Ilipoishia “Najuwa unaumia Jojo ila utazoea tu sababu hata Mimi nilikuwaΒ kama wewe siku ya kwanza naanza kazi, nilikuwa mnyonge,Β sikuzoea kuvaa hivi ila ilinibidi nikubali hali halisi”Β
Alisema Shonaa akiwa ananiangalia vizuri kama vile alikuwaΒ akinikagua, nilionesha lile tabasamu fekiΒ
“Kuna nini?” Nilimuuliza, alinishika nywele zangu akazibanaΒ kwa kutumia mpira aliokuwa ameushika mkononiΒ
“Wewe ni mzuri sana Jojo” Alisema kisha aliachia tabasamuΒ lililotoka moyoni mwake kabisa, hata mimi niliachia tabasamuΒ lililotoka moyoniΒ
“Asante!” Nilimshukuru, tulikuwa wawili tu sababu wengineΒ walienda zamu ya Jioni hiyo kurudi hadi asubuhi.
EndeleaΒ
SEHEMU YA TATU
“Vumilia Jojo utakuwa sawa tu” Alisema tena Shonaa kishaΒ alinyanyuka akatoka ndani, alikuwa na moyo wa peke yake, kunaΒ wakati nilijiona nipo sawa pindi ninapozungumza na Shonaa.Β
Nilijilaza kitandani, kutokana na ule uchovu nilijikutaΒ nikipitiwa na Usingizi, niliamka mishale ya saa tatu usiku,Β nilimuona Shonaa akivaa nguo, alivalia Baibui hadiΒ nilishangaa, nilihitaji kumuuliza anaenda wapi?Β
“Shonaa unaenda wapi tena?” Nilimuuliza nikiwa ninatabasamu,Β kiufupi alipendeza sanaΒ
“Naenda kwa Bwana wangu” Alijibu akiwa anajipodoa,Β nilinyanyuka kwanza ili niseme kituΒ
“Bwana wako? Ina maana umeolewa?”Β
“Hapana ni Boyfriend tu, vipi mbona unanishangaa?”Β
“Umependeza sana unaonekana ni mwenye Heshima kubwa snaaΒ Shonaa” Nilisema, nilimfanya achekeΒ
“Ndio nina heshima kwani naonekana sina heshima?” AliniulizaΒ
“Hapana…ninachomaanisha yale mavazi ya kazini yanakufanyaΒ uwe tofauti sana na jinsi ulivyo sasa” NilisemaΒ
“Jojo Maisha haya yatakufundisha vitu vingi sana, yatumieΒ vizuri uone kile ambacho macho yako ya kawaida hayaweziΒ kuona”Β
“Una maana gani Shonaa?”Β
Shonaa hakunijibu chochote, alipomaliza kujiandaa aliondokaΒ zake, nilipata muda wa kuwa peke yangu, usiku huo niliona niΒ bora niwasiliane na Msonjo ili anipe mrejesho wa kileΒ alichozungumza na Bosi Muntaza, nilipiga simu lakiniΒ haikupokelewa hadi baadaye kidogo aliponipigia yeyeΒ
“Griii! Grii!” Ulikuwa ni mlio wa simu yangu, ilikuwa tayariΒ nimepitiwa na Usingizi, niliamka na kuipokeaΒ
“Hallo Msonjo” Nilisema kwa sauti ya uchovuΒ
“Mambo Jojo” Alisema MsonjoΒ
“Mambo mabaya Msonjo vipi umeshaongea na Bosi anipe nauli?”
