Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Saba (07)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Saba (07)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 18, 2024Updated:October 28, 202412 Comments10 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Yote yaliyo mema, mazuri na yenye uelekeo mzuri zaidi, mudaΒ  siyo mrefu maono yangu yatadhihirika” Sikutaka kuendeleaΒ  kumuuliza, nilimwambiaΒ 

    “Sawa Mama nasubiria hayo Mema, nipo chumbani kwangu”Β  Nilisema kisha nilielekea Chumbani kwangu, tulikuwa tukiishiΒ  Watu watatu tu, yaani Mimi, Mama na Mdada wa kazi. HadiΒ  naondoka sikujuwa Mama na Osman walikuwa wamewasiliana naΒ  kuambiana kuwa nilienda kwa Osman. EndeleaΒ 

    SEHEMU YA SABA

    Ila ndani ya moyo wangu nilihisi amani sababu tayari nilikuwaΒ  nimeshamuomba msamaha Osman, na pia nilikuwa nimeweka mamboΒ  sawa kwa Mama yangu. Siku zilipita, niliendelea na kazi,Β  Mapenzi yangu kwa Mosses yaliendelea bila tatizo lolote tenaΒ  alikuwa akininyenyekea sana tofauti na mwanzo, kaziΒ  ziliendelea kule kwenye kampuni ya Osman, niliendelea kupataΒ  uzoefu huku ukaribu kati yangu na Osman ukizidi kuongezeka.Β  Osman alikuwa akiumwa sana ila alikuwa akijikaza mno mbeleΒ  yangu ila sura yake ilionesha wazi kuwa alikuwa akiumwa,Β  sikutaka kumuuliza sana sababu kama ningekuwa na unuhimu waΒ  kulijuwa hilo angelikuwa ameshaniambia muda mrefu.

    Alinipeleka sehemu mbalimbali, ndani na nje ya Nchi,Β  alinifundisha vingi sana Osman. Namna tulivyokuwa tumezoeanaΒ  kama ikitokea umetuona kwa mara ya kwanza ingekuwa rahisiΒ  kuhisi ni wapenzi, Osman alikuwa akijaribu kunionesha hisiaΒ  zake lakini hakusema kwa kinywa chake, nakumbuka siku yanguΒ  ya kuzaliwa alininunulia gari aina ya Cadilac, aliniandaliaΒ  kila kitu kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa, nilimuarikaΒ  Mosses kwasababu ndiye Mwanaume aliyekuwa akinipa furaha.Β 

    Mama aliniita pembeni, akaniulizaΒ 

    “Hivi Jacklin unatumia ubongo wako vizuri kuwaza?” AliulizaΒ  kwa sauti ya Juu sababu kulikuwa na kelele za Mziki, wakatiΒ  huo Watu ndio walikuwa wakifika nyumbani kwetu kwenye hiyoΒ  sherehe ya siku ya kuzaliwaΒ 

    “Mama! Nimefanya kitu gani kibaya?” NilimuulizaΒ 

    “Mosses amefuata nini hapa? Hii ni sherehe yako wewe, OsmanΒ  amefanya kila kitu bado unashindwa hata kumuheshimu?” AlisemaΒ  Mama ilinibidi nishushe mzuka wanguΒ 

    “Hivi Mama kwanini tunaishi kwa kuhofia fulani atasema nini?Β  Osman ni rafiki yangu, na Bosi wangu. Kuniandalia shereheΒ  haimaanishi mimi na yeye ni wapenzi Mama, Nitasherehekea vipiΒ  siku yangu ya kuzaliwa bila Mosses?” Nilimuuliza MamaΒ 

    “Huyo Mosses anajulikana na nani? Amekusaidia nini hadi hiviΒ  sasa kama siyo kula pesa yako ambayo imetokana na Osman?Β  Jacklin, hujui kilichopo kichwani kwa Osman na hujui kwaniniΒ  aliandaa hii sherehe yako ya kuzaliwa. Unaiyona ile gariΒ  pale? Ile ni zawadi kutoka kwa Osman, huyo Mosses wakoΒ  anaweza kukununulia japo Pikipiki?” Mama alisema na nilionaΒ  wazi alikuwa amepaniki.Β 

