Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Viwanja 10 Vinavyotumika Kwenye EURO2024 Ujerumani
    Biriani la Ulaya

    Viwanja 10 Vinavyotumika Kwenye EURO2024 Ujerumani

    Living ShayoBy Living ShayoJune 20, 2024Updated:June 26, 20241 Comment6 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Viwanja 10 Vinavyotumika Kwenye EURO2024 Ujerumani
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Nchi ya Ujerumani ni mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Ulaya 2024 (Euro 2024), takribani miaka 18 imepita tangu Ujerumani kuandaa Kombe la Dunia, ambalo Italia ilishinda.

    Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya zitafanyika msimu wa joto kuanzia Juni 14 hadi Julai 14 2024 katika viwanja 10 nchini Ujerumani. Viwanja tisa kati ya kumi vilitumika katika Kombe la Dunia la 2006, isipokuwa Dusseldorf Arena.

     

    Ni muhimu kukumbuka kuwa jiji la Munich ni mwenyeji kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kuwa miongoni mwa majiji11 kuwa mwenyeji wa shindano hilo katika msimu wa joto wa 2021

     

    1. Olympiastadion

    Ni uwanja ambao mechi za timu ya Hertha Berlin (ambayo kwa sasa inashiriki ligi ya daraja la pili) huchezwa, ulikuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya 1936, fainali ya Kombe la Dunia ya 2006 na fainali ya Ligi ya Mabingwa 2015, na umekuwa mwenyeji wa fainali ya Kombe la Ujerumani kila mwaka tangu 1985.

    Uwanja huu una uwezo wa kubeba watazamaji elfu 71 katika jiji la Berlin, utakuwa mwenyeji wa fainali ya Kombe la mataifa ya Ulaya 2024 mnamo Julai 14.

     

    Ulifunguliwa Agosti 1936 wakati wa utawala wa Wanazi na ukakarabatiwa 2000 na 2004. Berlin, ambao kwa sasa ndio mji mkuu wa Ujerumani baada ya kuunganishwa 1990, ni moja ya miji inayovutia. Jiji hilo linalovutia watalii, limejaa historia na utamaduni, kama vile lango la Brandenburg na mnara wa televisheni wenye urefu wa mita 368.

     

    1. Allianz arena

    Uwanja huo ulijengwa na klabu ya Bayern Munich mwaka 1860, ukafunguliwa mwaka 2005.

    Ulikuwa mwenyeji wa ufunguzi wa Kombe la Dunia la 2006 na fainali ya Ligi ya Mabingwa ya ulaya 2012, wakati Chelsea ilipoishinda mwenyeji Bayern Munich kwa mikwaju ya penalty. Pia mechi za Kombe la Ulaya la 2020 katika msimu wa joto wa 2021 zilichezwa katika uwanja huu.

     

    Huu ndio uwanja ambao mechi ya ufunguzi kati ya Ujerumani na Scotland Juni 14 utapigwa hapa majira ya saa 4 usiku kwa saa za afrika mashariki.

     

    Jiji la Munich lina wakazi takribani milioni 1.6. Ni jiji la tatu kwa ukubwa nchini Ujerumani, eneo lililojaa historia, majumba, bustani na kitovu cha unywaji bia.

     

    1. Signal Iduna Park

    Uwanja wa timu ya Borussia Dortmund ni mojawapo ya viwanja maarufu duniani kutokana na ukuta wa njano wa mashabiki. Ulifunguliwa mwaka 1974 na ukafanyiwa ukarabati 2003 na una uwezo wa kubeba mashabiki elfu 62, Umetumika kwenye mechi muhimu, ikiwa ni pamoja na Fainali ya Kombe la UEFA ya 2001 kati ya Liverpool ya Uingereza na Alaves ya Uhispania.

    Utatumika kucheza moja ya mechi mbili za nusu fainali katika Kombe la Ulaya la 2024.

    Dortmund ni kitovu cha utamaduni wa eneo la Ruhr. Eneo hilo lilikuwa maarufu miaka hamsini kwa makaa ya mawe, chuma na bia, lakini kwa sasa ni maarufu kwa teknolojia.

