Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nne
“Assssh” aligumia Faudhia kutokana na maumivu ya kujigonga kwenye meza, Mohd hakutaka kusubiri alimrushia ngumi mfululizo, ngumi ambazo zilimpekeka Fuadhia ukutani, bahati mbaya ngumi nyingi zilimpata na kumfanya aumie usoni
Mohd alimpiga Faudhia mateke mfululizo eneo la mbavu huku akimwambia
“Unakufa leo” Alisema huku akiwa anamuangalia Faudhia akiwa anaanguka chini. Endelea
SEHEMU YA SITA
Mohd alimsindikiza Faudhia kwa teke kali lililomzimisha Faudhia, Mohd alitoa kifaa kidogo ambacho kilikuwa na sindano ya sumu ndani yake, aliitoa kisha alimkita Faudhia eneo la shingo.
Baada ya kuhakikisha amemdunga alielekea Kuvuta kochi kisha aliitafuta simu yake ambayo ndiyo ilikuwa muhimu sana kisha Bastola yake ambayo ingekuja kuwa ushahidi pale, aliichukua Bastola na simu kisha aliondoka eneo hilo.
Sekunde kumi na tano baadaye sindano ya sumu ilianza kufanya kazi yake, Faudhia alishtuka huku akiwa anateswa na sumu ambayo ilikuwa ikisambaa kwa kasi mwilini, alijikuta akianza kuishiwa nguvu, alijivuta kisha alifungua kibegi chake kidogo alitoa sindano, alivuta dawa haraka kutoka kwenye chupa kidogo kisha alijidunga sindano akiwa anavuja damu, kisha alianguka chini na kuzima.
Usiku huo, Mzee Shomari alikuwa akisubiria simu ya Mohd ili kumpa taarifa ya kifo cha Faudhia. Alikuwa kwnye kiti cha walemavu akitembea sebleni ndani ya Jengo la China plaza jengo ambalo walilifanya kuwa makao yao ya siri walipoanza kupanga mipango ya Kigaidi, jengo hilo lilikuwa la rafiki yake aliyeko Uholanzi ambaye ndiye aliyekuwa anafadhili ugaidi.
Alianza kukumbuka miaka mingi iliyopita katika Jiji la Mbeya.
Siku ambayo alikamatwa Baada ya kumuuwa Mama yake Diana, alimtazama kwa hasira sana Faudhia, alijenga chuki na kisasi kwa Faudhia. Mzee Shomari alipelekwa Kituo cha polisi, alipewa mateso makali sana ikiwemo kuwekwa kwenye beseni lenye maji na kukosa pumzi, alikumbuka jinsi alivyopigwa hadi kuvunjwa mguu na ndiyo sababu ya yeye kuwa mlamavu ndiyo maana anatembea kwenye kiti cha walemavu.
Alipelekwa mahakamani baada ya kupata matibabu ya mguu kisha alihukumiwa kifungo cha Maisha jela, alipofika huko alikutana na mzungu aliyeitwa Damian, alijenga urafiki na Mzungu huyo ambaye alikuwa na kesi ya kusafirisha madini kinyume cha sheria kutoka Tanzania kwenda Thailand, walishibana wakiwa gerezani.
Akiwa anaendelea kuwaza kilichotokea baada ya kufungwa, simu ya Mzee Shomari iliita alipopokea alisikia sauti ya Mohd ikimwambia
“Faudhia ni damu baridi” Alisema akiwa na maana kuwa ameshamuuwa, Mzee Shomari alishangaa sana kwa jinsi ambavyo alimuuwa Faudhia kisha alimuuliza
“Upo wapi?”
“Nipo njiani narudi Dar” Alisema Mohd
“Tukio lilikuwaje?” Alihoji Mzee Shomari kwa unakini mkubwa huku akionekana alikuwa mwenye akili sana
Mohd alimsimulia Mzee Shomari tukio lilivyotokea kisha Mzee Shomari alisema
“Ukifika Chalinze utaona kuna prado nyeusi, itumie” Alisema Mzee Shomari kisha alikata simu. Alisogea na kutazama chini, aliliona namna jiji la Dar lilivyokuwa likiwaka taa huku barabara ya kutoka Karume kwenda Kariakoo ikiwa nyeupe hakuna Mtu wala gari
Alinyanyua simu yake akapiga simu mahali kisha akasema
“Case Clossed ( Kesi imeisha ) ” alikata simu akajisukuma na kuingia kwenye chumba kingine.
Masaa matano baadaye Mohd alifika Chalinze usiku sana akiwa na gari yake aina ya Toyota V8, mji ulikuwa kimya kabisa, alilliona Prado likiwa linawasha hazard kuashiria kuwa lilikuwa ndiyo gari ambalo Mohd alitakiwa kulitumia, haraka alishuka na kulielekea gari hilo, alipoingia aliangaza ndani ya gari hilo ili kuona kama kulikuwa na Mtu lakini gari hilo halikuwa na Mtu, alivuta funguo na kuiwasha, kitendo cha kuwasha tu gari hilo lililipuka, Mohd alifia ndani ya gari hilo, pembezoni kulikuwa na roli, ndani ya Roli kulikuwa na Mtu ambaye alisikika akiongea na simu akisema
“Target eliminated ( Mlengwa amemalizwa )” kisha roli hilo liliwashwa na kueleka Upande wa morogoro.
