Ilipoishia “Desmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwaย na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha Desmondย alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafikaย eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawaย huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake Noelaย
“Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” Aliulizaย
“Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee naย majukumu mengine”ย
“Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingiaย kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na piaย ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipangaย kuonana na Noela. Endelea
SEHEMU YA PILI
Waliagiza chakula kwa pamoja kisha walianza kula hukuย wakizungumza masuala yao ya kimapenzi, japo Desmond alikuwaย akicheka ila akili yake ilikuwa kule Hospitalini alipo Mkeย wake, ucheshi wa hapa na pale uliendelea huku wakinyweshanaย na kulishana, ghafla simu ya Desmond iliita, kutokana na hofuย aliyonayo alijikuta akiangusha glasi ya Juisi ikamwagikiaย kwenye nguo ya Noelaย
“Oooh samahani mpenzi naomba nipokee simu” Alisema Desmondย
“Usijali Joshua, naenda chooni mara moja” Alisema Noela kishaย alinyanyuka akaelekea chooni kwa ajili ya kujisafisha.ย
Aliingia chooni akajisafisha vizuri lakini wakati anatokaย alikutana na Nesi Lucia, walikuwa ni marafiki wa zamani sana,ย basi walipoonana walikumbatiana kwa furahaย
“Eeeh za Maiaka Noela?” aliuliza Luciaย
“Nzuri, jamani Lucia umekuwa mzuri hivyo jamani” Alisemaย Noela kisha alimkumbatia tena Luciaย
“Oooh Miaka mingi imepita Maisha yapoje?” aliuliza Luciaย
“Mungu anasaidia, kuna kipindi nilisikia umekuwa Mwanasheriaย mzuri sana Nchini”ย
“Yeah!! Mimi ni Mwanasheria pia mpelelezi nina kampuni yanguย Binafsi japo bado nipo serikalini, wewe je?” Alisema Noelaย kisha alitupa swali kwa rafiki yake huyo wa zamaniย
“Namshukuru Mungu mimi ni Nesi napambana na wagonjwa” Alijibuย Lucia kisha walicheka kwa pamoja, walipeana namba za simuย kisha Lucia aliulizaย
“Kumbe unakujaga hapa kula?”ย
“Ndio mara nyingi sana ila leo nipo na Shemeji yako”ย
“Oooh! natamani kumuona jamani, hapana shaka ni mzuri kamaย wewe mwenyewe” Alisema Luciaย
“Ha!ha!ha! hujaacha utani tu, haya twende ukamuone” Alisemaย Noelaย
“Haya twende mara moja, ni muda sana aisee kweli Maishaย yanabadilika” Alisema Lucia kisha stori zao zingineย ziliendelea, Desmond alikuwa bize na simu hivyo hakujuwa kamaย Mpenzi wake ameongoznaa na nesi anayemuhudumia Mke wakeย Hospitalini.
