Ilipoishia “Ndiyo! Unapaswa kukubali kuolewa na Osman ili apone naΒ afanyiwe upasuaji wa kupandikiza figo” Mama alirudia kauliΒ yake, akili yangu ilihama na kumuwaza Mosses, manenoΒ aliyoyasema wakati naondoka kwake, achilia mapenzi yanguΒ kwakeΒ
“Mama naweza vipi kuolewa na Osman, siyo chaguo langu lile,Β wala siyo aina ya Mwanaume ninayemtaka katika Maisha yangu,Β Mama nina Mtu wangu….Siwezi” Nilisema huku nikiwa ninalia,Β chozi lilikuwa likinivuja. EndeleaΒ
SEHEMU YA TISA
Aliingia Bilionea Dhabi, alitukuta tukiwa katikati yaΒ maongezi yetu. Mzee Dhabi aliponiona alitabasamu tuu, alikuwaΒ ameongozana na Mke wake ambaye ni Mama Mzazi wa Osman,Β Alinisogelea kisha aliniambiaΒ
“Jacklin! Hujakosea, upo sahihi, ni ngumu sana kuolewa naΒ Mwanaume ambaye hayupo ndani ya moyo wako, upo sahihi sababuΒ huwezi ndiyo maana uliondoka jana Usiku. Lakini Jacklin, hebuΒ tazama macho ya Mama yake Osman, ona lile chozi kwanza”Β Niligeuza macho yangu kumtazama Mama yake Osman, Ni kweliΒ alikuwa akivuja mchoziΒ
“Analia kwasababu Osman ni Mtoto wake wa kipekee, hana MtotoΒ mwingine kama ulivyo wewe kwa Mama yako, lile chozi ndiloΒ ambalo Mama yako alikuwa akilia wakati alipopoteza tumaini laΒ wewe kuishi. Unakumbuka kilichotokea, Mungu alimleta OsmanΒ katika Maisha yako, alipambana hata kutoa figo lake iliΒ upone, hakufanya kwa ajili ya mapenzi bali kwa huruma yakeΒ kwa Mama yako, ulilala Jacklin hukumuona Mama yako alivyokuwaΒ anahangaika hata kutaka kutoa figo lake akuwekee wewe”Β Bilionea Dhabi alizungumza maneno mazito sana ambayoΒ yalimfanya Mama ajiinamie akiwa analiaΒ
“Nakuomba sana Jacklin, okoa Maisha ya Mwanangu, hatuna MtotoΒ mwingine zaidi yake, Osman ndiye Maisha yetu, kufa au kuponaΒ kwa Osman kunakutegemea wewe Jacklin” Alisema Mzee DhabiΒ kisha alienda kuketi kando ya Mke wake, maneno yakeΒ yalinifanya nishindwe kuendelea kuketi pale sebleniΒ nilikimbilia chumbani kwangu. Ni kweli Osman alijitoa naΒ kuhakikisha Maisha yangu yanarudi, tumaini la Mama yanguΒ linarudi, leo yupo Kitndani na Mimi ndiye ninayepaswaΒ kumuamsha, Daaah roho iliniuma sana.Β
“Usilie Mama Jacklin, Binti yako ni Mtu mzima anajuwaΒ anachokifanya. Kama amekataa kumsaidia Osman hakuna njiaΒ nyingine tutaondoka naye kuelekea Dubai tukajaribu huko,Β ikishindikana basi haikuwa ridhki yetu kuwa na Osman” AlisemaΒ Baba yake Osman, Mama yake Osman alikuwa akilia huku akiwaΒ amejifunika na kitambaa alishindwa hata kusema chochote, MamaΒ yangu alinyanyuka na kunifuata chumbani, alinikuta nikiwaΒ nimeshikilia simu yangu, alisogea kisha aliketi kando yanguΒ kwa upole sana alisemaΒ
“Jacklin Mwanangu! Nilikuzaa na kukulea katika Mazingira yaΒ kujuwa nini Maana ya utu na shida, pengine ndiyo nguvuΒ iliyomvuta Osman kuja kwenye Maisha yako, alikuja kama MasiaΒ akaokoa Maisha yako, leo amegeuka kikwazo cha furaha yako.Β Nikiwa kama Mama yako nakueleza jinsi ninavyojisikia Jacklin”Β Alisema Mama kisha alifikicha jicho lake moja ambalo lilikuwaΒ likimwaga chozi