Siku iliyofuata, Chogo alipewa kazi na Mzee Shomari ya kuhakikisha anaifahamu ilipo chemba ya siri ambayo pesa hizo za Kimarekani zilikuwa zimehifadhiwa, Mtu pekee ambaye alidhaniwa kuwa anajuwa ilipo alikuwa ni Gavana wa Benki hiyo. Pesa ambazo akina Chogo walikuwa wanazitaka zilikuwa ni pesa za siri ambazo Tanzania iliyauzia madini Nchi ya Saudi Arabia. Chogo alirudi ndani ya chumba ambacho Gavana alikuwemo na Mke wake, alikuwa ameweka rehani maisha ya mmoja wa wafanyakazi wa Benki hiyo ili Gavana aseme mahali ambapo pesa hizo zilikuwa zimehifadhiwa.
Gavana alimuuliza Chogo amajuwaje kama ndani ya Benki kuna pesa za siri ambazo zilitokana na mauzo ya madini
“Acha kuuliza maswali ambayo kamwe hutoweza kupata majibu yake, sema ilipo chemba ya siri vinginevyo namuuwa huyu!!” Alisema Chogo huku Bastola ikiwa kichwani kwa Mfanyakazi huyo
Gavana alikaa kimya hakuonekana kumtetea Mfanyakazi asiuawe, alimtazama Mke wake kisha alirudisha macho kwa chogo.
“Umejuwaje?” Aliuliza tena kwa mshangao mkubwa sana, Chogo alionekana kuwa ni Mtu katili mwenye hasira sana, alimpiga risasi mfanyakazi kisha akamwambia Gavana
“Nakupa masaa matatu uoneshe ilipo chemba ya siri” Chogo alisema kisha aliondoka ndani ya chumba hicho.
Upande wa pili, Mzee Shayo alianza kuingiwa na wasiwasi kuhusu vijana wake wawili aliowatumainia, simu ya Mohd haikupatikana baada ya kuuawa ndani ya gari, simu ya Faudhia iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, ilimpa mashaka juu ya usalama wao, alijitahidi sana kupiga simu lakini simu yake haikuweza kumpa majibu ya nini kilichokuwa kimetokea huko Arusha kwenye operesheni ya kujuwa kuhusu Chogo, alituma Askari wengine wa Kitengo kuelekea Arusha kwa ajili ya kuwatafuta Mohd na Faudhia.
Punde alipokea simu ya Rais iliyomtaka aende Ikulu haraka sana, kutoka Kigamboni yalipo makao makuu ya Kitengo cha siri cha Usalama wa Taifa ilimchukua dakika kadhaa, tayali hali ya tahadhari ilitangazwa hivyo hakukutakiwa Mtu yeyote kutoka ndani, Jiji lilikuwa kimya sana kama makazi yaliyotelekezwa, Mzee Shayo alifika hadi Ikulu kisha alienda kwenye chumba cha siri ambacho Rais na Waziri Mkuu walikuwa wamehifadhiwa.
Rais alihitaji kujuwa Mzee Shayo alifikia wapi katika harakati za kupambana na Kikosi hicho cha Kigaidi, waliketi watu watatu na kuanza kuzungumza, Mzee Shayo alimwambia Rais kuwa ametuma vijana kuelekea Arusha mbako inaaminika kuwa Gaidi namba moja aliyeiteka Benki kuu anatokea huko
“Huo ni ujinga Shayo! Unafuatilia historia ya Mtu badala ya kupambana naye sasa hivi, hadi umalize kuijuwa historia yake pengine gaidi atakuwa amemaliza kazi yake na kuondoka Nchini. Benki ipo chini yao Shayo, historia histori historia itasaidia nini?” Aliuliza Rais akionekana kuwa mwenye hasira
“Mkuu kila jambo linahitaji taaluma katika utendaji, kabla ya kutatua tatizo ni lazima tuangalie lilipoanzia itatusaidia kujuwa ukubwa wake!” Alijitetea Mzee Shayo
“Hivi kweli ulistahili kuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Taifa? Magaidi wamechukua silaha Lugalo na makambi mengine, tayari Nchi hii imekuwa kisiwa cha vita unayajuwa madhara yake? Kiasi kikubwa vita hii utapigana wewe na vijana wako, jeshi lipo katika hali ngumu ya kujinasua” Alisema Rais huku akionekana kuanza kususa mazungumzo hayo, Waziri Mkuu akamwambia Mzee Shayo
