Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Tatu (03)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Tatu (03)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 13, 2024Updated:October 28, 202415 Comments10 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Yaani Mama kisa tu ana hela basi umechanganikiwa kiasiΒ  hicho, kweli umasikini mbaya sana Mama, ila usijali siku siyoΒ  nyingi nitaanza kazi nitakufanyia kila kitu, sawa Mama?”Β 

    “Mmh! Sawa” Mama alisema kisha aliondoka zake ila aliniachaΒ  na jambo la kufikiria ndani ya akili yangu, nilikumbukaΒ  kitendo chake cha kuondoka pale wodini baada ya MossesΒ  kuingia, ila ni yeye ndiye aliyempigia simu Mosses baada yaΒ  kuchukua namba kwenye simu yangu.Β  Endelea

    SEHEMU YA TATU

    Sikutaka sana kuanza kufikiria hilo jambo, niliona ni boraΒ  niwasiliane na Mosses maana baada ya kuachana naye kuleΒ  Hospitali sikuongea naye kabisa, simu ya Mosses ilikuwaΒ  imezimwa, ilinipa maumivu makali sana ndani ya moyo wangu,Β  nilijigeuza geuza kisha Usingizi ulinichukua.Β 

    Kulipopambazuka nilianza kuhisi hali ya tofauti, mwiliΒ  ulianza kuchoka hadi nilijishangaa, Mama aliendeleaΒ  kunihudumia huku akiendelea kutafuta uwezekano wa kupataΒ  Figo, alienda kwa daktari ambaye aliunganishwa na Osman,Β  upatikanaji wa Figo ulikuwa mgumu sana huku hali yanguΒ  ikizidi kudhohofu, nilikuwa napewa dawa tu nimeze, maumivuΒ  niliyokuwa nikiyasikia kwenye tumbo langu yalikuwa makaliΒ  sana nilitamani hata kufa kabisa, kwa siku zote hizoΒ  sikumuona wala kumpata Mosses kwenye simu, ilizidi kunifanyaΒ  niwe mgonjwa zaidi.Β 

    “Mama Mosses hapatikani leo siku ya kumi na mbili”Β  Nilimueleza MamaΒ 

    “Usijali pengine amepatwa na tatizo kama hapa anapajuwa basiΒ  atakuja siku moja” Alisema Mama, angalau alinipa moyo naΒ  tumaini, lakini nilimuuliza

    “Haya maumivu makali yanatokana na nini Mama? Mwili wanguΒ  hauna nguvu kabisa nazidi kudhohofu” Nilipomuuliza nilionaΒ  macho ya Mama yaliyojaa maumivu, alitamani kulia lakiniΒ  hakusema shida iliyokuwa ikinisumbuaΒ 

    “Utapona Mwanangu! Mungu ni mwingi wa huruma, atakujalia afyaΒ  njema Binti yangu” Alisema Mama kisha alininywesha ujiΒ 

    “Hivi umewasiliana na Osman Mama?” Nilimuuliza MamaΒ 

    “Ndiyo usiwe na wasiwasi ukipona tu utaanza kazi, pumzika kwaΒ  sasa” Mama alikuwa ameshamaliza kuninywesha uji, alinifuta naΒ  kuondoka zake, alipofika chumbani kwake alilia sana sababuΒ  tumaini la Mimi kupona lilikuwa hafifu sana, siku zilisogea.Β 

    Mama pamoja na daktari walijitahidi kutafuta Mtu wa kunitoleaΒ  Figo, walitangaza dau kubwa kadili siku zilivyokuwa zikiendaΒ  ila waliojitokeza walikuwa ni Watu wenye Afya zisizoridhisha,Β  figo zao pia zilionekana kuwa na Hitilafu, hazikufaa.Β  Ilipofika siku ya 20 nilipekwa Hospitalini nikiwa katika haliΒ  mbaya sana, nilikuwa sijitambui kabisa. Mama yangu alikuwaΒ  Mtu wa kulia kila wakati, pesa ilipatikana kwa ajili ya FigoΒ  lakini mtoaji wa figo hakupatikana, daktari alimwambia MamaΒ 

    “Hakuna namna tunaweza kufanya, nahisi kukata tamaa MamaΒ  Jacklin” Alisema Daktari wakiwa ofisini kwa Daktari huyoΒ  aliyeitwa Dokta SimonΒ 