    “Samahani Mama” Nilisema, nilikuwa sipendi kumuona Mama yanguΒ  akiwa katika hali ya kuhuzunika kisa MimiΒ 

    “Mwambie huyo Mosses aondoke hapa kabla Osman hajafika, OsmanΒ  ni mfadhili wetu hivyo ni lazima tuheshimu hisia zake” MamaΒ  alisema Maneno ya mwisho kisha aliondoka pale, aliniacha naΒ  mawazo lukuki sana nikajiuliza maswali mengi ambayo sikuwa naΒ  majibu yakeΒ 

    Nikiwa nimesimama alikuja Mosses akiwa ameshikilia glasiΒ  yenye kinywaji, aliniulizaΒ 

    “Mama alikuwa anasemaje? Nimewaona kama mlikuwa mkigombanaΒ  hivi” nilimtazama Mosses kisha nilitabasamu tu nikamwambia

    “Hapana kuna jambo alikuwa ananielekeza ndio tukawaΒ  hatuelewani, lakini usijali” nilisemaΒ 

    “Mlisema Sherehe inaanza saa moja usiku, sasa inakimbilia saaΒ  mbili, anasubiriwa nani?” Aliuliza Mosses, nilikosa chaΒ  kumjibu. Mara zilisikika honi za gari huko nje,Β 

    “Wageni hao hebu twende” Nilisema lakini Mosses alinishikaΒ  mkono akanivuta pembezoni kwenye mnazi. Alitupa glasiΒ  pembeni, akaanza kunila mate yangu. Nilishindwa kujizuiaΒ  nikajikuta namba sapoti Mosses, eneo ambalo sisi tulikuwaΒ  tumesimama lilikuwa na mwanga hafifu sana.Β 

    Wakati magari yanaingia sisi tulikuwa bize kupeana mate paleΒ  kwenye mnazi, bahati mbaya Osman aliangalia tulipo japoΒ  hakunitambua kutokana na lile giza. Alikuwa ameingia na BabaΒ  na Mama yake, Zilipokuja kuwashwa taa zote ndipo tuliposhtukaΒ  tukaacha ule mchezo, ila mashine ya Mosses ilikuwa imesimama.Β  Tuligawana njia, mimi nilipitia upande wangu na Mosses upandeΒ  wake, nilipowaona Wazazi wa Osman nilishangaa sana sababu waoΒ  walikuwa Dubai au inamaana walikuja kwa ajili ya ShereheΒ  yangu ya siku ya kuzaliwa tu au kulikuwa na jamboΒ  lililowaleta pale? Nilisimama kwa sekunde kadhaa kabla yaΒ  kujitokeza huku bado mawazo yakiwa yananizonga kichwaniΒ  kwangu, sikuamini Sherehe yangu ya kuzaliwa ihudhuriwe naΒ  Bilionea Mkubwa kama Baba yake Osman?Β 

    Nilipojitokeza sikuonesha dalili yoyote kuwa nilikuwaΒ  nimetingwa na mawazo, nilienda kumsalimia Baba yake Osman,Β  alikuwa akinipenda sana na mara zote alikuwa akisema natembeaΒ  na kiungo chao japo alikuwa akisema kama utani ila ilikuwa niΒ  kweli nilikuwa natembea na figo ya Osman, tulicheka pamoja,Β  nilipogeuka nilikutana na Mama yake Osman naye alitabasamu,Β  tulisalimiana vizuri sana, ilikuwa ni sherehe ndogoΒ  iliyobadilika na kuwa kubwa tena yenye heshima sana hadi WatuΒ  tuliowaarika walishangaa. Walinionesha mahali alipo Osman,Β  alikuwa amesimama na rafiki zake, nilienda kumsalimia hukuΒ  macho yangu yakimtafuta Mosses alipo, Osman alinikumbatiaΒ  kisha alinishika mkono huku akiendelea kuniuliza maswali yaΒ  hapa na paleΒ 

    Punde shughuli ilianza, Mama yangu sikumuona kabisa licha yaΒ  kupepesa macho huku na kule. MC wa shughuli aliniita katikatiΒ  ya Watu waliokuwa wamesimama, nilitembea taratibu sababuΒ  nilivalia gauni refu lenye rangi ya Dhahabu. Nijisifie tuΒ  maana ukisubiria kusifiwa hapa Duniani utazeeka, nilipendezaΒ  mno.