Bahati nzuri ile anageuka anawaona Lucia na Noela wakiendaย alipo, Desmond aliinama chiniย
“Ina maana Nesi Lucia na Noela wanafahamiana, ooohย nimeshaharibu hapa, vipi kama Lucia akimwambia Noela kuwaย nina Mke?” alijiuliza Desmond, aliponyanyua tena kichwaย alimuona Noela akiwa peke yake, alishangaa sana wakatiย sekunde chache alikuwa ameongozana na Lucia, Noela aliketiย
“Mwenzio yupo wapi?” alihoji Desmond kwa umakini sanaย
“Ni rafiki yangu yule kumbe ulimuona, anaitwa Lucia ni nesi,ย nilisoma naye kitambo” Alijibu bila wasiwasi Noela lakiniย hakutatua kiu ya Desmond ya kutaka kujuwa alikuwa ameendaย wapiย
“Yupo wapi sasa?” Alihoji Desmondย
“Amepigiwa simu kuwa kuna Mgonjwa amerudisha fahamu hivyoย ameelekea Hospitali” Kusikia hivyo Desmond alijuwa moja kwaย moja ni Mke wake Mandyย
“Amerudisha fahamu, hajataja chochote?” aliuliza Desmond kamaย Mtu aliyeingiwa na kichaaย
“Kutaja chochote? Nani unamzungumzia”ย
“Aah samahani, siwezi kuendelea kuwa hapa mpenzi” Alisemaย Desmond kisha aliondoka hapo mbio mbioย
“Hivi huyu Mwanaume anan nini siku hizi mbona amekuwa naย tabia za hovyo? mara hapokei simu mara anazungumza vituย sivielewi” Alijiuliza Noela kwa sauti iliyoambatana na kilioย kidogo.ย
Haraka haraka Desmond alifika Hospitalini ambako Mandyย alikuwa amelazwa, alikuwa amechoka mwili na akili yote hukuย hofu yake ikiwa kwa Mandy kuwa ameamka, alipofika wodiniย alimkuta Mandy akiwa amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua,ย pembezoni kukiwa na daktari, wahudumu wote wa afya ndani yaย Hospitali hiyo walikuwa wakimfahamu Desmond, yule Daktariย alimuulizaย
“Mbona upo hivyo Desmond” Aliuliza akiwa anafanya kazi yake,ย Desmond alitikisa kichwa chake kisha alitoka wodini humoย akiwa amechoka sana, kiasi fulani alishusha pumzi zake baadaย ya kugundua kuwa Mandy alikuwa hajazinduka, alishika sehemuย ya moyo wake kama ishara ya hali yake ya wasiwasi.ย
************
Jioni Noela aliporudi nyumbani kwao alijikuta akikosa raha,ย mvua ilikuwa ikinyesha hivyo alijifungia chumbani kwake,ย alianza kupitia mafaili ya kazi zilizo mbele yake. Kilaย alichokisoma hakikuingia kwenye akili yake, alijiona anaย mzigo mzito kichwani pake.ย
Alijilaza kitandani akiwa hoi kwa mawazo, Desmondย alimchanganya sana kwa jinsi alivyobadilika ghafla, hakujuwaย jambo zito lililo kichwani pa Desmond ambaye yeye alikuwaย akimfahamu kama Joshua, wakati anawaza baadhi ya mamboย alijikuta akikumbuka tukio la mchana alivyokutana na rafikiย yake wa zamani ambaye ni nesi Lucia. Alifikiria amtafuteย maana baada ya kupeana namba ule mchana hakuna aliyemtafutaย mwenzake, alinyanyua simu yake akampigia, simu iliita kwaย kitambo kidogo kabla ya kupokelewa.ย
“Hello Lucia” Alisema Noelaย
“Abee kipenzi! nilitingwa kidogo nikasema nikutafute baadaye”ย Alisema pia Luciaย
“Oooh nafikiri hiyo baadaye ndiyo hii, hebu subiri vipi haliย ya huyo Mgonjwa wako uliyemkimbilia?” Aliuliza Noela maanaย alipoachana na Lucia ule mchana alikuwa alikimbilia Hospitaliย
“Namshukuru Mungu anaendelea vizuri sana, sijui shem wanguย japo sikubahatika kuonana naye” Alisema Luciaย
“Naye yuko poa Lucia, usijali utamuona siku moja” Alisemaย Noelaย