    “Unaposema hivyo daktari unanipa wakati mgumu wa kuangaliaΒ  mbele, sitaki kuamini kama siku za kuishi za Jacklin zimefikaΒ  mwisho, Huyu ndiye Binti yangu wa pekee, sisi ni masikiniΒ  sana, basi toa figo yangu kwa ajili ya Binti yangu” AlisemaΒ  Mama, ilifika wakati ambao Mama alishindwa kuhimili maumivuΒ  aliyokuwa akiyasikia katika kifua chakeΒ 

    “Mama Jacklin, umri wako na hilo jambo haviwezi kwendaΒ  sambamba. Najuwa tumaini ni dogo sana katika jambo hili,Β  lakini…”Β 

    “Dokta, kama kufa Mimi kutamsaidia Binti yangu hilo siyoΒ  tatizo, hajawahi kuishi Maisha ya furaha katika Maisha yake,Β  ndiyo kwanza alikuwa amepata kazi….leo afe aaaah hapana”Β  Alisema Mama akiwa analia, alionesha uchungu wake kwanguΒ 

    “Sawa Mama! Ngoja tuiangalie kama itafaa” Alisema DoktaΒ  Simon, kisha waliongozana hadi chumba cha Uchunguzi. MamaΒ  alitakiwa kufanyiwa uchunguzi wa figo yake ili niwekewe MimiΒ  nipate kunusuru Maisha yangu ambayo yalikuwa hatua za mwishoΒ  sana.

    Huu ndiyo upendo ambao Mama huwa nao kwa Mtoto wake,Β  watakukimbia wote katika Maisha lakini Mama yako atasimamaΒ  kwa ajili yako kila siku za Maisha yako, Mama alianzaΒ  kufanyiwa uchunguzi. Bahati mbaya figo ya Mama ilikuwa naΒ  Mawe hivyo isingeliweza kunifaa, Mama alilia sanaΒ 

    “Dokta weka hiyo hiyo ili Jacklin aamke, tumaini langu niΒ  yeye pekee” Mama alilia hadi Dokta Simon alidondosha ChoziΒ  lakeΒ 

    “Mama usilie, tuna siku 10 zilizobakia, Mungu atafanya wepesiΒ  wa hili jambo, kwasasa Jacklin anahitaji Maombi” AlisemaΒ  Dokta Simon, Mama alifikiria afanye nini, alichukua namba yaΒ  Mosses kisha aliipiga akiwa HospitaliniΒ 

    Bahati nzuri siku hiyo simu ya Mosses iliita aliipokea, MamaΒ  alimueleza Mosses hali ya afya yangu kwa wakati huo, MossesΒ  alimwambia Mama kuwa alipata tatizo ndiyo maana alishindwaΒ  kuja akaahdi kuwa atakuja Hospitalini. Kweli, Mchana MossesΒ  alifika Hospitalini, aliishuhudia hali ya Afya yangu ambayoΒ  alisimuliwa kama hadithi za Amza Stories, alikubali kuwa MimiΒ  nilikuwa mgonjwa sana kwa jinsi nilivyodhohofu, pumua yanguΒ  ilikuwa ya shida mnoΒ 

    “Hali ndiyo hiyo, leo siku ya tatu haongei wala hafumbuiΒ  Macho. Kama unampenda Jacklin jitolee Mosses Mungu atakulipaΒ  kwa wema wako” Mama alisema, walikuwa wodini wakiwa na yuleΒ  Daktari SimonΒ 

    “Mama Mimi nitajitoa kwenye nini tena ikiwa mmetangaza dauΒ  kubwa na bado figo haijapatikana, tumuombee Jacklin pengineΒ  Mungu atampa nafuu” Alisema MossesΒ 

    “Kuomba tunaomba lakini hatuwezi kukaa kimya bila kufanyaΒ  jitihada zozote Baba, mimi leo siku ya tatu sijala chochote,Β  nione sina raha kwasababu ya Jacklin” Alisema Mama hukuΒ  akibubujika Mchozi, Dokta Simon aliingilia kati akamwambiaΒ  MossesΒ 

    “Ndugu najuwa inaweza kuwa ngumu kwako lakini kama huyu MtuΒ  ana umuhimu kwako jitolee figo moja kwa ajili ya kumuamsha”Β  Alisema Dokta, Mosses alishtuka akaulizaΒ 

