Ilipoishia “Fanya haraka” Akaelekezwa mahali ambapo angemwona Matilda,Β japo dakika mbili zisingetoshea kuzungumza naye ila alihitajiΒ kumwona na kupata uhakika kua ana Mtoto na Bosi wake,Β akapelekwa chumba kimoja ambacho kilikua rasmi kwa ajili yaΒ kuonana na Mahabusu, akasubiria hapo Matilda aletwe, sekundeΒ chache Matilda akafika hapo akiwa ameongozana na yule PolisiΒ
Hakumkumbuka Jack sababu alimwona kwa Mara ya kwanza paleΒ ofisini kwa James hivyo ilikua rahisi kwake kukubali kuonanaΒ na Jack, akaketi huku akiwa anamtazama sana JackΒ
“Samahani na pole Matilda, Naitwa Jack” Alijitambulisha JackΒ
“Unanifahamu Mimi?” akauliza Matilda akionekana alikuaΒ ameteswa sana, uso ulikua na majeraha kadhaaΒ
“Ndiyo nakufahamu japo si sana”Β Endelea
SEHEMU YA SITAΒ
“Mbona Mimi sikufahamu?” akauliza MatildaΒ
“Mimi ni mfanyakazi wa James, nimekuja nahitaji kujua baadhiΒ ya vitu kutoka kwako” Akasema JackΒ
“Kwahiyo James amekutuma uje kwangu unilaghai kwa kutegemeaΒ kua nitakubali si ndiyo, sikia nikwambie kitu kimoja,Β Nimeamua kuishi Maisha ambayo sitaki kuitwa Msaliti na MtotoΒ wangu, nitasimama naye hadi mwisho na kama unafikiria utawezaΒ basi nakwambia katu hautoweza kunishawishi kwa chochote kile,Β nenda kamwambie James, kama Mtoto wangu atakufa basi atabebaΒ msalaba na kamwe sitakubali” Alisema kwa hasira sana MatildaΒ hadi yule polisi akaona ni bora amrejeshe Mahabusu maanaΒ kusingezungumzika kabisaΒ
“Sina nia hiyo Matilda nakuomba unisikilize” akazungumzaΒ lakini Matilda aliondolewa hapo, kisha baadaye yule polisiΒ akamfuata JackΒ
“Usirudi tena, hii ilikua nafasi pekee”Β
“Lakini sikua na nia ya kumkasirisha kabisa, nilihitajiΒ kumsaidia” Akasema JackΒ
“Hayo hayanihusu Mimi, nimetenda wema niliopaswa kukutendea,Β utamsaidiaje ni juu yako” Akasema Polisi huku akimtaka JackΒ aondoke Kiunyonge sana tofauti na alivyoingia kituoni, JackΒ alionekana akishusha ngazi kwa kutumia kiatu chake kirefu,Β Macho yake yakatua waliposimama Mchungaji na Mama Naomi, MaraΒ moja wakasogea karibu kumpokeaΒ
“Vipi umefanikiwa kumwona?” akauliza MchungajiΒ
“Anaendeleaje?” akauliza Mama Naomi huku nyuso zao zikioneshaΒ shahuku kubwa ya kutaka kujua kilichotokea huko ndaniΒ
“Hataki kuzungumza na Mimi, inaonesha ana maumivu makaliΒ sana” Akasema Jack akiwa anasogea karibu na gari yake,Β Mchungaji na Mama Naomi wakiwa wanamfuataΒ
“Yupo salama?” akauliza Mchungaji, Jack akatikisa kichwa kamaΒ ishara ya kua Matilda hayupo salama.Β
“Niambie Matilda amekuaje?” alihoji Mchungaji, yeye ndiyeΒ aliyempokea Matilda kanisani kwa mara ya kwanza. hivyoΒ Matilda kwake ni sawa na Mtoto wa kumzaa.Β
“Siwezi kuzungumza nahitaji kutuliza akili kuona ninamsaidiaΒ vipi, Tutawasiliana” akasema Jack kisha akaingia kwenye gariΒ yake na kuondoka hapo haraka sana, akawaacha Mchungaji naΒ Mama Naomi wakiwa hawajui kilichoendelea kati ya Jack naΒ Matilda.Β
“Ni bora angeeleza kiilichotokea kuliko kukaa kimya, hapanaΒ shaka amemwona Matilda, roho inaniuma sana” Alisema MamaΒ Naomi akionekana kujawa na uchungu, chozi lilimlenga, alikuaΒ hajatulia tokea asubuhi kwa ajili ya MatildaΒ
