Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Wachezaji Hawa SIMBA Wamecheza Dakikika Nyingi NBCPL
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Wachezaji Hawa SIMBA Wamecheza Dakikika Nyingi NBCPL

    MhaririBy MhaririDecember 28, 20231 Comment2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Kapteni Msaidizi wa klabu ya Simba
    Kapteni Msaidizi wa klabu ya Simba ambae ni kinara wa kucheza dk nyingi zaidi.
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ligi Kuu ya NBC imesimama kwa takribani wiki tatu kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza leo Visiwani Zanzibar.

    Wakati Ligi ikiwa imesimama tayari klabu ya Simba mechi 10 na ikishinda mechi saba huku wakitoka  sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

    Wakati wanaanza msimu kikosi cha simba kilikuwa na kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ lakini hadi ligi inasimama kupisha michuano hiyo timu ipo kwenye mikono ya kocha Abdelhak Benchikha.

    Katika mechi hizo kuna wachezaji ambao wamecheza dakika nyingi kuliko wengine.

    Makala hii inakuletea wachezaji watano wa klabu ya Simba ambao wamecheza dakika nyingi zaidi

    1. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’

    Mlinzi wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ambaye ni nahodha msaidizi ndiye amecheza dakika nyingi kuliko mchezaji yoyote.

    Zimbwe Jr amecheza dakika 900 ambazo ni sawa na kucheza mechi zote 10 kwa dakika 90 bila kufanyiwa mabadiliko.

    Katika michezo hiyo Zimbwe amecheza kwa uwezo mkubwa huku akisaidia kupatikana kwa mabao matatu (assist).

    1. Che Fondoh Malone

    Mlinzi mpya wa kati, Che Fondoh Malone anashika nafasi ya pili akiwa amecheza dakika 891.

    Raia huyo wa Cameroon amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi chetu huku akitengeneza maelewano mazuri na mlinzi Henock Inonga.

    1. Shomari Kapombe

    Mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji waandamizi kikosini ambaye kiwango chake hakijawahi kuwa na shaka

    Kapombe ni muhimili wa timu yetu upande wa kulia na amekuwa akitengeneza mabao mengi ya kufunga pamoja na nafasi kutokana na ubora wake.

    Katika mechi 10 tulizocheza mpaka sasa, Kapombe amesaidia kupatikana kwa mabao matatu (assist).

    1. Fabrice Ngoma

    Kiungo mkabaji, Fabrice Ngoma wala haitaji maelezo mengi kuelezea uwezo wake uwanjani.

    Ngoma ameingia kwenye kikosi moja kwa moja na anashika nafasi ya nne kwenye orodha ya wachezaji waliocheza dakika nyingi akiwa amecheza dakika 885.

    Katika mechi hizo Ngoma amefanikiwa kufunga bao moja akiwa hatoa assist yoyote.

    1. Saido Ntibazonkiza

    Kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza anakamikisha idadi ya wachezaji watano waliocheza dakika nyingi mpaka sasa ligi ikiwa imesimama.

    Ntibazonkiza ambaye ni mfungaji bora wa msimu uliopita amecheza dakika akiwa amefunga mabao manne huku akisaidia kupatikana kwa jingine moja.

    Endelea kusoma zaidi kuhusu ligi kuu bara kwa kugusa hapa.

    simba sc zimbwe jr

    1 Comment

    1. Pingback: how to buy tadalafil online

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.