Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nne

“Na siku zote Muuwaji hawezi kuishi, ndiyo maana nilikutoa  gerezani ili uje kuitafuta haki iliyoporwa na Faudhia”  Alikazia Mzee Shomari kisha alimruhusu Diana kuelekea ndani  ya Benki, mpango wa Mzee Shomari ulikuwa ni Kumuuwa Faudhia,  kisha kuiba pesa za kimarekani ambazo zilihifadhiwa ndani ya  Benki hiyo katika chemba ya siri, ilikuwa ni zaidi ya Dola  Bilioni 900 , alimtumia Chogo kama ngao ya kufanya mambo yake  huku akiweka ubia na rafiki yake wa zamani ambaye alikuwa  akiishi Uholanzi, ndiye aliyemtoa jela na kumfadhili pesa za  kufanya ugaidi Tanzania, hivyo Mzee Shomari alikuwa ndiye  Gaidi aliyekuwa akiratibu mipango yote, alikusanya vijana na  kuwapatia silaha nzito, akiwemo Diana na Martin Gimbo maarufu  kama Chogo 

Jinsi alivyowapata Diana na Chogo utakuja kufahamu mbele,  hebu tosonge.. 

Usiku ulikuwa umeingia, ndani ya Jiji la Arusha, Faudhia  alikuwa akimlaumu Mohd kwa kosa la Kumuuwa Mama yake na  Martin Gimbo.

SEHEMU YA TANO

“Hakukuwa na sababu ya kuuwa Watu wasio na hatia Mohd, umeuwa  Mwalimu, umeuwa Bibi na Mjukuu wake” Alisema Faudhia kwa  hasira sana 

“Unanilaumu kwa kutekeleza mipango yangu ya kazi? Unanilaumu  kwa kusafiaha ushahidi wa mwote tulimopita? Faudhia wewe siyo  Mfanyakazi wa kanisa au msikiti, wewe ni askari wa siri wa  kitengo cha Usalama wa Taifa! Sisi tunauwa kwa ajili ya  Taifa” Alijitetea Mohd 

“Unauwa kwa ajili ya usalama wa Taifa? Taifa lipi? Kuuwa Watu  wasio na hatia ndio majukumu ya Usalama wa Taifa? Pengine  umeelewa vibaya mafunzo uliyoyapata, siwezi kuendelea kufanya  kazi na wewe Mohd” Alisema Faudhia kisha alipiga simu kwa  Mzee Shayo akamwambia ambadilishie Mtu wa kufanya naye kazi 

“Kwanini unataka abadilishwe?” Alihoji Mzee Shayo kwa njia ya  simu 

“Sijisikii uhuru wa kuifanya kazi yangu” Alisema Faudhia huku  akiwa anamtazama Mohd ambaye alikuwa na hasira sana akiwa  ameketi kwenye kiti

“Faudhia Mwanangu..” kabla hata hajamaliza alikatiswa na  Faudhia 

“Baba nimesema nibadilishie huyu Mtu” Alisema kwa hasira na  sauti ya juu kuonesha msisitizo kuwa alikuwa akimaanisha  alichokisema na hakikuwa utani. 

“Mpe simu Mohd,” mara moja Mohd alipewa simu na Faudhia,  kabla hajaongea na Mzee Shayo alimtazma sana kwa hasira  Faudhia. 

“Natoa amri ya wewe kurudi Makao Makuu haraka sana” Alisema  Mzee Shayo 

“Lakini Mkuu..” kabla Mohd hajamaliza kujitetea alikatishwa  na Mzee Shayo 

“Hakuna cha Lakini Mohd, rudi Makao makuu” Alisistiza Mzee  Shayo, mara moja Mohd alimtupia simu Faudhia kisha alichukua  koti lake akatoka chumbani hapo lakini kwa bahati mbaya  alikuwa amesahau simu yake ambayo ilikuwa kwenye kochi,  kitendo cha Mohd kutoka ndani ya chumba hicho, simu yake  ilianza kuita, Faudhia alinyanyuka na kuangalia aliyekuwa  akipiga 

Aliona namba imeandikwa Boss, alifikiria afanye kitu gani  aipokee au aiache iendelee kuita hadi ikate, aliichukua na  kuchungulia dirishani, alimuona Mohd akilielekea gari lake  kwa ajili ya kuondoka, aliona ni bora aipokee simu hiyo  sababu alimtilia sana Mashaka kuwa huenda akawa sio Mtu mzuri  kutokana na mauwaji ya Watu wasio na hatia ambayo alikuwa  akiyafanya. 

