Ilipoishia “Shiiiโผโ Baba Mkwe akanipa ishara katili ya kunitaka nikae kimya vinginevyo kile kisuย kingeingia mwilini mwangu. Kisha akachuchumaa na kuniambia
โLeo utajuwa ni kwanini uliolewa Bintiโ Alisema halafu akayaongea maneno fulaniย nisiyoyaelewa, nakumbuka kabisa hayakuwa maneno ya lugha ya Kiswahili bali lughaย nisiyoifahamu na wala si Kiingereza wala Kiarabu. Wale Watu wakasimama kisha wakaendaย kupotelea kwenye kona za kile chumba kilichojaa harufu ya Udi. Endeleaย
SEHEMU YA NNEย
Nilikua kama naangalia filamu vile, hata wewe msomaji unaweza fikiria ilikua ni filamu naย ninakusimulia hapa. Hapana ni Simulizi ya kweli, simulizi hii ikusaidie kufanya chaguo sahihiย wakati wa kuolewa au Kuowa ili usije pitia kama Mimi, haya mambo siyo tu kwa Mwanamkeย hata Mwanaume anaweza tendewa hivi. Tuendelee sasaย
Mate hayakumezeka wala pumzi hazikutulia, yule Mzee alikua amenikata jicho kali kishaย kaniambia kwa maneno yenye vituo vingi kuashiria kuwa anamaanisha anachokisema,ย akaniambiaย
โUmeolewa ili uje kuishi na Misukule hapa, huu ndiyo utajiri wangu. Wewe siyo wa kwanzaย kuolewa na Salehe, walioenda kinyume walifia humu na kupotea kabisa wao pamoja na Familiaย zaoโ Yaani nilizidi kuishiwa nguvu, Mungu wangu jasho lilinitoka kama nimemwagiwa maji.ย Kisha Mzee akaendeleaย
โHii ni nyumba yangu Mimi siyo ya Salehe, yule ni Mtoto wangu na ndiye anayenisaidia Mimi.ย Utakua unafanya mapenzi na Msukule mmoja mmoja Kila baada ya Siku tatu. Usijaribuย kutoroka ndani ya nyumba hii wala kutoa siri popote, narudia kwa Msistizo ili ueleweย ninachomaanisha. Utawaponza Wazazi wako kwa Ujinga wako mwenyeweโ Chozi lilizidiย kunitoka kisha yule Mzee akasimama akaninyooshea Kidoleย
โUtafanya niyatakayo ili kuilinda familia yako, hutaruhusiwa kutumia simu na hutatoka njeย isipokua kwa maagizo maalum kutoka Kwanguโ kisha yule Mzee aliondoka zake na kunichaย ndani ya kile chumba, wala hakunifungia kuonesha kuwa anajiamini na anachokisema. Kiukweliย Nililia sana kwa kwikwi, nililia Mno sababu niliona wazi kuwa ili wazazi Wangu wawe salama napaswa kutumikia Misukule ya yule Mzee na kama nataka kuwa huru basi nitawapoteza Wazaziย wangu ambao hawakuwa na Hatia yoyote ile.ย
Katika Maisha yangu niliutunza usichana wangu kwa ajili ya Mume wangu lakini nililazinikaย kuutoa kwa Misukule, nilijilaumu kwa kumwamini Salehe, nilimlaani sana. Nikiwa ninaliaย akaingia tena yule Mzee akiwa amehamaki akaniulizaย
โSimu yako ipo wapi?โ alishikilia kisu mkononi, sikupepesa maneno nilimpa simu mara mojaย kisha akaondoka nayo. Wala hakufunga mlango aliuwacha wazi ikiwa ni ishara ya kuniruhusuย kuwa huru ndani ya nyumba lakini siyo kuondoka, ndiyo kwa mara ya kwanza katika Maishaย yangu niliushuhudia Uchawi wa waziwazi.ย
Basi, nilirudi chumbani nikiwa ninalia, nilikua mwenyewe kwenye Maisha yangu. Sikuwa naย Mtu wa kumueeleza ninayopita, sikuwa na msaada na pengine kaburi langu lingekuwa ndani yaย ile nyumba. Kitu cha kwanza kufanya kilikua ni kufuta chozi langu, kwanini niliruhusuย lidondoke chozi langu lenye thamani kubwa. Hata ningelia vipi isingelisaidia Mimi kuponaย ย
Nilijiegemeza kwenye Mto nikatafakari mengi, nikapata jibu la uhakika kabisa kuwa siku ileย nilifanya mapenzi na Msukule na ndiye aliyenitoa Usichana wangu kwa mara ya kwanzaย nikifikiria ni Salehe. Kitu fulani cha uchungu kilijaa kifuani pangu, hakika nilitendewa unyamaย sana na Salehe na Baba yake. Nilijua Baba na Mama wangekuwa na wasiwasi na Mimi kamaย nitakaa kwa siku nyingi pasi na kuwasiliana nao lakini ningefanya nini sasa na ilinibidi nikae naoย mbali ili kuokoa Maisha yao.ย ย
โEeh Mungu, umeniptisha kwenye Mtihani gani sasa. Hukuona mitihani mingine rahisi kwanguย isipokua huu?โ Nilituma lawama ma maswali kwa Mungu wangu, kumbe ukiona Mtuย anamkufuru Mungu si kwa kutaka bali kwa kukosa majibu sahihi ya kuondoka kwenye matatizo.ย ย
