Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya sita
“Kama lilivyo tamu penzi lako, basi nahitaji uniambie wapi ilipo chemba ya siri iliyohifadhi pesa za Kimarekani” Alisema Chogo akiwa anavaa nguo zake, alipomaliza alikuwa bado hajapata jibu kutoka kwa Selina ambaye alikuwa akitetemeka kwa woga
“Ukimya wako unaashiria kuwa ni bora ufe kuliko kusema ilipo Chemba si ndiyo?” Aliuliza tena Chogo, safari hii alibadilisha sura yake na kujaza hasira
“Tafadhali usiniuwe, ipo chumba namba 43” Alisema Selina . Endelea
SEHEMU YA SITA
“Hebu twende huko” Alisema Chogo kisha aliongozana na Selina, waliingia ndani ya Lift kisha safari ilianza kuelekea juu ya Ghorofa hilo la Benki, walipofika huko Selina alimuonesha ilipo chemba, ilikuwa imefichwa nyuma ya Kioo kikubwa ambacho kwa Mtu mwingine ni ngumu kujuwa kuwa eneo hilo kulikuwa kumehifadhiwa Mabilioni ya Dola za Kimarekani ambazo zilitokana na mauzo ya Siri ya Madini ambayo Rais na Waziri Mkuu walifanya Biashara hiyo kisiri
“Fungua” Alisema Chogo, Selina alibonyeza mahali kisha kioo kilijivuta pembeni, kulikuwa na mlango wa Umeme eneo hilo, palitakiwa kuingizwa namba za siri, Selina aliingiza namba za siri na Mlango huo ulifunguka, Chogo hakuamini macho yake, kwa mara ya kwanza katika Maisha yake alishuhudia kiasi kikubwa cha pesa, chumba kilijaa pesa nyingi za kimarekani
“Woww!!” Alisema Chogo akionesha kufurahi sana, alimfuata Selina na kumpiga busu kama ishara ya furaha baada ya kukutana na kiasi hicho ambacho ndicho kilichowafanya waiteke Benki hiyo na baadhi ya Miji na kambi za Jeshi.
“Nakuwa Bilionea muda siyo mrefu Selina, ilikuwa ni ndoto ya Maisha yangu kuja kuwa Bilionea mkubwa Afrika” Alisema Chogo huku akiruka kwa furaha kisha aliendelea kusema
“Hatimaye Baba yangu atalala kwa amani baada ya kuhakikisha nasomba kiasi hiki cha pesa” Aliposema hivi Selina alipata shahuku ya Kumuuliza Chogo
“Baba yako atalala kwa amani? Anahusiana vipi na pesa hizi?” Alihoji huku akiwa anautazama mgongo wa Chogo, alipogeuka alimpa jibu Selina
“Miaka mingi nikiwa na umri wa miaka 10, Baba yangu alikuwa akifanya kazi kwenye mgodi wa Melerani, alipokuwa akichimba alikutana na Jiwe kubwa sana la dini, alienda kuwaambia viongozi wa mgodi huo ambao walielekea pamoja chini kuliangalia, walipothibitisha kuwa Jiwe hilo lilikuwa ni dini lenye thamani kubwa sana walimuuwa Baba yangu kisha walitoa taarifa kuwa amefukiwa na kifusi, niliishi maisha magumu sana. Nilimuaga Mama kuwa naenda Mjini , bahati mbaya nilipata ajali ya gari, kitu pekee kilichonisaidia nilirushwa dirishani na kutumbukia kwenye maporomoko, wengine wote walikufa kwenye ajali hiyo, aliyenisaidia alikuwa ni rafiki wa Baba yangu ambaye alinieleza kila kilichotokea, Mama yangu pia alikufa kwa presha baada ya kusikia kuwa nimepata ajali. Sikuwa na sababu ya kurudi Arusha, yule rafiki wa Baba aliniambia napaswa kulipa kisasi kwa kila kilichomfika Baba yangu”
“Alinisafirisha na kunipeleka Colombia, niliishi huko na kufundishwa biashara ya uuzaji wa madawa ya kulevya, jinsi ya kutumia silaha na mapigano, baadaye nilirudi Tanzania na kutengeneza kundi la ESS, lengo ni kusomba pesa zote zilizotokana na Mauzo ya Madini ambazo Rais na Waziri Mkuu waliifanya Biashara kwa siri sana, wewe ukiwa unalifahamu hilo Selina.” aliposema hivi Selina aliinamia Chini, Chogo alikuwa akiongea kwa Uchungu sana lakini kwa namna alivyoelezea ilionesha wazi kuwa Chogo alidanganywa na Mzee Shomari ili Mzee Shomari afanikishe lengo fulani, kupitia ugaidi huo tayari alishasomba madini kwenye migodi mingi Na kilichokuwa kimebakia ni hicho kiasi kikubwa cha pesa ambacho endapo kitachukuliwa basi alipanga kuwauwa Diana na Chogo kisha atimke zake Uholanzi kwa rafiki yake.