“Nimeongea naye ila kasema hawezi kupoteza pesa yake kwa MtuΒ ambaye hajafanya kazi yoyote” Alinijibu Msonjo, moyo uliniumaΒ sanaΒ
“Sasa Msonjo….huwezi kuazima sehemu nikifika nitakurudishiaΒ tafadhari”Β
“Mmh! Jojo nisikuongopee hapa sina wa kumuazima pesa,Β ninachoweza kukushauri ni kwamba fanya kazi kwa muda iliΒ uweze kuipata hiyo pesa”.Β
“Yaani Msonjo katika vitu nimebugi katika Maisha yangu basiΒ ni kuja huku Dar, naona kama nipo kwenye chumba chenye gizaΒ na joto kali, najiona mwenyewe tu na sina Mtu wa kunisaidia”Β Nilisema, Chozi lilianza kunilenga, Msonjo aligundua kuwaΒ nakaribia kulia kutokana na jinsi sauti yangu ilivyokuwaΒ ikitoka.Β
“Jojo huna sababu ya Kulia, pambana huko Dar….pengineΒ baadaye unaweza ukabadilisha kauli baada ya kuona mamboΒ yanakunyookea, cha Msingi sasa hivi kaza Buti” Alisema MsonjoΒ kwa maneno rahisi sana, niliona siwezi kuupata MsaadaΒ niliokuwa nautaka kutoka kwake nilimuagaΒ
“Msonjo….nakutakia Usiku mwema” Nilisema kishaΒ jilisikikizia jibu la Msonjo lakiji hakujibu chochote kile,Β nilikata simu na kuanza kulia, niliona kama Msonjo alikuwaΒ ameniuza Jiji Dar, nililitazmaa Begi langu, nilikumbuka ninaΒ elfu kumi tu tena hata Jiji silijui kabisaa.Β
“Eeh Malaika wa Mama yangu naomba Mniongoze, nahisi kushindwaΒ na kukata tamaa kabisa, Mungu unaniona?” Nilisema huku choziΒ likinibubujika, ilikuwa mishale ya saa nne za Usiku. MlangoΒ uligongwa tena mgongaji aliita jina la Shonaa, ilikuwa niΒ sauti ya Mama wa Makamo aliyeonesha kuwa na jazba ya jamboΒ fulani mana jinsi alivyoita Mmh!!Β
“Shonaa hayupo” Nilijibu nikiwa chumbaniΒ
“Njoo wewe” Alisema Mama huyo kwa shari sana, sikumjuwa naΒ wala hakuwa akinijuwa, basi niliingiwa na woga sana nilitokaΒ ndani.Β
“Shikamoo Mama” Nilimsalimu kwa adabu sanaΒ
“Shikamoo mwenyewe, kama unaona hiyo shikamoo Mali basi ikateΒ iweke kwenye sufuria igeuke nyama ya Mbuzi…hivi nyieΒ mnatuchukuliaje humu ndani?” Aliuliza kwa shari ile ile
“Kwani kuna nini Mama yangu” Nilimuuliza maana woga ulikuwaΒ umenishikaΒ
“Hebu twende” Alinishika mkono kwa nguvu akawa ananipelekaΒ njia ya Chooni, aliniingiza hadi chooniΒ
“Nini kile?” Alionesha kidole kwenye karo la Choo, Aah yaaniΒ kulikuwa na haja kubwa iliyokuwa haijamwagiwa majiΒ
“Hizo pombe mnazokunywa sisi tumekunywa kitambo na tukaziachaΒ sababu hazina faida yoyote, wenyewe mnaona Ujanja si ndiyo?Β Sasa safisha hapo haraka sana nataka kuoga” Alisema Mama huyoΒ kwa hasira sanaΒ
“Lakini Mama mimi ni mgeni hapa na sijui chochote kile”Β Nilijitetea kwa sauti ya chini sana, mkononi nilikuwaΒ nimeshikilia simu yangu ndogo, sasa yule Mama alinisukumizaΒ nishike Fagio, simu ikaangukia kwenye shimo la chooΒ
“Simu yangu” Nilisema kwa maumivu makali sana, simu ileΒ ilikuwa ndio msaada mkubwa kwangu kuwasiliana na Msonjo naΒ Watu wengine ambao walikuwa Tabora.Β