“Naomba urudi nyumbani giza linaanza kuingia, pesa hiiΒ itakusaidia. Mimi narudi kanisani kwa ajili yaΒ maombi….Najua shetani yupo mahali anafanya kazi yake”Β Akasema Mchungaji kisha akampatia noti ya Elfu Kumi MamaΒ NaomiΒ
“Lakini Mchungaji natamani nilale hapa ili nijue MatildaΒ anapitia wakati gani, naona kama tunamzika Matilda bilaΒ kusikia kilio chake” Akasema Mama Naomi akiwa ameshika notiΒ mkononi huku chozi likianza kuvujaΒ
“Usilie..Hakuna marefu yasiyo na Ncha, kua na imani kua MunguΒ atatenda na Matilda atatoka”
“Sawa Mchungaji” Alisema Mama Naomi, akaita Bajaji kwa ajiliΒ ya kurejea anapoishi maana kwa muda huo ingekua shughuli pevuΒ kupata daladala, kwa wanaoishi Dar wanajua liingiapo gizaΒ vurugu za kugombania usafiri zinavyochukua sura tofauti.Β
Mchungaji alisubiria hadi Mama Naomi alipoondoka ndipo nayeΒ akaondoka kituoni.Β
********Β
Mawazo chungu mzima yalikua yakipita kwenye kichwa chaΒ Bilionea James, alikunywa pombe ili kuondoa mawazo yaliyokuaΒ kichwani pake, moyo wake haukua na pingamizi kua Mtoto PatraΒ alikua ni damu yake lakini Neema alikua na ujauzito ambaoΒ aliamini wazi ni wake.Β
Alikua na tumaini kubwa la kupata Mtoto ambaye angekuja kuaΒ Mrithi wa utajiri wake uliokithiri, hakupokea simu ya NeemaΒ wala Mama yake Neema, alizidi kuchanganikiwa, licha yaΒ utajiri alio nao lakini alijikuta katika wakati mgumu sanaΒ kisa Mtoto, akifikiria namna Matilda na Mtoto wanavyotesekaΒ anajikuta akikuna kichwa chake, alitamani sana kumsaidiaΒ Matilda lakini pia wazo la kua Mtoto afe lilikua likimtawala,Β kauli ya Matilda kua atahakikisha anamfilisi ilianza kumyimaΒ raha, akamtafuta Chilo ili apate ushauriΒ
“Yupo sahihi sababu ana Mtoto ambaye akipimwa DNAΒ itagundulika wazi ni wako, akikufungulia kesi unafikiriaΒ utatokea wapi Kaka? Hii serikali haiangalii una pesa kiasiΒ gani, kwa kifupi alichosema ana uhakika nacho James” AlisemaΒ Chilo wakiwa wameketi mahali wakipeana UshauriΒ
“Sasa nifanye nini, Nimhudumie Mtoto kisha nimtoe Matilda?”Β
“Kama amekataa kurejea kwao hata kama utafanya yote badoΒ atakugandamiza James, Kama nilivyokwambia serikali ipo machoΒ sana kwa kesi za namna hii”Β
“Sasa unanishauri lipi Kaka”Β
“Kubali kua Patra ni Binti yako, mlee kama Binti yako, mfanyeΒ Matilda aone mpo pamoja kisha mfanye wa siri ili Neema asijueΒ chochote hadi pale atakapojifungua”Β
“Ushauri wako ni mzuri sana, nimetafakari usiku kuchaΒ nawezaje kumaliza hili jambo katika namna ambayo itaniachaΒ salama”Β
“Ikishindikana njia hiyo Kaka juwa kua hilo jambo ni gumuΒ kuliko ufikiliavyo, hapana shaka Matilda ana hasira naweΒ kwasababu anahisi wewe umeshilikiana na Neema ili kumwekaΒ yeye ndani” Alisema ChiloΒ
“Naamini Patra akipatiwa matibabu hilo haliwezi kua shida kwaΒ Matilda, ikibidi nitamtibia nje ya Nchi ili Matilda aende naΒ Mtoto huko, hadi wao watakaporejea Nchini nitakuwaΒ nimejipanga vizuri kuhakikisha hakuna kinachoharibika”Β
“Tena hapo utakua umeuwa ndege wawili kwa jiwe moja Kaka,Β Acha Neema aamini kua Matilda amerudi kwao lakini upande waΒ pili unapambana kuhakikisha anatibiwa, naamini utashinda”Β