“Kuna hazina kubwa sana pale Benki pengine ndiyo sababu ya Ugaidi huu, hakikisha unafaulu Shayo, vinginevyo hatutokuelewa” Alisema Waziri Mkuu kisha Mzee Shayo alinyanyuka na kuaga, alipoondoka Rais alimuuliza Waziri Mkuu
“Nani anajuwa ilipo chemba iliyohifadhiwa pesa?” Aliuliza akiwa makini sana
“Kuna Mdada wa pale Benki anaitwa Selina, yeye bahati mbaya yupo ndani ya Benki na ameshikiliwa kama watafanikiwa kumtambuwa basi mpango wote utavurugika” Alisema Waziri Mkuu na kumpa muda wa kutafakari Rais
“Una hakika Gavana hajui chochote?” Aliuliza Rais
“Gavana anajuwa kuhusu pesa iliyohifadhiwa Benki ila hajui iliwekwa wapi sababu mpango ulifanywa kuwa siri kama ulivyoagizwa”. Alijibu Waziri Mkuu
“Nina uhakika hawawezi kuchukua pesa za Kitanzania watahitaji zile Dola, hili jambo sitaki lifahamike popote na kama itatokea Mtu amejuwa basi katisha Maisha yake” Aliagiza Rais
Naaam!! Mzee Shayo alipotoka Ikulu alihitaji kwenda kutembelea makazi yake yaliyopo Mikocheni B, alikuwa akitembea kwa siri sana hadi alipofika, Kisha aliingia kwenye chumba ambacho alikuwa akikitumia kufanya kazi zake, aliketi ili kujipa utulivu huku akifikiria afanye nini.
•••••••••••••••••••••••••••••••••
Nje kidogo ya Jiji la Arusha, kulionekana gari moja nyeusi aina ya prado ikiwa imeacha barabara na kukita kwenye Mti
Tukio hilo lilionekana kutokea muda mrefu uliopita kutokana na ukimya ambao ulikuwepo, ndani ya gari hiyo alikuwemo Faudhia akiwa ameegemea usukani, alikurupuka kama Mzimu kutoka kifo.
“Uhhhh” alisikia maumivu makali ya kichwa, alionekana kuchoka sana, alifungua mlango na kutoka ndani ya gari, alijivuta hadi chini ya Mti, aliitoa simu yake kisha aliiangalia alikuwa ametafutwa na Nani, aliona ni Mkuu wa Kitengo alikuwa amempigia zaidi ya mara 40, alimpigia Mkuu huyo
“Aah Baba!!” Alisema Faudhia akionekana kuwa na maumivu makali kisha alikohoa na kuanza kumtia hofu Mzee Shayo
“Faudhia upo sawa?” Alihoji Mzee Shayo
“Nilichungulia mlango wa kuzimu lakini bahati nzuri mafunzo yamenisaidia kujinasua” Alisema Faudhia
“Mohd yuko wapi?” Alihoji Mzee Shayo
“Baba!! Mohd ndiye aliyetaka kunipeleka kuzimu, nimeshtuka anafanya kazi upande wa Magaidi, anatumika upande huo na sijui ametumika kwa muda gani, alipewa agizo la kunimaliza” Alisema Faudhia
“What? ( Nini? )” aliuliza kwa mshituko sana Mzee Shayo.
“Ndio…alafu, Mhusika Mkuu wa ugaidi ni Mzee Shomari” Alisema Faudhia na kumuacha kinywa wazi Mzee Shayo
“Una uhakika na maneno yako Faudhia? Mzee Shomari si yupo gerezani?” Aliuliza Mzee Shayo,
“Hapana, nina uhakika na ninachozungumza na yeye ndiye aliyetoa maagizo ya kuuawa kwangu, nahisi ni yeye ndiye aliyehitaji kunimaliza kabla sijavuka mpaka wa Namanga” Alisema Faudhia
“Shit!! Sasa kwanini wametumia nguvu kubwa ya kuzuia habari za Chogo ikiwa gaidi namba moja ni Mzee Shomari?” Aliuliza Mzee Shayo
“Kuna mtego mahali, inavyoonekana kuna mchezo unachezwa hapa Baba” Alisema Faudhia
“Upo wapi kwa sasa?” Alihoji Mzee Shayo
“Nipo nje kidogo ya Jiji la Arusha, jiji hili si salama tena Kwasasa”
“Sikia Faudhia, ni lazima umalize hiyo kazi, fuatilia ujuwe ni kwanini Chogo anafichwa, kuna ufunguo wa hili jambo katika Maisha ya Chogo, hujapata fununu yoyote?”