“Pole sana, lakini kufanya hivi huoni kama unahatarisha Maisha yako zaidi?” Aliuliza Selina
“Maisha yangu yalishakuwa kwenye hatari baada ya Baba yangu kufariki huko Mgodini, nilifanya kazi za hatari pale Arusha nikiwa bado shule, nani alijali?” Alisema Chogo kisha alikaa juu ya pesa
“Unahisi unaweza ukatoka hapa ukiwa salama?” Aliuliza Selina
“Baada ya Masaa 24 nitatoka hapa nikiwa na kiasi hiki cha pesa” Alisema Chogo.
Ndani ya Makao makuu ya Kitengo cha Usalama wa Taifa huko Kigamboni, Mzee Shayo alikuwa ameketi akisubiria simu ya Faudhia, hakuwa na taarifa yoyote iliyomhusu Faudhia maana mara ya mwisho walipeana majukumu ya kufanya kwa kila mmoja wakati Faudhia akirudi Arusha Mzee Shayo akienda gereza la Segerea huko Tabata.
Wakati Mzee Shayo anamtafakari Faudhia, huyo Faudhia alikuwa akihangaika namna ya kulifungua Brifkesi lile, kila namba waliyoingiza haikufungua Brifkesi hilo, Faudhia alimtaka yule Mdada kusimamisha gari, kisha alishuka na kutafuta jiwe kubwa, alipasua ile Brifkesi, ndani yake kulikuwa na karatasi zilizoandikwa ” MPANGO ESS”
Haraka Faudhia alichukua kila kitu na kurudi ndani ya gari, alimwambia yule Mdada kuwa aendeshe mwendo wa kasi huku yeye akisoma karatasi hizo ambazo zilionesha kuwa mpango wote wa Ugaidi ulisukwa humo ndiyo maana ulienda kufukiwa ndani ya shimo walilodai kuwa ni kaburi la Martin Gimbo, hivyo basi mpango wa kundi la ESS ulipangwa muda mrefu hata kabla Ya hiyo ajali ya kutengenezwa ya Martin Gimbo.
Karatasi hizo zilikuwa na siri nzito za mipango yote ya Mzee Shomari Nchini Tanzania, kwanza karatasi hizo zilisema ni wapi Mzee Shomari ataweka kambi yaani kule kwenye jengo la China Plaza, pili jinsi madini yatakavyokuwa yanaibwa na kupelekwa Nje ya Nchi, tatu jinsi watavyokiondoa kiasi kikubwa cha pesa ndani ya Benki kuu, Nne jinsi alivyowatumia askari jeshi kupandikiza mabomu katika kambi zote Tanzania kisha akawa na rimoti ya kuongoza mabomu hayo ndiyo maana jeshi hawakuweza kutoka na kwenda kuzuia Ugaidi kwa hofu ya kambi zao kulipuliwa, Tano jinsi alivyo tengeneza ajali ya Basi na kumpata Chogo kisha kumjaza chuki na maneno ya kupandikiza ili aichukie Nchi yake, lengo likiwa kumsadia yeye Mzee Shomari kufanya Ugaidi na kuiba alivyokusudia Tanzania.
Karatasi hiyo ilikuwa na michoro ya namna walivyotengeneza njia ya Chini kwa chini kutokea Msikiti wa Maamur Upanga hadi Benki Kuu, hivyo wangeitumia njia hiyo kuondoka na pesa bila askari kujuwa kuwa walikuwa wameshatimka, Faudhia aliendelea kusoma na kuujuwa mpango wa Mzee Shomari kuanzia A hadi Z, ghafla gari yao iligongwa kwa nyuma na gari moja aina ya Toyota Mkonga nje
Alipochungulia alimuona Diana akiwa ndani ya gari hilo
“Shit!!” Alisema Faudhia akiwa tayari ameshafahamu kila kitu, Diana alijitahdi kutaka kuwasiliana na Mzee Shomari na kumwambia kuwa mpango wao unaweza kwenda songombingo sababu Faudhia ameshajuwa kila kitu lakini mawasiliano yalikuwa yamekata, alichotaka kufanya Diana ni kumzuia kwanza Faudhia asifanye chochote hata kulisogelea Jiji la Dar-es-salaam sababu yalibakia masaa chini ya 24 ili wamalize kazi yao.