    “Nitoe nini?”Β 

    “Figo kwa ajili ya Mpenzi wako” Alijibu Dokta Simon huku MamaΒ  akiwa analia pembeni,

    “Nitoe figo? Hiyo ni hatari sana Dokta nitafanya vyote lakiniΒ  siyo kutoa figo yangu, ingekuwa wote wanaopendana wanatoleanaΒ  viungo basi hii Dunia ingejaa walemavu kila kona” AlisemaΒ  Mosses, Maneno yake yalimchukiza sana Mama alinyanyuka naΒ  kumpiga kofi MossesΒ 

    “Mama hupaswi kufanya hivyo hapa ni Hospitalini istoshe niΒ  wodini ambako panahitaji utulivu sana” Alisema Dokta SimonΒ 

    “Dokta huyu ni mshenzi anawezaje kusema maneno ya kikatiliΒ  namna hiyo hakuona neno lingine la kusema? Huyu si ndiyeΒ  ambaye alikuwa akikupa furaha, leo amelala hujali tena siΒ  ndiyo?” Alihoji Mama huku akiwa anahema juu juuΒ 

    “Unathubutu vipi kunipiga Mimi? Unanijuwa Mimi? Kama MaishaΒ  yake ni muhimu kwangu basi hata kwako ni Muhimu kwanini weweΒ  usitoe hiyo figo? Siwezi kutoa kiungo kisa Mapenzi tena kwaΒ  kiumbe anayeitwa Mwanamke, Jacklin akipona Mimi nipo akifaΒ  Maisha yataendelea” Alisema Mosses kisha aliondoka Wodini,Β  Mama alilia sana, kauli ya Mosses ilizidi kumfanya akateΒ  tamaa, Dokta Simon alimwambia MamaΒ 

    “Siku bado zipo tuzidi kufanya jitihada na Maombi” AlisemaΒ  kisha aliondoka zake, Mama aliendelea kulia kwa kukata tamaaΒ  alinisogelea akasemaΒ 

    “Jacklin nimekuzaa kwa shida sana, nimekulea kwa tabu mno,Β  leo nakupoteza Mama kwa shida sana, Nisamehe Mama yakoΒ  nimefanya jitihada zote lakini nimeshindwa Mimi sababu hataΒ  Mungu hayupo upande wangu tena” Maneno ya Mama niliyasikia,Β  Chozi lilinivuja, sikuwa na nguvu ya kufanya chochote kileΒ 

    β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’Β 

    Ndani ya Dubai, Kilichompeleka Osman Dubai kilikuwa niΒ  kumtafuta Zahra, achana na kiasi kikubwa cha pesa ambachoΒ  Mwanamke huyo aliondoka nacho na kwenda huko kuishi naΒ  Mwanaume mwingine, Osman alikuwa akimpenda sana MwanamkeΒ  huyo, jitihada za kumpata Zahra ziligonga mwamba. AlirudiΒ  Nchini, aliitafuta Familia ya Zahra lakini wazazi wa ZahraΒ  walionekana kufurahia ambacho Bitni yao alikifianya.Β 

    Hawakuwa na huruma, Osman alijitoa sana kuhakikisha Maisha yaΒ  Wazazi wa Zahra yanakuwa bora, aliwajengea jumba la kifahari,Β  aliwanunulia magari ya kutembelea, alibadilisha Maisha yaoΒ  kwa kiasi kikubwa sana, Osman aliondoka na kwenda kwenyeΒ  gari, alikumbuka jinsi ambavyo aliishi kwa furaha na amani naΒ  Zahra, alilia sana, Maumivu yalijaa ndani ya kifua chakeΒ  alipoikumbuka meseji ya mwisho ambayo Zahra aliituma, mesejiΒ  hiyo ilisema

    “Osman! Najua ujumbe wangu utakupa maumivu makali sana lakiniΒ  inabidi uupokee sababu ndiyo maamuzi yangu, asante kwaΒ  kubadilisha Maisha ya Wazazi wangu kwa kiasi kikubwa lakiniΒ  hukuwa chaguo la Moyo wangu japo ulinipenda sana, kwasasaΒ  mimi nipo Dubai na Mwanaume ambaye ninampenda. UsiwazumbueΒ  wazazi wangu wala usinitafute, pesa zote zilizo kwenyeΒ  akaunti yako ya Benki nimezichukua, unaweza kujiona MjingaΒ  lakini hiyo ndiyo nguvu ya Mapenzi ambayo ninayo, nilikufanyaΒ  ukawa dhahifu kwangu! Nakutakia Maisha Mema, ni Mimi Zahra”Β 