“Tulionana na Mama yake Chogo, alisema Mwanaye alifariki Miaka mingi kwa ajali ya gari na alituonesha na kaburi lake, lakini pia alituonesha picha ya Mtu aliyeleta Maiti ya Chogo alikuwa ni Mzee Shomari” Alisema Faudhia
“Hapo kuna taarifa juu ya taarifa, tukio juu ya Tukio, hiyo picha iliyopigwa Mzee Shomari alikuwa katika pozi lipi?” Aliuliza Mzee Shayo akiwa nyumbani kwake Mikocheni
“Ilionekana ni picha iliyopigwa bila Mzee Shomari kujiandaa, alikuwa akiongea na Mtu mwingine”
“Yes! Yes! Rudi Arusha haraka sana Faudhia, hakikisha unafahamu stori nzima, naelekea gerezani kujuwa kuhusu taarifa ya Mzee Shomari”
“Sawa Baba” Alisema Faudhia kisha alikata simu, alishusha pumzi zake, alikuwa na kazi nzito iliyojaa hatari mbele yake.
Waligawana majukumu, Faudhia alirudi Arusha, Mzee Shayo alielekea gereza la Segerea haraka sana, alitumia usafiri wa pikipiki ambao aliamini asingeliweza kuchelewa wala kudhurika, Watu wachache sana ndio waliokuwa wakifanya safari za hapa na pale ila shughuli zilikuwa zimesimama kabisa, ilimchukua takribani dakika 50 kutoka Mikocheni hadi Lilipo gereza la Segerea, alikuwa akifahamika hivyo aliingia moja kwa moja hadi kwa Mkuu wa gereza na kumuuliza kuhusu Mzee Shomari, alichojibiwa kilimchosha sana. Naaam!! Alipewa sasa simulizi ya Mzee Shomari akiwa gerezani hadi alivyotoweka
“Baada ya kufungwa alikaa miezi kadhaa tuu, baadaye kulitokea uvamizi hapa na hatimaye alitoroshwa ila ilifahamika kuwa baada ya kutoroka aliondoka Nchini na rafiki yake Mzungu ambaye alikuwa mfungwa mwenzake wakaelekea Uholanzi” Alieleza Mkuu wa Magereza
“Shit!” Alisema Mzee Shayo na kukumbuka wakati tukio hilo linatokea yeye alikuwa mapumziko Nchini Moroco
“Asante!” Alisema kisha aliondoka gerezani hapo akiwa na uhakika kuwa maneno ya Faudhia yalikuwa kweli ila alijiuliza sababu hasa ya ugaidi huo ilikuwa nini.
Aliondoka hapo kichwa kikiwa kimejaa moto, mzigo mzito wa kupambana ulikuwa kichwani pake, Rais alikuwa akimkalia kooni kila wakati asijuwe afanyaje.
Upande wa Faudhia alikuwa tayari amerejea ndani ya Jiji la Arusha kuendelea kuutafuta ukweli kuhusu Chogo, alishaambiwa ni Hospitali gani ilitoa gari kwa ajili ya kusafirisha mwili wa Chogo, gari gani alipata nalo ajali, alifikiria aanzie wapi, aliona ni bora awasiliane na kampuni ya usafirishaji ambayo ilidaiwa gari lao ndio lilipata ajali na kupelekea kifo cha Chogo, alipfika aliambiwa kampuni hiyo imefungwa kwa muda mrefu. Alikutana na mdada mmoja ambaye alionekana kuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo, alijaribu kumbembeleza ili aseme chochote lakini mdada huyo aligoma kabisa, aliona ni bora aondoke.
Alipofika kwenye gari, aliketi na kutafakari aingilie wapi, alipata wazo la kwenda Hospitalini. Lakini akiwa anawasha gari alitazama Side Mirror aliona kuna Mtu akitoka hapo akiwa na kikaratasi mfano wa tiketi hivi, alishangaa wakati aliambiwa hakuna huduma katika kampuni hiyo, aliona ni bora azuge anaondoka, Naam! Alisogeza gari na kuificha mahali kisha alirudi taratibu na kukuta mlango wa kampuni umefunguliwa wote wakati mwanzo ulikuwa umefungwa, kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa wakitoka hapo, alifikiria huenda wakawa wateja, alipoona Watu wameisha, aliingia humo kisha haraka alitoa bastola yake na kumuonesha Mdada huyo. Faudhia Aligeuza maneno ya kibao kilichoandikwa HUDUMA INAPATIKANA akaweka TUMEFUNGA KWA MUDA.
Mdada huyo alionekana kujawa na hofu sana asijuwe anapaswa kufanya nini,
“Ulisema huduma zimesitishwa muda sasa lakini kumbe ulikuwa unajuwa unachokifanya si ndiyo?” Mdada aliendelea kutetemeka sana
“Niambie unafahamu nini kuhusu ajali mbaya ya gari iliyotokea Miaka iliyopita, unamfahamu vipi Chogo? Ukifanya ujanja wowote nazibua kichwa chako” Alisema Faudhia
“Naomba tafadhali usiniuwe nina ndugu ambao wananitegemea Mimi” Alisema Mdada huyo akiwa analia
“Kama unataka nisikuuwe basi sema ukweli unafahamu nini kuhusu Chogo na kwanini ulikuwa unaficha jambo?” Aliuliza kwa masistizo Faudhia huku akijuwa fika kuwa eneo hilo halikuwa salama sana kwake, kwa hofu ya kuuawa Mdada alianza kufunguka
“Nitasema kila kitu ila naomba usiniuwe”
“Mimi ni Undercover wa kitengo, unapaswa kusema ukweli sababu bila hivyo shingo yako itakuwa halali ya risasi nitakayo ifyatu hapa” Alisema Faudhia kwa msistizo sana.