“Anaitwa Nani vile?” aliuliza Lucia, Noela alikaa kimya kwaย sekunde chache kisha akamjibuย
“Anaitwa Joshua”ย
“Ohooo ana jina la kipekee, natumaini ni mzuri kama wewe”ย Alisema Lucia kisha wote walicheka kisha waliagana kwaย kutakiana jioni njema na mara moja simu ilikatwa.ย
Noela alishusha pumzi zake, angalau kidogo alijiona hanaย mzigo mzito kichwani.ย
Mara mlango wa chumba chake uligongwa, alijisomba kitandaniย akaenda kuufungua, alikuwa ni Mama yake aliyezoea kumuitaย Mlamiย
“Vipi Mlami?” Alihoji Noela, alimtazama Mama yake alikuwaย ameshikilia kikombe cha Maziwa
“Na hii baridi nimekuletea maziwa ya moto Binti yangu, vipiย ulizungumza na Joshua?” Aliuliza Mama yake Noela akiwaย anampatia Noela kikombe chenye maziwa, Noela alikipokea kishaย alimjibu Mama yake akamwambiaย
“Ndiyo Mama! Lakini Joshua siku hizi simuelewi elewi” Alisemaย kisha alipiga maziwa kidogoย
“Humuelewi? Kwani amekuwaje!” Aliuliza Mama Noelaย
“Wee Mlami acha tu, nitakueleza vizuri Mama. Nikutakie jioniย njema” Alisema Noela kisha alifunga mlango, hali hiiย ilimfanya Mama yake Noela kupata mawazo ya jambo lipiย lililokuwa likimsibu Binti yake.ย
Siku iliyofuata mapema sana Desmond alikuwa ofisini kwakeย akiendelea na kazi, alionekana kuwa bize sana siku hiyoย kuliko hata kawaida yake. Akiwa anaendelea na kazi alisikiaย simu yake ikiita, alipotupa macho kwenye kioo aliona niย askari ambaye alikuwa alichunguza tukio la kifo cha Mamaย Mandy ambaye alionana naye kule Hospitalini, ndiye aliyekuwaย akimpigia Desmond. Aliishika simu akiwa ana tafakari hukuย akijiuliza askari huyo alikuwa akitaka kusema nini?ย
“Kwanini ananipigia leo?” Alijiuliza huku simu ikizidi kuita,ย aliweka sauti vizuri kisha aliipokeaย
“Hallo” Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa umakini wa hali yaย juuย
“Mr. Desmond, mtuhumiwa namba moja wa kifo cha Mama Mandyย ameonekana kwenye kijiji kimoja kinachoitwa Pendahili ambachoย kipo kaskazini mwa Mkoa jirani, tukimpata yeye tutakuwaย tumepata ufumbuzi wa kesi hii” Ilisikika sauti ya Askariย huyo, Desmond alishtuka sana akaulizaย
“Unamaanisha Sanga?”ย
“Ndiyo! Mfanyakazi wenu wa ndani aliyepotea baada ya tukioย lile lililopelekea Mkeo kuwa katika koma”ย
“Amekamatwa?”ย
“Bado hajakamatwa ila tayari tumetuma polisi kuelekea hukoย sasa hivi” Alisema Askari huyoย
“Haya asante kwa taarifa” Alisema Desmond kisha alikata simuย hiyo haraka sana
“Sanga anawezaje kurudi Kijijini kwao wakati tulikubalianaย aende mbali?” Alijiuliza Desmond akiwa ameshikilia simu yake,ย akakumbuka jinsi ilivyokuwa siku ya Tukioย
Alikumbuka jinsi alivyokuwa akiongea na Huyo Sanga ambayeย alikuwa ni mfanyakazi wao wa ndani wakati huo Mwili wa Mandyย ukiwa katika ngazi ukivuja damu. Desmond alikuwa ametapakaaย damu mikononi, alimwambia Sanga akiwa katika hali yaย Kuchanganikiwa sanaย
“Polisi watakuja hapa watakukamata Sanga kwasababu kuanziaย sasa wewe ndiye Muuwaji uliyemuuwa Mke wangu! Ukikamatwaย utaozea jela, nakupa pesa uwende mbali sana na usirudi”ย Alisema Desmond kisha alipandisha juu akarudi na kiasiย kikubwa cha pesa akampa Sangaย
