Mvua ilikuwa ikinyesha, moyo wangu ulijawa na tabasamu kubwaΒ sana, nilijinyoosha ili kuianza siku mpya ambayo ilianza kwaΒ hali ya hewa kuwa nzuri yenye ubaridi. Niliposhika simu yanguΒ niliona picha ya Mwanaume niliyempenda sana. Niliiweka kwenyeΒ kioo cha simu yangu, alikuwa akiitwa Mosses, alikuwa niΒ mwanaume aliyeuteka moyo wangu sana, nilimpenda kwa nguvuΒ zangu zote, hisia zangu ziliniambia Mosses ndiye Mume wangu.Β
Tabasamu lilikuwa limejaa usoni pangu, nilimpigia Mosses iliΒ niweze kusikia sauti yake, sauti ambayo ilikuwa ndiyo tulizoΒ pekee la nafsi yangu!Β
“Hello My love” Nilisikia sauti ya Mosses ikisema, basi moyoΒ wangu ulifurahi sana, wewe msomaji unaweza kuwa shahidi waΒ hili ile furaha unayoipata unapoongea na mpenzi wako nyakatiΒ za asubuhi basi ndiyo iliyonivaa wakati huo. Kwanza nilihemaΒ kidogo ili niweze kumjibu MossesΒ
“Mambo Mpenzi, bado haujaamka?” Nilimuuliza Mosses kwa sautiΒ iliyojaa bashasha. Mosses alinijibuΒ
“Ndiyo naamka Mpenzi, yaani huwezi amini nimetoka kukuwazaΒ muda huu nawe ndiyo unanipigia, hakika tunaishi katika DuniaΒ yetu iliyojaa Huba zito Jacklin” Alisema Mosses, mara zoteΒ alikuwa na maneno matamu sana kwangu kitu ambacho kilinifanyaΒ nizidi kuvutiwa nawe, mara mlango wa chumba changu uligongwa,Β nilisikia sauti ya Mama ikiwa inaniita.Β
“Samahani Mosses, Mama ananiita” nilisemaΒ
“Haya ukimaliza niambie” Alisema MossesΒ
“Sawa Mume wangu mtarajiwa” Nilisema kisha nilimwambia kuwaΒ nampenda sana na kamwe sitoweza kumsaliti. Mara moja nilikataΒ simu, nilinyanyuka kitandani na kwenda kuitika wito wa MamaΒ
“Shikamoo Mama” Nilimsalimia baada ya kuwa nimeshafunguaΒ mlango, nilikuwa nafikicha macho yangu kutokana na MwangaΒ uliokuwa ukimulika macho yangu.
“Marhaba!! Ndiyo unaamka sasa hivi Jacklin? Umesahau kama leoΒ unatakiwa kwenda kwenye Interview?” Alisema MamaΒ
“Oooh Mungu wangu nilishasahau ngoja nijiandae Mama” NilisemaΒ kisha nilikimbilia Bafuni kuoga, siku hiyo ilikuwa ni siku yaΒ Jumatatu nilipaswa kwenda kwenye interview ya kazi katikaΒ kampuni moja ambayo niliomba nafasi miezi michache iliyopita,Β Mama alinitazama hadi nazama Bafuni kisha aliingia chumbaniΒ kwangu na kuanza kukagua vitu vyangu.Β
Aliona kadi za mapenzi ambazo Mosses alikuwa akinitumia,Β alitikisa kichwa chake kisha aliondoka chumbani kwangu.Β
Asubuhi hiyo hiyo, kwenye moja ya jumba la kifahari alikuwepoΒ Mtoto wa kitajiri aliyeitwa Osman, alikuwa mweupe mwenyeΒ asili ya uarabu, ndiye mmiliki wa kampuni ambayo MimiΒ nilitakiwa kwenda kufanyiwa usaili kwa ajili ya kazi, huyuΒ Osman ni Mwanaume mwenye maumivu makali ndani ya moyo wakeΒ kwani miezi miwili iliyopita aliachwa na MwanamkeΒ aliyetarajia kumuowa, Mwanamke huyo aliitwa Zahra, huyo ZahraΒ alitoroka na kiasi kikubwa cha pesa kisha kwenda nje ya Nchi,Β alimtumia ujumbe Osman kuwa hamuhitaji tena katika MaishaΒ yake, tokea siku hiyo Osman amekuwa ni Mwanaume mwenyeΒ kuutafuta upendo wa kweli.Β