“Nyooo! Usinilegezee sauti, hebu fanya Usafi fastaa” AlisemaΒ Mama huyo, kwa jisni alivyochukia ilinilazimu haraka sanaΒ kushika fagio, Mama huyo alitoka nje. Macho yangu yalijaaΒ machozi ya maumivu makali sana niliwaza ndani ya akili yanguΒ
“Haya ndiyo Maisha gani jamani ni Bora ningekufa njaa Tabora,Β Mama umeniacha unaona sasa yanayonikuta Mwanao” NilijisemeaΒ huku chozi likizidi kunibubujika, nilifanya Usafi nikiwaΒ ninalia hadi nilipomaliza kisha nilitokaΒ
“Subiria hapo hapo niangalie Kama umesafisha vizuri” AlisemaΒ Mama huyo kisha aliingia chooni kuangalia, baada ya sekundeΒ chache alitokaΒ
“Bahati yako, haya sepa” Alisema, nilimuogopa mno, ilinibidiΒ haraka nishike njia ya kurudi ndani, nyuma nilisikia sautiΒ yake akicheka kisha alisemaΒ
“Mjini shule” Jamani niliumia sana, moyo ulimwaga chozi laΒ damu lenye Maumivu, nilikuwa Msichana mpole sana ambayeΒ sikuweza kujibizana na Mtu yeyote yule.Β
Nilipofika chumbani niliongeza kilio, Chozi lilinimwagikaΒ nikiwa nimejitupa kitandani. Jiji la Dar liligeuka kuwaΒ chungu sana kwangu, kabla hata sijatulia nilisikia tenaΒ Mlango ukigongwa, niliogopa sana nilijifuta chozi harakaΒ kisha niliuliza
“Nani?” Niliuliza kwa sauti ya upole mno tena iliyojaa wogaΒ
“Fungua wewe” nilisikia sauti ya Mdada mmoja ambayeΒ tulimuacha akiwa amelala asubuhi, ilikuwa ni sautiΒ iliyoambatana na Ulevi.Β
Mara moja nilienda kumfungulia, ile nafungua tu nilikutana naΒ tusi la nguoni, tena aliyetukanwa alikuwa ni Marehemu MamaΒ yangu MasikiniΒ
“Malaya wewe! Unajiona mzuri ndio hufungui mlango eeeh?”Β Alisema yule Mdada, nilichukia sana kisha nilienda chumbaniΒ wala sikutaka kubishana naye. Alikuwa ameongozana naΒ Mwanaume, wote walikuja chumbani.Β
Yaani kilichonikausha kilio changu kilikuwa ni kitendo chaoΒ cha kuondoa nguo zao zote kisha kuanza kufanya mapenzi mbeleΒ yangu bila hata Aibu, sikuweza kuwavumilia nilitoka chumbani,Β kelele zao zilikuwa juu hata sebleni niliona hapakuwa salamaΒ kwangu, nilienda nje kabisa. Ndani ya muda mfupi nilikutanaΒ na matukio yaliyoniacha kinywa wazi, mambo ambayo nilikuwaΒ nasimuliwa na Watu kuwa wameona katika filamu ndiyo nilikuwaΒ nikiyashuhudia kwa macho yangu, nilitamani sana kumpigia simuΒ Shonaa nimueleze maana angalau yeye tulikuwa tukiiva chunguΒ kimoja lakini ndiyo hivyo tena simu ilikuwa imeingia Chooni.Β
Nilikaa nje kwa zaidi ya Masaa mawili nikiwa ninalia, baadayeΒ nilirudi ndani, palikuwa pametulia, basi nilifunga mlangoΒ kisha nilijilaza kwenye kochi nikiwa nimevalia zangu dera.Β
Sijui hata ilikuwa ni saa ngapi, nilishtuka tu nilihisi mkonoΒ ukinichezea makalio yangu, nilipoamka nilimuona yule MwanaumeΒ ambaye alikuja na yule Mdada. NilimuulizaΒ