Yule Mdada aliendesha kwa woga sana huku akijitahidi kukwepa risasi ambazo Diana alikuwa anazimimina kwa lengo la kuwazuia, Mdada alijikuta akigonga Mti baada ya kuondolewa barabarani na Diana, Ukimya ulitawala sana kwenye gari ya akina Faudhia
Diana alishuka kwenye gari akiwa na Bastola yake, alisogea kwa tahadhari sana kuelekea lilipo gari la akina Faudhia huku akijuwa fika kuwa haitokuwa rahisi kumnasa Faudhia kutokana na mafunzo aliyonayo. Alipofika alimkuta Yule Mdada pekee, hakumuona Faudhia
“Fauhdia yupo wapi?” Alihoji Diana, yule Mdada alionekana kujawa na woga, ilibidi aoneshe mahali ambapo Faudhia alikuwepo, Naam! Alikuwa nyuma ya Mti mkubwa ulio jirani na eneo walilopata Ajali. Baada ya kuona ameshajulikana alipo, haraka Faudhia aliuwahi mkono wa Diana ambao ulikuwa umeshikilia Bastola, wakawa wananyang’anyana Bastola mkononi mwa Diana, hatimaye iliangukia pembeni.
“Diana hupaswi kufanya hivi, ningekuwa nataka kukuuwa ningekuuwa tokea kule tulipokuacha, ila nilikuacha ili utafakari maneno yangu!! Mzee Shomari ndiye aliyemuuwa Mama yako siyo Mimi” Alisema Faudhia akiwa anamtazama Diana kwa jicho lililojaa umakini sana
“Ni bora ungeniuwa pale pale Faudhia ila kuniacha hai ni kosa kubwa sana, unafikiri nitapotea kwa maneno yako? Lazima nilipe kisasi cha kifo cha Mama yangu” Alisema Diana kisha alikaa mkao wake kwa ajili ya kupambana na Faudhia.
Kama kawaida yake alijirusha sambasoti na kutua karibu zaidi na Faudhia, aliona pigo la ngumi lililotumwa na Faudhia, alikwepa kisha aliinuka na teke la mkunjo na kumpiga Faudhia begani, kisha alijifytua na kumkata ngwara Faudhia ambaye alinguka chini hata hivyo haraka alijiokota. Faudhia aliona ni bora apambane na rafiki yake huyo ili kuliokoa Taifa.
Alivuta taswira fupi ya mafunzo aliyoyapata Mexico kisha alimtazama Diana ambaye alionekana dhahiri kuwa alijawa na hasira sana, alifanya kama anamfuata hivi kisha alijifyetua na kutua pembeni akajikuta anautazama mgongo wa Diana, alimsindikiza na teka kali ambalo lilimsomba Diana hadi kwenye mti, alichukia sana Diana aliokota gongo la mti kisha alilitumia kama silaha kupambana na Faudhia ambaye alikuwa tayari amedhamiria kama kufa yeye au kufa Diana maana alijaribu sana kumueleza ukweli wa kilichotokea hadi Mama yake akafa.
Faudhia alirusha ngumi mfululizo bila kupumzika, Diana alijitahidi kuzizuia lakini hakufanikiwa kuzuia zote alijikuta akiruhusu ngumi kadhaa kwenye kifua chake, pale pale alikohoa damu. Faudhia hakuhitaji maongezi tena bali alichotaka ni kuhakikisha anatembea ndani ya muda ili awahi kuzuia mpango wa Mzee Shomari. Diana kila alipojaribu kumsogelea Faudhia alikunbana na kadhia ya mapigo matakatifu yaliyozidi kumfanya ateme damu, Faudhia hakuwa na huruma tena na rafiki yake alijirusha na kutua mbele ya Diana kisha akafanya kama anataka kukimbia alafu akajikunja na kumvaa Diana eneo la shingo kisha akampa kabali ya miguu shingoni.
Hali ilianza kuwa ngumu kwa Diana alijikuta akianza kukosa hewa, alipiga miguu ya Faudhia akiomba aachwe lakini tayari mzimu wa kazi ulikuwa umempanda sana Faudhia, alihakikisha anambana hadi alipokatisha uhai wa Diana, alipohakikisha kuwa Diana ameshakufa alimuacha kisha alimwambia yule Mdada kuwa wanapaswa kuondoka haraka sana, walirudi nyuma wakachukua gari ya Diana kisha waliingia Barabarani kwa ajili ya kuelekea Dar-es-salaam.
Mdada alikuwa akiendesha gari kwa hofu huku akijikuta akiwa na maswali mengi ya kumuuliza Faudhia, alianza kumuuliza
“Wewe ni nani na kwanini unafuatiliwa?” Faudhia alimtazama yule Mdada kisha alimwambia
“Naitwa Faudhia, mimi ni undercover wa kitengo cha Usalama wa Taifa” Alijibu Faudhia kisha alionekana kusahau jambo
“Wewe unaitwa Nani?” Aliuliza Faudhia
“Naitwa Matilda”
“Ooh!! Sawa Matilda nashukuru kukufahamu pia nashukuru kwa msaada wako, kama si wewe ningelikuwa nimeshakufa” Alisema Faudhia, Matilda aliuliza tena.