“Ilikuwa ni siku ya Jumatano, nilikuwa ndiyo kwanza nimeanza ajira hapa, alikuja Baba Mmoja mlemavu wa mguu, umri wake ulikuwa umeenda na kusema kuwa anahitaji kuongea na Bosi wetu, bahati nzuri Bosi alikuwa ofisini kwake, Baba huyo alionekana kuwa ni Mtu mwenye fedha nyingi. Alienda kwa Bosi na sikujuwa kuwa alikuwa anaongea nini na Bosi, baadaye alitoka kisha aliniaga kuwa anaondoka, Baada ya dakika 15 Bosi alikuja na kuniambia kuwa kuna kijana atakuja kwa ajili ya kusafiri, nafikiri ndiyo huyo ambaye unamuulizia ila jna lake siwezi kulikumbuka, aliniambia akija nimuoneshe mahali pa kwenda kulala, ilikuwa ni ndani ya Ofisi hii kabla haijajengwa upya. Nilichukulia ni jambo la kawaida tuu, alipokuja kijana majira ya saa moja usiku nilimkatia tiketi kisha nilimuonesha mahali pa kwenda kulala, inaonesha Yule Baba alkuwa akimfuatilia kijana huyo maana baada ya kijana huyo kwenda kulala yule Baba alikuja”
“Aliniuliza Kijana yupo wapi, nilimuelekeza alipo sababu nilimjuwa Baba huyo baada ya kuja mchana na kuzungumza na Bosi, muda mchache baadaye Bosi naye alikuja kisha aliniuliza alipo kijana nilimueleza alipo, alielekea huko na ukimya ulitawala, nilianza kusinzia lakini baadaye nilishtuka baada ya Bosi kuniita na kuniambia kuwa napaswa kuondoka usiku huo, nilikuwa na zamu ya kukesha hivyo kuambiwa vile nilifurahi ili nikalale, lakini nilipoangalia vizuri niligundua yule Baba alikuwa akimsubiria Bosi nje ila alitoka na begi kubwa hivi ambalo hata sikuliona wakati linaingia, nilifunga na kuondoka zangu!!” Alisema Mdada huyo huku akihema juu juu, Faudhia alishusha Bastola yake baada ya kugudua sasa alikuwa akiongea ukweli, alijuwa Baba huyo alikuwa ni Mzee Shomari.
“Enhee ilikuwaje baada ya hapo?”aliuliza tena Faudhia
“Baada ya hapo, siku iliyofuata niliambiwa nisiende kazini ila nitalipwa pesa ya siku kitu ambacho kilizidi kunipa furaha, Mchana kupitia taarifa ya habari nilisikia taarifa kuwa basi la Kampuni yetu lilipata ajali wakati likiwa linafanya safari, Hakuna aliyepona katika ajali hiyo…lakini Bosi alinisistiza sana nisije nikasema chochote kuhusu yule Baba kuja usiku na yule kijana” Alisimulia Mdada huyo ambaye alikuwa mnene kiasi
“Sasa usiri wako umepelekea Nchi kuzama kwenye Lindi la Ugaidi wa kutisha, muda siyo mrefu jiji hili litakuwa chini ya ESS, kama unaweza kuongozana na mimi twende” Alisema Faudhia akimwambia Mdada huyo ambaye alishapukia
Alionekana kuchanganikiwa, waliingia kwenye gari kisha gari liliondoka eneo hilo kuelekea yalipokuwa makazi ya Mama yake Martin Gimbo, miili ya Mama Martin na Mjukuu wake ilishaanza kutoa harufu humo ndani, Faudhia aliingia kutafuta chochote kitakachomuwezesha kufukua kaburi hilo ambalo lilisemekana kuwa ni kaburi la Martin Gimbo.
“Naomba unisaidie hapa, tukishamaliza tunaondoka” Alisema Faudhia kisha alimpatia chepe mdada huyo, walianza kufukua kaburi hilo. Iliwachukua zaidi ya saa nzima hadi kumaliza, chini walikutana na sanduku kubwa ambalo kwa kawaida lilikuwa ni sanduku la kuhifadhia mwili wakati wa kuzika. Walifanikiwa kulivuta juu, wakati huo walianza kusikia milio ya Risasi kwa mbali huku gari za polisi zikiliza ving’ora vyake.