Haikua rahisi kwa Jack kupata Usingizi usiku huo, taswira yaΒ Patra namna anavyoteseka Hospitalini iliendelea kujirudiaΒ katika Ufahamu wake wa akili, alijikuta akiwa katika nyakatiΒ ambayo kila alichokiwaza kilizidi kuibomoa akili yake, ikawaΒ ngumu kuukubali ukweli kua Bosi wake James alikua ametendaΒ unyama ule.Β
*****Β
Asubuhi mapema, Jack akaondoka katika makazi yake, alifungaΒ safari kuelekea kwa Mama yake James. Naam! alihitaji zaidiΒ kujua baadhi ya mambo ambayo yangemfanya apate njia yaΒ kulianza jambo hilo ambalo aliona wazi lilimhitaji kwa kiasiΒ kikubwa, alipahafahamu kwa Mama yake James, hata Mama yakeΒ James alikua akimfahamu sana Jack, alipomwona alimkaribishaΒ ndani.Β
Jua lilikua tayari limeshaanza kuchoma na kuunguza ngozi,Β chai ikawa tayari, wakaketi mezani kwa ajili ya kuzungumza,Β Mama James alishagundua kua kuna jambo lililomleta Jack paleΒ
“Karibu sana Jacklin” Alisema Mama yake JamesΒ
“Ahsante Mama”Β
“Umenisusa sana Mwanangu”Β
“Aaah Mama unajua majukumu ni mengi nakosa hata muda wa kujaΒ huku siku hizi”Β
“Wala usijali naelewa”Β
“Mama kuna jambo linanitatiza sana katika akili yangu,Β limekua ni jambo lililobadili kabisa mtazamo wangu juu yaΒ James” Alisema Jack kisha alimtazama Mama yake James ambayeΒ alikaa vizuri kumsikiliza huku chai ikiwa inatoa mvuke
“Jambo lipi hilo mbona unanitisha Jack”Β
“Mama….sijui hata nianzie wapi, naomba kujua, James anaΒ watoto wangapi?” aliuliza Jack, Mama James akashusha pumziΒ baada ya kusikia swali hiloΒ
“James hana Mtoto..”Β
“Una hakika Mama?”Β
“Jack, Mimi ndiye Mama Mzazi wa James, akiwa na jambo niΒ lazima anishirikishe……Hajawahi niambia chochote kileΒ kuhusu kua na Mtoto, isipokua yupo Msichana anayetarajiaΒ kumzalia Mtoto, huyu namfahamu sababu alishawahi kumletaΒ Hapa, zaidi ya hapo hakuna Jack…sijui ni kwanini umeulizaΒ Β hilo swali”Β
“Mama naomba nikwambie hili jambo, pengine nitatua mzigoΒ fulani kichwani pangu, James ana Mtoto ana miaka mitatu sasaΒ anaitwa Patra” Alisema Jack, Mama James akashtuka kidogoΒ
“James ana Mtoto? hilo haliwezekani Jack, hawezi kua na MtotoΒ alafu anifiche Mimi, angeniambia tu” akasema Mama JamesΒ
“Hata Mimi nilishtuka na sikuamini kama wewe ambavyo huamini,Β Mama,,James kua na Mtoto siyo tatizo ila tatizo ni kwanbaΒ amemkataa huyo Mtoto kwasababu ni Mlemavu, na HapaΒ ninapozungumza Mtoto huyo yupo Hospitali Magomeni hali yakeΒ siyo nzuri, Mama wa Mtoto yupo polisi kwa kesi ambayoΒ inaonekana wazi kua James ameitengeneza…”Β
“Jack hivi unajua unazungumza maneno mazito sana ambayoΒ hayaingii akilini mwangu, James hajawahi niambia kua anaΒ Mtoto. Hili jipya kulisikia.”Β
“Mama hiyo ndiyo hali halisi, Mtoto amefanana sana na James.Β Nimekuja hapa sababu sitaki Mjukuu wako azidi kuteseka,Β sikujua kama James hakukwambia kuhusu hili, Mama nakuombaΒ fanya jambo katika hili vinginevyo Mtoto anaweza kufarikiΒ kule Hospitalini” Akasema Jack akiwa na uso ulio poteza nuru,Β alihitaji huruma ya Mama James kuingilia kati huku akiaminiΒ fika kua si rahisi kumfikia James ambaye ndiye Bosi wakeΒ
“Jack nahitaji kwanza kumwona huyo Mtoto ”Β
“Kama tunaweza ongozana Hospitali muda huu itakua vizuriΒ Mama”