    “Leo ni siku nzuri na nyenye baraka kutoka kwa Mungu, nduguΒ  yetu Jacklin leo ametimiza miaka 28. Bahati ilioje kwake niΒ  kwamba sherehe yake imehudhuriwa na Bilionea ambaye ndiyeΒ  Baba wa Osman ambaye pia ameandaa shughuli hii kwa ajili yaΒ  Jacklin” Alisema MC kisha Watu walipiga makofi mengi sana,Β  bado nilikuwa nikiangaza macho yangu kumtafuta Mosses, bahatiΒ  nzuri nilimuona akiwa amesimama nyuma akiwa anaangalia tukioΒ  lilivyokuwa likiendelea.Β 

    Nilitabasamu ili tu mambo yaende ila nilipoteza uwezo waΒ  kujiamini kabisa, MC aliendeleaΒ 

    “Namkaribisha Osman Dhabi aje mbele atuambie siku ya leoΒ  amemuandalia nini Jacklin” Makofi mengi yalipigwa, BilioneaΒ  Mzee Dhabi naye alikuwa akifurahi pamoja na Mke wake hapoΒ  ndipo nilipomuona Mama yangu akiwa amesimama kando ya familiaΒ  hiyo ya Kitajiri, Mama alinipa ishara ya kukubaliΒ  kitakachotokea pale, nilishindwa kumuelewa ni kwaniniΒ  nikubali kwasababu sikujuwa kilichotaka kwenda kutokea. OsmanΒ  alipofika karibu na Mimi alisemaΒ 

    “Wakati nakutana na Jacklin kwa mara ya kwanza nilimuona niΒ  Mwanamke Msumbufu, asiyejali, mkorofi lakini nilivyokujaΒ  kumuelewa niligundua ni Mwanamke wa tofauti sana” AlisemaΒ  Osman, wote walipiga makofi hata Mimi nilitabasamu maanaΒ  nilikumbuka jinsi nilivyokutana na Osman kuanzia kwenyeΒ  Pikipiki hadi kwenye mvua, nilicheka.Β 

    “Kwa muda mfupi anenitengenezea kumbukumbu zisizofutikaΒ  katika Maisha yangu, leo kwenye siku yake ya kuzaliwaΒ  nilifikiria ni zawadi gani naweza kumpa ili afurahi, nilionaΒ  nimnunulie gari aina ya Cadilac escaled ya Mwaka 2021”Β  Shangwe ziliibuka pale, makofi yalipigwa sanaΒ 

    “Gari hii ina thamani ya Milioni 600, ni zawadi ambayo moyoΒ  wangu umeridhia kwake lakini pia napenda kumuomba Jacklin”Β  Alisema Osman kisha alipiga magoti akanitazama, nikaiyonaΒ  ishara kuwa anataka kunivika pete kidoleni, nilishtukaΒ  nilipomuona Akitoa pete kwenye mfuko wa koti lake la sutiΒ 

    “Nipe ruhusa niwe Mumeo Jacklin, maneno haya si rahisi MtotoΒ  akayazungumza mbele ya Wazazi wake lakini nimeshindwaΒ  kufikisha hisia hizi kwako, nimeona leo ni wakati sahihi waΒ  kufanya hivi” Nilimtazama Osman kama vile nataka kumuulizaΒ  maswali ambayo hata sikujuwa niulizaje, nilipogeuza machoΒ  nilikutana na Mosses, Mama na Wazazi wa Osman, wote walikuwaΒ  kimya kusikiliza nitasemaje. Niliishiwa nguvu jamani

    Osman alinishika mkono akawa ananivisha ile pete taratibu,Β  nilikuwa kama Mgonjwa wa koma, ghafla nilishtuka nikasemaΒ 

    “Hapana Osman, siwezi” nilisema kisha niliivua ile peteΒ  nikamtupia Osman, Watu walijawa na mshangao mkubwa sana,Β  Chozi lilimbubujika OsmanΒ 