***ย
Masaa yalienda, sikupata hata lepe la kuusingizia Usingizi yaani nilikua na kichwa kizito sanaย japo Usiku ulikua umeenda. Hakuna sauti ya kutisha niliacha kuisikia Usiku huu, yaani Mzeeย Mwinyimkuu alinionesha Uchawi dhahiri kabisa. Sauti za Watoto Wachanga nilizisikia bilaย kificho, nyimbo za ajabu ajabu ziliimbwa na kuchezwa nikajiona kama nimeshafika kuzimu.ย Nikazikumbuka Riwaya kadhaa nilizokua nazisoma mtandaoni na stori za hapa na pale juu yaย Uchawi, nilikua siziamini lakini hatimaye nilijikuta ndani ya moja ya Riwaya ya kutisha sana.ย
Mimi Saida nilikosa majibu ya maswali yote hata yale madogo niliyojiuliza. Bundi walisikikaย Usiku kucha, hadi kuna pambazuka nilikua macho hata taa sikuizima kwa kuhofia kuingiliwaย tena na yule Msukule. Kukesha macho usiku mzima haikua rahisi, macho yalivimba hasaย ukizingatia nililia sanaย
Niliogopa kutoka chumbani, sikuwa na amani kama siku ya kwanza. Nilikaa kitandani nikipigaย Mihayo, mara Mlango uligongwa, nilishtuka nkasema moyoni sasa naenda kupelekwa kwaย Misukule, hofu ikaamka upya ndani yangu lakini nikamsikia Mzee Mwinyimkuu akisemaย
โAmka uandae chai harakaโ alisema kwa jazba fulani baada ya kugonga kwa kitambo kishaย nikayasikia makubhasi yake yakifanya safari kutoka mlangoni kwangu. Moyo ulinidunda sanaย kiukweli, sikuwa na raha wala amani yoyote ile. Ningefanya nini zaidi ya kuamka na kwendaย kumwandalia chai yule Mzee, Binafsi sikuhisi njaa kabisa licha ya kutokula jana kutwa nzima.ย
Niliufungua Mlango taratibu sana, nikasikia kama Mtu anafanya Usafi hivi, nilipoangalia vizuriย niliona tu ufagio pekee ukifagia bila kumwona aliyeushikilia ule ufagio, nusura nizame tenaย ndani kwa woga lakini nikapata kiu ya kuona zaidi. Huuuโผ! Uchawi unatisha sana naย nimeushuhudia laivu bila chenga, niliporudisha macho tena sikuona chochote isipokua nyumbaย ilikua safi sana
Basi nikaanza safari fupi ya kupita koridoni na kuelekea jikoni kuandaa chai ya Mzeeย Mwinyimkuu. Ile naingia tu nikakutana naye ndunda ndunda.ย
โMuda wote ulikua unafanya nini wewe?โ aliniuliza kwa hasira sana kama vile tulikuaย tumegombana. Hofu ilinianza upya hata sikuweza kutoa sauti yoyote ile, nikainamia chini,ย Jamani nilikuja kushtukizwa na kibao cha shavu la kushoto hadi nikahisi giza. Alinipiga kibaoย kizito hadi nikapepesuka pembeni, mateso makali yalianza kwanguย
Sikuweza kutoa sauti yoyote ile isipokua chozi na maumivu yaliyojaa ndani ya Moyo wangu.ย
โUsiniletee upumbavu, hukuja kulala hapa wala kutembea. Kumbuka maneno yangu, Utafiaย humu ukileta kiburi, pesa hii hapa Nunua chapati urudi harakaโ alisema Mzee Mwinyimkuu,ย akanipa Elfu tano mpya kabisa. Kisha yeye aliondoka zake akaelekea sebleni, alionekanaย anajiamini na maneno yake ndiyo maana aliniruhusu nitoke nikamnunulie Chapati, wakati natakaย kutoka akapaza sauti yake akaniambia ninunue chapati za hela yoteย
Sikuwa na maswali mengi kuwa chapati zinaenda kuliwa na Nani sababu hata ule Mchichaย nilikua na uhakika kuwa unaliwa na Misukule niliyoiona Usiku. Nilihisi kukonda kwa siku mojaย tu ya hekaheka, nilitoka nikafungua geti kisha nikatoka ndani, taratibu nikawa naeleka kwa yuleย Mama anayeuza Chapati nyumba kama ya Nne hivi kutoka nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu.ย
Macho yangu yaliitazama sana ile nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, nje Watu walikuaย wakiendelea na shughuli zao, niliamini hakuna anayejuwa kinachoendelea. Nilitamaniย nimsimulie Mtu pengine nimwombe msaada lakini nikakumbuka onyo nililopewa na Mzeeย Mwinyimkuu, Ah! Hamu iliniisha……….ย
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TANO YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx
15 Comments
Duuuh kuna kitu cha kujifunza apa
Ndo Iko nilichowambia ndo Cha kujifunza
Gud gud
Kwaiyo apo mabinti mjufunze msitunze bikra nadhan nyie wenyewe mmejionea kwa mwenzenu Saida YANGU NI AYO
Jamani Saida hadi huruma๐๐
Uchawi upo kweli tuwe makini na wanaume watakao tuowa
Simulizi ya vitisho yenye maajabu na mafunzo makubwa kwa wanwake na wanaume wanaopenda Mimama.
Huwezi jua tabia za mtu hvihvi tu
Salehe Namba mbili ni Wewe
Ya Leo fupi sn Admin jmn Hila ianzidi kunoga . Nawza tu Saida kwann anashinda ht kusema MUNGU nisaidie . Dah! Hapo kwenye kuwapa misukule kwa zamu shindwa shetani .๐คญ
Sa itakuwaje
Yaleo fupi sna boss
Wendelezo kak
Kikubwa kuomba Mungu
nc4vte
if7dcv
hrr09y