     

    1. MHP Arena

    Uwanja huo umekarabatiwa na kuwa wa kisasa zaidi tangu kujengwa kwake 1933 na una uwezo wa kubeba watu elfu 51. Ulitumika katika Kombe la Dunia la 1974 na 2006, Kombe la Ulaya la 1988 na fainali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa 1959 na 1988, pamoja na Riadha ya Dunia ya 1993. Upo katika mji wa Stuttgart, ni mojawapo ya miji muhimu ya viwandani na makao makuu ya watengenezaji magari ya Mercedes

    5 Volksparkstadion

    Uwanja huo ulifunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka1953, ukafanyiwa ukarabati mwaka 2000, na kuandaa mechi za Kombe la Ulaya la 1988 na Kombe la Dunia la 1974 na 2006. Volksparkstadion upo katika mji wa Hamburg, mji wenye bandari kubwa ya kimataifa, historia tajiri ya kitamaduni, usanifu mzuri majengo na maisha ya usiku ambayo huwa kivutio kwa watalii wengi na una uwezo wa kubeba watazamaji elfu 49.

     

     

    1. Mercur Spiel Arena

    Unamilikiwa na timu ya Fortuna DΓΌsseldorf, ambayo ilishiriki mara ya mwisho ligi kuu katika msimu wa 2019/2020.

     

    Uwanja huo, ambao zamani ulijulikana kama Reheinstaedon, ulikuwa mwenyeji wa mechi za hatua ya makundi za Kombe la Ulaya la 1988 na una uwezo wa kubeba watu elfu 47

    Dusseldorf, mji mkuu wa jimbo la Rhine-Westphalia Kaskazini, mji huo una wakazi 650,000. Rhine-Westphalia ni jimbo lenye watu wengi zaidi nchini Ujerumani.

     

    1. RheinEnergieStadion

    Uwanja wa klabu ya Cologne, ilishuka daraja hadi daraja la pili, ulikarabatiwa kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2006, baada ya kufunguliwa mwaka 1923 na kufanyiwa ukarabati wa awamu ya kwanza mwaka 1975. Ulikuwa mwenyeji wa mechi za Kombe la Ulaya 1988, Kombe la Shirikisho 2005 na Kombe la Dunia la 2006.

     

    Tangu 2010, hutumika kwa fainali ya Kombe la Wanawake la Ujerumani, pamoja na mechi za kandanda za Amerika, kwa mpira wa magongo na matamasha na una uwezo wa kubeba watazamaji elfu 43.

     

    Cologne nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja. Ni nyumbani kwa maeneo muhimu zaidi ya watalii nchini Ujerumani kama Kanisa Kuu la St. Peter, urithi wa dunia wa UNESCO.

     

    1. Deutsche Bank Park

    Uwanja wa timu ya Frankfurt ambao ulifunguliwa Mei 1925 ambao unabeba watazamaji elfu 47. Ulikuwa mwenyeji wa mechi za Kombe la Dunia la 1974, ikijumuisha ufunguzi, Kombe la Ulaya la 1988, Kombe la Shirikisho la 2005 na Kombe la Dunia la 2006. Frankfurt ni eneo la kimataifa la fedha na biashara, mji huo uko kwenye kingo za mto Main. Ni jiji la tano kwa ukubwa nchini Ujerumani na maghorofa yake ya kipekee limepewa jina la utani “Manhattan.”

     

    1. Red Bull

    Ni uwanja wa kisasa wenye paa la kisasa ambalo lilifunguliwa mwaka 2004. Ni uwanja pekee utakao chezewa kombe la Ulaya katika eneo la iliyokuwa Ujerumani Mashariki unaobeba watazamaji elfu 40.

    Ulitumika katika mechi za Kombe la Dunia la 2006. Ni uwanja wa klabu mpya ya RB Leipzig tangu 2010. Mji wa Leipzig umejaa historia na ndipo alipoishi mwanamuziki Johann Bach siku za nyuma. Mji huo ulishuhudia maandamano ya amani mwaka 1989 huku Ujerumani ikijiandaa kuunganisha sehemu hizo mbili.

     

     

    1. Veltins, elfu 50

    Uwanja huo ulifunguliwa mwaka 2001 na ni nyumbani kwa timu ya Schalke FC, bingwa mara saba wa Ujerumani na kwa sasa inashiriki ligi ya daraja la pili. Una paa linaloweza kufunguliwa na kufungwa. Uwanja huo uliandaa fainali ya Ligi ya Mabingwa ya 2004 na robo fainali ya Kombe la Dunia la 2006.

    Upo katika jiji la Gelsenkirchen, lililokuwa maarufu kwa makaa ya mawe na chuma, lakini siku hizi ni kijani kibichi, sinema, safari za boti, na viwanda vya kale

    SOMA ZAIDI: Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    UEFA EURO 2024 UEFA EURO 2024 GERMAN

    1 Comment

    1. 𝔫𝔒𝔬 π”§π”―πŸ€ŸπŸ˜ on June 20, 2024 10:30 am

      mmh hatari sana hadi team ya league daraja la pili ina uwanja wake πŸ˜‚πŸ‘‹

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.