    “Jacklin tafadhali, fanya kwa ajili ya Wazazi wangu nakuomba”Β  Alisema OsmanΒ 

    “Siwezi Osman, siwezi kuidhurumu nafsi yangu, siwezi kuuzaΒ  upendo wangu Osman, unajuwa fika nina Mtu wangu” Nilisema,Β  Watu walikuwa kimya sana kusikiliza maongezi yetuΒ 

    “Jacklin, hili ni ombi langu kwako, baada ya hapa sitakuwa naΒ  uwezo wa kukuomba chochote tena, tafadhali” Alisema OsmanΒ  kisha aliushika mkono wangu ili anivishe tena ile pete,Β  nilimsukuma kisha niliondoka pale, nilikimbilia nje kabisa,Β  Mosses alinifuata huko nje, tulichukua Bajaji na kuondokaΒ  pale nyumbani. Nilipomsukuma Osman alianguka, hali yakeΒ  ilibadilika alikimbizwa Hospitalini, Hekaheka ilikuwa kubwaΒ  pale nyumbani, Watu walikuwa wakijiuliza kulikoni, Mzee DhabiΒ  alihangaika kwa ajili ya Mtoto wake. Muda mchache watuΒ  waliondoka pale nyumbani, alibakia Mama akiwa analia tu, namiΒ  nilikuwa nikilia ndani ya Bajaji, siyo kwamba nilikuwaΒ  simpendi Osman ila tayari nilikuwa na Mwanaume niliyempendaΒ  ambaye ni Mosses.Β 

    Nilikuwa nimeshabadilisha hali ya hewa, nililia sana nikiwaΒ  ndani ya Bajaji, Mosses alinibembeleza hadi tulipofika kwake.Β 

    Tukiwa chumbani aliniulizaΒ 

    “Nini kinaendelea Jacklin?” Aliniuliza akiwa amekaa pembeni,Β  chozi lilikuwa likinibubujika, nilimuwaza Mama yangu,Β  nilijuwa nimemkosea sana.Β 

    “Mosses, hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Osman,Β  nimeshangaa ameita wazazi wake kwenye sherehe yangu yaΒ  kuzaliwa istoshe hakuwahi kuongelea kuhusu mapenziΒ  nimeshangaa alipotaka kunivesha pete” Nilisema huku nikiwaΒ  najifuta mchozi, simu yangu ilikuwa ikiita sana na aliyekuwaΒ  akinipigia alikuwa ni Mama yangu, niliamuwa kuizima kabisa.Β 

    “Yule ndiyo amebadilisha Maisha yenu?” Aliniuliza “Ndiyo Mosses, ni yeye”

    “Haiingii akilini Mtu aje tu atake kukuvesha pete, lazimaΒ  kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kati yenu”Β 

    “Mosses tafadhali naomba uniamini, nisingelimkimbia kwa ajiliΒ  yako, ile ni familia ya kitajiri sana. Kama siyo weweΒ  ningelikuwa nimekubali lile jambo ila upo wewe MwanaumeΒ  nikupendaye Mosses” nilisema kisha nilimuona MossesΒ  akitafakari jambo, kilio changu kilikata nikawaza labdaΒ  alikuwa anataka aniacheΒ 

    “Hebu tuliza akili yako Jacklin, kesho asubuhi tutaongeaΒ  jambo moja” Alisema Mosses, nilipata muda wa kupumzika.Β 

    β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’Β 

    Mama yangu hakulala, hakula chakula, alikesha kunipigia simuΒ  bila kupokea majibu yoyote. Usiku ulikuwa mwingi ilimbidiΒ  aingie ndani, Usiku huo taarifa kutoka maabara zilisema haliΒ  ya Osman inaweza kuwa mbaya zaidi baada ya miezi mwiliΒ  kutokana na figo lingine kufanya kazi kwa kiwango kidogoΒ  sana. Taarifa hii ilikuwa mbaya na isiyopendeza kabisa, MzeeΒ  Dhabi na Mke wake walihuzunika sana, walimuuliza Dokta SimonΒ 