    Ulikuwa ndiyo ujumbe wa Zahra baada ya hapo simu yakeΒ  haikupatikana tena,, alipoupata ujunbe huo Osman alipotezaΒ  fahamu akaenda kuzinduka kwenye Hospitali ya Dokta Simon,Β  aliishi Maisha yaliyojaa maumivu na aliapa kuwa hatokujaΒ  kupenda tena.Β 

    Basi, alifuta chozi akiwa ndani ya gari yake ya kifahari,Β  alipotoka kwa Wazazi wa Zahra alikuja moja kwa mojaΒ  Hospitalini maana aliwasiliana na Mama na akaambiwa kuwa haliΒ  yangu siyo nzuri na haina tumaini.Β 

    Alimkuta Mama akiwa analia nje, Osman alimuuliza Mama “Hali yake kwasasa ipoje Mama?” Alimuuliza baada ya salamΒ 

    “Kama nilivyokueleza Baba, hali ya Jacklin ni mbaya sana,Β  ninahofu juu ya uhai wake” Alisema Mama akiwa anaendeleaΒ  kumwaga choziΒ 

    “Pole Mama, wakati mwingine Dunia inakuwa katili sana, naombaΒ  nikamuone” Alisema Osman, walirudi wodini, Osman aliponionaΒ  hakuamini kama ni Mimi ndiye niliyemchachafya siku kadhaaΒ  zilizopita, nilikuwa nimekonda sana, nilikuwa nikipumua kwaΒ  shida sana, alidondosha chozi akamuuliza MamaΒ 

    “Upatikanaji wa figo?” Mama alitikisa kichwa kuashiria kuwaΒ  hakukuwa na uwezekano wa kupatikana figo kabisa japoΒ  zilisalia siku 10Β 

    “Nitarudi Mama” Osman alitoka haraka akaelekea ofisini kwaΒ  Dokta Simon.Β 

    “Bilonea Kijana karibu sana” Alisema Dokta Simon sababuΒ  alikuwa akimfahamu sana Kwa ukaribu OsmanΒ 

    “Dokta Simon, Mama Jacklin amesema uwezekano wa kupatikanaΒ  Figo ni mdogo sana, nataka kusikia kutoka kwako!”Β 

    “Huo ndiyo ukweli Osman, kilichobakia ni kudra za MwenyeziΒ  Mungu pekee, tumepima Watu wengi lakini hakuna hata mmojaΒ mwenye figo yenye afadhali alafu kibaya zaidi Mpenzi wa huyoΒ  Jacklin amegoma kufanya hivyo” Alisema Dokta SimonΒ 

    “Nitatoa Figo yangu” Alisema Osman, kauli hii ilimshtua sanaΒ  Dokta SimonΒ 

    “Unatoa figo yako? Umefikiria mara mbili Osman? Hii familiaΒ  inakuhusu nini wewe ikiwa mpenzi wa Jacklin amekataa, ufanyeΒ  hivyo wewe kama Nani? Umesahau kilichokutokea Osman?”Β  Aliuliza Dokta SimonΒ 

    “Natoa kama Binadamu niliyeguswa na hili Dokta Simon, MaishaΒ  ya yule Msichana ni tunu Kwa Mama yake, ni furaha kwenyeΒ  macho ya Mama yake ambaye muda wote analia. Umewahi kufikiriaΒ  jinsi Mama yule anavyokosa raha kwasbabu ya Binti yake?Β  Unajuwa ni furaha kiasi gani ataisikia endapo Binti yakeΒ  atasimama tena?” Aliuliza Osman kwa hisia kali sanaΒ 

    “Fikiria mara mbili sikushauri kufanya hivyo Osman, wewe niΒ  Bilionea Mkubwa hupaswi kuishi Maisha yenye kasoro kiasiΒ  hicho!”Β 