Asubuhi hiyo Osman aliondoka kwenye jumba hilo na kuelekeaΒ kwenye kampuni ambayo mimi nilikuwa naenda kufanya usaili,Β kutokana na mvua kubwa kunyesha kulisababisha foleni kubwaΒ iliyoniweka kwa zaidi ya dakika hamsini, nilikuwa tayariΒ Β nimechelewa kwenye Usahili, pembezoni mwangu kulikuwa na gariΒ aina ya Benzi nyeusi, alionekana huyo Osman akiwa anaangaliaΒ sana saa yake, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza namuona, jinsiΒ alivyokuwa akihangaika kuangalia saa yake ilinipa moyo kuwaΒ siyo mimi tu niliyechelewa kwenye jambo bali tupo wengiΒ pasipo kujuwa huyo Mtu ndiye mmiliki wa hiyo kampuni.Β
Nikiwa kwenye daladala, Mosses alinipigia akaniuliza nikoΒ wapi, kiukweli jinsi nilivyokurupuka nyumbani sikuweza hataΒ kumuaga kuwa naenda kwenye Usahili, ilinibidi nimueleze kuwaΒ nipo kwenye daladala naelekea kwenye Usahili ila nimechelewa.Β
“Kama ni hivyo basi chukua pikipiki nitakutumia pesa kidogoΒ ulipe maana hapo utazidi kuchelewa” Alisema Mosses,Β alinifanya nitabasamu, niliona ndiye Mwanaume anayenijaliΒ kuliko Wanaume wote Duniani. Basi nilishuka, nilimuona piaΒ Osman naye akishuka kwenye gari, sote tulitazama upande mmojaΒ tukaita pikipiki moja iliyokuwa karibu, ilitushangaza kuonaΒ sote tunamuita Bodaboda huyo, Osman alinitazama namiΒ nilimtazama kwa sekunde kadhaa kisha alinisogelea sababu yuleΒ Bodaboda alikuwa akija kwangu, si unajuwa tena MwanamkeΒ ananguvu kubwa sana kwa Mwanaume? Basi ndivyo ilivyokuwa kwaΒ Bodaboda huyoΒ
“Samahani Dada yangu naomba usubirie Pikipiki nyingine mimiΒ nina dharura kuna Watu wananisubiria!” Alisema Osman, manenoΒ yake yalinifanya nimuulizeΒ
“Ina maana wewe ndiye mwenye haraka peke yako? Hata MimiΒ nasubiriwa huko ninakoenda hivyo wewe ndiye unayepaswaΒ kusubiria nyingine” Nilisema kwa haiba ya kike, ilikuwa ndiyoΒ mara ya kwanza namuona Osman, sikujuwa kama ndiye mmiliki waΒ hiyo kampuni niliyokuwa naenda kwenye Usahili. BodabodaΒ aliingilia katiΒ
“Kwani wewe Bro unaenda wapi na wewe Sistaa unaenda wapi?”Β Aliuliza Bodaboda huyoΒ
“JM Motors” NilisemaΒ
“JM Motors” Alisema Osman, sote tulijikuta tukiitaja sehemuΒ moja ambayo ndiyo hiyo kampuni ya Uuzaji wa Magari kutokaΒ DubaiΒ
“Sasa si unaona mlitaka kunikosesha pesa za vichwa viwili,Β panda sistaa huyo jamaa aje kwa nyuma” Alisema Bodaboda hukuΒ manyunyu yakianza tenaΒ
“Siwezi kuanza, apande yeye mimi nitakaa nyuma” Nilisema,Β Osman alicheka tu kisha alisemaΒ
“Naitwa Osman Dhabi” alinipatia Mkono kwa lengo la kutakaΒ kunifahamu pia lakini sikutaka mazoea naye kabisa, sikumpaΒ mkono wangu, Osman alitabasamu tu kisha alipanda kwenyeΒ pikipiki kisha nami nilifuatia. Safari ilianza kuelekea JMΒ Motors, Osman alionekana kuwa muongeaji kiasi, niliwasikiaΒ wakiongea kuhusu Wanawake ili sikutaka kujali sana, mwendo waΒ dakika kama 30 hivi tulifika JM Motors huku mvua ikianzaΒ kuchanganya, Niliposhuka tu nilikimbilia kujihifadhi kwenyeΒ maegesho ya Magari nikiwa natetema baridi, Osman alilipa pesaΒ ya Pikipiki kisha yule Bodaboda aliondoka, niliangalia simuΒ yangu kuona kama Mosses alikuwa amenitumia pesa ya PikipikiΒ lakini alikuwa bado hajatuma.Β
Osman alisogea akaniambiaΒ
“Nimeshalipa usijali” Alisema kisha alitabasamu tu, kwanguΒ niliona kama amenidharau hivi, nilifungua pochi yangu nikatoaΒ elfu tano ambayo ndiyo ilibakia hiyo hiyo ya kurudiaΒ nyumbani, nilimpa Osman
“Huwa sipendi vitu vya Bure” Nilisema kwa hasiraΒ
