Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Pili-02)
    Hadithi

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Pili-02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaApril 24, 2025Updated:April 27, 202542 Comments9 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi

    Caren alisimama baada ya kuniona simjibu alichokua akinisemesha, nilianza kuhema kwa kasi,  hofu ilikua imenitawala vya kutosha. 

    “Kuna nini Celin?” aliniuliza, nilimjibu Caren kwa sauti ya chini iliyojaa hofu na mtetemo wa  Uwoga uliopitiliza. 

    “Kuna Mtu nyuma yetu” Nilitamani kulia kwa jinsi woga ulivyokua umenishika, Caren aligeuka  nyuma kisha akarejesha macho kwangu. Akaangua kicheko na kuanza kuongea kama mlevi . Endelea

    SEHEMU YA PILI

    “Kumbe umekunywa pombe Celin, Ha!ha! Hakuna Mtu. Ulisema hautumii pombe mbona  umelewa ha!ha!ha!” Haraka niligeuka nyuma, hapakua na yeyote yule, lakini hisia yangu ya  ndani iliniambia yule Mzee analifahamu jambo fulani kuhusu nyumba yetu. Nilitabasamu ili tu  kumfanya Caren aamini kua nilikua nimelewa kidogo. 

    Tuliporudi ndani tulikuta Watu wakiendelea na tafrija hiyo fupi, baadaye mishale kama ya saa  tano hivi walitawanyika na kutuacha Wana Familia pekee, Mimi, Baba na Mama. Kwakua Usiku  ulikua mwingi, Baba akatuambia tukalale, asubuhi tutafanya kazi ya kuweka mazingira sawa.  Mimi niliingia chumbani kwangu, chumba changu kilikua juu. 

    Baada ya kuingia chumbani nilijikuta nikiendelea kufikiria hatua za yule Mzee, bahati nzuri  dirisha langu lilikua likiitazama vizuri nyumba ya yule Mzee, nilisogea taratibu hadi dirishani  kisha nilichungulia, palikua kimya sana. Hapakua na dalili ya Mtu yeyote yule, nilisimama hapo  kwa zaidi ya dakika kumi lakini sikuambulia chochote kile. 

    Nilikata shauri nikaingia bafuni kuoga kisha nilipomaliza nilirudi kitandani na kupumzika. *** 

    Nilichokiona, nilichokihisi kilibakia ndani yangu. Sikupenda kuwaingiza wazazi wangu kwenye  presha ya aina yoyote ile, kama ukweli nitautafuta mwenyewe. 

    Siku iliyofuata ilianza kwa baridi kali sana, nilipaswa kuelekea chuoni. Nilijiandaa, baada ya  dakika kama kumi nilikua tayari kwa ajili ya kuondoka na kuelekea chuoni. 

    Niliwaaga wazazi wangu kisha niliondoka. Nilipofika nje nilipata wazo la kubadilisha njia,  niligeuka na kuelekea upande wa nyumba ya yule Mzee, mara zote nyumba yake ipo kimya.  Hapasikiki sauti ya aina yoyote ile, nilipiga hatua zangu za taratibu nikiwa nimevalia viatu virefu  kama buti hivi, suruali nyeusi na shati jekundu kisha koti la kunikinga na baridi. 

    Nafsi yangu ilizidi kuniambia kua kuna jambo napaswa kulijua kuhusu nyumba yetu mpya, Mtu  pekee ambaye alionesha hisia ya kujua jambo alikua ni huyu Mzee wa ajabu. Basi, nilipofika  aneo la geti lake niliona pameandikwa ‘Mwanzo wa Mwisho’  

    “Mwanzo wa Mwisho?” niliyarudia maandishi yaliyopo getini, nilihema. Yalikua ni maneno  magumu kiasi kwamba sikuelewa chochote kile, hisia mbaya dhidi ya huyu Mzee ilichipua zaidi  ndani yangu. Wakati huo jua lilikua likianza kuchomoza kwa mbali, palikua na mwanga wa  kutosha, upepo wa hapa na pale. 