“Mohd! Muuwe Faudhia sasa hivi kisha urudi hapa” Ilisikika  sauti ambayo Faudhia aliitambua, ilikuwa ni sauti ya kizee ya  Mzee Shomari, mara moja aligundua kuwa Mohd alikuwa ni askari  aliyekuwa akifanya kazi na magaidi, akatambuwa kuwa  kilichobakia kwake ni kifo pekee. Alipochungulia tena  alimuona Mohd akiwa anapiga hatua kurudi ndani baada ya  kugundua kuwa amesahau simu yake, Faudhia alimtazama vizuri  Mohd akiwa bado amesimama pale pale, Mohd alikifikia kitasa  cha mlango bila kujuwa kuwa Faudhia alikuwa amemshtukia kuwa  ni Mamluki anayekisaliti kitengo cha Usalama wa Taifa. 

Alipofungua mlango alimkuta Faudhia akiwa amesimama, Unajuwa  Mohd alikuwa ni askari wa kitengo cha Usalama wa Taifa hivyo  alipoingia tu aligundua kuwa kuna jambo ambalo halikuwa sawa,  alimtazama sana Faudhia akiwa ameganda pale mlangoni,  walikutanisha macho yao ya Kijasusi huku kila mmoja akiwa  anamsoma mwenzake.

Mara simu ya Mohd iliita tena na mpigaji alikuwa ni yule yule  Mzee Shomari, aliisikilizia kidogo kisha aliifuata simu  lakini kabla hajapokea Faudhia alimnyooshea Mohd Bastola 

“Tulia hivyo hivyo Msaliti wewe, kumbe wewe ni mamluki  unayefanya kazi na Mzee Shomari? Nilikuwa nakutilia mashaka  sana Mohd” Alisema Faudhia, Mohd alikuwa amesimama huku simu  ikiendelea kuita mkononi mwake 

“Isogeze hiyo simu kwangu” Alisema tena Faudhia huku  akihakikisha kuwa Mohd hachomoki wala hafanyi ujanja wa aina  yoyote ile. Mohd alimtazama Faudhia kisha alimsoma jinsi  alivyokuwa amesimama ila Faudhia alishtuka mapema kuwa Mohd  anamsoma kisha akamwambia. 

“Ujanja wowote utakaoufanya Mohd napasua kichwa chako”  Alisema Faudhia, Mohd aliinama kidogo kisha aliiburuza simu  ikafika kwenye miguu ya Faudhia 

“Umeanza kutumika upande huo kwa muda gani?” Aliuliza Faudhia  huku akizuga ili ainame aichukue simu 

“Faudhia! Usifikiri kamwe naweza nikasema chochote au hii  siri ikafika makao makuu, katu kitengo hakita ifahamu hii  siri” Alisema Mohd kwa kujiamini kisha alishusha mikono yake  akamwambia Faudhia 

“Si ulikuwa unataka kunitwanga risasi? Fanya hivyo kabla  sijakuwahi” Alisema maneno yaliyojaa ulaghai Mkubwa, ilikuwa  ngumu kwa Faudhia kumuuwa Mohd, alichotaka ni kufikisha  taarifa kwenye kitengo cha Usalama wa Taifa. 