“Samahani sikujuwa kama ungechukia, upo hapa kwa ajili yaΒ Usahili?” AliniulizaΒ
“Ukijuwa itakusaidia nini? Sihitaji mazoea ya kijinga”Β Nilisema kisha niliekea ambako Watu walikuwa wakiingia, OsmanΒ alitabasamu tu akiwa ndani ya Shati jeupe ambalo lilikuwaΒ limeloa na suruali nyeusi iliyomkaa vizuri, moyo wanguΒ uliniambia kuwa Mwanaume huyo alikuwa na mvuto sana ilaΒ alikuwa na dharau.Β
Nilipofika ndani nilielekea mapokezi, niliambiwa kuwa BosiΒ anayepaswa kutufanyia Usahili bado hajafika hivyo nilioneshwaΒ chumba ambacho Watu wanaotakiwa kusahiliwa walikuwepo, wakatiΒ natembea nilihisi kupoteza kitu. Ndiyo, nilisahau BahashaΒ yenye vyeti vyangu ndani ya ile Daladala.Β
Roho iliniuma sana na sikuuona umuhimu wa Usahili tena,Β nilitamani kuondoka lakini yule Mdada alisemaΒ
“Ingia chumba hicho Bosi huyo anakuja” Alikuwa kamaΒ amenishtua hivi, haraka niliekelea kwenye chumba hicho bilaΒ kugeuka nyuma.Β
Nilijaribu kumtumia ujumbe Mosses lakini hakujibu, nilimpigiaΒ lakini hakupokea simu yangu, nilijiona nina mzigo ndani yaΒ moyo wangu, nilimpigia Mama kumueleza hali halisi, aliniambiaΒ kuwa alibakiwa na pesa ile aliyonipa hivyo labda baadayeΒ anaweza akapata kisha akanitumia.Β
Osman alielekea ofisini kwake, alibadilisha nguo zake huko,Β alikuwa ni Kijana wa kisasa na mwenye pesa sana, alikuwaΒ akisimamia miradi mingi ya Baba yake Mzee Dhabi aliyekoΒ Dubai.Β
Tulipaswa kusubiria kwa zaidi ya saa nzima, njaa ilikuwaΒ ikizidi kuniuma, Mdada mmoja aliye jirani yangu aliniambiaΒ
“Jinsi ulivyolowa na unasema umesahau vyeti jiandae kwaΒ maneno ya shombo, huyo Bosi ni kijana tu, msafi sana, alafuΒ mzuri, huoni zimetangazwa nafasi wanawake wengi ndiyoΒ waliojitokeza tena wakiwa wamevalia vizuri zaidi yako!”Β Alisema kwa sauti ya Chini, nilimjibuΒ
“Sikuja kwenye mashindao ya urembo nimekuja kutafuta kazi,Β kama sitopata nitatafuta kwingine, siwezi kuwa Mtumwa waΒ umasikini wangu” Nilimjibu, nilimkata kauli hakusema tena, niΒ kweli alichokuwa amekisema Wasichana walikuwa wakijipodoaΒ sana ili wakiingia huko wakamshawishi huyo Bosi ambaye mimiΒ nimetoka kuzozana naye bila kujuwa.Β
Jina langu lilikuwa la kwanza kuitwa, niliomba niwe wa mwishoΒ sababu nguo zangu zilikuwa zinavuja maji, bahati nzuri MdadaΒ aliyekuja kuniita alinielewa, Basi walianza kwenda hukoΒ pasipo kurudi hadi pale nilipobakia peke yangu ndani yaΒ Chumba hicho. Maneno ya yule Mdada yalizidi kujirudia kwenyeΒ ufahamu wangu, kwa kiasi kikubwa yalianza kunitisha sana.Β Basi, zamu yangu ilipofika nilivuta pumzi kwa nguvu ndaniΒ kisha nilizitoa ili kuondoa hali ya woga ambayo nilionaΒ inaanza kuniandama, nilikuwa kama kichaa hivi sababu nguoΒ bado zilikuwa mbichi, sikuwa na vyeti vya elimu yangu yaΒ Biashara.Β
Nilipiga hatua ndogo ndogo kuelekea kwenye ofisi kwa ajili yaΒ Usahili, nilipoingia nilipigwa na butwaa, nilimuona OsmanΒ akiwa ameinama anaandika jambo, yule Mdada alimwambia OsmanΒ
“Bosi, huyu wa mwisho anaitwa Jacklin, alitakiwa kuwa waΒ kwanza ili hakuwa tayari” Alisema, Osman hakunyanyua machoΒ yake, alisemaΒ