Faudhia alianza kuligonga ili lifunguke, bahati nzuri alipata nyundo ndani ya nyumba hiyo kisha alifanikiwa zoezi la kulifungua Sanduku hilo, yule Mdada alitazama pembeni kwa hofu ya kuona mabaki ya mwili wa marehemu Martin Gimbo, bahati mbaya ndani ya Sanduku hilo kulikuwa na brifkesi ndogo na siyo mifupa wala mabaki ya mwili wa Martin Gimbo
“Yes! Martin Gimbo ndiye Chogo” Alisema Faudhia huku akimtazama Mdada huyo ambaye hakulijuwa hata jina lake. Alilichukua Brifkesi hilo lakini hata kabla hawajapiga hatua hata moja, Faudhia alisindikizwa chini na teke kali lililopigwa kwa ustadi wa hali ya juu, ghafla alihisi ganzi mkono wa kulia, aliliachia brifkesi hilo huku akiwa anaanguka chini, Sanduku lilidakwa
Faudhia alishangaa namna upigaji wa teke hilo ulivyotumia akili na ustadi wa hali ya juu sana, aligeuka kumtazama aliyekuwa amempiga teke hilo, alikutana na sura aliyoifahamu. Naaam! Alikuwa ni rafiki yake wa zamani Diana, Diana alikuwa ndani ya Koti jeusi, sketi nyeusi, pia alikuwa amevalia wigi jeusi.
“Diana ni wewe?” Alihoji Faudhia, hakutegemea kukutana na Diana katika nyakati hizo, aliona kama yupo ndotoni japo alishatumiwa picha ya Miongoni mwa Watu waliokuwa wakiendesha ugaidi Tanzania.
Faudhia alijivuta na kusimama japo kwa maumivu makali, teke alilopigwa lilimfanya ahisi kizunguzungu.
“Umewezeje?” Aliuliza Faudhia
“Kwasababu nimekusubiria kwa zaidi ya miaka 7 Faudhia, nimekusubiri kwa lengo moja tu la kukupeleka kuzimu” Alisema Diana kisha aliweka Brifkesi pembeni, yule Mdada alivyoona hivyo alikimbia eneo hilo sababu alijuwa kuna hatari kubwa inaenda kutokea hapo muda mchache ujao.
“Ulinisubiria unipeleke kuzimu?” Alihoji Faudhia “Ndiyo! Kwasababu ulimuuwa Mama yangu” alisema Diana
“Diana itakuwa umekosea njia, mimi nimemuuwa Mama yako? Ina maana nawe umeingia kwenye mtego wa Mzee Shomari? Diana mnatumika na huyo Mzee ili atimize lengo lake, nisikilize rafiki yangu!! Mimi sikuuwa Mama yako bali yeye Mzee Shomari ndiye aliyefanya hivyo na hiyo ndiyo sababu ya yeye kukaa jela, amka kutoka usingizini Diana” Alisema Faudhia
“Leo tutaona Faudhia kati yangu Mimi na wewe nani yupo Usingizini, Ukifa naondoka na Brifkesi, nikifa unaondoka na Brifkesi” Alisema Diana huku akijiandaa kupambana na Faudhia
“Diana hebu nisikilize, hujapoteza kila kitu katika Maisha yako, una muda wa kubadilisha kila kitu, ungana na Mimi tumdhibiti Mzee Shomari” Alisema Faudhia, maneno ya Faudhia hayakubadilisha Chochote, Diana alikaa mkao wa kuanza kumshambulia Faudhia. Alianza kumfuata Faudhia kama Simba mwenye njaa huku Faudhia akiwa anarudi nyuma ili afikirie namna ya kumzuia Diana.
Faudhia aligundua haraka kuwa Diana alikuwa anatumia pigano maarufu nchini China linaloitwa Wing Chun, alijuwa sasa kumbe Diana alikuwa na taaluma ya mapigano ya Martial arts
Alipomfikia alitua kwenye mapaja ya Faudhia kisha alijirusha na kumzunguka kwa nyuma kisha aligusa mfupa hadimu sana nyuma ya mgongo wa Faudhia, kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, Faudhia alihisi kukatika kwenye uti wa mgongo ila alijikaza asianguke, alifanya haraka na kumgeukia Diana kisha alijipanga kupambana naye, alimwambia
“Acha Diana, Acha unachofanya kumbuka sisi ni marafiki” Alisema Faudhia
“Ningekuwa rafiki yako usingelithubutu kuniulia Mama yangu, alikukosea nini yule?” Alisema Diana huku akionekana kuzidi kujawa na hasira, alijiandaa tena kumpa pigo lingine la Wing Chun…Faudhia alijitahidi kuisoma mikimbio ya Diana ambayo ilikuwa ya haraka mno.
