Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » YANGA Yatakiwa Kulipa Uharibifu Kwa Mkapa
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    YANGA Yatakiwa Kulipa Uharibifu Kwa Mkapa

    MhaririBy MhaririDecember 11, 20231 Comment2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Tanzania National Stadium ( Benjamin Mkapa National Stadium)
    Uwanja wa Taifa wa Tanzania unaofahamika kama uwanja wa Benjamin Mkapa
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imewasilisha malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kuwataka klabu ya Yanga kugharamia uharibifu uliofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wao dhidi ya Al Ahly .

    Kupitia barua hiyo, Wizara imekemea vikali kitendo hicho kilichotokea na kuutaka uongozi wa klabu ya Yanga kuwasiliana na uongozi wa uwanja ili kubaini ukubwa wa uharibifu huo. Barua ya Wizara inasema ,

    Wizara ilitoa kibali cha kufanyika kwa mchezo wa kimataifa kati ya Yanga SC (Tanzania) dhidi ya Al-Ahly (Misri) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliofanyika tarehe 2 Desemba, 2023 majira ya Jioni.

    Hata hivyo, Wizara imepokea malalamiko kutoka kwa Uongozi wa Uwanja ambapo mashabiki wa Klabu ya Yanga wanalalamikiwa kwa kuwasha fataki wakati mchezo ukiendelea na kusababisha vurugu zilizopelekea baadhi ya viti kung’olewa.

    Wizara inakemea vikali kitendo hiki na kuwataka Klabu ya Yanga mara moja kuwasiliana na Uongozi wa Uwanja ili kuweza kubaini ukubwa wa tatizo na kuona namna bora ya kulitatua.

    Kwa barua hii, Wizara inawasilisha rasmi malalamiko haya kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuwa ndiye mdhamini wa vilabu hivi kwa maombi ya matumizi ya Uwanja huu ili kuwajulisha Klabu ya Yanga SC kuwa inapaswa kugharamia matengenezo ya viti vilivyong’olewa na Mashabiki wakati wa mchezo huu.

    Aidha kuwaonya mashabiki wao kuacha mara moja tabia hizi ili uendelea kustawisha michezo
    na kuulinda Uwanja wa Benjamin Mkapa.

    Maoni yako ni yapi baada ya kusoma kile ambacho Wizara imeweza kukitoa? Usisahau kusoma zaidi taarifa zetu hapa.

    yanga

    1 Comment

    1. Pingback: Kombe La Dunia Kwa Vilabu Kuanza Kesho Saudi Arabia - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.