“Moyo wangu umevunjika Jacklin, furaha imenitoweka kamaΒ Kizimikavyo kibatari wakati wa upepo Mkali, Jacklin Mama yakoΒ nimeumia sana. Siku Osman akiondoka hapa Duniani ndiyoΒ itakuwa mwisho wako kusikia sauti yangu, yule KijanaΒ alirudisha tumaini kwenye moyo wangu, alinifanya nijisikieΒ amani sana lakini leo umeiondoa yote” Mama alisema,Β nilitamani kumjibu na Kumwambia kuwa kama nitaolewa na OsmanΒ basi Mosses atasambaza video zangu za faragha, hadi MamaΒ anaondoka chumbani kwangu mdomo wangu ulikuwa mzito sana kamaΒ samaki aliyejaza maji mengiΒ
Niliangalia ujumbe ambao Mosses aliutuma, alikuwaΒ akinikumbusha kuwa endapo nitamuacha atasambaza hizo video,Β nilivujisha chozi machoni mwangu. Yalikuwa ni maumivu makaliΒ sana ambayo hata sikuwahi kuyahisi katika Maisha yangu.Β Nilipaswa kuokoa Maisha ya Osman kama ambavyo aliokoa yanguΒ ila ningefanya kitu gani? Kama video zitasambaa naweza hataΒ kujitoa uhai kukwepa aibu nzito lakini je Mama yangu MzaziΒ akiziona video hizo naye atakuwa katika hali gani? VipiΒ Familia ya Osman itajisikia vipi, ndio maana nasema kilikuwaΒ ni kipindi kizito na kigumu kwangu.Β
Mama aliporudi Sebleni hakuwakuta Baba na Mama yake Osman,Β aliangusha kilio kama kuna Mtu amefariki, nilishtuka naΒ niliumia sana. Nyumba ilikosa ile amani iliyokuwepo Mwanzo,Β ukimya ulitawala hakuna aliyetoa neno lolote zaidi ya sautiΒ za kufungwa na kufunguliwa kwa milango. Nilijitupa kitandaniΒ nikawaza sana nifanye jambo gani ili kumsaida Osman bilaΒ kuchukua uamuzi ambao ungesababisha kusambaa kwa video hizoΒ za faragha. Kadili nilivyokuwa natulia kitandani ndivyo pichaΒ ya tukio la kukataa kuvishwa pete na Osman lilivyokuwaΒ linajirudia katika akili yangu, nilikosa utulivu kama MtuΒ anayesumbuliwa na mizimu, niliamka bado Mama alikuwaΒ akiendelea kulia, nikiwa kama Mtoto nilijivuta kwendaΒ kumbembeleza.Β
Nilimkuta akiwa amekaa chini ameegemea sofa, niliketi kwaΒ adabu na utulivu mkubwa sana, Mama alihisi ujio wanguΒ alitulia kimya huku akihema sana. Nilishusha pumzi zanguΒ kisha nilisemaΒ
“Samahani Mama najuwa nimekuvunja moyo ila..” Kabla hataΒ sijamaliza nilichokitaka kukisema Mama alinikatishaΒ
“Ishia hapo hapo Jacklin, Wazazi ambao Mtoto wao aliokoa uhaiΒ wako wameondoka kwasababu umekataa kuokoa uhai wa Mtoto wao,Β nimeonekana Mama mbaya sana, Mama mbinafsi ambaye hajaliΒ kuhusu Mtoto wa mwingine” Alisema Mama kisha aliendelea
“Kama Osman atakufa basi juwa ni kwasababu yako, hupaswiΒ kusameheka katika hilo Jacklin” Alimaliza kusema kishaΒ alinyanyuka na kwenda zake chumbani kwake, choziΒ lilinimwagika Mimi Jacklin niliona kila Kiti kipo dhidiΒ yangu, sikuwa na Mtu wa kunisemea kabisa.Β
Usiku ulipofika niliondoka nyumbani nilienda kulala Hotelini,Β nilihitaji muda wa kuwa peke yangu ili niweze kutafakariΒ mambo kwa umakini zaidi. Nilizima simu zangu ili nisipateΒ usumbufu wowote ule, hakuna aliyejuwa niko wapi, Si MossesΒ wala Mama yangu niliyemwambia, nilitaka kutafakari ili nijuweΒ nafanya nini katika kipindi kigumu kama hiki.Β