    Niligeuka kuangalia nyumbani kwetu, kisha nilitazama tena pale getini, sikupata tafsiri ya haraka  haraka juu ya yale maneno. Nilimeza funda zito la mate, nilitazama saa yangu, ilisoma ni saa  2:13 Asubuhi. 

    Niliona bado nina muda wa kutosha kabla ya kuelekea chuoni pengine naweza kuzungumza na  yule Mzee angalau nipate ufumbuzi wa maswali magumu yaliyojaa kichwani pangu. Nilisita-sita  lakini niliweza kugonga geti

    Palikua kimya sana kama sehemu isiyotembelewa na Mtu kabisa. Niligonga tena, nikagonga  zaidi kwa kutumia mkono wangu wa kushoto huku nikisema 

    “Kuna yeyote?” nilikua makini sikutaka wazazi wangu wajue chochote kile, palikua kimya sana.  Nilikata tamaa, sikuona dalili ya kufunguliwa Geti hilo dogo. Nililipa mgongo lile geti kisha  niliondoka hapo, nikasogea Barabara kuu nikapanda treni iliyokua ikielekea katikati ya Jiji, huko  ndiko nilikokua ninasoma. 

    Niliketi siti namba 25, kando yangu alikuwepo Bibi mmoja. Nilimsalimu kwa heshima sana,  baada ya treni kuondoka aliniuliza 

    “Kuna jambo linakutatiza?” sijui aliweza vipi kujua kua nilikua natatizwa na jambo fulani,  niliachia tabasamu kiasi ili kumjibu yule Bibi.  

    “Kiasi, hata hivyo ni jambo la kawaida” nilimjibu, hakusema chochote. Alikaa kimya nami  nilikaa kimya nikisubiria kusikia angesema nini lakini aliendelea kukaa kimya. Dakika kama  kumi hivi, yule Bibi akaniambia 

    “Nashuka kituo kinachofuata, kua makini sana Mjukuu wangu. Unakaribia kupoteza Watu  uwapendao kwa mpigo, kua jasiri. Wakati mwingine Maisha yanatupeleka shimoni makusudi”  Moyo wangu ulilipuka mithiri ya Volkano, simjui yule Bibi. Aliwezaje kuongea maneno mazito  kiasi kile, Watu niliowapenda sana walikua ni Wazazi wangu 

    “Samahani unasemaje?” nilimkujia sura yangu, aliachia tabasamu tu akaniambia 

    “Huwezi kuwaokoa, Hatma imewafikia” maneno yake yalikua mazito sana, kiasi kwamba  yalinifanya nilegee mwili mzima. Nilihisi ganzi moyoni mwangu, huzuni na hisia ya hasira.  Nikiwa ninaendelea kuyarudia maneno yake, mara treni ilikua imefika kituoni, yule Bibi  alishuka kisha alisimama akinipungia mkono wa kuniaga. 

    Moyo uliniuma sana, hata safari yangu ya kuelekea chuoni niliiona kua ilikua nzito sana. Hapo  hapo nikaitoa simu yangu kwenye begi nikampigia Mama yangu kumuuliza kama walikua  salama. Mama alinitoa hofu, hata sauti yake ilionesha palikua shwari kabisa. 

    Pumzi niliyoishusha ilikua kubwa, ilishuka kama gia ya gari. Kifua kilikua kizito, presha siyo  presha, yale maneno yalikua yanazidi kunipigia kelele masikioni mwangu. Ndani ya siku mbili  nilikutana na mauzauza ya kutisha, nilipiga moyo konde nikiamini hakuna anayeweza kuijua  hatma ya Mtu mwingine isipokua Mungu pekee. 

    Nilipofika chuoni, nilikua na maswali mengi kichwani. Nilijiinamia kwenye meza, nilihisi kama  nilikua nimebeba mzigo mzito sana kichwani mwangu. Nikiwa hapo alikuja Caren, akanifanyia  utani ambao haukua kipaumbele kwangu 

    “Una shida gani Celin?” aliniuliza, niliweka mikono yangu usoni, nilitamani kumueleza Caren  lakini sikupata ujasiri wa kufanya hivyo. 

    “Celin, niambie una tatizo gani?” aliniuliza tena, bado nilikua kimya nikimwangalia. 