“Wewe ni Nani na Unataka nini?” Niliuliza huku nikiwaΒ nimejaza woga kwenye kifua changu, nilijisogeza nyuma kabisaΒ ya KochiΒ
“Shiii” Alinipa ishara kuwa sipaswi kusema chochote kile,Β alitoa kisu akaniambiaΒ
“Ukipiga kelele Nakuchoma kisu sasa hivi” Alisema akiwaΒ ananionesha na ishara kabisa jinsi atakavyo nichoma hichoΒ kisu.Β
Kwa mara ya kwanza katika Maisha yangu niliona MunguΒ amenitazama, yule Mdada alikuwa ameamka hakumuona Mtu wakeΒ hivyo akaja sebleni na kukuta yule jamaa akiwa amenishikiliaΒ kisu, aliposikia sauti ya Mwanamke wake alikitupa kile kisu.Β
Bahati nzuri taa ilikuwa inawaka maana nilikuwa siwezi kulalaΒ bila taa, alikiona kile kisuΒ
“Unaniacha chumbani unakuja kwa huyu Malaya si ndiyo?”Β Alisema yule Mdada, nilihema juu juuΒ
“Unafanya nini hapa?” Alihoji yule Mdada, alimshushia kipigoΒ yule Mwanaume hadi nilishangaa, Mwanamke anaweza vipi kumpigaΒ Mwanaume namna ile? Hadi niliingilia kati maana alishamtoaΒ damu kinywaniΒ
“Wewe malaya hayakuhusu haya, una kesi na Mimi kwahiyo subiriΒ hivyo hivyo” Alisema yule Mdada, basi aliendelea kumpiga,Β alipochoka alimwambiaΒ
“Tembea nisikuone tena hapa Shwaini Mkubwa wewe” Alisema yuleΒ Mdada, yule Jamaa aliposikia hivyo aliona kama vile alikuwaΒ ametembelewa na Malaika mtoa roho alafu akamuacha basiΒ alijipigiza kwenye mlango akafungua na kukimbia zake,Β nilijikuta nikicheka japo kwa sauti ya chini maana Yule MdadaΒ naye alicheka kidogo kisha aliacha kucheka alafu akaniangaliaΒ kwa jicho kaliΒ
“Ukijilegeza utaliwa!” Alisema yule mdada kisha aliongozaΒ kuelekea chumbaniΒ
“Samahani”nilisema kwa woga, alisimamaΒ
“Unaitwa Nani?” Nilimuuliza, alicheka kisha alinijibu “Sarafina” Alijibu na kuingia chumbani.Β
Japo mambo yale yalikuwa mageni kwangu na yenye kuniumiza ilaΒ yalinifundisha vitu vingi sana ambavyo hata kama ningesomaΒ hadi ngazi ya digrii nisingeliweza kujifunza. UsingiziΒ haukuja kabisaa nilikaa macho hadi niliposikia adhanaΒ wakiazini msikiti wa jirani ndipo nilipofahamu kuwa palikuwaΒ pamepambazuka.Β
Tulikuwa na zamu ya kwenda kule Dar City Mimi na Shonaa,Β nilijiandaa. Muda ulienda nikiwa ninamsubiria Shonaa, JuaΒ lilipoanza kutua Shonaa alirudi akiwa mwenye furaha,Β alinionesha kiasi cha pesa alichokiingiza.Β
Kilikuwa ni zaidi ya laki moja, niliitamani pesa hiyo maanaΒ kama ningeliipata basi ingenitosha kwa Nauli ya kuelekeaΒ Tabora, aliketi lakini aliniona nikiwa sina fruaha kabisa. Nini Kitaendelea
Usikose SEHEMU YA NNE ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx
7 Comments
Kazi nzur sanah panaanza kuchangamka
Mimi mgeni jamn lakin nimeipenda san
Adimin una pepo yako pekee
Jinsi ilvyo nikiisoma navuta picha kma naitzma kwnye Tv ani
Ni dar tu ndo wanaume wanapigwa na wanawake
Daah masikin msonjo umemponza mtoto wa watu
ntbybi