Hali ya Osman haikuwa nzuri kabisa kule Hospitalini, alikuwaΒ kila azindukapo anataja jina langu tu, alikuwa anachomwaΒ sindano za usingizi ili kumtuliza. Familia ya Bilionea DhabiΒ iliingia gizani, tumaini lao juu yangu liliondoka kabisa,Β wakiwa nyumbani kwao Mke wa Bilionea Dhabi alimwambia MumeΒ wakeΒ
“Twende kwa mara ya mwisho kuzungumza na Jacklin kamaΒ atakataa kwa kinywa chake basi hatutokuwa na namna nyingineΒ bali kuondoka na Osman” Alisema kwa sauti ya Kimama iliyojaaΒ maumivu ya kumuona Mtoto wake akiwa kitandani na hana tumainiΒ lolote lileΒ
“Sasa hata kama tutafanya hivyo Mama Osman, Binti haweziΒ badili msimamo wake, hampendi Osman na hilo lipo wazi sana”Β Alijibu Baba yake Osman, Mara mlango uligongwaΒ
“Ingia” Alisema Bilionea Dhabi baada ya kumtambua aliyekuwaΒ akigonga, alikuwa ni MlinziΒ
“Samahani Baba na Mama, kuna mgeni hapo nje anasema anahitajiΒ kuonana na Osman” Alisema Mlinzi huyo baada ya kuwa tayariΒ ameingia ndani, Mzee Dhabi aliangalia saa yake aliona niΒ mishale ya saa 4 za Usiku alimuuliza MlinziΒ
“Huyo Mtu yupoje?”Β
“Mwanamke, mweupe” Alisema Mlinzi kisha alitabasamu tu baadaΒ ya alichotaka kukisema kuhisi hakina maana hapo mbele ya MzeeΒ Dhabi na Mke wake lakini Mzee Dhabi alimuelewa MlinziΒ akamrahisishiaΒ
“Mzuri Eeh” Basi mlinzi alitoa tabasamu zitoΒ
“Mh! Atakuwa Nani huyo!” Alisema Bilionea Dhabi kishaΒ alitafakari
“Utamjuwa vipi bila kumuona, Mlete” Alidakia Mke wa MzeeΒ Dhabi. Mara moja Mlinzi aliondoka, dakika moja baadayeΒ alirudi akiwa ameambatana na Mgeni huyoΒ
Mzee Dhabi na Mke wake walisimama kwa Mshangao Mkubwa sanaΒ baada ya kumuona Mgeni huyo kisha Mzee Dhabi alisemaΒ
“Mlinzi nenda” Mlinzi aliondoka zakeΒ
- β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’Β
“Zahra?”Β
“Zahra?” Mzee Dhabi na Mke wake alisema kwa pamoja baada yaΒ kumuona Zahra mbele yao, Si unamkumbuka Zahra? Ni yuleΒ Mwanamke aliyechota kiasi kikubwa cha pesa na kutimkia zakeΒ Ughaibuni, alikuwa ni mpenzi wa Osman ambaye aliuteka moyo waΒ Osman miezi kadhaa iliyopita aliondoka na kusema kuwa anaΒ Mwanaume mwingine hivyo Osman asihangaike kumtafuta, tukioΒ hilo lilisababisha Osman kupata Mshituko na kukimbizwaΒ Hospitalini.Β
Zahra alishtuka kuwaona Wazazi wa Osman, alitetemeka kwa HofuΒ
“Hebu keti” Alisema Mzee Dhabi, wote waliketi kisha MzeeΒ Dhabi na Mke wake walitazamanaΒ
“Ni wewe Zahra au tunaota ndoto ya Mchana?” Aliuliza MamaΒ yake OsmanΒ
“Ni Mimi Mama naomba msamaha wenu kwa kila kilichotokea,Β natamani kumuomba msamaha Osman na ndiyo sababu ya kuja hapa”Β Alisema ZahraΒ
“Unataka kumuomba Msamaha Osman?”Β
“Ndiyo Baba! Najuta kwa kila nilichomfanyia.Β
“Nifuate” Alisema Mzee Dhabi, walitoka ndani Bilionea DhabiΒ na Zahra, waliingia kwenye gari ya kifahari ya Mzee huyoΒ kisha safari ilianza, Zahra hakujuwa alikuwa akipelekwa wapiΒ
“Baba tunaenda wapi?” Alihoji ZahraΒ
“Si umesema unataka kumuomba msamaha Osman? ”Β
“Ndiyo Baba”Β
“Tunaenda alipo Osman”