“Sawa!!” Mama James na Jack wakakubaliana kua waelekeeΒ Hospitali kwa ajili ya kumwona Patra.Β
Asubuhi hiyo, Neema akaelekea kituo cha polisi, akazungumzaΒ na yule polisi ambaye alishapewa pesa ili kumshikiliaΒ Matilda, wakazungumza kwa dakika kadhaa kisha Neema akaondokaΒ hapo, kitendo cha kupokea simu ya polisi kua James aliendaΒ Polisi kilimfanya atengeneze mpango mwingine kwa ajili yaΒ kutekeleza takwa lake kwa Matilda ambaye kadili mudaΒ ulivyokua ukienda alikua akiendelea kuteseka pale kituo chaΒ polisi, yule polisi akarudi ndani ya kituo maana maongeziΒ yalifanyika ndani ya gari ya Neema.Β
Masaa matatu yakapita baada ya polisi kuzungumza na Neema,Β Mchungaji George alikua nje ya kituo hicho huku akimpa MamaΒ Naomi jukumu la kushinda kule Hospitali, gari ya polisiΒ ikatoka. Mchungaji akaitazama sana gari hiyo pasipo kujuaΒ kulikua na mpango ambao Neema alikua amepanga kuufanya.Β Matilda alikua akihamishwa hapo kituoni muda huo huku ndaniΒ ya kituo cha polisi kukiwa na jarada la kuachwa huru kwaΒ Matilda, nje kidogo ya kituo Neema aliingia kwenye gari baadaΒ ya kuliona gari la Polisi likitoka hapo, akalifuata kwaΒ nyuma.Β
*********Β
“Dada, huyu ni Mama yake James” Ilikua ni sauti ya Jack, MamaΒ Naomi alimuona Mama James kwa mara ya kwanza, akamsalimia kwaΒ heshima sanaΒ
“Mama huyu ni kama ndugu kwa Matilda ndiye anayeshinda hapaΒ Hospitali kuangalia hali ya Mjukuu wako” Alisema Jack, MamaΒ James hakutaka kuyaamini maneno ya Jack hadi paleΒ atakapomwona Patra, wakapewa ruhusa na Daktari kishaΒ wakaingia ndani ya wodi, Mama James akamwona Patra kwa maraΒ ya kwanza, alikua katika Mshangao Mkubwa sana, sura ya PatraΒ ilikua imefanana sana na sura ya James, Chozi la Mama JamesΒ likaanza kutiririka kila alivyozidi kumwangalia Patra, siyoΒ tu kwasababu ni Mjukuu wake bali kilichomliza ni jinsiΒ ambavyo Patra alikua juu ya kitanda akipigania uhai wake,Β Mashine pekee ndizo zilizokua zikimpa uhai Mtoto huyoΒ
“Kwanini hukuniambia James?” aliuliza Mama yake James akiwaΒ ameshikilia kitanda kwa uchungu mkubwa sana, Jack akasogea naΒ kumshika Mkono Mama James akimtaka atulize hasira zakeΒ
“Mama hiyo ndiyo hali halisi, jinsi unavyoumia wewe ndivyoΒ ambavyo Mama wa Mtoto huyu anaumia akiwa kituo cha polisi”Β Alisema Jack huku Mama Naomi akiwa ametulia kimya
“Jack, miaka yangu 65 katika huu uso wa Dunia, sikuwahiΒ kuumia kama ambavyo leo naumia, hili ni Pigo Takatifu kwangu,Β najiuliza kwanini James hakutaka kusema juu ya ujauzito hadiΒ Mtoto anazaliwa, Sina Mtoto mwingine zaidi ya James, pengineΒ sina Mjukuu zaidi ya huyu aliyelala hapa, lazima nipiganieΒ uhai wake” Alisema Mama yake James.Β
“Lakini Mama pamoja na yote, sitaki James agundue kua MimiΒ ndiye niliyekupa hizi taarifa”Β
“Hilo usijali Jack, kikubwa ni huyu Mtoto awe salama,Β atahamishwa hapa na kutibiwa kwa siri, kwakua James alimkataaΒ huyu Mimi nitalifanya hili kwa siri sana, pia nipo tayariΒ kuandaa wakili kwa ajili ya huyo Msichana aliye polisi,Β nitalimaliza hili bila kuharibu upande wowote ule” AkasemaΒ Mama yake JamesΒ
