Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Udhaifu Na Ubora Wa Yanga Kwenye Mifumo Hii Kiwanjani
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Udhaifu Na Ubora Wa Yanga Kwenye Mifumo Hii Kiwanjani

    Baraka JohanessBy Baraka JohanessJuly 30, 2024Updated:July 30, 20245 Comments3 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ukiitazama klabu ya Yanga katika jicho la kishabiki unaweza kuiona namna ambavyo ina balaa inavyokua kiwanjani ambapo kwetu sisi tunaowaangalia katika jicho la namna wanavyotekeleza mifumo ya kocha wao Gamondi pia tunaweza kuitazama kwa namna mbili ambapo tunaingalia katika mifumo yao ambapo ni upande wa ubora na pia katika udhaifu.

    Huu hapa uchambuzi mfupi kabisa wa mifumo ya uchezaji wa yanga ambapo kama nilivyosema hapo awali tunaangalia  udhaifu na ubora wao pale wanapokua na mpira lakini pia wanapokua hawana mpira kiwanjani.

    Katika mechi za hivi karibuni ambazo ni za maandalizi ya msimu, klabu ya Yanga wameanza na mfumo wa 4-2-3-1 kwenye makaratasi ambapo wachezaji walijipanga hivi :

    Yanga walipokuwa na mpira walitaka kuunda muundo ambao ungewafanya wawe na idadi kubwa golini hasa kwa kutumia eneo la kati ambapo Aziz Ki, Dube na Maxi walipanga kuathiri eneo hilo

    Lakini muundo wao na mpango wa kutumia eneo la kati haukuwa kama Gamondi alivyotaka kwani ukitazama katika mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs tumeona jinsi ambavyo Nabi pia ni muumini wa kulitumia sana eneo la kati hivyo kukawa na msongamano eneo la kati ikabidi yanga wamtumie Kibabage kama beki wa kulia anaecheza sana juu ya uwanja kisha wakiwa na mpira Abuya acheze kama Kiungo wa pembeni mshambuliaji (LCM) akisaidiana na Mzize eneo hilo kitendo kilicholazimisha Yanga kucheza muundo huu.

    Kisha wakiwa hawana mpira walikuwa na miundo miwili muundo wa kwanza ni 4-1-4-1 muundo wapili ukiwa 4-4-2 ikitegemea katika eneo ambalo Duke Abuya yupo mana mara nyingi alikuwa alicheza pembeni ya aucho lakini kuna mda ilimbidi akabie juu sana ya uwanja

     

    Basi huo ndo ulikuwa uchezaji wa yanga

     

    Ubora wao ulikuwa huu hapa:

    1. Walikuwa na umbo zuri sana wakiwa hawana mpira kila mchezaji anarudi nyuma kwajili ya kuweka idadi kubwa ya wachezaji kwenye boksi lao
    2. Waliweza sana kumlazimisha kaizer chiefs kutokucheza kwa amani endapo walianza mashambulizi kwenye boksi lao yani kutokea nyuma (Aziz Ki , Dube, Mzize ) na baadhi ya maeneo Duke alikuwa Karibu sana na safu ya ushambuliaji ili kuweka presha kubwa

    Udhaifu wa Yanga

    1. Yanga walipoteza sana Mipira ya pili tena kwa hatari zaidi mipira ilikuwa ikizagaa nje ya lango lao wamshukuru mungu kaizer chiefs hawakuwa wakatili leo
    2. Kama ilikuwa ni mbinu ya mchezo sawa muhimu ni matokeo . Lakini wameshindwa kuumiliki mpira hasa kipindi cha pili kuanzia dakika ya 70 Narudia tena kaizer walikuwa wazuri sana leo wapole sana hawakuwa wakatili wamekaa sana na mpira

     

    Note: Ni kama Gamondi amebadilisha staili ya uchezaji kutoka msimu jana kuanzia wachezaji anaowategemea

    Msimu jana ilikuwa Pacome , Maxi na Aziz lakini sasa hivi nimemuona Max Nzengeli ndio amepewa uhuru afanye lolote uwanjani

    SOMA ZAIDI: Barua Kwenu Washambuliaji Kuelekea Msimu Wa 2024/2025

    kikosi cha Yanga leo Mifumo ya Yanga kiwanjani simba sc yanga yanga vs simba sc

    5 Comments

    1. Rweyemamu on July 30, 2024 2:10 pm

      Katika dakika 90 on target za yanga zilikuwa tano wakapata goli nne,ivyo kwenye udhaifu wa pili sikuungi mkono, naamini ni mbinu tu kwamba tuwaache wamiliki mpira alafu tuwafanyie pressing ambazo zilifanya wafanye makosa kwa magoli matatu,ivyo Kaizer kumiliki mpira sio udhaifu bali ni mbinu za mwalimu

      Reply
      • Mr ochu on August 2, 2024 9:16 am

        Yes,unaujua mpira

        Reply
    2. Pingback: Bisris Norte Inahitajika  Kwa Timu Zetu Kimataifa

    3. Mr ochu on August 2, 2024 9:30 am

      Yanga hawakuwa dhaifu kama ulivyofikiwa wewe kwa upeo wako, hakuna atayokubishia kwa sababu ndivyo ulivyoamini.
      Ila nimwambie kitu yanga walikuwa wanawatengeneza kaizer waingie kwenye mfumo wao yanga,na kaizer iliingia mfumoni wakapigwa 4,usiombee uingie kwenye mfumo wao yanga utaumia.Amini usiamini.kaizer waliingia kwenye mfumo.

      Reply
    4. Dj_kanyenye on August 6, 2024 12:47 pm

      Yanga ila kwa sasa ni tishioo sana

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.