Mohd alianza kumsogelea Faudhia taratbu huku akizidi kuongea  maneno ambayo yalimchanganya Faudhia 

“Wewe ndiyo sababu ya Mama yako kufa, hukustahili kubaki hai  kwa uchafu ambao ulikuwa ukimfanyia Mama yako, laiti kama  taarifa hizi zitavuja ndani ya kitengo basi hautokuwa na sifa  ya kuwa Undercover!! Mtu ambaye amemsaliti Mama yake kwa Baba  yake anaweza vipi kutunza siri za Nchi hii” Alisema Mohd huku  akizidi kusogea, Maneno ya Mohd yalimtia uchungu sana  Faudhia, ni kama alitoneshwa kidonda kilichoanza kukauka 

“Acha Mohd! Achaaaaa” Alisema Faudhia kisha aliweka kidole  sehemu ya kufyatulia risasi ili ammalize Mohd, haraka Mohd  alimuwahi Fadhia na kuushika mkono ambao ulikuwa na Bastola,  Faudhia alipofyatua risasi zote zilipiga juu ya dali. Mohd  alimkunja Faudhia na kumpa mateke matatu ya Mbavu kabla ya  Faudhia kujikunjua

Bastola ilikuwa chini, aliponyanyuka Faudhia alijikuta akiwa  mikono mitupu 

“Nilikwambia hii siri haiwezi kufika kitengo cha Uslama wa  Taifa, kwakuwa nimepigiwa simu nirudi Makao makuu basi wewe  utaonekana umeuawa kwa kuvamiwa hapa Hotelini.” Alisema Mohd  huku akiwa anakunja Shati lake, alikuwa ni mwanaume mwenye  mazoezi na roho ya kikatili sana. 

“Mradi wa kukutengeneza wewe uje kuwa Askari wa kitengo  unafia hapa rasmi” Alisema Mohd kisha alimfuata Faudhia  ambaye alikuwa amejiandaa kukabiliana naye, alirusha ngumi  mfululizo ambazo zote Faudhia alizikwepa lakini alifanya  ujanja wakati anamaliza kurusha ngumi ya mwisho alikunjua  Mguu wa kulia na kumpiga teke la tumbo Faudhia, alijikuta  akianguka chini kisha alijinyanyua na kupanga pambano upya. 

Wote walikuwa na mafunzo ya Kijeshi hivyo kila mmoja alijuwa  namna ya kupambana, Faudhia alijibu mapigo kwa kumpa mateke  mawili yaliyofika hadi kwenye kifua cha Mohd, alisogezwa  pembeni karibu na mlango ambapo kochi lipo, aliangalia chini  kulikuwa na Bastola, pembeni kulikuwa na simu yake yenye siri  nzito, aliona ni bora afanye ujanja. 

Aliokota mto wa kochi kisha alimtupia Faudhia usomi kisha  aliinama ili aichukue bastola lakini Faudhia alikuwa shapu,  kabla hajaokota Bastola alipigwa teke la Mgongo kisha Faudhia  akaipiga teke ile simu na Bastola vikaingia uvunguni mwa  Kochi, alimlazimisha Mohd apambane kwanza. 

Mohd aliinuka na kunvaa Faudhia, aliambulia kutupwa chini  kutokana na namna Faudhia alivyo Shapu. Kabla hajakaa sawa  alipokea ngumi la shingo ambalo lilimsogeza kwenye kochi,  kabla hajatulia tena Faudhia alimpelekea Mohd teke ambalo  Mohd alilidaka kisha alitumia nguvu kubwa alimsukuma Faudhia  ambaye aliangukia kwenye meza 

“Assssh” aligumia Faudhia kutokana na maumivu ya kujigonga  kwenye meza, Mohd hakutaka kusubiri alimrushia ngumi  mfululizo, ngumi ambazo zilimpekeka Fuadhia ukutani, bahati  mbaya ngumi nyingi zilimpata na kumfanya aumie usoni 

Mohd alimpiga Faudhia mateke mfululizo eneo la mbavu huku  akimwambia 

“Unakufa leo” Alisema huku akiwa anamuangalia Faudhia akiwa  anaanguka chini.

Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA SITA

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

11 Comments

Leave A Reply

Exit mobile version