    “Jana usiku ulikua hivi, unanificha kitu. Hata hivyo nimepewa hii barua nikupatie” Nilishtuka  kidogo 

    “Imetoka wapi?”  

    “Nimepewa na Bibi mmoja hapo nje amesema nikupatie wewe” Nilishtuka sana, niliogopa kisha  nilikimbilia nje ya geti la chuo, nilitazama huku na kule kama ningemwoma huyo Bibi, nilikua  na uhakika huwenda ni yule Bibi niliyekutana naye kwenye Treni muda mchache uliopita. Mara  Caren alifika 

    “Sikuelewi Celin, kuna nini?” aliniuliza, nilimsogelea nikiwa nina hisia ya hofu na Mashaka  makubwa. 

    “Yupoje?” 

    “Mwembamba, amevaa koti la suti lililochakaa. Gauni la bluu, halafu amevalia raba chini” sifa  alizozitaja Caren zilifanana na sifa za yule Bibi niliyekutana naye kwenye treni. 

    “Caren kuna kitu hakipo sawa, nilikutana na huyo Bibi kwenye treni. Ameongea maneno ya  kutisha sana, nipe hiyo Barua” Haraka Caren alinipatia Barua kisha niliifungua haraka,  nilikutana na karatasi nyeupe iliyoandikwa jina moja ‘ZENA’ 

    “Zena” nilisema kwa hofu, nilirudi nyuma nyuma nikiwa nina hofu hadi pale nilipofika mwisho  nikakutana na ukuta wa uzio wa chuo, Caren alisogea naye akiwa kwenye Mshangao mkubwa  sana. Jina la Zena liliandikwa kwa herufi kubwa na wino mwekundu. Chozi lilikua linanitoka  huku ile kauli kua nitapoteza niwapendao kwa Mpigo ilikua ikijirudia akilini mwangu. 

    Zena ni rafiki yetu, tokea nimefika chuo sikumwona. Nikamuuliza Caren 

    “Umemwona popote?” 

    “Nani?” 

    “Zena” 

    “Hapana, nilijaribu kumpigia nilipofika chuo lakini simu yake ilikua ikiita tu. Hebu niweke wazi  kuna nini?” Caren aliniuliza kwa hofu huku akiweka mikono yake kichwake pake, alikua njia  panda nami sikua na muda wa kumweleza zaidi. 

    “Twende kwake Caren, tafadhali twende” nilisema huku chozi likizidi kunibubujika. Nilikua na  uchungu moyoni mwangu, nilianza kuwa na wasiwasi kua kuna jambo lililomfika zena. Maneno  ya yule Bibi yalizidi kujirudia akilini mwangu. Nilisimamisha Taxi haraka, tuliingia kwenye Taxi  huku Caren akinilazimisha niseme kinachoendelea, nilikua ninalia tu.

    “Sasa Celin, usiposema nitajua nini. Yule Bibi ni Nani yako, kwanini amekutumia Barua yenye  jina la Zena?” aliniuliza Caren alikua amejawa na hofu, wasiwasi kwa pamoja. Niligeuka  kumtazama huku chozi likinibubujika  

    “Sali, lisimfike lolote. Dunia inanigeuka Caren” nilisema kwa Uchungu, sikuweza kuongea  zaidi. Nilihisi uzito uliopitiliza, nilihisi kuchanganikiwa huku sura na maneno ya yule Bibi kizee  yakizidi kuendelea kutembea kichwani kwangu.  

    Zena alikua anaishi kilomita chache kutoka pale chuoni, wastani wa nusu saa tulikua  tumeshafika mahali alipokua amepanga. Niligonga geti kwa nguvu kisha tulisubiria kwa sekunde  kadhaa kisha geti lilifunguliwa na Mama mwenye nyumba. 

    Alionesha tabasamu mbele yetu sababu alikua akitufahamu, tulikua tukienda hapo mara kwa  mara lakini safari hii hakuna aliyerudisha tabasamu. Tulimpita kama wanariadha wa mbio ndefu  za Marathon, breki tulifunga mlangoni kwa Zena 

    Tulisimama kwa sekunde kadhaa za kuhesabu, mlango ulionekana kua wazi sababu palikua na  upenyo mdogo. Tulitazamana, sura ya Caren ilijaa maswali mengi yasiyo na Majibu, sikuweza  kumweleza chochote kile hadi muda huo. 