“Sawa anaweza akaketi” Alisema bila kuniangalia usoni,Β nilitamani kuondoka maana kwa jinsi nilivyomjibu vibayaΒ kuanzia kule barabarani hadi tunafika ofisini kwakeΒ sikufikiria kama atanisikiliza, basi niliketi hivyo hivyoΒ kama Mtu aliyeyavulia maji nguo, Sharti ayaoge. NilisubiriaΒ kwa sekunde kadhaa, yule Mdada aliondoka, baadaye OsmanΒ alinyanyua kichwa chake, aliponiona alinitazama kwaΒ kunishangaa kama vile alikuwa hajawahi kuniona.Β
“Karibu” Alisema Osman, jicho lake niliona lilikuwa na ujumbeΒ fulani kwenye hisia zangu, alinitazama kama vile alikuwaΒ akitengeneza kitu alafu akawa anakiangalia kama kipo sawa,Β nilihisi pengine kwasababu nilikuwa nimeloa na pia nilimsemeaΒ vibaya.Β
“Asante!” Nilisema kwa sauti iliyojaa aibuΒ
“Naitwa Osman Dhabi, ni Mmiliki wa kampuni hii, UnaitwaΒ nani?” Aliniuliza kama vile hakuna kilichotokea baina yetu,Β ilinifanya niwe na maswali mengi kichwani kwanguΒ
“Naitwa Jacklin Sembu, nimekuja kwa ajili ya Usahili wa kazi”Β Nilisema nikiwa nimeinamia chini, Osman aliniambiaΒ
“Sina haja ya kukufanyia Usahili sababu nimeshakufanyiaΒ tukiwa njiani, sitaki kuingilia Maisha yako Jacklin lakiniΒ kuna wakati unapaswa kuacha jeuri yako” Alisema kishaΒ alichukua barua akaniambiaΒ
“Hii uje nayo baada ya siku saba, nilihitaji nafasi ya MtuΒ mmoja pekee, nimechagua kufanya kazi na wewe” Alisema Osman,Β nilijikuta nikitabasamu kwa shida sana, ni kweli nilikuwaΒ nahitaji hiyo kazi kwa udi na uvumba lakini niliishiwa manenoΒ ya kuyasema mbele ya Osman, nilijiona nimeelemewa kabisa,Β nafsi ilinisuta nikasemaΒ
“Nashukuru na Mungu akubariki”Β
“Usijali Jacklin, ubaya haulipwi kwa ubaya katu, ubayaΒ hulipwa kwa mazuri yasiyosahaulika” Alisema tena kishaΒ alinipa mkono ambao niliukataa kule barabarani, ilinibidiΒ niupokee, aliuchezea kidogo mkono wangu kwa kunisabahiΒ
“Nakutakia siku njema” Alisema Osman kisha aliendelea na kaziΒ zake, nilinyanyuka kisha niliangalia kiti nilichokaliaΒ niliona kimeloa maji ambayo yalikuwa yakinichuruzika,Β niliondoka ofisini kwa Osman nikiwa mwenye furaha sana.Β Mosses hakunipigia kabisa wakati alisema angenipa pesa yaΒ kulipia usafiri, basi nililazimika kumpigia MamaΒ
“Jacklin Mwanangu sijapata pesa kama unaweza kusubiria hadiΒ jioni sawa” Alisema MamaΒ
“Usijali Mama nitarudi tu” Nilisema, sikuwa na pesa ya nauliΒ ya kurudia nyumbani alafu mvua ilikuwa ikinyesha sana,Β kulikuwa na hali ya radi pia, nilifikiria kama OsmanΒ angelinikuta pale nje ingeleta picha mbaya zaidi, nilifikiriaΒ pia ile pesa niliyompa kwa hasira, nilijilaumu sana kwaΒ kiburi changu. Basi niliingia kwenye mvua, nilivua viatuΒ vyangu. Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Pili Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ


19 Comments
Tamu balaaaa
Nshaanza kuipenda
Hiii mashine
Nice one
Kama naanza kuielewa hivi
Himenifunza kutulia bila papala
Hii naon itakua ya moto sana alafu wifanye iwe ndefu kidogo sasa na matukio mengi mengi kidogo
Aaah weehππ₯°
Hiii imeenda
Ipo vizuri
Najifunza vitu vingi sana kupitia liwaya hizi ππΎ
https://chat.whatsapp.com/K7bQpacPX2oGwBOn19mQ7z
https://chat.whatsapp.com/K7bQpacPX2oGwBOn19mQ7z
Group la mkeka
Oa admini iko poah sanaaaa….achiaaa ilooo dudeee lingneee
Simulizi tamuu sanaa
Simulizi tamuu sanaa
Hii enyewe kabisaππ½..
Nimeipenda
3ttvjp