Usiku huo nilikuwa nimeamua jambo moja, kumsaidia OsmanΒ kwasababu alisaidia Maisha yangu, akili yangu iliniambia kuwaΒ Osman alikuwa mwenye huruma na mapenzi ya kweli kuliko MossesΒ ambaye alianza kutishia kusambaza video zangu za Faragha.Β Niliondoka Hotelini nikaelekea nyumbani, NilipochunguliaΒ ndani nilimuona Mama akiwa amekaa kando ya Mlango waΒ kuingilia ndani nilijuwa tu alikuwa akinitafuta japoΒ alinichunia, nilitabasamu sababu Mama yangu alikuwa ni MamaΒ mwenye upendo wa Hali ya juu sana kwangu, nilifuangua geti,Β nilitupa macho upande wa kushoto nililiona lile gariΒ aliloninunulia Osman kwenye siku yangu ya Kuzaliwa, moyoΒ uliniuma sana.Β
Nilisogea alipo Mama kisha nilimwambiaΒ
“Mama nipeleke Hospitalini alipo Osman” Kauli yangu ilimfanyaΒ Mama anitazame mara mbili mbiliΒ
“Mama moyo wangu unaniambia tufanye haraka sana” NilisemaΒ nikiwa kwenye hali ya Haraka, lilikuwa ni jambo ambalo MamaΒ alikuwa akilisubiria. Haraka alikimbilia ndani akatoka naΒ mtandio, tulitoka tukachukua Tax kisha safari ya kuelekeaΒ Hospitali ilianza.Β
Upande wa pili, Baba Osman na Zahra walikuwa wanaingiaΒ Hospitalini, walisogeza gari kwenye maegesho kisha walielekeaΒ Wodini ambako Osman alikuwepoΒ
“Baba Osman anaumwa? Mbona umenileta Hospitalini?” AliulizaΒ ZahraΒ
“Ndiyo Osman ni Mgonjwa sana ndiyo maana nimekuleta hapaΒ Zahra” Alijibu Baba Osman, walishuka kisha walielekea ilipoΒ wodi hiyo. Bahati nzuri walikutana na Dokta Simon ambayeΒ alikuwa akitoka wodini humo, alipomuona Zahra alishangaa sanaΒ
“Najuwa una maswali mengi Simon lakini hiyo ndiyo haliΒ halisi” alielezea Mzee Dhabi baada ya kuisoma sura ya DoktaΒ Simon ilivyokuwaΒ
“Lakini Mzee, Osman hapaswi kushtushwa na jambo lingineΒ mnaweza kumpoteza kabisa, kwanini aje leo?”Β
“Maswali yako Simon hayawezi kujibiwa kwasasa, nina imani naΒ hiki atakachokiona Osman” Aliesema Mzee DhabiΒ
“Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo MachoΒ angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisemaΒ Dokta Simon
“Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….TwendeΒ Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra,Β waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta SimonΒ
Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman,Β aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa.Β Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuonaΒ Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, MwanmkeΒ ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio.Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ
Β Β
11 Comments
https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J
Dah toa nyingine ata usiku wa leoππ
Nimepumua baada ya kumaliza kusoma
Dah naona kesho mbal tuendeleee hadith imejoga sasa apo kwa akili ya haraka haraka julieth akimuona zarha atagoma ten kumhudumia osman π€π€π€uwiiiiiiiiiiii hadith tam nyie πππππππ€π€π€π€π€NATAFTA MPENZ KAMA OSMANπ€
Lete mbili juzi uliruka
Mshtuko umuue osman wazazi wa osman wamfukuze jack moses amuache jack mama yake ammchukie hyo pumzi itakuwa ya mwsho
Mtunzi apewe maua yake π πΉ
Jmn wanawake!!! π€π€ khaa
Sehemu ya nane IPO wapi
gu8eva
wwyvk2