Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Simba Wakifanya Hiki Wanamfunga Al Ahly Mapema Tu
    Africa | CAF

    Simba Wakifanya Hiki Wanamfunga Al Ahly Mapema Tu

    Living ShayoBy Living ShayoMarch 29, 20241 Comment4 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ni Simba dhidi ya Al Ahly moja kati ya mchezo  mkubwa na wenye matokeo ya kufurahisha kwa timu zote mbili, kwa sasa hakuna timu isiyomjua mwenzake wamekutana zaidi ya mara ya tatu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mara mbili pekee wakikutana kwenye mchezo wa African Football League.

    Michuano ya Ligi ya Mabingwa mpaka sasa baina yao wawili wamekutana mara 4 huku mara mbili wakikutana kwenye African Football League AFL na kufanya kuwa michezo sita (6), katika michezo hiyo 4 ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Simba SC akiibuka na ushindi mara 2 na Al Ahly naye akishinda mara 2 huku yakifungwa jumla ya magoli 8 huku Simba SC akifunga magoli mawili pekee na Al Ahly akifunga magoli sita. Uzuri ni kuwa michezo hiyo 4 ilikuwa ya Makundi ambapo msimu wa 2018/2019 walikutana kwenye kundi D Simba akiibuka na ushindi 1-0 nyumbani na akipoteza 5-0 ugenini pia msimu wa 2020/2021 walikutana tena na kila mmoja akiibuka na ushindi wa 1-0 nyumbani kwake.

    Nje ya michuano ya CAF Champions League Simba SC na Al Ahly SC wamekutana tena kwenye michuano ya African Football League kwenye hatua ya mtoano ambapo mchezo wa kwanza Simba SC walitoka Sare ya 2-2 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa na kutoa tena sare ya 1-1 nchini Misri Nyumbani kwa Al Ahly na kutolewa kwa goli la ugenini.

    Wachezaji wanaongoza mpaka sasa kufunga magoli baina yao walipokutana mara zote sita, nne za CAFCL na mbili za AFL ni kiungo wa Simba SC Sadio Kanoute pamoja na KMahmoud Kahraba ambao wote wamefanikiwa kufunga magoli mawili  na yote wamefunga kwenye michuano ya AFL huku Karim Nedved naye akifunga mawili kwenye CAFCL Pia kwenye CAFCL wapo wengine wakiwa wamefunga magoli mojamoja kwa wachezaji mbalimbali akiwemo Medie Kagere, Luis Miquissone kwa upande wa Simba SC na Mohamed Sherif, Amr Al Sulaya, Ali Maaloul, Junior Ajayi pamoja na Karim Nedved kwa upande wa Al Ahly.

    Michezo yao mitano ya mwisho msimu huu kwenye mashindano yote Al Ahly wamefanikiwa kufunga magoli jumla ya magoli 12 na wakiruhusu magoli matano na kwa upande wa Simba SC wamefunga magoli 14 na wakiruhusu magoli matatu.

    Timu zote mbili ni waumini wakubwa wa kuweka mpira chini kwa pasi fupi fupi wakitokea chini, Simba SC wamekuwa wakitumia zaidi mfumo wa 4-2-3-1 ambapo wamekuwa wakitumia zaidi viungo watatu kushambulia na wawili wakikaba huku wakisimama na mshambuliaji mmoja pia kwa upande wa Al Ahly wamekuwa wakitumia zaidi mfumo wa 4-3-3 ambapo Reda Slim, Antony Modeste na Karim Fouad wakisimama eneo la ushambuliaji huku Emam Ashour, Marwan Attia na Mohamed Kashfa wakiwa eneo la kati (kiungo) kusaidia mashambulizi na kukaba pia huku Mohamed Kashfa na Marwan Atti wakitumika zaidi kukaba na kushambulia na Emam Ashour akiwa zaidi eneo la kushambulia.

    Uzuri ni kuwa kila timu ina nafasi ya kuweza kufunga goli na hiyo inachagizwa na matokeo ya michezo mitano ya mwisho ya michuano yote wakiwa wamefunga magoli huku wakiwa na wastani mdogo wa kufungwa magoli, pia pale timu hizi zinapokutana daima panakuwa na upatikanaji wa goli hivyo kiufupi kuna asilimia kubwa mchezo huo usimalizike bila kupatikana goli kwa timu zote mbili.

    Namna timu zote mbili zikicheza inachagiza kushuhudia mchezo mzuri ambao timu zote hazina mchezo wa kubaki nyuma tofauti kubwa kwao ni kuwa Al Ahly wakivuka kwenye nusu yao wamekuwa wakiongeza kasi ya kushambulia zaidi tofauti na Simba SC ambao wao wamekuwa wakicheza taratibu na wakati mwingine wakitumia mipira mirefu na “Press” ndogo kwa mpinzani wao wakiwa na mpira.

    Kipi Simba SC wafanye ili waweze kuibuka na Ushindi ? Kikubwa ni wao kutumia zaidi nafasi chache watakazopata kufunga magoli na kuepuka kupoteza ovyo nafasi hizo. Upi udhaifu wa Al Ahly ni kuwa na mchezo wa kutoka zaidi hususa maeneo yao ya pembeni ambapo Percy Tau na wakati mwingine Emam Ashour wakishambulia zaidi upande huo, huko ndiyo maeneo ambayo Simba SC wakiyatumia vizuri wanaweza kupata nafasi kivipi ? Uchezaji wao mara nyingi wanajaa eneo la kati kuanzia wakianzisha mashambulizi. Upi ni ubora wa Al Ahly? Kubwa zaidi ni eneo Lao la kiungo wamekuwa bora sana eneo ilo uwepo wa viungo wao Aliou Dieng na Marwan Attia pamoja na Kashfa.

    Ubora upi wa Simba SC ? Ni eneo Lao la nyuma wamekuwa bora sana na wakitekeleza majukumu yao vizuri pamoja na eneo Lao la ushambuliaji wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi japokuwa matumizi Ya nafasi yamekuwa kidogo tofauti na wapinzani wao ambao wamekuwa na uwiano mkubwa zaidi wa kupiga mashuti yanayolenga lango zaidi japoku nao wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi.

    Tutashuhudia mchezo mzuri wenye mbinu na ubora kwa wachezaji wa timu zote mbili, Simba SC wanapaswa kutumia zaidi nafasi zao kwa usahihi.

    SOMA ZAIDI: Yanga Akimfunga Mamelodi Kwa Mkapa Anafuzu Nusu Fainali

    simba vs al ahly

    1 Comment

    1. Pingback: Kuhusu Simba Nilitegemea Baada Ya Kumuona Mchezaji Huyu - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.