Alifanya kama vile anamkimbia, alimpa mgongo kisha alipohisi Diana yupo nyuma karibu na kumnasa alimchumpa na kugusa mguu mmoja kwenye mti kisha alijipindua na kukutana na Diana ambaye hakutegemea kama Faudhia angejifyetua kisha Faudhia alimpa teke la Maana Diana, alisogezwa pembeni huku akitema damu, ilizidi kumpa hasira, alimfuata tena na kufanya mpambano huo uzidi kuwa mtamu. Ilikuwa ni vita kati ya marafiki wawili waliogeuka kuwa maadui, ndipo walipothibitisha kuwa kuna Msitari mwembamba sana kati ya Upendo na chuki.
Ulikuwa ni mpambano mkali sana, vita ya kurushiana ngumi ilitanda, Ilikuwa kama vile walikuwa wakipeana zamu, dakika tatu kwa Faudhia na dakika tatu kwa Diana. Wakati wanapigana lile Brifkesi lilikuwa pembeni, Faudhia hakujuwa kulikuwa na jambo gani ndani ya Bridkesi hilo jeusi.
Jua lilikuwa likiendelea kuwaka kwa ukali wake. Kutokana na ile sumu ambayo iliingizwa mwilini mwake na Mohd japo alijitahidi kuizuia kwa kujichoma sindano ila ilianza kumletea shida alianza kutokwa jasho, ndio muda ambao Diana aliutumia kumfanyia kitu mbaya Faudhia.
Alipeleka ngumi zaidi ya 10 mfululizo, Faudhia alijitahidi kadiri ya uwezo wake kuzipangua lakini hakuwa na nguvu ya kuzipangua zote alijikuta akiruhusu mwili wake kukutana na ngumi nzito za Diana, alijikutana akishuka chini na kupiga magoti, Diana alilichukua lile brifkesi kisha alimwambia Faudhia
“Onja uchungu wa kifo ambao ulimpatia Mama yangu” Alichomoa sindano ili aweze kumchoma Faudhia
“Diana! Umesahau kila kitu? Kumbuka wewe ni nani, Mzee Shomari anakutumia” Alisema Faudhia japo kwa shida sana huku akihisi kizunguzungu, Diana alitoa kichupa kidogo kisha alifyonza sumu kwa kutumia sindano
“Niliwahi kusimuliwa kuwa Mtu anayekaribia kufa huwa na majuto sana ila nakushangaa wewe Faudhia bado unakaidi kuwa hukumuuwa Mama yangu” Diana alimsongelea Faudhia, alimshika nywele na kupindisha shingo kisha alimchoma sindano, kabla hajaruhusu sumu iweze kusambaa mwilini mwa Faudhia, alipigwa na kitu kizito kichwani, Diana alishindwa kumalizia zoezi, alijitahidi kugeuka lakini alishindwa alijikuta akianguka chini na kupoteza fahamu. Nyuma yake alisimama yule Mdada ambaye alimpa taarifa ya ajali ya Basi, Naam! Ndiye aliyempiga na kitu kizito Diana.
Faudhia alimwambia Mdada huyo kuwa
“Chukua Brifkesi tuondoke hapa, si unajuwa kuendesha gari?” Aliuliza
“Ndio najuwa”
“Tuondoke hapa haraka sana” Alisema Faudhia, hakutaka kummaliza Diana siku hiyo sababu licha ya uadui bado alimtambuwa Diana kama rafiki yake, yule Mdada alimsaidia Faudhia kuingia kwenye gari walilokuja nalo, Milio ya risasi ilitanda kila kona ya Jiji la Arusha, isingelikuwa salama kwa Faudhia kuendelea kukaa hapo
“Tunaenda wapi?” Alihoji mdada akiwa anaingia barabara kuu
“Dar-es-salaam” Alisema Faudhia huku akilifungua Brifkesi hilo ili ajuwe ndani yake kulikuwa na nini na kwanini lilizikwa.
••••••••••••••••••••••••••••••••
Jina la Selina lilifika mikononi mwa Chogo, aliambiwa kuwa ndiye anayefahamu ilipo chemba ya siri iliyohifadhi kiasi kikubwa cha pesa, Chogo alitoka kwenye moja ya Chumba baada ya kumaliza kuzungumza na Mzee Shomari na kupewa taarifa hiyo kuwa kuna Mwanamke anaitwa Selina na yupo ndani ya Benki, yeye pekee ndiye anayefahamu ilipo chemba ya siri. Chogo alitoka akiwa ameshikilia Bunduki aina ya AK47
Mateka walikuwa wamekaa chini kando ya sehemu ya Mapokezi, alipofika aliuliza
“Selina ni nani?” Ilikuwa ni sauti iliyojaa mamlaka sana, aliuliza kwa kumaanisha kuwa alikuwa akimuhitaji Mdada huyo. Selina mwenyewe aliposikia hivyo alijuwa ni kitu gani Magaidi hao walikuwa wakihitaji, baadhi ya Magaidi sura zao walizificha Ila baadhi hawakuzificha akiweno Chogo ambaye waliamini hawezi kutambulika kwa urahisi.
