am

      I’m very pleased to discover this website. I want to to thank you
      for your time just for this wonderful read!! I definitely appreciated every little bit
      of it and i also have you bookmarked to check out new stuff on your site.

      Reply
    22. Frederick174 on April 28, 2025 1:38 pm

      Good https://rb.gy/4gq2o4

      Reply
    23. Cathbert on May 2, 2025 2:52 pm

      Iko poa xnaa

      Reply
    24. Laksana Petir Hk Rabu on May 7, 2025 4:57 am

      Write more, thats all I have to say. Literally, it seems as though you relied on the video to make your point.
      You clearly know what youre talking about, why waste your intelligence on just posting videos to your site when you could be giving us something
      informative to read?

      http://w1.paitowarnasgp.cfd/

      Reply
    25. Prediksi Jitu Togel Cambodia on May 25, 2025 9:00 pm

      Hmm is anyone else having problems with the pictures on this blog loading?
      I’m trying to determine if its a problem on my end or if
      it’s the blog. Any responses would be greatly appreciated.

      http://w2.prediksijitutogel.xyz/

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.