Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Mashabiki SIMBA Wanahitaji Mabadiliko Makubwa Sio Propaganda
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Mashabiki SIMBA Wanahitaji Mabadiliko Makubwa Sio Propaganda

    MhaririBy MhaririApril 7, 2024Updated:April 12, 202414 Comments2 Mins Read10K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Kikosi cha Simba
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Mhariri katika pitapita zangu mtandaoni nimekutana na chapisho la mchambuzi lakini pia ni shabiki wa klabu ya Simba Farhan Kihamu ambapo anasema haya yafuatayo:

    MCHAKATO WA MABADILIKO, hapa nazungumzia mfumo ambapo sasa ifike wakati tufahamu wapi tumefikia na mkwamo upo wapi, mwaka wa nne sasa simulizi ni zile zile ila klabu haiwezi kusajili Wanachama wapya, hii ni sehemu moja wapo muhimu sana.

    Simba inapoteza watu wangapi wenye uwezo wa kuwa Viongozi wa hii timu kwa vigezo vya kukosa kadi? Simba inapoteza mawazo mengi mapya haswa kutoka kwa vijana ambao vision yao ni mpya, matokeo yake kwa zaidi ya miaka 20 sasa sura ni zile zile hakuna watu wengi wa mawazo mapya kwenye hii dunia mpya.

    Mfumo wa mabadiliko utaleta Wanachama wapya wa kizazi cha kuhoji kwa mifano na takwimu na sio kwenda kula korosho na maji tu vikaoni, as long as klabu haitokamilisha huu mchakato basi mkwamo utakuwa mkubwa eneo hili kwakuwa Shabiki ana kazi mbili tu kushangilia na kuzomea, ila Mwanachama ndio ana uwezo wa kuhoji.

    SERA YA USAJILI, Sijui Viongozi wameshasahau kuwa Simba ile bora ilikuwa mseto wa Wachezaji wengi bora wazawa ambao ndio wengi zaidi kwenye timu yoyote Tanzania, tulikuwa na MO Ibrahim, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, John Bocco, Aishi Manula, Tshaba, Kapombe, Mkude Jonas, Ndemla! Kila staa wa Kitanzania alisaini Simba.

    Tumekuwa wazifo kunasa saini za Wazawa wale ambao bora, soko lina Mchezaji kama Pascal Msindo kasaini tena Azam, soko lina wakina Feisal Salum, Kagoma na wengine wengi ila tumepoteza power ya ushawishi? Ama pesa? Kuna sera tumeziacha ikiwemo hii ya Wazawa bora.

    PROPAGANDA, Tunaishi sana kwa maneno maneno na propaganda nyingi tunasahau mambo yetu ya msingi! Tumetolewa na Al Ahly tunasahau hii ni robo fainali ya tano tunatoka, wapi tunakwama? Wapi tuongeze nguvu? Nani anategea? Ila wote tunaiwaza na kumcheka Yanga kutolewa, Simba alikuwa na ndoto ya Nusu na Yanga alikuwa na ndoto ya makundi, nani wa kumcheka mwenzake?

    Tumeenda Misri tupo busy na Fiston Mayele, makosa yale yale ya Cesar Manzoki yanajirudia tena! Asiposaini Simba? Waandishi tukiwachana tunaitwa tumetumika lakini klabu inatumia muda mwingi kwenye propaganda, tunapaswa kubadilika! Mbaya wanajua mashabiki wao wanapenda nini, ndio ubaya.

    Nipo tayari kusahihishwa, nipo kwenye safari ya kujifunza na hayo ni maoni yangu.

    MAONI YAKO NI YAPI MDAU WA KIJIWENI? Niandikie hapa chini

    habari za simba
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.