Muda wote huo Mama yake Naomi alikua akilia kwa furaha baadaΒ ya mzigo huo kutuliwa, mzigo ulikua mzito upande wao maanaΒ ilikua ni ngumu sana kupata pesa za matibabu ya Mtoto.Β
Mama James akazungumza na uongozi wa Hospitali kwa ajili yaΒ kumhamisha Patra kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya Upasuaji,Β jambo hilo likafanyika haraka sana, Gari maalum ya wagonjwaΒ ikaondoka na Patra na Mama Naomi huku Jack na Mama JamesΒ Β
wakielekea Polisi kwa ajili ya kuzungumza na Matilda, hadiΒ kufikia muda huo hakuna aliyajua kua Matilda alikuaΒ ameondolewa kituo cha polisi huku mpango huo ukisukwa naΒ Neema.Β
Safari ya gari ya polisi ilikua ni nje kabisa ya Jiji laΒ Dar-es-salaam, palikua na jumba moja lililo kando ya Msitu,Β Matilda akaingizwa ndani ya jumba hilo lililoonekana kutuliaΒ sana, Neema akaingia pia.Β
“Kua Makini nimefanya kwa upande wangu, nahitaji hicho kiasiΒ kabla ya kupambazuka ili kama kuna kitakachotokea nisife kamaΒ Mzoga” Akasema Polisi ambaye alicheza mchezo huo waΒ kumhamisha Matilda na kuaandaa Jarada kua aliachiwa huruΒ
“Ndani ya Masaa 12 kuanzia sasa kiasi kitakua ndani yaΒ akaunti yako, ondoa shaka. Ahsante kwa hili, nikwambie tu kuaΒ kazi yako imeishia hapa lakini si mwisho wa Mimi na wewe, huuΒ ni mwanzo mzuri” Alisema Neema kisha akatoa bahasha ambayoΒ ilikua imetuna akampatia Polisi huyo, Polisi akachunguliaΒ akaona alichokiona ambacho kilimfanya atabasamu, kishaΒ akaondoka hapo mara moja.
Matilda hakujua amepelekwa wapi, Nani aliye nyuma ya mchezoΒ huo, mara akasikia mlango ukifunguliwa katika chumba ambachoΒ alikuwepo, akamwona Neema akiingia, aliongozana na WanaumeΒ wawili ambao walijazia vizuri, Matilda hakusema chochoteΒ baada ya kumwona NeemaΒ
“Ulihisi natania Matilda, pengine hujui wewe ni kikwazo kiasiΒ gani katika mipango yangu, uwepo wako ni tatizo kubwa kwangu”Β Alisema NeemaΒ
“Mimi sijakuzuia kumzalia James, lakini siwezi kuishiΒ mafichoni kisa wewe” Akasema Matilda, akapigwa kofiΒ
“Hivi unajua unazungumza nini wewe Mshenzi? James ana MtotoΒ mmoja tu, huyu aliye tumboni na si vinginevyo, kwanini unakuaΒ king’ang’anizi, sasa utakua hapa na Dunia itakutafuta sanaΒ Matilda, hakuna atakayekuja kukusaidia hapa, na kamaΒ utaendelea kuleta ubishi basi nitamuuwa Binti yako” AlisemaΒ Neema, alionesha wazi kua hakua Mtu wa masiala kabisaΒ
“Unasemaje….Umuuwe Mtoto wangu? laiti kama kitamkutaΒ chochote Patra basi nitakulipiza”Β
“Hata haumaanishi, utatokaje hapa hilo ni suala unalopaswaΒ kujiuliza kisha ndiyo uwaze utanizuia vipi…” Neema akatoaΒ simu yake kisha akamwonesha video ambayo ilivuruga akili yaΒ Matilda, video hiyo ilimwonesha Neema akiwa katika wodiΒ ambayo Patra alikua amelazwa, ilimdhihirishia wazi MatildaΒ kua Neema anaweza akafanya chochote kwa ajili ya kumdhuruΒ Patra.Β
Tayari Mama James na Jack walikua wamefika kituoni, wakatoaΒ maelezo kua wanahitaji kumwona Matilda, wakaambiwa kuaΒ Matilda alikua ameachiwa huru muda mchache uliopita,Β iliwashangaza sana sababu kama angelikua ameachiwa huru basiΒ wangemwonaΒ
“Afande Mimi nimekaa hapo nje kwa takribani masaa matano,Β kama angekua ameachiwa basi ningemwona lakini sikumwona hebuΒ angalia vizuri” Akadakia Mchungaji GeorgeΒ