“Na yule ni nani? Inaonekana mlikuwa mnafahamiana, kwani ulimuuwa Mama yake?” Alihoji tena Huyo Mdada
aliyejitambulisha kama Matilda
“Hapana!! Sikumuuwa Mama yake, yule anaitwa Diana ni rafiki niliyesoma naye huko Mbeya, sijui hata alijiingiza vipi kwenye ugaidi” Alisema Faudhia kisha alirudisha macho yake mbele, safari yao ilizidi kusonga mbele
- •••••••••••••••••
Ndani ya Jengo la China plaza, Mzee Shomari alikuwa bize kumtafuta Diana kwa njia ya simu lakini simu ya Diana haikupokelewa, alimtafuta kwa zaidi ya masaa mawili jambo ambalo lilianza kumpa wasiwasi, alipoona simu zake hazipokelewi alimpigia Chogo ndani ya Benki kuu kisha akamwambia
“Diana hapatikani kwa zaidi ya masaa mawili, maliza mchakato haraka iwezekanavyo” Alipomaliza kumpa maelekezo Chogo, alipiga simu Arusha kwa Mtu mwingine wa kazi kisha alimuagiza kuelekea kwenye kaburi kuangalia kama mzigo utakuwa umechukuliwa
Chogo alipopata maelekezo ya kuendelea na mchakato aliita vijana wake kisha aliwaambia
“Weka pesa zote ndani ya mabegi” Aliposema hivi vijana wake haraka walifungua mfuko mmoja mkubwa sana ambao ulikuwa na mabegi mengi kisha zoezi la kuweka pesa lilianza mara moja.
Zilikuwa ni pesa nyingi mno, walishindilia kwenye mabegi hayo ambayo yalikuwa makubwa na meusi, tayali gari lilikuwa limeshaandaliwa ndani ya Msikiti wa Maamur kwa ajili ya kubeba pesa hizo ambazo watapita nazo chini kwa chini kutokea Posta hadi Upanga.
Kule Ikulu, Rais alikuwa katika hali ya wasiwasi mno endapo chemba ya siri ingefahamika kupitia kwa mdada ambaye anajulikana kama Selina, lakini tayari Selina alikuwa ameshaonesha ilipo chemba ya siri na tayari pesa zilishaanza kuchotwa huko, yeye na Waziri Mkuu walionekana kuficha kuhusu biashara hiyo ya madini ambayo waliifanya kwa siri sana ili baadaye pesa hizo zihamishwe kwa siri kwenda Marekani.
“Naomba niongee na Shayo haraka” Alisema Rais, mara moja Waziri Mkuu alipiga simu kwa mkuu wa kitengo cha Usalama wa Taifa ambaye hadi kufikia wakati huo hakujuwa Faudhia alikuwa wapi, ni mzima au amekufa ila Faudhia alikuwa barabarani kuelekea Dar kwa ajili ya kuzuia mpango wa Mzee Shomari.
Mara moja simu ya Mzee Shayo ilipokelewa na maongezi kati ya Mzee Shayo na Rais yalianza, Rais alisikika kwa kupoa sana tofauti na mwanzo ambapo alionesha hasira sana kwa Mzee Shayo
“Shayo!!” Aliita Rais
“Naam Mkuu” Aliitika Mzee Shayo
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA NANE
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
15 Comments
Duuh! Nilidhani Diana angemuelewa Faudhia
Halooooo Hadithi Tamu Mnoo Hiii
Daaaah jaman mnaishia kwny utam ivoo mbn but iko vzur Sanaa hii story kongole to mwandishi
Ongera sana kikweli mambo ni 🔥🔥 Diana bye bye
🔥🔥🔥🔥🔥
Mambo yanazidi kuwa ya motooo🔥🔥🔥
Daaah kwa nin diana hakutaka kumwelewa rafiki yake😒😒
🔥🔥🔥
Naomba kuipata yote tafadhali nitalipia
duuu leo kifupi
Mambo ni moto
Admin kwan unatumia mfumo gan kutumia na mdaga maana cjajua kila ck kila baada ya mda gan na mda gan unatuma uwe na utalatibu ili tujue maana husomek story ni nzul ila utoaji wako haupo sawa nilipenda jinsi ulivyo kuwa unatoa simuliz ya mama niachie mume wangu nikajua itakayo kuja utaweka mfumo mzuli zaid lakin apa ume long kuliko iliyo pita
Aisee vitu vyangu hivi napenda hadi natamani episode ziungane hongera sana mtunzi
4kgbe4
Bila kuchoka 👊