    “Mkamilifu ni Mungu pekee, nitatoa Figo yangu kuokoa MaishaΒ  yake” Alisema Osman kisha aliondoka akarudi Wodini, DoktaΒ  Simon hakukubaliana na uamuzi wa Osman alinyanyua simu naΒ  kuwapigia Wazazi wa Osman, aliwapata taarifa hiyo ambayoΒ  iliwakasirisha sana Wazazi wa OsmanΒ 

    Basi, Osman aliporudi alimwambia Mama kuwa nitapona na kuanzaΒ  kazi mara moja, japo Mama alikuwa katika hali ya huzuni sanaΒ  ila maneno ya Osman yalimjaza tumaini.Β 

    Alipotoka Hospitalini Osman alikuwa mwenye mawazo na maumivuΒ  makali sana, alipigiwa simu na Wazazi wake na kumtaka aachaneΒ  na mpango wa kutaka kutoa figo kwani haitokuwa na faidaΒ  yoyote kwake, Wazazi wa Osman waliamini kuwa Osman alikuwaΒ  akitaka kutoa figo kwa ajili ya Mapenzi, walinuonya sana kwaΒ  kile kilichomtokea kwa Zahra ila Osman aliwaambia Wazazi wakeΒ  kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Mimi bali ni ubinadamu tuΒ  wa kutaka kuhakikisha afya yangu inaimarika.Β 

    Osman aliwasiliana na Hospitali nyingine ambayo ingefanyaΒ  operesheni ya kupandikiza figo kwenye mwili wangu, kutokanaΒ  na utajiri alionao aliweza kupata Hospitali Nchini India,Β  tulisafiri kwenda huko. Osman alishauriwa na kuambiwa kilaΒ  kitu kiafya kuhusu uamuzi wake.Β 

    Nini Kitaendelea? Osman atatoa FIGO? Usikose Sehemu Ya NNE Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ 

    Pumzi ya mwisho

    15 Comments

    1. Farnoush on October 13, 2024 4:21 pm

      Duuuh Osman ni mwanaume wa maanaπŸ˜‚

      Reply
      • Charz jr😎 on October 13, 2024 4:31 pm

        Ila sas ili ujue binadamu jauπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ au ngoja …. nisiharibu uhondo siku ikifikia ntakwambiaa…hii tamthiliya inaweza kuliza watu huko mbele πŸ₯²πŸ₯²πŸ₯² me siyo mtabiri akin

        Reply
    2. Charz jr😎 on October 13, 2024 4:30 pm

      😎 mule mule baba admin…..hujai kosea

      Reply
    3. Tumpe on October 13, 2024 5:09 pm

      Sas huyu binti akitaka kutukera apone af arud kumpenda mosses tena wakat osman katoa figo hap😁

      Reply
    4. Calvin paul on October 13, 2024 5:30 pm

      Wanaume kama osman tumebaki wachache sanaa

      Reply
      • Joyce on October 14, 2024 12:44 pm

        Calvin kabisa πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

        Reply
    5. Lus twaxie on October 13, 2024 5:38 pm

      Huyu dada nna was was akipona …atanboaaaa

      Reply
      • Kevin Winton mwasambiri on October 14, 2024 12:55 am

        Niko njia Panda naomba mosses
        Afutwe uhusika😣

        Reply
    6. Chingu on October 13, 2024 5:43 pm

      Huu uzi sio poa hatariii kama ungekuwa unaachia mbili mbili vile daah hatariiπŸ”₯πŸ”₯

      Reply
    7. Stella on October 13, 2024 6:24 pm

      Yani wanawake sisi Sijui kama atakumbuka wema Na fadhila
      πŸ˜’

      Reply
    8. Junior on October 13, 2024 8:39 pm

      Mmmh tusubili namba 04 πŸ€”πŸ€”

      Reply
    9. Henderson on October 13, 2024 11:15 pm

      NAUZA FIGO +255788414957

      Reply
    10. Sabiti on October 14, 2024 12:15 am

      !!!!!!!! Kuna mtu ata πŸ’”

      Reply
    11. Dj Shoti on October 14, 2024 1:30 am

      πŸ˜†πŸ˜…

      Reply
    12. πŸ”— 🎁 BTC Reward: 0.25 BTC added. Collect today > https://graph.org/WITHDRAW-YOUR-COINS-07-23?hs=9d402d3509ba896702cfa514aed6dd28& πŸ”— on August 24, 2025 3:54 am

      mlwzm9

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE β€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.