“Jarada lake hili hapa, sisi tunafanya kazi kwa maandishi,Β tayari ameachiwa huru. Hatukuona sababu ya kumshikilia kwaniΒ Mlalamikaji alikuja na kusema kua haitaji kuendelea na kesi”Β Alisema tena yule polisiΒ
“Polisi Mimi ni Mama wa mlalamikaji, nimekuja kwa ajili yaΒ kumwona huyo Binti tafadhali” Alisema Mama James
“Jamani nimeshawaambia kua Msichana ameachiwa, jukumu laΒ kujua yupo wapi ni la kwenu sababu kwetu ameshatoka”Β Akasistiza polisi huku akionekana haitaji kuendelea kubishanaΒ naoΒ
Taratibu watatu wakashusha ngazi hadi chini, Jack akapigaΒ simu Hospitali ambako walikua wameenda kwa ajili ya Matibabu,Β wakapata taarifa kua Matilda hakwenda huko. Taharuki ikawaΒ kubwa, hakuna aliyejua mahali ambapo Matilda alikua ameendaΒ
“Sasa atakua ameenda wapi au ameelekea kule Hospitali ambakoΒ Mtoto amehamishwa?” akauliza Jack, akili zao zikawaza kwaΒ pamoja kua huwenda Matilda akawa ameenda huko, mara moja MamaΒ James na Jack wakaelekea Magomeni ilipo Hospitali ya JM.Β
Wakati wao wanatoka kituo cha polisi, gari nyingine nyeusi yaΒ kifahari ikaingia hapo, akashuka James, yaani kama angewahiΒ kidogo tu angekutana na Mama yake na Mfanyakazi wake hapoΒ Kituoni, James alihitaji kuzungumza na Matilda, hakujua kuaΒ Matilda alikua ameondolewa hapo na Neema, akaingia naΒ kujitambulisha, akapewa maelezo yale yale ambayo Akina JackΒ walipewa, haraka akatoka hapo akajaribu kuipiga simu ya Matilda lakini haikuita, akampigiaΒ simu NeemaΒ
“Neema Nahitaji kuongea nawe sasa hivi, nieleze mahali ulipo”Β Akasema James, akaelezwa mahali ambapo Neema alikuwepo,Β akawasha gari kuelekea huko.Β
Ilikua ni nje kabisa ya Mji, kitu ambacho kilianza kumpaΒ Mashaka James, akasogea hadi kwenye jengo ambalo NeemaΒ alikuwa amemuelekeza James aende, Palikua ni msituni. JengoΒ hilo lilikua katika eneo la peke yake kabisa, JamesΒ aliposhuka macho yake yakawa kwenye jengo hilo lililo kimyaΒ sana, James akasogea kama alivyoelekezwa na NeemaΒ
Alipoingia alisikia sauti ya Matilda ikiita, akashtuka sanaΒ akaenda hadi kwenye hicho chumba akamkuta Matilda akiwaΒ amefungwa kambaΒ
“Matilda?” akaita James kisha akamkimbilia Matilda alipokuaΒ amekaa, Chozi lilikua likimbubujika Matilda, James akamwambiaΒ MatildaΒ
“Nataka nikutoe hapa sawa?” Akawa anafungua kamba lakiniΒ akasikia Watu wakija kwenye chumba hicho, James akashtuka,Β alipogeuka akamwona Neema, Masudi na wanaume wengine wawiliΒ
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SITA Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
10 Comments
Leo wa kwanza Mimi jamani but story is very very π₯π₯π₯
Mambo ni motooo
Jins nlivyonashauku natamn miendelez Sasa hv
Wow nautamani uo mwisho wa neemaπ₯
Inavitia kuendelea kusoma hadi rahaaa,tuone ni kitakiri kwa jemsi na maltida wake
Daaaah jmn huyu Neema ana roho mbaya kiasi hiki πππ
Yaani hi dunia jamaa anapigania mimba ambayo syo yake ..wanaume tuna tabu sana..
Adimini una baya ukifa uhozi ukiozo unuki twend Kaz sanaoma simulizi kama naangalia TV yan yan dah
Namuona James akitapeliwa, Neema kuishia pabaya
r97ubn