Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Mashabiki Yanga Msimfurahie PACOME Tekelezeni Wajibu
    Africa | CAF

    Mashabiki Yanga Msimfurahie PACOME Tekelezeni Wajibu

    MhaririBy MhaririFebruary 19, 2024No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Mashabiki wa Yanga
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Nadhani katika mechi ambayo kwa hivi sasa mashabiki wa klabu ya Yanga walikua wanaisubiria kwa hamu kubwa zaidi ni mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CR Belouizdad ambao utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

    Huu ni mchezo ambao umebeba taswira nzima ya kundi D ambalo yuko Medeama , Al Ahly, Yanga Pamoja na CR Belouizdad ambapo mpaka sasa ni wazi kuwa yoyote anaweza kushinda mchezo huu kwa sababu kundi hili la Yanga halihitaji ramli bali linahitaji ushinde nyumbani kwako kwanza halafu wao wengine ndio wakupigie hesabu wewe.

    Nyenzo muhimu zaidi pia uwanjani ukiachilia wachezaji na mbinu za kocha basi ni uwepo wa shabiki ambaye anaingia uwanjani kwa ajili ya kuipa hamasa timu yake na kuhakikisha kuwa wanashinda mchezo huu muhimu kabisa ila kumbuka kuwa mashabiki wanapaswa kuhakikisha kuwa wanakwenda kuwatendea haki wachezaji wao kwa kwenda uwanjani tena kwa wingi,

    Tunafahamu pia kuwa kuna wakati mashabiki huwa wasumbufu haswa changamoto za kupambana na kutafuta tiketi siku ya mechi jambo ambalo kwangu mimi huwa linanikera, tayari klabu wameshatangaza viingilio vya mechi na tayari tiketi zimeanza kuuzwa mtandaoni hivyo ni muhimu sana kwa mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kununua tiketi mapema kabisa na uzuri ni kwamba mchezo huu utakua siku ya wikiendi hivyo ni wazi itakua ni siku ya mapumziko.

    Umefika wakati wa kuachana na kununua tiketi siku ya mechi ili kuepuka kuuziwa tiketi feki na badala yake wanatakiwa kununua na kuingia mapema kabisa uwanjani kusubiria mtanange huu ambao utaweka asilimia kubwa kwa klabu ya Yanga kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya mataifa barani Afrika.

    SOMA ZAIDI: Kiburi Cha Chama Kinalindwa Na Mashabiki Wa Simba

    taarifa za yanga yanga
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.