    “Kwanini hukusema kabla Osman hajachukua uamuzi wa kuondoaΒ  figo moja?” Ilikuwa ni sauti yenye maumivu sana iliyotokaΒ  kwenye kinywa cha Bilionea DhabiΒ 

    “Niliongea naye kabla ya kuchukua uamuzi huo, cha ajabuΒ  alimuhamisha mgonjwa na kwenda kufanya upasuaji India,Β  aliniomba nisiwaambie chochote kwasababu alikuwa na uhakikaΒ  wa kupata figo haraka iwezekanavyo. Tukio lililotokea leoΒ  siyo tu limemletea mshituko bali mfadhahiko mkubwa ndaniΒ  yake” Alisema Dokta Simon, Chozi lilimbubujika Mama yakeΒ  Osman, alikuwa ndiyo Mtoto wao wa pekee hawakubatika kupataΒ  Mtoto mwingineΒ 

    “Laiti kama mioyo ingekuwa inahamishika basi ningehamishaΒ  moyo wa Osman, mara zote tuliamini tukimpa pesa nyingi MtotoΒ  wetu itampa jeuri na kuondoa mapenzi katika Moyo wake lakiniΒ  Osman amekuwa dhahifu sana linapokuja suala la Mapenzi” MzeeΒ  Dhabi alimtuliza Mke wakeΒ 

    “Dokta inahitajika huduma gani kwa Mtoto wangu, HospitaliΒ  gani Duniani, Pesa Kiasi gani? Nipo tayari kutoa nusu yaΒ  utajiri wangu kwa ajili ya Osman” Alisema Mzee Dhabi, DoktaΒ  Simon alimwambia Mzee DhabiΒ 

    “Unaweza ukapata figo, ukapata kila kitu lakini huweziΒ  kuuondoa mfadhahiko alionao Mwanao. Kitu cha kwanza niΒ kumuondolea mfadhahiko Osman ili kumuandaa kwa ajili yaΒ  upasuaji wa kupandikiza figo” Alisema Dokta SimonΒ 

    “Pesa siyo tatizo Simon, niambie hiyo huduma inapatikanaΒ  Hospitali gani Duniani, kiasi gani kinahitajika?” AliulizaΒ  Bilionea Dhabi, walionesha kumpenda sana Mtoto wao.Β 

    “Mfadhahiko huondolewa na kilichosababisha mfadhahiko,Β  tumaini alilokuwa nalo ndilo lenye kuuondoa huo mfadhahiko waΒ  Osman”Β 

    “Unamaanisha nini?”Β 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ 

    Pumzi ya mwisho

    12 Comments

    1. catherine Arod on October 18, 2024 2:53 pm

      Duh ya moto sana.

      Reply
    2. Samuel FA on October 18, 2024 4:17 pm

      Duuuuh….. Si mchezooooπŸ™†πŸ”₯

      Reply
    3. Fredy on October 18, 2024 4:19 pm

      Hadithi tamu Sana

      Reply
    4. Qassim Ituja on October 18, 2024 5:09 pm

      Pumzi ya mwisho kipande kimoja Ni kitamu sana, ladha haiishi, ongeza viwe viwili kwa siku chief

      Reply
    5. Charz jr😎 on October 18, 2024 5:30 pm

      😊😊 mpka kieleweke

      Reply
    6. Roda on October 18, 2024 8:17 pm

      Huyo dada anatia hasira 😀😣😠hv ana akili zote mpuuzi huyoooo

      Reply
    7. G shirima on October 18, 2024 8:52 pm

      Aise imenigusa sana dah

      Reply
      • Azimara on October 19, 2024 5:07 pm

        Hadithi tamu balaaa

        Reply
    8. Hamis on October 19, 2024 5:49 am

      Kwan adinimi story unatowa wap mbon kama muvi iv tunaangalia jamani

      Reply
    9. Agustine on October 19, 2024 11:57 am

      Admin nikutmie shingap unitmie vipande vyote

      Reply
      • Yulia kimario on October 19, 2024 4:47 pm

        πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

        Reply
    10. Chrispin on October 20, 2024 9:14 pm

      Nzurii

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.