Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Ligi Kuu Bara Iko Kwenye Vita Ya Mfungaji Bora Kiungo
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Ligi Kuu Bara Iko Kwenye Vita Ya Mfungaji Bora Kiungo

    Living ShayoBy Living ShayoApril 16, 2024Updated:April 16, 202411 Comments4 Mins Read999 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Ligi Kuu
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ligi kuu ya NBC imefikia mzunguko wa 22Β  ikiwa ni raundi ya pili ya msimu huu 2023/2024 msimu ambao umekuwa na mabadiliko makubwa sana kuanzia viwanja, udhamini kwa vilabu, jezi na namna ya uchezaji kiwanjani.

    Lakini pia ndiyo msimu ambao umeshuhudia ukiwa na wageni wengi waliyoonyesha ubora wa kiwango kile ambacho muda mrefu tulitamani kukiona, siyo kwa wageni wa Simba na Yanga tu bali hata Tabora Utd, Azam FC, Coastal Union, Ihefu FC, Singida FG na Kagera Sugar. Huu ndiyo msimu ambao wachezaji wageni wameonyesha maana halisi ya wao kuvuka mipaka hadi ardhi yenye mlima mrefu Kilimanjaro mbuga bora na yenye hadhi Afrika ya Serengeti.

    Wachezaji wengi kwa nafasi mbalimbali wameonyesha viwango bora na kuileta maana halisi ya Ligi namba 6 za ubora barani Afrika, siyo golikipa, mabeki, washambuliaji na viungo wote wameipa hadhi ya namba sita. Mpaka sasa magolikipa wengi wageni wamekuwa bora Djigui Diara wa Yanga SC akiwa na β€œClean sheet” tano, John Noble wa Tabora Utd, Jonathani Nahimana wa Namungo au kinara wa β€œClean sheet” Matampi kutokea Coastal Union na wala siyo Ayoub Lakred wa Simba SC wote wameidhaminisha Visa ya kuingia Tanzania kuwa ni halali kwao.

    Uwepo wa wageni wengi kwenye ligi kuu umewapa nafasi makocha wao kufanya vizuri kwani wachezaji waliyonao wamekuwa bora wakisaidiana na wazawa baadhi, hakuna kocha ambaye haitji huduma ya Henock Inonga na Che Malone wa Simba SC, Benjamini Tamimu wa Ihefu FC, Duke Abuya au Yao Attouhala, Clatous Chama, Max Nzengeli na Joyce Lomalisa wa Yanga SC ni wakati wa kujivunia uwepo wao kwenye Ligi yetu imeongeza ubora wa baadhi ya vilabu vyetu na hiyo ahitaji kuficha.

    Moja ya nafasi ambayo wageni wameitendea haki kwa msimu huu ni Kiungo, inaweza ikawa huu ndiyo msimu ambao Ligi yetu imepata kuwa na viungo wengi wazuri kuliko misimu yote tokea kuruhusiwa kusajili wageni kwenye vilabu vyetu, haina haja ya kubisha sana wala kuweka mjadala kwani takwimu zao zinajieleza kuanzia kufunga hadi kutengeneza magoli wakati pekee wa kufurahia uwepo wao kwani wengi wao ndiyo sehemu ya wachezaji muhimu kwenye vilabu vyao.

    Orodha ya wanaongoza kwa kufunga magoli ligi kuu imeshikiliwa na viungo wengi kuliko washambuliajiΒ  kwenye 10 bora kuna wachezaji saba wa kigeni huku watano kati yao wakiwa ni viungo wakiongozwa na Stephane Aziz Ki wa Yanga SC mwenye magoli 5 akifatiwa na Max Nzengeli wa Yanga SC na Marouf Tchakei wa Ihefu FC wenye magoli 8, Kipre Junior wa Azam FC naye akiwa na nane na Jean Baleke wa Simba (ambaye hivi sasa hayupo kikosini.

    Nje ya kufunga orodha wa kutengeneza magoli inaongozwa na wageni watatu Kipre Junior wa Azam FC akiwa na β€œAssist” 8Β  akifatiwa na Yao Attohoula wa Yanga SC na β€œAssist” 7 , takwimu zao ni nzuri lakini nje ya takwimu hizo wamekuwa na kiwango bora kuanzia namna ya uchezaji wao imekuwa bora sana hakuna mpenda soka ndani ya nchi hii asiyefurahia sana yao ya uchezaji kiwanjani ni fahari kwetu wazawa kumiliki wachezaji wa kigeni wenye uwezo nzuri kama msimu huu, imetupa nafasi ya kujivunia nafasi 12 ya ruhusa ya kuwa na wageni kwenye timu.