    Nilipopiga hatua kuusogelea mlango, Caren alinishika mkono akaniuliza 

    “Nini kinaendelea Celin?” Alianza kuniuliza kwa sauti ya chini iliyojaa kilio cha hisia kali ya  hofu na woga kwa pamoja. Ni kama Caren alikua amenielewa, nilitikisa kichwa kumdhihirishia  kua Zena alikua shidani. Chozi lilikua likitububujika, nyuma yetu alifika Mama mwenye nyumba 

    “Mabinti, kuna nini?” aliuliza yule Mama Mtu mzima, ndiye mmiliki wa nyumba ambayo Zena  alikua amepanga kwa ajili ya masomo ya Chuo. Niligeuka kumtazama huku chozi likinibubujika,  naye Mama akautazama Mlango wa Zena, akiwa kama Mtu mzima alikua ameelewa kua Zena  alikua matatizoni na pengine alikua ameshakufa.  

    Macho yake pia yalimlenga kwa Mchozi. Nilielekeza macho yangu mbele kisha niliufungua  mlango taratibu, nikautosa mguu wangu ndani ya chumba, nilichokiona kilinifanya nipige yowe  kali la kuchanganikiwa. 

    Kila mmoja wetu aliingia kushuhudia kile ambacho macho yangu yalikuwa shuhuda wa kwanza.  Zena alikua akining’inia kwenye kitanzi cha Khanga kilichofungwa kwenye feni, alikua  akizungushwa huku na kule kama Mzigo usio na thamani tena, ama kweli utu wa Mtu ni uhai  wake 

    Zena alikua amekufa muda mrefu sana, binafsi nililia kwa uchungu sana. Mama mwenye  nyumba akakimbilia kumwita Mjumbe na mwenyekiti wa Mtaa. Bila hata kutumia vipimo  walithibitisha kifo cha Zena, rafiki aliyenipokea chuoni na kunifundisha Maisha ya Chuo jinsi  yalivyo.

    Tulipishana Mwaka mmoja wa kuingia chuoni, alinitendea wema kila nyakati. Hata wakati  ambao alipaswa kufurahi alinipa furaha yake na kisha yeye alibakiwa na huzuni yangu.  Nilimwona akiwa anafunguliwa kutoka juu ya feni akiwa amevalia gauni lake jekundu. 

    Hakika maneno ya yule Bibi yalianza kutimia, nilimpoteza mmoja nimpendaye. Nilijiegemeza  ukutani nikilia kwa kwikwi nikiushuhudia mwili wa Zena ukiondolewa na Askari Polisi  waliokua hapo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa. 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATU 

    COMMENTS ZIWE NYINGI SASA 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

    riwaya mpya Riwaya Nyumba Ya Majini Kijiweni Riwaya Ya Kisasi Changu riwaya ya koti jeusi riwaya za bure riwaya za kijasusi

    42 Comments

    1. Jeannette4357 on April 24, 2025 7:05 am

      Very good https://shorturl.at/2breu

      Reply
      • Atiya on April 24, 2025 7:35 pm

        Mh atali

        Reply
    2. Wasokye Ramazani on April 24, 2025 10:17 am

      Mmmm, hii noma, hachia kipande kingine tuone nani anafata kufa baada ya ZENA, Hooo Zena R.I.P !!!