“Kumbuka hupaswi kwenda Kijijini kwenu wala kujulikana mahaliย ulipo” Sanga naye alikuwa amechanganikiwa alipokea pesa hizoย kisha alikimbia nyumbani hapo, kisha Desmond aligeukaย akamtazama Mke wake ambaye aliamini alikuwa amekufa,ย alichukua bastola akajipiga begani, aligumia kwa maumivuย akajilaza chini kisha akapiga simu polisi, walipofika polisiย Desmond aliwaambia polisi hao kuwa aliyefanya matukio hayoย alikuwa ni Mfanyakazi wao wa ndani aliyeitwa Sanga.ย
Tokea siku hiyo Sanga aliyafutwa kila kona huku akihusishwaย na tukio la kutaka kufanya jaribio la kumuuwa Mandy pamoja naย Desmond, tukio hilo likahusishwa kitaalam na ufichaji wa siriย ya kifo cha Mama Mandy ambacho kilitokea miezi miwiliย iliyopita kabla ya tukio hilo.ย
Desmond alimaliza kukumbuka kisha alisemaย
“Sanga ukikamatwa utatoa siri ya ulichokiona, sitoruhusu hiloย litokee” Mara moja Desmond aliondoka ofisini hapo akachukuaย gari yake akaanza safari ya kuelekea kwenye kijiji hichoย ambacho alitokea Sanga. Aliendesha gari kwa spidi sana iliย awahi kabla ya polisi kumkamata Sanga.ย
Upande wa pili, Noela alikuwa akimpigia simu sana Desmondย bila mafanikio ya kupokelewa kwa simu hiyo hali iliyomfanyaย azidi kuwa na wasiwasi na mpenzi wake huyo, alimuita Zandaย akampa kazi ya kumtafuta Desmond kwa njia ya mtandao iliย ijulikane mahali alipo Desmond, hofu na mashaka vilianzaย kumuingia Noela huku akitafakari mpenzi wake huyo alikuwaย akipitia jambo gani maana alikuwa haeleweki, ndani ya dakikaย kadhaa mtandao ulionesha alipo Desmond, alikuwa akitoka njeย ya Jiji hilo.
“Aaas!! Anaenda wapi!?” Alijiuliza sana Noela kisha alichukuaย kibegi chake akaondoka ofisini hapo.ย
Safari ya Desmond kuelekea Kijijini ilizidi kusonga mbele,ย lengo likiwa kumzuia Sanga asiingie mikononi mwa polisi,ย alizidi kuunguza mpira kwa spidi kali sana.ย
Ndani ya masaa matano Desmond alifanikiwa kufika Kijijiniย hapo.ย
Alikijua vizuri kijiji hicho sababu yeye ndiye aliyemfuataย Sanga akawe mfanyakazi, alivalia kofia kisha alishuka kwenyeย gari yake, mbele aliona gari yenye nembo ya polisi hivyoย alitambuwa fika kuwa polisi walikuwa wameshafika eneo hilo,ย alijitahidi kutembea kwa tahadhari huku macho yake yakiangazaย huku na kule, bahati ilioje kabla hata hajafika nyumbaniย anakoishi Sanga alimuona Sanga akiwa amejificha sehemu,ย hapana shaka hata Sanga alihitaji kuwakwepa askari hao. Machoย ya Sanga na Desmond yaligongana kisha haraka Desmond aliendaย hadi alipojificha Sangaย
“Umefanya nini Sanga?” Alihoji Desmond akiwa amejificha hapoย na Sangaย
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATU
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Painย
15 Comments
Dah ๐ aisee tamu sana jmn
Kazi nzur sana kaka
Hadithi imeanza kupamba moto
Asante sana Kaka Mkubwa
Nimekuwa nikijifunza mengi kupitia simulizi zako
More Love from Kenya โค๏ธ
Waoooooo
Kisanga kwa sanga๐ค
Sanga anataka kuleta Baraaa
Duuuh hatariii
Kaz ipo mbona
Admin fany mpango tupate love and pain sehemu ya 3 na kuendelea maan n nzuri san
Admin fany mpango tupate love and pain sehemu ya 3 na kuendelea maan n nzuri san
SIMULIZI|MPANGO HASI( NEGATIVE PLAN ) SEHEMU YA KWANZA.
SIMULIZI ya Kijasusi MTUNZI ABYAS MZIGUA.
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/668
ufr91d
4zvenr
xs8x3q
w3y8iv