    Namna wanavyocheza na viwango wanavyoonyesha ni dhahiri kuwa kuna nafasi kubwa Tuzo ya Mchezaji bora, Kipa Bora pamoja mshambuliaji bora (mfungaji bora) basi zikachukuliwa na wachezaji hao na hata watakaowania kwa kiasi kikubwa idadi Ya wachezaji wengi watakuwa wageni.

    Hata hivyo uwepo wao imesaidia kuongeza jitihada kwa wazawa wetu kupambana na kuamini wanaweza imekuwa chachu kwao kupambania namba na baadhi yao imewapa nafasi ya kwenda nje ndani ya msimu huu, jicho langu laona huu msimu wageni watachukua Tuzo nyingi sana mwisho wa msimu ila uzuri ni kuwa wamekuwa bora sana na ilo halijifichi kwa nafasi tatu ambazo ni kipa, beki na viungo.

    SOMA ZAIDI: Barua Kwako Mo Dewji Rais Wa Heshima Simba ScΒ 

    kikosi ch simba kikosi cha yanga ligi kuu bara simba vs yanga yanga vs simba

    11 Comments

    1. Ndabilenze Ndabilenze on April 16, 2024 11:20 am

      Kozi Bora
      1. Diara djigue πŸ”₯
      2. Yao attohouraπŸ€•
      3. Lomalisa mtambalaπŸ€‘
      4. Bacca Ibrahim πŸ‘
      5. Inonga πŸ–
      6. Aucho Khalid
      7. Nzengeli max mpira 😎
      8. Feisal SalimπŸ€›
      9. Wazili junior🀝
      10. Ki πŸ˜†πŸ”‘πŸ—οΈ
      11. Pacome 😷

      Sub.
      1. Ayoub
      2. Lusajo m.
      3. Msindo
      4. Job
      5. Lawi
      6. Jakaminko
      7. Kibu
      8. Mudathiri
      9. Adam adam
      10. Mzize
      11. Silla

      ✍️ [email protected]

      Reply
      • Heisgrammy on April 16, 2024 1:08 pm

        SIMBA
        Lakreed
        Mwenda
        Mohammed hussein
        Che malone
        Innonga
        Mzamiru
        Kanoute
        Ngoma
        Kibu denis
        Chama
        Onana
        Substitution:::::
        1:Ngoma
        2:Kennedy juma
        3:Ally salim
        4:Jobe
        5:Hussein kazi

        Reply
    2. Ally suleh on April 18, 2024 8:07 am

      Hilo halipingwi na yeyote kiatu no cha ki azizi

      Reply
    3. John on August 29, 2024 12:10 am

      Nice

      Reply
    4. πŸ“ Notification: TRANSFER 1.954527 BTC. Receive =>> https://graph.org/Ticket--58146-05-02?hs=452cfce80aaee0e1288ba9b9988e3424& πŸ“ on May 4, 2025 8:47 am

      4s1qkp

      Reply
    5. πŸ“‚ Ticket- SENDING 1.750614 BTC. Next >> https://graph.org/Ticket--58146-05-02?hs=452cfce80aaee0e1288ba9b9988e3424& πŸ“‚ on May 11, 2025 1:55 am

      39ce46

      Reply
    6. πŸ–‡ Reminder- + 1.270189 bitcoin. Assure >>> https://yandex.com/poll/5JjqQt7R61CTYdYVd17t6p?hs=452cfce80aaee0e1288ba9b9988e3424& πŸ–‡ on May 25, 2025 6:12 am

      sg5nyc

      Reply
    7. πŸ”© Email; TRANSFER 1,183853 BTC. Receive =>> https://yandex.com/poll/T1TnDbUc4R9aLX7Nzhj1Cy?hs=452cfce80aaee0e1288ba9b9988e3424& πŸ”© on May 25, 2025 6:18 am

      wkgb3b

      Reply
    8. πŸ”– Reminder; TRANSFER 1,430666 BTC. Assure > https://yandex.com/poll/T1TnDbUc4R9aLX7Nzhj1Cy?hs=452cfce80aaee0e1288ba9b9988e3424& πŸ”– on June 4, 2025 2:24 pm

      ism7ws

      Reply
    9. 🏷 Email; TRANSACTION 1.301794 BTC. Verify > https://yandex.com/poll/enter/BXidu5Ewa8hnAFoFznqSi9?hs=452cfce80aaee0e1288ba9b9988e3424& 🏷 on June 6, 2025 10:46 am

      ug5utr

      Reply
    10. πŸ”’ Reminder: Operation 1,462866 BTC. Go to withdrawal >>> https://yandex.com/poll/76RuKke5vYn6W1hp2wxzvb?hs=452cfce80aaee0e1288ba9b9988e3424& πŸ”’ on June 15, 2025 9:53 am

      lf84v6

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.