      Reply
    3. Neema gervas on April 24, 2025 4:03 pm

      Hatari💐💐

      Reply
      • Aura on April 24, 2025 7:49 pm

        Daah 😞🥺🥺 zena R.I.P who is next 🥺
        Achia nyingine kijiweni tupo pamoja

        Reply
    4. Rio on April 24, 2025 7:09 pm

      Daah hii kalii

      Reply
    5. alle on April 24, 2025 7:11 pm

      imeanxa kaa story naona imeanza kugeuka kua zile hallowin movieza wazungu 😂😂

      Reply
      • Aura on April 24, 2025 7:50 pm

        Daah 😞🥺🥺 zena R.I.P who is next 🥺
        Achia nyingine kijiweni tupo pamoja km

        Reply
        • Alvin audax on April 24, 2025 8:10 pm

          Daah!bonge la storry

          Reply
      • Salama on April 26, 2025 12:23 pm

        ❤️

        Reply
    6. Manka on April 24, 2025 7:33 pm

      Ooh I can’t wait

      Reply
    7. Manka on April 24, 2025 7:34 pm

      OMG 😳

      Reply
    8. Aura on April 24, 2025 7:46 pm

      Daah 😞🥺🥺 zena R.I.P who is next 🥺
      Achia nyingine kijiweni tupo pamoja

      Reply
    9. Zoulovie_store on April 24, 2025 8:17 pm

      Duuuuh

      Reply
    10. Yuster on April 24, 2025 9:46 pm

      Dunia inamgeuka Celin

      Reply
    11. Karimu on April 24, 2025 10:14 pm

      Aah hakika ipo vyema🤗

      Reply
    12. Çlãssïçjr_10 on April 24, 2025 10:25 pm

      Kama muvi flani ivi 😂
      Dondosha cha tatu

      Reply
      • Abdallah Tenge on April 25, 2025 8:02 pm

        Duuuu

        Reply
    13. Alhaji Kising'a on April 25, 2025 12:34 am

      Hakika utu wa mtu ni uhai wake.

      Reply
      • Abdallah Tenge on April 25, 2025 8:04 pm

        Ntakutafuta mkuu tuandae bajeti tufanye movie hii story

        Reply
    14. KingzJeelay on April 25, 2025 5:12 am

      Mwanzoni nilihofia nikajua ni wazaz wake❤️‍🔥❤️‍🔥
      Anewei RIP Kwa Zena na pole Kwa Celin..
      Mola ampe ujasiri kwakwel.🥲🥲🙄🙄

      Reply
    15. Crystal859 on April 25, 2025 5:34 am

      Good https://lc.cx/xjXBQT

      Reply
    16. Astery Komba on April 25, 2025 8:11 am

      hii nimeikubali

      Reply
    17. sara g on April 25, 2025 11:31 am

      Nomaah san jmn R.I.P zenaa joomn

      Reply
    18. Posiano on April 25, 2025 4:20 pm

      Nimeipenda iko vizur sana mkuu

      Reply
      • Ole mbuzi on April 25, 2025 5:21 pm

        Amini hiki chuma

        Reply
        • Sumaiya on April 30, 2025 5:45 pm

          Jamn inatishaaaa km tamthiliya vile mmh kweli maisha ni uhai

          Reply
          • Justin Peter on April 30, 2025 11:27 pm

            Halafu mm naisoma usiku 🥷

            Reply
    19. Ole mbuzi on April 25, 2025 5:20 pm

      Aah hii riwaya ni nzuri sana ina mafunzo makubwa sana ndani yake.

      Reply
    20. Hamisi halidi on April 25, 2025 6:42 pm

      Mbona inaogopesha

      Reply
    21. G shirima on April 26, 2025 8:09 pm

      Kwani ufalime wa zombie imeishia wap

      Reply
    22. Anastasia1774 on April 29, 2025 12:50 pm

      Very good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    23. Warren1037 on April 29, 2025 2:26 pm

      Awesome https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    24. Greyson4045 on April 29, 2025 8:02 pm

      Very good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    25. Marc874 on April 30, 2025 3:15 am

      Good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    26. Omar4331 on April 30, 2025 7:08 pm

      Very good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    27. Justin Peter on April 30, 2025 11:25 pm

      🤔🙆

      Reply
    28. Emily1797 on May 1, 2025 12:33 am

      Awesome https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    29. Cathbert on May 1, 2025 10:20 am

      Nyumba ya kununua sio mzuri sana
      Bora ukajenge ya kwako tu..

      Reply
    30. Terrence1625 on May 1, 2025 10:30 am

      Very good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    31. Marley1596 on May 1, 2025 2:30 pm

      Very good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    32. Emanuely Daudy on May 5, 2025 11:18 pm

      Iko powa sana tatu please

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.