“Selina ni nani?” Aliuliza tena Chogo kisha aliiandaa bunduki kwa lengo la kuleta kitisho
“Mimi hapa” alijitokeza huyo aliyeitwa Selina akiwa amevalia sare za wafanyakazi wa Benki, alikuwa Mwanamke mmoja mzuri mweusi mwenye rasta asilia.
“Mleteni” Alisema Chogo, mara moja Selina alisogezwa mahali aliposimama Chogo, Selina alionekana kuwa muoga sana, Chogo alimwambia Selina
“Usiogope sababu una kazi moja tu ya kufanya, ukishamaliza nitakuacha huru sawa?” Alisema akiwa anatabasamu, Selina aliitikia kwa woga kisha Chogo alisema
“Tuongozane” Alimpa ishara Selina amfuate kwenye moja ya chumba.
Nje ya Benki polisi walizingira benki hiyo wakiwa na silaha za moto huku wakiwa na tahadhari kubwa, walikuwa wakitumia kipaza sauti kuzungumza, Chogo alipofika Chumbani na Selina alimwambia
“Nisubirie hapa, naenda kuongea na polisi” Alisema kisha alichukua AK47 na kuelekea nje ya Benki hiyo.
Kitendo cha Chogo kutoka nje ya Benki kilileta utayari kwa polisi na vitengo vyote vilivyokuwa makini na Benki, Chogo alitoka akiwa hajavaa shati, mwili wali wake ulijaa michoro mingi, alionekana kujiamini sana huku polisi wakiambiana kuwa wanapaswa kumsikiliza sababu alikuwa na mateka ndani ya Benki
Chogo alisimama katikati ya Barabara iliyotoka kivukoni kwenda mjini kisha aliwauliza polisi
“Mlitaka nitoke ndani, nimeshatoka, mlikuwa mnasemaje?” Aliuliza kwa ujasiri, kipaza sauti kilisikika
“Kwanza tunahitaji usalama wa mateka wote walio ndani ya Benki, pili tunataka kujuwa mnahitaji nini?”
“Oooh! Siwezi kuuwa Raia ambao hawana kosa lolote, ila mkileta ujanja nitauwa kila Mtu ndani ya Benki, masaa 24 yajayo nitaiachia Benki hii” Alisema Chogo kisha alirudi ndani ya Benki, hakuna askari hata mmoja aliyejaribu kumshambulia Chogo, moja kwa moja alienda kwenye kile chumba alichomuacha Selina, aliweka Bunduki pembeni kisha alifunga mlango, Chogo alimtazama Selina kwa jicho la kumtamani sana ukizingatia sketi ya Selina ilikuwa imepasuka kidogo hivyo paja lilikuwa nje
Selina alikuwa mwingi wa kutetemeka, Chogo alimfuata Selina kisha alimtandika busu, alimshika matiti na Makalio, alimvua nguo Selina na kumbaka, baada ya kumaliza alimwambia Selina
“Kama lilivyo tamu penzi lako, basi nahitaji uniambie wapi ilipo chemba ya siri iliyohifadhi pesa za Kimarekani” Alisema Chogo akiwa anavaa nguo zake, alipomaliza alikuwa bado hajapata jibu kutoka kwa Selina ambaye alikuwa akitetemeka kwa woga
“Ukimya wako unaashiria kuwa ni bora ufe kuliko kusema ilipo Chemba si ndiyo?” Aliuliza tena Chogo, safari hii alibadilisha sura yake na kujaza hasira
“Tafadhali usiniuwe, ipo chumba namba 43” Alisema Selina
LEO NIMEWEKA NDEFU SANA COMMENTS ZIKIWA CHACHE NARUDI KWENYE KUWEKA FUPI
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA SABA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
24 Comments
Leo kwel ni ndefu had nimefulai
Hongera
Nimeipenda
Haha admini usitunyanyase ww weka unay0jiskia fupi au ndefu ss tunas0ma t 😂
Leo Kweli Nimefrahia Saana Kuusoma Hii Story
Hongera san ni nzur na ya kuvutia unasoma lkin kam vile ni video ipo mbele yko unaiagalia💯
Hongera ndefu alafu tamu
Asante sana leo ndefu
Nzuri sana
Ndo kusema chogo alikua na ugwadu🤣🤣🤣🤣
Nzur sana boss leo mzigo wa uhakika
Leo imefika mahala pake..
Mashaallah asante
Imekaa pouuuwaa
Aah Admin we nouma ,, Leo ndefu Hadi Raha💪
Apo sawa admin 🔥🔥
nzuri san
Ya Leo imekuwa ndefu pia nzuri..Bigup Sana Admin
Aisee kuipata yote tunabonyeza ngapi mkuu😅😅😅✅️
Story nzuri inavutia sana inanifanya kila saaa niwe naingia kwenye kundi kuitafta jitahdi luifanya iwe ndefu pia itoke kwa wakati
Mbona ya Saba hutoi Admin sio poa bwana
Tumesubir sana huweki
nzuri sana
7x51ai